Hahahahhahah Afro kumbe ulienda kanisani mwaka 2000? lakini si unajua siku ukitembea uchi unakutana na wakwe zako
Una mpango wa kwenda kokote katikati ya mwaka huu? Mie nilikuwa na mpango, na bado ninao, wa kwenda kushangaa wanyama huko mbuga ya Mikumi. Pia nina mpango wa kufanya marekebisho madogomadogo katika nyumba ninayoishi kwa sababu mwenye nyumba wangu kagoma kunikarabatia. Pia nina mpango wa kukutana na watu hapa kijijini na kujuzana hili na lile kama ilivyo ada kila siku.
Lakini ati pamoja na kuwa na mipango yote hii ambayo inasubiri utekelezaji jamaa wananambia ati tarehe 21 /05 /2011 dunia yetu inafika tamati, au kwa kiswahili rahisi ni kwamba tarehe hiyo ndio 'mwisho wa dunia', namaanisha ' Kiama'.
Waliokuja na habari hizi ni jamaa fulani huko Carlifornia, Marekani, ambao wanasemekana kutumia fursa hiyo kujiongezea umaarufu kwa kutafuta air time kwenye vyombo vya habari.
Jamaa hawa waliokuja na habari hizi za 'mwisho wa dunia' ni wafuasi wa dini ya Kikristo wenye msimamo mkali wanaoongozwa na mtangazaji wa radio, Harold Camping, anayetangaza katika radio ya Family Radio Network.
Akitumia mistari ya Biblia, jamaa huyu amesema kwamba dunia itafika tamati miaka 7 ,000 kutokea mafuriko makubwa katika uso wa dunia, na kwa mujibu wa kalenda yake ni kwamba mwisho wa dunia yetu ni Mei 21.
Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa Harold kufanya utabiri kama huu kwani mwaka 1994 kutabiri kuwa mwaka huo dunia ilikuwa ikifikia tamati lakini cha kustaajabisha hadi leo bado yupo pamoja na wafuasi wake. Siku zote amekuwa na namna ya kujitetea utabiri wake unapokwenda kombo, " Kuna wakati Mungu anakuonesha mambo lakini hakuoneshi kwa ukamilifu wote.
Ni miaka mitatu iliyopita ndipo Mungu amenionesha ukweli wote." Lakini mara hii, Harold amekuwa akisisitiza kwamba yuko sahihi kabisa tofauti na mwaka 1994 , na mara hii emungwa mkono na watu wasiopungua 50 , akiwemo Gary Vollmer, mwajiriwa katika wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ambaye amechukua likizo ya bila malipo, likizo inayokwisha tarehe 23 Mei.
Gary amesema hategemei kurejea kwa mwajiri wake kwani tarehe 21 Mei atakuwa ' amekwishanyakuliwa'.
Enewei, nimefurahi kufahamiana na kila mmoja tuliyekutana na kubadilishana hili na lile hapa kijijini. Iwapo kweli tarehe 21 litatokea la kutokea tukutane upande wa pili. Chiazzzzz.
bora yesheeee kila kitu kinkuwa kigumu bwana.alaaa:A S 103:
Hakuna aijuaye siku wala saa hata malaika Math.24:36-38 Thes.5:2-3 2Pet.3:10 siku ya Bwana itakuja kama mwivi so sidanganyiki ng'o
Hakuna aijuaye siku wala saa hata malaika Math.24:36-38 Thes.5:2-3 2Pet.3:10 siku ya Bwana itakuja kama mwivi so sidanganyiki ng'o
waambie hao hata malaika mkuu hajui sembuse binadam.mimi siogopi wala nini?Hakuna mtu ajuaye siku wala saa....hata Mwana ila BABA peke yake....
Hakuna aijuaye siku wala saa hata malaika Math.24:36-38 Thes.5:2-3 2Pet.3:10 siku ya Bwana itakuja kama mwivi so sidanganyiki ng'o
Hakuna aijuaye siku wala saa hata malaika Math.24:36-38 Thes.5:2-3 2Pet.3:10 siku ya Bwana itakuja kama mwivi so sidanganyiki ng'o