Kwa Wasanii wa Muziki: Tukuze Muziki wetu tuache kurukaruka na Miziki ya watu.

Daby

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
33,648
75,732
Naelewa Muziki ni biashara lakini kwa upande mwingine ni tunu na utambulisho wa jamii.

Wasanii wetu wamekuwa wanatukosea saana na wanaukosea utamaduni wetu. Tumekuwa ni watu wa kurukiarukia Muziki wa mataifa mengine bila kujua tunaua Muziki wetu.

Miaka ya 2010 kwenda chini tulijitahidi na tuliliteka soko la Africa mashariki. Baada ya hapo Wasanii wetu wote wakakimbilia kwenye Kwaito. Miaka miwili haikukata Kwaito ikakosa soko. Tukahamia kwa wanigeria. Muziki wetu ukazikwa.

Leo tumehamia kwenye Amapiano tena. Muda sio mrefu tutahamia kwengine.

Kinachotokea tunashindwa kuliteka soko la Africa kwasababu hatufanyi kilichochetu. Niwahahakikishie hata tuwe na msanii mzuri kiasi gani akiimba Amapiano hawezi kumpiku Msanii wa SA. The reason is simple... Ukifanya unachokijua utatumia nguvu kidogo.

- Tukuze Singeli...tuwafanye Wasouth Africa na Wanigeria waimbe Singeli. Leo tunayasaidia mataifa mengi kutangaza Miziki yao. Wacongo wamestick kwenye Miziki wao na kimataifa wanafanya vizuri saana.

Diamond akiimba na Koffi wimbo wenye mahadhi ya Kikongo na wimbo ukawa mkubwa credits nyingi haziendi kwa Diamond na Tanzania, zinaenda Congo.
 
Ila we jamaa sa mbona hueleweki kama sigara kali?

Kule si umesema dunia imebadilika yaliyokua yanafanyika zamani na kupendwa saizi hayana nafasi kwenye mziki wa sasa na ukapendekeza kina nikki mbishi waimbe soft music ili kuendana na mfumo?

Sasa huoni hata hao unao waona wanaimba amapiano wanafanya hivyo kwa ajili ya biashara?
 
Wasanii wa bongo wengi wao ni felia..hata 4m4 wachache wamefika..hawatumii elimu wanatumia hisia na ujinga wao ndio man nyimbo zao nyingi zimejaa matusi na mipasho..wengi vilaza na wote wana kadi za ccm mfukoni..usitegemee jambo la maana kutoka kwao wanalaana ya ccm..ndio mana hawana ubunifu binafsi wanaigaiga tu kila linalokuja.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila we jamaa sa mbona hueleweki kama sigara kali?

Kule si umesema dunia imebadilika yaliyokua yanafanyika zamani na kupendwa saizi hayana nafasi kwenye mziki wa sasa na ukapendekeza kina nikki mbishi waimbe soft music ili kuendana na mfumo?

Sasa huoni hata hao unao waona wanaimba amapiano wanafanya hivyo kwa ajili ya biashara?
Hukunielewa...

Nitakupa mfano mdogo uweze kunielewa.

Leo South Africa Kwaito na Bacardi hazina soko na hakuna wanaoimba hata Dj Cleo mwenyewe kabadilika na soko.

Wote wamekimbilia Amapiano. Amapiano ni mtoto wa Bacardi na Kwaito. Hopefully baada ya muda Amapiano atazaa.

Umeeelewa?
 
Nashindwa kujua kama nimeelewa au sijaelewa probably kwasababu siko familiar na hiyo miziki

Ila nacho kiona ni kama unataka kujenga hoja kua watu wastick kwenye mziki fulani ambao kama ni wa asili pasipo kukimbilia miziki inayofanywa na mataifa mengine ambayo ni kama asili yao

Mpaka hapo nimekuelewa?
 
Exactly.... Kisha baada ya kustick kwenye chako unauwanja mpana wa kuzalisha genre nzuri zaidi.
 
Sisapoti amapiano sisapoti singeli,hivi kwa singeli mnaonaje kuwa ni mziki wenye mpangilio si bora mchiriku at least naweza elewa!.. tuboreshe bongo fleva yetu wasanii wawe wabunifu nachojua kuhusu mziki sio aina fulani bali ni ubunifu tu unaweza chukua radha za miaka ya 80 huko ukaziboresha na ngoma ikawa bingo!. Mfano Bruno Mars miziki yake inaradha ya zamani lakini ni Moto ati..

Warudi kuboresha radha ya bongo fleva
 
Siku maproducer wakianza kuheshimiwa na kupata stahiki zao may tunaweza pata watu creative bongo maproducer wananyanyaswa.

Bongo kupata tone yetu tunaweza mfano nyimbo ya Harmonize-Mtaje, ile biti ni pure from Tanzania na nyimbo ni nzuri.

Bongo wasanii wakubwa wana amini wao ndio wanawabeba maproducer refer kwa Nahreel,Aby Dady ,Harmy B,Man Walter nk, ndio maana maproducer wengi wazuri na wale wenye high creativity wanafanya mambo yao mengine sababu wanaona mziki hauwalipi.
 
Unadhani ni namna gani watengenezaji wa muziki wanaweza kupewa stahiki zao?
 
Sisapoti amapiano sisapoti singeli,hivi kwa singeli mnaonaje kuwa ni mziki wenye mpangilio si bora mchiriku at least naweza elewa!.. tuboreshe bongo fleva yetu wasanii wawe wabunifu nachojua kuhusu mziki sio aina fulani bali ni ubunifu tu unaweza chukua radha za miaka ya 80 huko ukaziboresha na ngoma ikawa bingo!. Mfano Bruno Mars miziki yake inaradha ya zamani lakini ni Moto ati..

Warudi kuboresha radha ya bongo fleva
View attachment 2055917
Singeli ni Muziki mkubwa saana usiuchukulie kawaida.

Kwanini Singeli? Muziki huanzia mtaani.
 
Unadhani ni namna gani watengenezaji wa muziki wanaweza kupewa stahiki zao?
Hapo sasa serikali yetu inabidi itilie mkazo ila hawa wasanii mpaka sasa sizani kama wanajua nini umuhimu wa producers.

Majani, Master Jay,Bizman, Lamar, Henriko, Duke Touch nk hawa sio hawapeni mziki ila hawaioni thamani yao kwenye mziki ndio maana wameamua kupiga mishe nyingine ili wapige hela.
 
Ila singeli mkuu hapana aisee, ni mziki ambao ni wa kuruka ruka tu hauna tone ya taratibu kwa wale wapenda nyimbo za taratibu.

Sidhani kama singeli ni chaguo sahihi, mbna bongo fleva ya kipindi kile ilikua gud sana. Kuna mdau hapo kataja wimbo wa mtaje wa harmonize lakini pia hata nyimbo nyingi za mondi pia na huyo harmo zile za zamani ile ni bongo fleva mkuu na ndizo zilizowapaisha.

Bongo fleva inajumuisha vyote vyote ukitaka ngoma za taratibu zipo, kuruka ruka utazipata japo nayo ina umagharibi kwa mbali lakini walau kuliko singeli aisee.
 
Na ndio maana alikiba Ana Baki kua ndo msaniii pekeee anaeweza kubeba catalog ya bongo flava kwa Sasa na kuibakisha kwenye mstari. Hapa siongelei ushabiki but fact.

Angalia tunzi zake za nyimbo na chaguzi za beats plus lyrics zinazo eleweka pasii na matusi . Utagundua n mtu ane elewa mziki mzuri.

Lakini ndo msaniii pekeee ambae tunaona haha yumbishwa na trending Ila kasimamia misingi anayo iamini tangu ana anza muziki mpaka Sasa.
Ahsante
 
HIVI TOKA LINI MZIKI WA SEHEMU FULANI YA NCHI UKAWA MZIKI TAMBULISHI WA NCHI HUSIKA??
SINGELI NI MUZIKI WA WAHUNI WA PWANI SIO MUZIKI TAMBULISHA TANZANIA
 
HIVI TOKA LINI MZIKI WA SEHEMU FULANI YA NCHI UKAWA MZIKI TAMBULISHI WA NCHI HUSIKA??
SINGELI NI MUZIKI WA WAHUNI WA PWANI SIO MUZIKI TAMBULISHA TANZANIA
Kila muziki una sehemu ulipoanzia lakini. Hata hiphop kuna sehemu ulianzia.
 
Back
Top Bottom