VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Kuna mambo ya kuyaletea utani au siasa lakini si Rais wa Jamhuri. Rais anapokuwepo,upo utambulisho wetu kama nchi, na kwa sisi wana-CCM, kielelezo cha juu kabisa cha kichama kwakuwa ndiye Mwenyekiti wetu wa Taifa wa chama. Rais si mtu/taasisi ya mchezo. Anapotua mahali,hupokelewa na wenyeji wa sehemu hiyo wakiongozwa na mkuu wa kiserikali wa sehemu husika. Hiyo ndiyo inayoonesha utofauti. Rais ni rais tu. Ni tofauti na wote.
Leo Dodoma, Rais Jakaya Mrisho Kikwete amelakiwa,pamoja na watu wengine, na Juliana Shonza na Mtela Mwampamba. Hawa vijana walitimuliwa uanachama CHADEMA na baadaye wakajiunga na CCM. Ndani ya chama hawana vyeo vyovyote. Ndani ya Serikali hawana wadhifa wowote. Iweje wao wamlaki Mh.Rais uwanja wa ndege Dodoma? Sioni kama walistahili kuwa hata sehemu ya watu wa kumlaki. Labda wangeenda 'kumvizia' Rais mahali ili wamsalimu.Si vile walivyofanya.
Naamini hivyo kiprotokali.
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam