Jukata kufufua madai katiba mpya Tanzania

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata) limesema mwaka 2020 litafufua mchakato wa kudai Katiba Mpya.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Februari Mosi 2020 na mkurugenzi mtendaji wa jukwaa hilo, Bob Wangwe katika mafunzo maalum ya asasi za kiraia kuhusu namna zinavyoweza kulinda haki zao za kikatiba.

Mchakato wa Katiba Mpya ulizinduliwa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete mwishoni mwa mwaka 2011 alipounda Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Hata hivyo, mchakato huo uliishia kwenye Bunge Maalumu la Katiba ambalo licha ya kupitisha Katiba Inayopendekezwa ambayo haijapigiwa kura ya maoni hadi leo, baadhi ya vyama vya upinzani vilijitoa na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).

Katika maelezo yake leo, Wangwe amesema katika mpango mkakati wao mwaka 2019 hadi 2025 jambo la kwanza ni kuanza kupigania katiba mpya, wanaanza mwaka 2020.

Amesema katiba ya sasa ya Tanzania haiheshimiwi, akisisitiza kuwa hilo halifanyiki makusudi, linatokana na udhaifu wa katiba hiyo aliyodai imetoa mamlaka makubwa kwa wenye madaraka.

“Jukata tunahuisha mjadala wa katiba na Februari, 2020 tutaleta wataalam wa masuala ya katiba wakiwemo kutoka nje ya nchi ili kuongeza nguvu kudai katiba,” amesema Wangwe.

Kuhusu mafunzo hayo amesema, “kama Asasi zenyewe hazijui haki zao za kikatiba ni wazi hazitaweza kupigania haki hizo kwa wananchi wengine . Mafunzo haya ni muhimu kwao hasa kwa wakati huu ambao mambo mengi yanayofanyika ni kinyume na katiba.”

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom