Julio: Kwa Simba hii ya sasa kuna wachezaji watano tu wanaoweza kuisaidia timu

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Kocha Jamhuri Kihwelo Julio amedai kuwa kikosi cha Simba cha sasa kina wachezaji watano tu ambao wanaweza kuisaidia timu ndiyo maana hakuna matokeo mazuri.

“Wachezaji wa sasa ambao wanaweza kuisaidia Simba hawazidi watano tu, jiulize ile Vipers iliyocheza na Simba kuna timu pale? Wale wangecheza na Simba ile ambayo ipo sawa wangekula tano,” anasema Julio.

Kuhusu Wazawa katika idadi hiyo ya watano wapo wawili na wageni ni watatu.

FploWPaWYAEIJ4B.jpg

Fp47w6HXgAA-nWB.jpg


Chanzo: Wasafi FM
 
Julio alipewa timu ya Under 20 kwenye mashindano ya AFCON ikala kichapo mechi zote na kubeba magoli 12 katika mechi tatu.
Si kila mchezaji anaweza kuja kuwa kocha mzuri.

Wachezaji wenye upeo mpana ambao huwa ni wachache sana katika ulimwengu wa soka ndiyo huwa wanaweza.
 
Goood, unafiki kaweka pembeni, na kakazia kwamba ile vipers iliyocheza na simba kuna timu pale?

Wanamfunga vipers kigoli kimoja kocha anatamani avue nguo zote kwa furaha🤔🤔🤔🤔 ndio simba ya sasa hiyo
 
Goood, unafiki kaweka pembeni, na kakazia kwamba ile vipers iliyocheza na simba kuna timu pale? Wanamfunga vipers kigoli kimoja kocha anatamani avue nguo zote kwa furaha🤔🤔🤔🤔 ndio simba ya sasa hiyo
Kwenye mpira yoyote anaweza kumfunga yoyote, sihitaji hata kukupa mifano kwa hiyo ukishinda lazima ushangilie.

Unaona gere kocha kuwa na mizuka ya kufa mtu. Hadi kuchapa anajua 🤣😂🤣
 
Kuna watu wamefurahi Julio kusema hivyo ila tulishakubaliana tusibishane tena mpira na watu ambao timu zao hazishiriki Super League ni kupoteza muda msiwajibu.
 
Kwa maana hiyo, ujumbe wa kutafsiri kiufundi ni kwamba Simba inatakiwa ifumue kikosi na kujengwa upya kwa kusajili wachezaji wa maana
 
Goood, unafiki kaweka pembeni, na kakazia kwamba ile vipers iliyocheza na simba kuna timu pale?

Wanamfunga vipers kigoli kimoja kocha anatamani avue nguo zote kwa furaha ndio simba ya sasa hiyo
Mnaidharau vipers kwa lipi hasa? Vipers hawa si ndiyo iliyompasua uto mbili kwa karai hapo Kwa Mkapa? Vipers hawa si ndiyo waliomtoa TP Mazembe ambao ndio uto wanajigamba kwamba wamempiga kigogo wa Afrika?

kama mnaona vipers ni vibonde kihivyo basi uto ni vibonde zaidi
 
Back
Top Bottom