GE2025 Jukwaa la wahariri lakemea kuhusu 'Kapteni Tesha'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali kauli na maudhui yaliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Oktoba 4, 2025, yakionesha watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi wakihamasisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiingiza katika siasa kupitia mapinduzi.

TEF imesema hatua hiyo ni hatari kwa amani ya nchi, uthabiti wa demokrasia na misingi ya kitaifa iliyoijenga Tanzania tangu uhuru, ikionya kuwa hoja kama hizo zinaweza kuathiri umoja wa Taifa na kuharibu taswira ya Jeshi linaloaminika barani Afrika.

Katika taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TEF tarehe 5 Oktoba 2025, Deodatus Balile, Jukwaa hilo limepongeza uamuzi wa haraka wa JWTZ kutoa taarifa ya kukanusha na kukemea vikali majaribio ya kulihusisha Jeshi na siasa, likinukuu sehemu ya taarifa hiyo ikisema:

"JWTZ inapenda kuutaarifu umma wa Watanzania, kuwa inaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu."

TEF imekumbusha kuwa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Tanzania imekuwa mfano wa demokrasia ya amani, huku chaguzi zikiendelea kufanyika kwa utulivu na wananchi wakiamua viongozi wao kupitia sanduku la kura si kwa mapinduzi.

“Tanzania ilijaribiwa mapinduzi mwaka 1964, 1969 na 1982, lakini kwa hekima ya viongozi na umoja wa wananchi, nchi yetu ilishinda majaribu hayo na kujenga mfumo thabiti unaotenganisha Jeshi na siasa. Wanajeshi wa Tanzania hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa msingi huu ndiyo ngao ya amani na utulivu wetu”, imesema taarifa hiyo.

TEF imeonya kuwa kauli za uchochezi dhidi ya Jeshi ni hatari na zinavunja misingi ya Taifa, ikitoa wito kwa vyama vya siasa, wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuzisambaza au kuzitumia kama nyenzo za kisiasa.

“Vyama vya siasa navyo visikalie kimya kauli zenye mwelekeo wa uchochezi. Kila chama kinapaswa kujitenga na matamko hayo kwa kuyalaani bila woga, kwa nia ya kulinda umoja, maisha na mali za watu wetu. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani, umoja na mshikamano. Njia pekee ya kuendeleza uongozi ni kupitia demokrasia na ridhaa ya wananchi”, imeeleza taarifa hiyo.
1759672258332.png

1759672298815.png
 
ZAMBIA, ALIYEJARIBU KULETA MAPINDUZI AWA SHUJAA WA TAIFA, AWA REJEA YA MASOMO MASHULENI, VYUONI NA MAKUMBUSHO

KESI YA UHAINI ZAMBIA, MSHTAKIWA AFUNGUKA ALIVYOPANGA NJAMA NA MAZINGIRA YAKE

Luteni Christopher Mwamba Luchembe

Katika mahojiano exclusive Luteni Mwamba Luchembe anafunguka miaka mingi baadaye nini kilimsukuma kuvamia studio za Shirika la Habari la Zambia ZBC mwaka 1990 kutangaza mapinduzi ya kungoa serikali ya chama dola UNIP iliyokuwa inaongozwa na Rais Kenneth Kaunda baba wa taifa hilo.

27 May 2022
Lusaka, Zambia
Luteni Mwamba Luchembe

View: https://m.youtube.com/watch?v=yY6JDPWaHuY
Former Zambian army officer Mwamba Luchembe reflects on the day he tried to overthrow Kenneth Kaunda in a military coup. (This interview was recorded while PF were in power and Kenneth Kaunda was still alive.)
Tulikuwa katika kambi yetu kilometa 500 kutoka mji mkuu wa taifa la Zambia, jiji la Lusaka.

