Juhudi za kutaka kumnyamazisha Askofu Mwamakula na Kanisa analoliongoza. hazitafanikiwa!

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula ni Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na pia ndiye Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches - WFMRC) ambapo alichaguliwa katika nafasi hii mnamo Februari 2018 katika Mkutano wa Dunia uliofanyika Nairobi, Kenya. Makanisa yanayounda WFMRC yapo katika nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan Kusini, Ufilipino, Alaska (USA), Honduras, Cambodia, Cuba, Suriname, USA Continental nk.

Shughuli za Mwamakula kama Askofu Mkuu wa Kanisa hili zimekuwa zikifanyika wazi pasipo kificho ikiwemo kubariki na kuwaweka wakfu Wachungaji katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda; kumuweka wakfu Askofu wa Kenya mjini Ruiru (Novemba 2017); kumuweka wakfu Askofu wa Alebtong, Uganda (Januari 2018); kumuweka wakfu Askofu wa Lira, Uganda (Novemba 2018); kumuweka wakfu Askofu Msaidizi wa Tanzania mjini Lira Uganda (Novemba 2018); na kumuweka wakfu Askofu wa Morogoro, Tanzania (Agosti 2019). Aidha, Ibada ya kumsimika Askofu Mkuu wa Sudan Kusini ambayo ilikuwa iongozwe na Askofu Mkuu Mwamakula mwaka huu ziliahirishwa kwa sababu ya ugonjwa wa Covid 19.

Siku ya Jumatatu, tarehe 10 Agosti 2020, baadhi ya Maaskofu wa Kanisa la Moravian Tanzania (KMT), wakiongozwa na Askofu Alinikisa Cheyo pamoja na Askofu mmoja mstaafu, wamejitokeza kupitia baadhi ya vyombo vya Habari nchini Tanzania wakitoa kauli ambazo zinaelekea kumshambulia na kumlenga moja kwa moja Askofu Mwamakula pamoja na Kanisa analoliongoza! Ifahimike kuwa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania linayo mifumo yake ya uendeshaji inayojitegemea ikiwemo Katiba, Liturgia, Kitabu cha Nyimbo na taratibu mbalimbali zilizokubaliwa na Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches - WFMRC)!

Inashangaza kuona Maaskofu hao kupitia msemaji wao wanajipa uhalali wa kujimilikisha neno Moravian! Ikumbukwe kuwa hapa Tanzania kuna madhehebu matatu ya Kimoravian nayo ni 1. Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania (KMUT); 2. Kanisa la Kiinjili la Moravian Tanzania (KKMT); na Majimbo yanayounda Kanisa la Moravian Tanzania (KMT) ambapo kila Kanisa linayo Katiba yake na mfumo wake wa Uongozi!

Inashangaza kuona Maaskofu hao wa KMT wanajipa cheo cha 'Baba wa Nyumba au Ukoo' hata kwa watu wasiowahusu na kujifanya kama wao ndio wasemaji wa Wamoraviani wote nchini Tanzania jambo ambalo siyo kweli. Ni heri wangelijikita katika kumaliza changamoto na migogoro yao kuliko kuanza kupambana na watu ambao hawapambani nao!

Inasikitisha sana na pia inashangaza zaidi kuona vyombo cha Habari kuacha weredi wao katika kuchakata habari na taarifa na kuamua kutoa taarifa za upande mmoja pasipo kujiridhisha na upande wa pili. Maadili ya Uandishi wa Habari na Vyombo vya Habari duniani kote yanatakataza wahusika kusikiliza upande mmoja na kutoa taarifa kwa kutegemea huo uliosikilizwa pasipo kujiridhisha au kuhoji ku - 'balance story' na upande wa pili.

Maaskofu hao wametoa siri kupitia tamko lao hilo jinsi gani walivyojitahidi kutaka kulinyamazisha Kanisa letu ikiwemo hata kuandika barua katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi! Walikuwa wanatumia 'watu wao' ili kuishikiza Wizara ilipige 'stop' Kanisa letu! Hii ni aibu kubwa sana kwa viongozi wa Kanisa kutamka mambo kama hayo hadharani! Kwa uelewa wao wanashindwa kuelewa kuwa hakuna binadamu aliyewahi kulinyamazisha Kanisa na watumishi wake wakafanikiwa!

Huko nyuma, nimeandika mara kadhaa kuhusu matukio mbalimbali ya kutaka kumnyamazisha Askofu Mwamakula yanayofanywa na watu wenye nguvu!

