jukwaa hili wadau wake ni wa 'ajabu' sana

poposindege

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
456
Reaction score
175
Kwa wa muda mrefu sana nimekuwa nikisoma sana taarifa mbalimbali za mtandao huu wa Jamiiforums,
kabla ya kuamua kujiunga baadae sana.Pamoja na kushiriki katika majukwaa tofauti humu JF,lakini ajabu kubwa niliyoiona
ni ktk Jukwaa hili la Tech,Gadgets & Science.Ajabu si jukwaa lenyewe bali wadau wake.Kwangu mimi nimewaona ni watu wa ajabu sana.
Kwani hima yao ni kutaka kuona wengine wanajua kile wanachokijua wao.Wapo tayari kutumia muda wao kutoa msaada kwa yule mwenye kuhitaji.Ni wepesi wa kusaidia pamoja na kuelekeza.
Kwangu mimi ndo jukwaa pekee Lililofanikiwa ktk malengo yake zaidi kuliko majukwaa mengine ambapo kumejaa vijembe,uzushi kashfa na kubezana.
Binafsi nakiri nimefaidika sana kupitia jukwaa hili,kwa kusoma thread zilizowekwa na wadau mbalimbali,au kwa kuuliza.
Ilikuwa niandike kwa kirefu sana,lakini nahofu kuwachosha kwani jukwaa hili si la story ni la kitaalamu zaidi,ila nasema hivi
kwamba wadau wa jukwaa hili ni wa ajabu sana,na ajabu yao ni kupenda wengine wajue wanachokijua wao.
Ahsanteni sana nimetoa dukuduku langu
 
Mkuu teknolojia haina siasa ndio maana huku unaona stori ni chache. Pia kwenye teknolojia huwezi ukajua kila kitu ndio maana humu ndani watu wanakuwa wepesi kusaidiana kwani kupitia kusaidiana huko kila mmoja anafaidika kujua mojawapo ya vitu alivyokuwa havijui. Pia mara zote wataalamu wanafanya kazi kitimu, hivyo jukwaa hili ni moja ya timu ya wataalamu.
 
Asante sana kwa pongezi zako..

Kifupi JF yote ni nzuri na majukwaa ambayo wachangiaji wake wako tayari ku-share info bila utata ni pamoja na hili na la UJASIRIAMALI...Ila kama unataka kupasuka kichwa nenda kule kwenye JUKWAA LA SIASA
 
hili jukwaa ni babu kuuubwa,hata simu ninayotumia sasa,nisingeijua kama sio jf.huku unapata matecno ya kufa mtu.jukwaa safi sana hili
 
Mwanzo lilikuwa na sifa hizo ulizotoa..lakini hivi karibuni limeingiliwa sana na watoto kama sio watu wazima wenye akili za kitoto.Na hapa,ndipo kwa mtazamo wangu,moderators wanapotakiwa kudhibiti mchakato wa uendeshashaji wa jukwaa hili.Wanatakiwa kuwadhibiti waharibifu hawa bila kujali kama wanapunguza wajumbe;maana huwezi kusema JF inakua wakati wajumbe wengine wanaingia kwa ajili ya kuleta mazaha na masikhara tu na kuharibu dhima nzima ya JF.

Juzi kuna bwana mdogo mmoja hivi aliweka post hapa,watu walipoanza kukosoa akaamua kutoa matusi na kusema alikuwa anajaribu kuweka tu kwa ajili ya kujifurahisha na kwa hiyo hakuhitaji watu kuchangia chochote.Hilo jambo moderators waliliona lakini waliruhusu malumbano yaendelee tu.Sasa hili kwa,mtazamo wangu,ni sawa na kulea uovu ambao matokeo yake,jukwaa hili litageuka kuwa kijiwe cha kupiga soga.

Upo ushahidi wa kutosha kwamba kuna wadau mashuhuri humu ambao mwanzo walikuwa mstari wa mbele kabisa ktk kuisaidia jamii,na wengi wetu tumenufaika sana,lakini siku hizi wanapita tu kimya kimya na wakati mwingine wanaingia kama guests tu. Hii imetokana na kuongezeka humu wajumbe wengi wenye mizaha na kejeli;hali iliyopelekea kuvunjika moyo kwa hawa wadau wetu waliokuwa wakitusaidia.

Kwa wazoefu,siku hizi ukiwa na tatizo unafanya kupm watalamu unaowafahamu backstage,wanakusaidia.Lakini je kwa junior members wasiowafahamu hawa watalamu,inakuwaje?Kimsingi hapo mwanzo suluhu ya matatizo yetu ilikuwa inapatikana wazi kwa faida hata ya watu wengine,na hili ndilo lilikuwa hasa lengo la jukwaa hili.Vitu vingi vilikuwa vikijadiliwa na watalamu waliobobea katika maswala hayo,hadi mtu unasema haswaa,hii ndio Jamii Forums bwana!