1990 hali ya kisiasa na kiuchumi ilikuwa mbaya, wananchi walikuwa na manunguniko mengi ikiwemo ugumu wa maisha, ughali wa bidhaa muhimu kama unga wa sembe, ukandamizaji wa kisiasa uliokuwa unafanywa na chama dola kongwe kimoja UNIP

Maandamano yakatokea jeshi la Polisi likatumwa kudhibiti mandamano hayo lakini wakazidiwa na nguvu ya umma uliojitokeza .

Rais Kaunda akatoa amri jeshi la ulinzi la Zambia watoke kambini kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Hivyo mimi nilikuwa katika Battalion 5 Kaoma, nasi tukapewa amri tuende Lusaka kuongeza nguvu kudhibiti maandamano.

Wakati tukiwa mesi tunakula chakula cha jeshi ambacho hatulipii, mawazo yetu yakaguswa na madhila ya wananchi wasiokuwa na uwezo wa kula ambao walijitokeza kwa wingi kuandamana huku sisi tukila chakula kwa uhakika kupitia kodi zao.

Hivyo tukaona nchi inaenda kubaya kutokana na kuwa na chama kimoja kongwe tawala kilichoishiwa mawazo ya kutanzua changamoto za raia.

Wazo letu likawa kuchukua nchi na kuiongoza kwa miezi sita huku tukijenga mazingira vyama angalau vitatu makini viundwe ili demokrasia iwepo nchini. Hatukutaka kuona vyama zaidi ya vitatu maana tunajua vyama vingine ni vya mfukoni ( briefcase) siyo vyama vya ukweli vya mawazo mbadala

Tukiamini demokrasia ya uwazi, uchaguzi huru, bunge makini vingeweza kuiondoa nchi ktk changamoto iliyokuwa nchi inapitia ...

Ndiyo maana niliongoza platoon iliyokuwa na wanajeshi 32 huku mimi ni kiwa ofisa wao hivyo jumla ya wanajeshi 33 tulivamia kituo cha taifa cha ZBC nami nikatoa tangazo la serikali kupinduliwa...

Tulikuwa tumekubaliana na kambi zingine za Kitwe, Mufulira n.k nao waingie ktk sehemu nyeti za utawala wa kiserikali ktk majimbo ili kukamilisha mapinduzi hayo...

Wananchi walijitokeza kwa wingi mtaani kufurahia tangazo la mapinduzi ya kijeshi. Hata hivyo wenzetu tuliokubaliana kuikamilisha kazi hivyo kote nchini walitugeuka.

Akatumwa askari mmoja mwandamizi atushawishi kuwa mapinduzi yetu hayakufanikiwa.

Nilikamatwa na kupelekwa kituo kikuu cha Central police nikafungiwa katika mahabusu upande wa wanawake, na wale mahabusu wote wanawake kwanza walihamishwa.

Wakaja wanajeshi wa idara ya utambuzi, maofisa wa usalama wa taifa na wa vyombo vingine kunihoji kwa muda wa wiki moja ktk selo hiyo ya wanawake.

Baada ya hapo walinipakiza ktk helicopter tukaelekea katika kambi nilitotokea iliyopo kilometa 500 kutoka Lusaka. Wakafanya upekuzi katika ofisi nikiyokuwa natumia kambini na katika nyumba niliyokuwa naishi kambini.

Wakanirejesha Lusaka hata hivyo usiku ulikuwa umeanza kuingia hivyo rubani wa helicopter akazima mawasiliano yote na kutua eneo mojawapo kwani rubani alitoa taarifa ya kuwa helicopter haina uwezo wa kusafiri usiku wa giza kufika Lusaka. Walizima mawasiliano ili kama kuna njama za wenzangu kuja kuniokoa zisifanikiwe.

Alfajiri na mapema tukamalizia safari yetu kwa usafiri wa barabara hii yote ikiwa ni njia ya medani, kwa waliopanga nami kufanya mapinduzi wasijue nilipo wala nini kimetokea kwangu mimi.

Mahojiano yakaendelea mjini Lusaka ktk nyumba maalum (safe house) kujaribu kupata habari zote za Mapinduzi na wahusika wote katika njama hii ya kupindua nchi.

