Jukumu la vyombo vya habari kwenye kuripoti afya ya uzazi na haki

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
1610962992237.png

Vyombo vya habari mbali na kuakisi yanayotokea kwenye jamii. Pia inapaswa kuwa mshiriki mkuu wa shughuli za maendeleo katika jamii, kutengeneza mitazamo ya watu na kufanya ulaghabishi kwenye maswala ya Afya ya uzazi na Haki.

Vyombo vya habari vina jukumu la kuripoti maswala ya Afya ya uzazi na haki na katika kufanikisha hilo wanahabari hawana budi kuzingatia yafuatayo:-

Kuwa na maarifa ya kutosha kuhusu maswala ya Afya ya uzazi na Haki.

Kuhamasisha mijadala ya umma kuhusu maswala ya Afya ya uzazi na Haki.

Kuvunja utamaduni wa ukimya kwenye maswala ya unyanyapaa, unyanyasaji na dhana zinazozunguka swala la Afya ya uzazi na Haki.

Kuihamasisha serikali kwenye jitihada za kusimamia malengo ya maendeleo endelevu yahusuyo Afya ya uzazi na Haki.

Kuheshimu faragha za watu, kwakua Afya ya uzazi ni mambo ya siri.

Kutotumia maneno ya taaluma ya Afya ambayo yatafanya hadhira yako isielewe , ikiwa utayatumia ni vyema kuyaelezea kwa undani.

Usitoe mchango kwenye maswala yanayowakandamiza wanawake.
 
waandishi wengi wa vyombo vya habari wamekariri bahasha za kaki kwanza ndiyo habari ipate nafasi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom