Mchambuzi
JF-Expert Member
- Aug 24, 2007
- 4,850
- 9,434
Katiba ya JMT inasema wazi kwamba moja ya sifa za kuwa mbunge ni uwe umemaliza darsa la saba, kwa mtaji huo, Mbowe kama kweli ni form four leaver, basi ana elimu ya juu zaidi ya ile inayotakiwa kikatiba; Pili, kuhusu uongozi wa kambi ya upinzani bungeni (na hata kamati za bunge), hakuna kanuni inayosema uongozi wa namna hiyo lazima uendane na kiwango fulani cha elimu kwani viongozi wa kambi za upinzani pamoja na kamati za bunge kwa mujibu wa Katiba ya nchi wanatokana na wabunge ambao wanatakiwa kuwa na angalau elimu ya darasa la saba; Hivyo hoja ya dada yetu haina mashiko;