Kwa hiyo basi,kwa mtazamo wangu,kama jukwaa hili litafikia hatua ya kuwa kijiwe tu cha kupiga soga na porojo,kwanza mimi lawama nitazipeleka kwa moderators kisha ndio watu wengine.Siku zote mizaha mizaha hutumbuka usaha!

Jukwaa lingine lililoingiliwa ni jukwaa la JF Doctor.Siku hizi kila mtu ni mtalaamu wa tiba.Na wakati mwingine mtu anaweza kuleta shida yake pale,lakini ukakuta page nzima hata zaidi ya moja ni mizaha,kupiga stories na kumention IDs za wenzao.Mwisho wa siku mleta mada anakata tamaa na kubakia na tatizo lake.Watu wamesahau kuwa si kila tatizo mtu ataenda hospitali;kuna matatizo mengine tiba yake ni ushauri tu.

Na hapo bado sijataja Jukwaa la Elimu na mambo ya akina mpigamsuli na wenzake.

Anyway,lakini hiyo ndiyo jamii tuliyonayo siku hizi.
 
ni kweli ulichosema,ma mods inabidi wawe makini na hawa wanaoleta mizaha na kutaka kuharibu lengo la jukwaa.Huyo alieweka post ya kipuuzi na kudai ameweka ili kujifurahisha mwenyewe,niliiona na kwa kweli sikuipenda.Watu kama hao inabidi wapigwe ban
Mwanzo lilikuwa na sifa hizo ulizotoa..lakini hivi karibuni limeingiliwa sana na watoto kama sio watu wazima wenye akili za kitoto.Na hapa,ndipo kwa mtazamo wangu,moderators wanapotakiwa kudhibiti mchakato wa uendeshashaji wa jukwaa hili.Wanatakiwa kuwadhibiti waharibifu hawa bila kujali kama wanapunguza wajumbe;maana huwezi kusema JF inakua wakati wajumbe wengine wanaingia kwa ajili ya kuleta mazaha na masikhara tu na kuharibu dhima nzima ya JF.

Juzi kuna bwana mdogo mmoja hivi aliweka post hapa,watu walipoanza kukosoa akaamua kutoa matusi na kusema alikuwa anajaribu kuweka tu kwa ajili ya kujifurahisha na kwa hiyo hakuhitaji watu kuchangia chochote.Hilo jambo moderators waliliona lakini waliruhusu malumbano yaendelee tu.Sasa hili kwa,mtazamo wangu,ni sawa na kulea uovu ambao matokeo yake,jukwaa hili litageuka kuwa kijiwe cha kupiga soga.

Upo ushahidi wa kutosha kwamba kuna wadau mashuhuri humu ambao mwanzo walikuwa mstari wa mbele kabisa ktk kuisaidia jamii,na wengi wetu tumenufaika sana,lakini siku hizi wanapita tu kimya kimya na wakati mwingine wanaingia kama guests tu. Hii imetokana na kuongezeka humu wajumbe wengi wenye mizaha na kejeli;hali iliyopelekea kuvunjika moyo kwa hawa wadau wetu waliokuwa wakitusaidia.

Kwa wazoefu,siku hizi ukiwa na tatizo unafanya kupm watalamu unaowafahamu backstage,wanakusaidia.Lakini je kwa junior members wasiowafahamu hawa watalamu,inakuwaje?Kimsingi hapo mwanzo suluhu ya matatizo yetu ilikuwa inapatikana wazi kwa faida hata ya watu wengine,na hili ndilo lilikuwa hasa lengo la jukwaa hili.Vitu vingi vilikuwa vikijadiliwa na watalamu waliobobea katika maswala hayo,hadi mtu unasema haswaa,hii ndio Jamii Forums bwana!

Kwa hiyo basi,kwa mtazamo wangu,kama jukwaa hili litafikia hatua ya kuwa kijiwe tu cha kupiga soga na porojo,kwanza mimi lawama nitazipeleka kwa moderators kisha ndio watu wengine.Siku zote mizaha mizaha hutumbuka usaha!

Jukwaa lingine lililoingiliwa ni jukwaa la JF Doctor.Siku hizi kila mtu ni mtalaamu wa tiba.Na wakati mwingine mtu anaweza kuleta shida yake pale,lakini ukakuta page nzima hata zaidi ya moja ni mizaha,kupiga stories na kumention IDs za wenzao.Mwisho wa siku mleta mada anakata tamaa na kubakia na tatizo lake.Watu wamesahau kuwa si kila tatizo mtu ataenda hospitali;kuna matatizo mengine tiba yake ni ushauri tu.

Na hapo bado sijataja Jukwaa la Elimu na mambo ya akina mpigamsuli na wenzake.

Anyway,lakini hiyo ndiyo jamii tuliyonayo siku hizi.
 
Mr. Mrimi ile siledi ya matusi ishaondolewa leo sijaiona ila ilinichekesha sana jamaa alipoanza kuwanyau watu
 
nina majukwaa mawili tu hata nitingwe vipi lazima niingie; siasa na hili basi.!!
 
That is the original "hacker" culture, before the term took a negative connotation.
 
Back
Top Bottom