Walitumia koleo / pliers kutoa meno yangu kavukavu bila ganzi, lakini situwasaliti wala kutaja wenzangu waliotayarisha jaribio la kuangusha serikali.

Baada ya kunisulubu hivyo, wakanirudisha kwa kificho kituo kikuu cha Polisi huku nikiwa na maumivu makali. Wakanipandisha ghorofani, watu wa Idara ya Usalama na wale wa Idara ya Utambuzi jeshini wakapanga mipango watawaambia nini raia hata polisi na wanajeshi watakaoniona.

Hivyo basi wakanivua nguo zote tukiwa ghorofani na kuzitupa kupitia dirishani. Kutoka juu ghorofani wakanitelemsha mzobemzobe mbiombio uchi wa mnyama nikiwa mtupu, kisha wale wote walikuwapo kituo kikuu cha Polisi wakanishangaa si polisi, raia na waandishi wa habari hata wapita njia wakabaki wanajiuliza kulikoni..

Watu wa Idara na Vyombo wakasema huyu ni kichaa aliyewehuka siku nyingi kabla ya mapinduzi, faili lipo jeshini na kwa vile alikunya sana Pombe na bangi ndiyo maana akatimka kwenda, kutangaza mapinduzi yale.

Baada ya miezi miwili nikastaafishwa jeshi kwa sababu za 'kiafya' yaani ugonjwa wa akili. Hata hivyo vyombo vya usalama vikamwambia rais pamoja na hii hadaa tuliyoitengeneza ukweli watu wanataka na wanaamini mabadiliko ya kuleta vyama vingi vya kisiasa. Hivyo ni bora rais aanzishe mchakato wa mabadiliko ya katiiba kuruhusu na kuafiki kwa moyo mkunjufu vyama vingi, demokrasia na uchaguzi huru kupitia tume huru ya uchaguzi.

Hivyo mwaka 1991 mchakato wa vyama vingi na katiba mpya vikapitishwa na bunge la Zambia kwa usimamizi wa karibu wa rais Kenneth Kaunda.

Mapinduzi yale yaliyoshindwa hata hivyo yalileta jambo chanya kuwa watu wanataka mfumo wa vyama vingi, yalionesha kuwa ukiritimba wa chama dola kongwe cha UNIP na rais nguvu yao ya ushawishi wa chama kimoja umepungua na wajitayarishe kuwa chama cha upinzani.

Kwa ujasiri wa Luteni Mwamba Luchembe kuongoza jaribio la mapinduzi , sasa anahesabika kama baba wa mabadiliko / reforms za kupatikana katiba mpya na demokrasia ya vyama vingi nchini Zambia.

Katika mitaala vya masomo ya uraia / civic Luteni Mwamba Luchembe anatokea ktk vitabu mashuleni kuwa alikuwa chachu ya mabadiliko yaliyoleta vyama vingi kuruhusiwa nchini Zambia.

Mbali ya watoto wa shule kusomeshwa mchango wake Luteni Mwamba Luchembe kuleta mabadiliko, sasa katika Makumbusho ya Taifa mjini Lusaka na makumbusho ya majimbo mbalimbali nchini Zambia picha yake ipo miongoni mwa watu waliotoa mchango kwa taifa la Zambia hadi kufikia lililopo sasa.

Rais Frederick Chiluba aliposhinda uchaguzi wa vyama vingi kupitia chama cha upinzani alimrejesha Luteni Mwamba Luchembe kazini na kumpa cheo mserereko hadi kuwa Captain kisha kumstaafisha kwa kumpatia pensheni stahiki ya cheo alichofikia.

Source : ken studio
 
“Vyama vya siasa navyo visikalie kimya kauli zenye mwelekeo wa uchochezi. Kila chama kinapaswa kujitenga na matamko hayo kwa kuyalaani bila woga, kwa nia ya kulinda umoja, maisha na mali za watu wetu. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani, umoja na mshikamano. Njia pekee ya kuendeleza uongozi ni kupitia demokrasia na ridhaa ya wananchi”, imeeleza taarifa hiyo.
Nadhani chama kubwa huko hapatoshi, Ila statement yao ndo itaamua kina Mwajuma na Mwalimu waseme nini.
Hii iko off script Balile.
 
02 September 2023
Makala maalum Ni nini kinachosababisha wimbi la mapinduzi ya kijeshi barani Afrika? | DW Habari Afrika

Yupi mwingine kiongozi wa Kiafrika njiani kupinduliwa na Jeshi - na itakuwa zamu ya nani?

View: https://m.youtube.com/watch?v=NS4aF11yWVQ
Kuanguka kwa kiongozi wa Gabon Ali Bongo kumewakera watawala wa mabavu na wanademokrasia vile vile.

Cameroon na Rwanda zote zilifanya mabadiliko ya haraka katika jeshi lao la juu ndani ya saa chache baada ya mapinduzi huko Libreville.

Na wana sababu nzuri ya kuwa na wasiwasi: Tangu Vita vya Pili vya Ulimwengu, nchi 45 kati ya 54 za bara hilo zimekumbwa na majaribio ya mapinduzi, na unyakuzi wa kijeshi unaongezeka tena sasa.

Mapinduzi nchini Gabon ni ya hivi punde zaidi katika mfululizo wa mashambulizi ya hivi karibuni ya kijeshi katika bara la Afrika. Nchi nyingine tano katika eneo hilo pia zimeshuhudia mapinduzi.

Hivi majuzi nchini Niger mwezi uliopita. Mnamo 2022, Burkina Faso iliona nafasi mbili katika chini ya miezi tisa. Mnamo 2021, Waziri Mkuu wa Sudan Abdulla Hamdok aliondolewa madarakani kwa nguvu za kijeshi, mwaka huo huo Guinea na Mali zilikumbwa na mapinduzi yao wenyewe
 
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali kauli na maudhui yaliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Oktoba 4, 2025, yakionesha watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi wakihamasisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiingiza katika siasa kupitia mapinduzi.

TEF imesema hatua hiyo ni hatari kwa amani ya nchi, uthabiti wa demokrasia na misingi ya kitaifa iliyoijenga Tanzania tangu uhuru, ikionya kuwa hoja kama hizo zinaweza kuathiri umoja wa Taifa na kuharibu taswira ya Jeshi linaloaminika barani Afrika.

Katika taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TEF tarehe 5 Oktoba 2025, Deodatus Balile, Jukwaa hilo limepongeza uamuzi wa haraka wa JWTZ kutoa taarifa ya kukanusha na kukemea vikali majaribio ya kulihusisha Jeshi na siasa, likinukuu sehemu ya taarifa hiyo ikisema:

"JWTZ inapenda kuutaarifu umma wa Watanzania, kuwa inaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu."

TEF imekumbusha kuwa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Tanzania imekuwa mfano wa demokrasia ya amani, huku chaguzi zikiendelea kufanyika kwa utulivu na wananchi wakiamua viongozi wao kupitia sanduku la kura si kwa mapinduzi.

“Tanzania ilijaribiwa mapinduzi mwaka 1964, 1969 na 1982, lakini kwa hekima ya viongozi na umoja wa wananchi, nchi yetu ilishinda majaribu hayo na kujenga mfumo thabiti unaotenganisha Jeshi na siasa. Wanajeshi wa Tanzania hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa msingi huu ndiyo ngao ya amani na utulivu wetu”, imesema taarifa hiyo.

TEF imeonya kuwa kauli za uchochezi dhidi ya Jeshi ni hatari na zinavunja misingi ya Taifa, ikitoa wito kwa vyama vya siasa, wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuzisambaza au kuzitumia kama nyenzo za kisiasa.

“Vyama vya siasa navyo visikalie kimya kauli zenye mwelekeo wa uchochezi. Kila chama kinapaswa kujitenga na matamko hayo kwa kuyalaani bila woga, kwa nia ya kulinda umoja, maisha na mali za watu wetu. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani, umoja na mshikamano. Njia pekee ya kuendeleza uongozi ni kupitia demokrasia na ridhaa ya wananchi”, imeeleza taarifa hiyo.
Huyu mpumbavu Balile hii nchi ikishapata ukombozi napendekeza Jeshi lianze na yeye kabla hata ya kina Samia, Abdul, Kikwete na Mchengerwa.

Pesa anazolipwa na Mafisadi zinampa kiburi sana hadi saivi anajiona anaweza kuwakemea hadi Wazalendo wetu waliokula kiapo kulifia hili Taifa.
 
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali kauli na maudhui yaliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Oktoba 4, 2025, yakionesha watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi wakihamasisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiingiza katika siasa kupitia mapinduzi.

TEF imesema hatua hiyo ni hatari kwa amani ya nchi, uthabiti wa demokrasia na misingi ya kitaifa iliyoijenga Tanzania tangu uhuru, ikionya kuwa hoja kama hizo zinaweza kuathiri umoja wa Taifa na kuharibu taswira ya Jeshi linaloaminika barani Afrika.

Katika taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TEF tarehe 5 Oktoba 2025, Deodatus Balile, Jukwaa hilo limepongeza uamuzi wa haraka wa JWTZ kutoa taarifa ya kukanusha na kukemea vikali majaribio ya kulihusisha Jeshi na siasa, likinukuu sehemu ya taarifa hiyo ikisema:

"JWTZ inapenda kuutaarifu umma wa Watanzania, kuwa inaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu."

TEF imekumbusha kuwa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Tanzania imekuwa mfano wa demokrasia ya amani, huku chaguzi zikiendelea kufanyika kwa utulivu na wananchi wakiamua viongozi wao kupitia sanduku la kura si kwa mapinduzi.

“Tanzania ilijaribiwa mapinduzi mwaka 1964, 1969 na 1982, lakini kwa hekima ya viongozi na umoja wa wananchi, nchi yetu ilishinda majaribu hayo na kujenga mfumo thabiti unaotenganisha Jeshi na siasa. Wanajeshi wa Tanzania hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa msingi huu ndiyo ngao ya amani na utulivu wetu”, imesema taarifa hiyo.

TEF imeonya kuwa kauli za uchochezi dhidi ya Jeshi ni hatari na zinavunja misingi ya Taifa, ikitoa wito kwa vyama vya siasa, wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuzisambaza au kuzitumia kama nyenzo za kisiasa.

“Vyama vya siasa navyo visikalie kimya kauli zenye mwelekeo wa uchochezi. Kila chama kinapaswa kujitenga na matamko hayo kwa kuyalaani bila woga, kwa nia ya kulinda umoja, maisha na mali za watu wetu. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani, umoja na mshikamano. Njia pekee ya kuendeleza uongozi ni kupitia demokrasia na ridhaa ya wananchi”, imeeleza taarifa hiyo.
Kama ni Wanaume ,wangeitisha Vyombo vya habari Sasa🤣🤣
 
CAPTAIN TESHA KUWA MAARUFU IMEKUWA TISHIO ?

TOKA MAKTABA :

Kisa cha mwezi September 1972 Dr. Hastings Kamuzu Banda apata hofu kuu kuona kuna raia asiye rais kupata umaarufu

View: https://m.youtube.com/watch?v=vvgC3RS3waE
Dr. Hastings Kamuzu Banda amtimua mwanamuziki nguli Percy Sledge baada ya kufanya tumbuizo la kufa mtu uwanja wa Kamuzu Stadium.

Baada ya rais Kamuzu Banda kuona jinsi umati wote uliojitokeza katika Uwanja wa Kamuzu Banda kuonesha hisia zao zote kwa mwanamuziki huyo na kumsahau rais huyo aliyekuwepo jukwaa kuu la VIP, mara baada ya tamasha hilo rais Dr. Kamuzu Banda akaamua kumpa deportation kwa hofu ya kuona kuna mtu anaweza kusababisha watu kwa muda kumsahau Ngwanzi Dr. Hastings Kamuzu Banda, hivyo vyombo vyake vya dola (State Apparatus) kumwambia ngwazi rais kuwa hii siyo dalili nzuri kwa utawala wake...

Tangu siku hiyo mwanamuziki huyo nyota akapigwa marufuku kutorejea Malawi tena, kosa ni mwanamuziki huyo kujaza kiwanja cha Kamuzu Band stadium kuliko mikutano yake ngwazi Dr. Hastings Kamuzu Banda.

Serikali ikadai mwanamuziki huyo amekosa maadili ya kitaifa ya Malawi ndiyo maana ametimuliwa ...

SOMA VISA VYA WANASIASA:
Source :Dar es Salaam ilikuwa Mecca ya vyama vya ukombozi, pia jiji la mapigano baina ya vyama hasimu vya ukombozi Afrika ya Kusini
 
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali kauli na maudhui yaliyosambazwa katika mitandao ya kijamii Oktoba 4, 2025, yakionesha watu wanaodaiwa kuwa wanajeshi wakihamasisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kujiingiza katika siasa kupitia mapinduzi.

TEF imesema hatua hiyo ni hatari kwa amani ya nchi, uthabiti wa demokrasia na misingi ya kitaifa iliyoijenga Tanzania tangu uhuru, ikionya kuwa hoja kama hizo zinaweza kuathiri umoja wa Taifa na kuharibu taswira ya Jeshi linaloaminika barani Afrika.

Katika taarifa iliyosainiwa na Mwenyekiti wa TEF tarehe 5 Oktoba 2025, Deodatus Balile, Jukwaa hilo limepongeza uamuzi wa haraka wa JWTZ kutoa taarifa ya kukanusha na kukemea vikali majaribio ya kulihusisha Jeshi na siasa, likinukuu sehemu ya taarifa hiyo ikisema:

"JWTZ inapenda kuutaarifu umma wa Watanzania, kuwa inaendelea kutekeleza majukumu yake kikatiba kwa uaminifu, utii na uhodari kwa kuzingatia kiapo chetu."

TEF imekumbusha kuwa tangu kurejeshwa kwa mfumo wa vyama vingi mwaka 1992, Tanzania imekuwa mfano wa demokrasia ya amani, huku chaguzi zikiendelea kufanyika kwa utulivu na wananchi wakiamua viongozi wao kupitia sanduku la kura si kwa mapinduzi.

“Tanzania ilijaribiwa mapinduzi mwaka 1964, 1969 na 1982, lakini kwa hekima ya viongozi na umoja wa wananchi, nchi yetu ilishinda majaribu hayo na kujenga mfumo thabiti unaotenganisha Jeshi na siasa. Wanajeshi wa Tanzania hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa msingi huu ndiyo ngao ya amani na utulivu wetu”, imesema taarifa hiyo.

TEF imeonya kuwa kauli za uchochezi dhidi ya Jeshi ni hatari na zinavunja misingi ya Taifa, ikitoa wito kwa vyama vya siasa, wananchi na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuepuka kuzisambaza au kuzitumia kama nyenzo za kisiasa.

“Vyama vya siasa navyo visikalie kimya kauli zenye mwelekeo wa uchochezi. Kila chama kinapaswa kujitenga na matamko hayo kwa kuyalaani bila woga, kwa nia ya kulinda umoja, maisha na mali za watu wetu. Tanzania imejengwa juu ya misingi ya amani, umoja na mshikamano. Njia pekee ya kuendeleza uongozi ni kupitia demokrasia na ridhaa ya wananchi”, imeeleza taarifa hiyo.
Bora hata jukwaa la cheka tu, si hili la watega bahasha za khaki kutoka kwa Msigwa!!
 
Back
Top Bottom