<br />Njoo siku moja moja mkuu.
Kwa wa muda mrefu sana nimekuwa nikisoma sana taarifa mbalimbali za mtandao huu wa Jamiiforums,
kabla ya kuamua kujiunga baadae sana.Pamoja na kushiriki katika majukwaa tofauti humu JF,lakini ajabu kubwa niliyoiona
ni ktk Jukwaa hili la Tech,Gadgets & Science.Ajabu si jukwaa lenyewe bali wadau wake.Kwangu mimi nimewaona ni watu wa ajabu sana.
Kwani hima yao ni kutaka kuona wengine wanajua kile wanachokijua wao.Wapo tayari kutumia muda wao kutoa msaada kwa yule mwenye kuhitaji.Ni wepesi wa kusaidia pamoja na kuelekeza.
Kwangu mimi ndo jukwaa pekee Lililofanikiwa ktk malengo yake zaidi kuliko majukwaa mengine ambapo kumejaa vijembe,uzushi kashfa na kubezana.
Binafsi nakiri nimefaidika sana kupitia jukwaa hili,kwa kusoma thread zilizowekwa na wadau mbalimbali,au kwa kuuliza.
Ilikuwa niandike kwa kirefu sana,lakini nahofu kuwachosha kwani jukwaa hili si la story ni la kitaalamu zaidi,ila nasema hivi
kwamba wadau wa jukwaa hili ni wa ajabu sana,na ajabu yao ni kupenda wengine wajue wanachokijua wao.
Ahsanteni sana nimetoa dukuduku langu
Kiongozi, nafurahi sana umetoa dukuduku lako kama ulivyohitimisha kwa kusema hivyo!!......lakini kulaumu majukwaa engine kuwa members wake si wa ajabu sana km wale wa tech ni kutofanya check and balance!!!!
Hebu tazama kwa mfano jukwaa la MMU, watu wanaomba ushauri na wanapewa ushauri kulingana na "LOGIC AND REASONING" maana yake ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja kwenye lile jukwaa, tofauti na jukwaa la tech ambalo lina jibu la moja kwa moja kwa tatizo na tech!!!!
Kwa kifupi majukwaa mengi yana majibu ya ''TRIAL AND ERRORS" tofauti na jukwaa la tech ambalo lina majibu ya kisayansi zaidi.......yaani nafananisha na mtu akuulize 1+1=2 hivi ndivyo jukwaa la tech linavyofanya kazi, lina scientific/technological answers!!!!!!!
Anachotaka kusema mdau wa hii mada ni kwamba majukwaa mengine hata kama mtu hajui kuhusu jambo atalopoka tu kama sio kwa kukubeza au kukupa ushauli ambao hata yeye hajawai kuutekeleza na kuona ukifanya kazi....alaf nadhan jf kuna under 18 humu baadhi ya majukwaa maana mambo wanayoyasema na kukushauli ni umburura tu...alaf kitu kingine unavyotembelea majukwaa ndo utajua ni mambo gani hasa wewe upo interestd in..mfano mimi siwezi kuingia kwenye siasa hata siku moja cz haipo moyoni lakini humu,na biashara, ndo kwangu...na kwenye buzness kuna watu wanamaoni mazuri ya buzness na projects ambazo walishawai kuzifanya,Kiongozi, nafurahi sana umetoa dukuduku lako kama ulivyohitimisha kwa kusema hivyo!!......lakini kulaumu majukwaa engine kuwa members wake si wa ajabu sana km wale wa tech ni kutofanya check and balance!!!!Hebu tazama kwa mfano jukwaa la MMU, watu wanaomba ushauri na wanapewa ushauri kulingana na "LOGIC AND REASONING" maana yake ni kwamba hakuna jibu la moja kwa moja kwenye lile jukwaa, tofauti na jukwaa la tech ambalo lina jibu la moja kwa moja kwa tatizo na tech!!!!Kwa kifupi majukwaa mengi yana majibu ya ''TRIAL AND ERRORS" tofauti na jukwaa la tech ambalo lina majibu ya kisayansi zaidi.......yaani nafananisha na mtu akuulize 1+1=2 hivi ndivyo jukwaa la tech linavyofanya kazi, lina scientific/technological answers!!!!!!!
Ukitaka kuwa na amani jukwaa hilo, wewe sifia CDM tu.
Aisee!Si ajabu jukwaa hili ni la ccm, na machadema watapiga kelele kama kawaida yao....
Vipo wapi hivyo vichwa mkuu mbona mie nimeshindwa kupewa ushauri wa namna ya kuhamisha contacts toka iphone 3GS kwenda samsung galaxy note? Au hakuna hiyo technology? BTW nakubali kuwa hili sio jukwaa la longolongo.Humu mna vichwa si mchezo.
