Jukwaa la Celebrity kwa sasa limevurugwa na watu hawa

Its Pancho

JF-Expert Member
Sep 21, 2018
14,185
22,589
Mwanzo jukwaa hili lilikuwa lina vitu vitamu vinavyohusu ma celebrity wetu na muziki wao kiujumla huku wanajamvi wakigusia pande zote kuhusu muziki wetu na lilinoga sana.

Ila majuzi hapa jamvini wamekuja chawa rundo humu ndani na kuharibu jukwaa kwa nyuzi za kichawa chawa ,ushabiki maandazi huku wakigeuza jukwaa kuwa Instagram ya umbea umbea. Na uteam bila wao kulipwa hata mia

Wakitoa nyuzi za kukatisha tamaa wasanii wengine wakienda mbali na kuingilia maisha yao binafsi na kuyakejeli. Yaani ukiingia jukwaa hili ni wao wanataka umtaje na kumsifia msanii mmoja tu yaani Diamond Platinumz.

Kwa mtindo huu tutasogeza mziki wetu mbele vipi? Maana hata Diamond mwenyewe anajitahid kuusogeza muziki mbele ila chawa wake ndo mnamuangusha.

Badilikeni tuongelee muziki wa wasanii na sio kupambanisha wasanii.
 
Wewe jamaa umejitoa kwenye uteam wakati kupitia tu uzi wako unaonesha wewe una uteam ndio maana unakasirika mtu kumsikia msanii fulani alafu unataka mawazo yako yafanane na yako.
 
Lakini mkuu mtoa mada nawe kama upo team pinzani vile
Sijawahi kufanya huo ujinga wa kuwa na team. Mbona mwenye media yetu huwa napiha ngoma za aina zote?

Hii ni kuonesha nasapoti kadri ya uwezo wangu

Natoa sifa na ushauri panapostahili

Huwa namjibu mtu kutokana na anavyokuja
 
Wewe jamaa umejitoa kwenye uteam wakati kupitia tu Uzi wako unaonesha wewe una uteam ndio maana unakasirika mtu kumsikia msanii fulani alafu unataka mawazo yako yafanane na yako
Hujaelewa na labda tu niambie hiyo team yangu unayosema ni IPI?
Ungejua kazi yangu wala usingeniletea uchawa hapa ..

Mbona sasa wewe huwa unataka mawazo yako yafanane na kila mtu? Mtu akipinga unasema chuki..

Badilika dogo kuna maisha baada ya uchawa
 
Sijawahi kufanya huo ujinga wa kuwa na team ..
Mbona mwenye media yetu huwa napiha ngoma za aina zote?

Hii ni kuonesha nasapoti kadri ya uwezo wangu ..
Natoa sifa na ushauri panapostahili .
Huwa namjibu mtu kutokana na anavyokuja
Wewe upo media gani?
 
Back
Top Bottom