Sisi tunaamini kuwa kuna nguvu kubwa iliyo nyuma ya Maaskofu hao waliotumia vyombo vya Habari ili kumshambulia Askofu Mwamakula na Kanisa analoliongoza. Hii ndio sababu hata vyombo vya Habari colic to to a malalamiko yao havikutaka hata kuchukua jitihada za kutafuta viongozi wa Kanisa letu ili kujiridhisha au ku-'balance' taarifa au habari yao kama maadili ya vyombo vya Habari yanavyotaka! Tunasubiri kuona kama vyombo hivyo vitawajibishwa na mamlaka husika!

Maaskofu hao wanamtuhumu Askofu Mwamakula na Kanisa lake kuwa 'wanapigia kampeni' baadhi ya vyama vya siasa, jambo ambalo siyo kweli. Askofu kama Kiongozi wa Dini alialikwa kwa nafasi yake na alitoa Sala kama Askofu. Maaskofu hao na wao wameonekana katika mikutano kadhaa ya kisiasa na kiserikali wakitoa Sala na kukaa katika viti vya mbele. Inaonekana wameumia sana katika nafsi zao wanapoona kuwa mtu wasiyempenda na Kanisa wasilolipenda wakikaribishwa sehemu mbalimbali. Wanasahau kabisa kuwa Mungu anaweza pia kuwatumia wadhaifu katika kutimiza mapenzi yake yasiyoweza kuhojiwa na binadamu ye yote (1Wakorintho 1:26-31)!

Sisi tunahisi kuwa pamoja na wivu na chuki binafsi, nyuma ya Maaskofu hawa kunaaweza kuwepo nguvu kubwa sana inayolenga kutaka kumdhoofisha Askofu Mwamakula kutokana na msimamo wake wa kupataza sauti na kutetea haki katika jamii!

Sisi tunatambua kuwa kama huduma anayofanya Askofu Mwamakula ina kibari kutoka kwa Mungu na kama Kanisa analoliongoza lina kibari kutoka kwa Mungu basi hakuna atakayeweza kuwanyamazisha.

Pamoja na nguvu kubwa iliyoko nyuma yao, ikiwemo kuzitegemea mamlaka walizozitaja kuwa wamekuwa wakiziandikia barua, sisi hatutaweka mategemeo yetu kwa wanadamu ingawa tunajua kuwa Mungu anaweza pia kuwatumia watu walioko katika mamlaka hizo kuweza kutenda haki juu yetu!

Tunapenda kuwajulisha waumini wote wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki pamoja na wale wote wanaotupenda kuwa vita imekwishatangazwa hadharani dhidi ya Kanisa hili na Kiongozi wake. Hata hivyo, tunawaomba wawe watulivu kwa kuwa hii ni vita ya kiroho na haya yanayoonekana ni matokeo tu ya kinachoendelea katika ulimwengu wa roho. Tuwaache wao wategemee mamlaka na vyombo vya Habari lakini sisi tumtegemee Mungu kama Neno lake linavyosema: "Hawa wanataja magari na hawa wanataja farasi, Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu (Zaburi 20:7).

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula, Ep. - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki & Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani (World Fellowship of Moravian Revival Churches - WFMRC)
 
Kanisa la Moravian Tanzania ni moja tu KMT hayo mengine ni vikundi vya uasi ikiwemo hili la Mwamakula
 
.....ukiwa kiongozi wa dini alafu ukawaingilia wanasiasa timing zao lazima tu watakunasibisha na siasa zao. Acha avune anachopanda. Mungu si mjinga asiyejua mnafiki na mtu mwema.
 
Hii roho ya unafiki ndani ya kanisa ni ya kale sana tuliiona kwa akina Anasi na Kayafa wakila njama na watawala namna watakavyomuuza Yesu kwao na kanisa lake.
Wakuu wa dini waliyo na roho ya uuaji kwa kuwa hawana mamlaka ya kumhukumu mtu kifo cha mwili hukimbilia kwa wenye mamlaka ili wahukumu kwa niaba yao.
Ukitaka kuona huyu nyoka wa kale ibilisi na sheitwan anatoka ndani ya pango lake wewe simamia haki na kweli.
Mwamakula japo sikufahamu kwa undani ila kwa kile ninachokufahamu kwacho ni kusimamia haki ya wasio na sauti hadharani bila woga.
Kwa hili nakuunga mkono na kanuni ya wenye haki dhidi ya madhulumati iko hivi,
Adui atakuja katika njia moja lakini Mungu atamtawanya katika njia saba. Na wavu walioutega sirini utawanasa wao wenyewe.
Shimo hili wanalolichimba watatumbukia wenyewe!!
 
Back
Top Bottom