Vipo wapi hivyo vichwa mkuu mbona mie nimeshindwa kupewa ushauri wa namna ya kuhamisha contacts toka iphone 3GS kwenda samsung galaxy note? Au hakuna hiyo technology? BTW nakubali kuwa hili sio jukwaa la longolongo.
Sawa Mkuu naendelea kuvumilia. Thanx japo kwa ushauriKumbuka ni volunteers wanaotoa muda wao wa ziada bure...uwe mvumilivu!
asante sana kwa pongezi zako..
Kifupi jf yote ni nzuri na majukwaa ambayo wachangiaji wake wako tayari ku-share info bila utata ni pamoja na hili na la ujasiriamali...ila kama unataka kupasuka kichwa nenda kule kwenye jukwaa la siasa
Sikiliza hommie,kwanza hata mimi nilijiunga kwa ile mkumbo tu kutaka kuwemo jukwaani,lakini kadri nilivyokuwa nalipitia jukwaa hili nilijikuta najifunza vitu nvingi mno ambapo baadae hata kule kuibiwa kibwegebwege na wataalamu au mafundi uchwara ikawa mwisho.Vitu vilivyomo humu ni zaidi ya shule,we jitahidi kuwepo humu na jipe muda halafu jipime baada ya mwaka mmoja utajikuta umepata elimu kubwa mno na uelewa zaidi kuhusu electronics.This is like my home sasa hivi. a free pot of valuable knowlegde.Mungu ibariki JF,Mungu ibariki Ed,Gadgets n Science forum.
Mrimi,,well said brother umemaliza kila kituMwanzo lilikuwa na sifa hizo ulizotoa..lakini hivi karibuni limeingiliwa sana na watoto kama sio watu wazima wenye akili za kitoto.Na hapa,ndipo kwa mtazamo wangu,moderators wanapotakiwa kudhibiti mchakato wa uendeshashaji wa jukwaa hili.Wanatakiwa kuwadhibiti waharibifu hawa bila kujali kama wanapunguza wajumbe;maana huwezi kusema JF inakua wakati wajumbe wengine wanaingia kwa ajili ya kuleta mazaha na masikhara tu na kuharibu dhima nzima ya JF.
Juzi kuna bwana mdogo mmoja hivi aliweka post hapa,watu walipoanza kukosoa akaamua kutoa matusi na kusema alikuwa anajaribu kuweka tu kwa ajili ya kujifurahisha na kwa hiyo hakuhitaji watu kuchangia chochote.Hilo jambo moderators waliliona lakini waliruhusu malumbano yaendelee tu.Sasa hili kwa,mtazamo wangu,ni sawa na kulea uovu ambao matokeo yake,jukwaa hili litageuka kuwa kijiwe cha kupiga soga.
Upo ushahidi wa kutosha kwamba kuna wadau mashuhuri humu ambao mwanzo walikuwa mstari wa mbele kabisa ktk kuisaidia jamii,na wengi wetu tumenufaika sana,lakini siku hizi wanapita tu kimya kimya na wakati mwingine wanaingia kama guests tu. Hii imetokana na kuongezeka humu wajumbe wengi wenye mizaha na kejeli;hali iliyopelekea kuvunjika moyo kwa hawa wadau wetu waliokuwa wakitusaidia.
Kwa wazoefu,siku hizi ukiwa na tatizo unafanya kupm watalamu unaowafahamu backstage,wanakusaidia.Lakini je kwa junior members wasiowafahamu hawa watalamu,inakuwaje?Kimsingi hapo mwanzo suluhu ya matatizo yetu ilikuwa inapatikana wazi kwa faida hata ya watu wengine,na hili ndilo lilikuwa hasa lengo la jukwaa hili.Vitu vingi vilikuwa vikijadiliwa na watalamu waliobobea katika maswala hayo,hadi mtu unasema haswaa,hii ndio Jamii Forums bwana!
Kwa hiyo basi,kwa mtazamo wangu,kama jukwaa hili litafikia hatua ya kuwa kijiwe tu cha kupiga soga na porojo,kwanza mimi lawama nitazipeleka kwa moderators kisha ndio watu wengine.Siku zote mizaha mizaha hutumbuka usaha!
Jukwaa lingine lililoingiliwa ni jukwaa la JF Doctor.Siku hizi kila mtu ni mtalaamu wa tiba.Na wakati mwingine mtu anaweza kuleta shida yake pale,lakini ukakuta page nzima hata zaidi ya moja ni mizaha,kupiga stories na kumention IDs za wenzao.Mwisho wa siku mleta mada anakata tamaa na kubakia na tatizo lake.Watu wamesahau kuwa si kila tatizo mtu ataenda hospitali;kuna matatizo mengine tiba yake ni ushauri tu.
Na hapo bado sijataja Jukwaa la Elimu na mambo ya akina mpigamsuli na wenzake.
Anyway,lakini hiyo ndiyo jamii tuliyonayo siku hizi.