Judgment Day: May 21, 2011 (Really?)

tena mmemuua osama bin ladeni? lazima iwe mwisho wa dunia kwa kweli...!!:A S 103:
 
hahah Afro kumbe ulienda kanisani mwaka 2000? lakini si unajua siku ukitembea uchi unakutana na wakwe zako
Hahahah
dahhhhh hakuna mwakAmpya mbaya kama ile sintosahau..mama yuko kule baba yuko wapi sijui ni wewe nawadogo zako mmekumbatiana mnasubiri kufa... dahhhhh
ndoo maana huu upuuzi siupi kipaumbele tena..
 
Hizi tetesi mbona zimeanza kushika kasi sana? Anyway 2subuli siku ifike tuone yupi mkweli.
 
Kama unajua neno la Mungu linasemaje, hakuna atakayekubabaisha, maana manabii wa uongo wamejaa tele tunawashuhudia na kila siku wanaongezeka, be ware friends! Na aliyetangaza habari hizo hapa Tz amesema kama unabii wake hautatimia afanywe kama manabii wengine wa walivyofanywa katika Biblia Takatifu, yaani kupigwa mawe hadi kufa!!!! Langu jicho na sikio :mod::mod::mod::mod::mod:
 
Una mpango wa kwenda kokote katikati ya mwaka huu? Mie nilikuwa na mpango, na bado ninao, wa kwenda kushangaa wanyama huko mbuga ya Mikumi. Pia nina mpango wa kufanya marekebisho madogomadogo katika nyumba ninayoishi kwa sababu mwenye nyumba wangu kagoma kunikarabatia. Pia nina mpango wa kukutana na watu hapa kijijini na kujuzana hili na lile kama ilivyo ada kila siku.

Lakini ati pamoja na kuwa na mipango yote hii ambayo inasubiri utekelezaji jamaa wananambia ati tarehe 21 /05 /2011 dunia yetu inafika tamati, au kwa kiswahili rahisi ni kwamba tarehe hiyo ndio 'mwisho wa dunia', namaanisha ' Kiama'.

Waliokuja na habari hizi ni jamaa fulani huko Carlifornia, Marekani, ambao wanasemekana kutumia fursa hiyo kujiongezea umaarufu kwa kutafuta air time kwenye vyombo vya habari.

Jamaa hawa waliokuja na habari hizi za 'mwisho wa dunia' ni wafuasi wa dini ya Kikristo wenye msimamo mkali wanaoongozwa na mtangazaji wa radio, Harold Camping, anayetangaza katika radio ya Family Radio Network.
Akitumia mistari ya Biblia, jamaa huyu amesema kwamba dunia itafika tamati miaka 7 ,000 kutokea mafuriko makubwa katika uso wa dunia, na kwa mujibu wa kalenda yake ni kwamba mwisho wa dunia yetu ni Mei 21.

Inasemekana hii si mara ya kwanza kwa Harold kufanya utabiri kama huu kwani mwaka 1994 kutabiri kuwa mwaka huo dunia ilikuwa ikifikia tamati lakini cha kustaajabisha hadi leo bado yupo pamoja na wafuasi wake. Siku zote amekuwa na namna ya kujitetea utabiri wake unapokwenda kombo, " Kuna wakati Mungu anakuonesha mambo lakini hakuoneshi kwa ukamilifu wote.

Ni miaka mitatu iliyopita ndipo Mungu amenionesha ukweli wote." Lakini mara hii, Harold amekuwa akisisitiza kwamba yuko sahihi kabisa tofauti na mwaka 1994 , na mara hii emungwa mkono na watu wasiopungua 50 , akiwemo Gary Vollmer, mwajiriwa katika wizara ya mambo ya ndani ya Marekani ambaye amechukua likizo ya bila malipo, likizo inayokwisha tarehe 23 Mei.

Gary amesema hategemei kurejea kwa mwajiri wake kwani tarehe 21 Mei atakuwa ' amekwishanyakuliwa'.

Enewei, nimefurahi kufahamiana na kila mmoja tuliyekutana na kubadilishana hili na lile hapa kijijini. Iwapo kweli tarehe 21 litatokea la kutokea tukutane upande wa pili. Chiazzzzz.

Kweli ,ni true story kaka ponda mali kufa kwaja.Ni tragedy bab kubwa kufa na kuacha pesa kibao bank na mali nyingi mitaani.
 
Yesu mwenyewe pamoja na Malaika ambao wako mbiguni imeandikwa hawajui siku ya mwisho...je nyie binadamu amabo mko ardhini mtajuaje? Mmeoneshwa na nani wakati Baba Mungu hata Mwanawe hajamwambia? hawa wachungaji wa pesa ndo wanawaharibu WaTanzania.. Mkaambiwa Loliondo na mkaenda...mnaaambiwa mwisho wa Dunia na mnaamini...hivi WaTanzania bado hatujajia Kuchuja eh.. Mpaka Taifa dogo lilipiku taifa kubwa kuliko lote Duniani. ambao inasemakana ni Marekani... ndo Mwisho wa Dunia....ndio umekaribia na hilo Taifa dogo litaipiku marekani likiongozwa na wahalifu...nafkiri mshaelewa ni Taifa gani na wahalifu gani...

Mpaka Israel na Palestina Waache kupigana ndio mwisho wa Dunia....
 
Hakuna aijuaye siku wala saa hata malaika Math.24:36-38 Thes.5:2-3 2Pet.3:10 siku ya Bwana itakuja kama mwivi so sidanganyiki ng'o

Ambacho hutaki ni kipi, kuijua siku na saa au dunia kwisha, naamini unatambua kuna kiama (mwisho wa dunia), na huo mwisho si mpango wa mwanadamu hivyo basi kujua au kutokujua tarehe hakusababishi dunia isiishe!!! Tukumbuke kuwa biblia ni maneno ya MUNGU awaambia watu atakayo kwa wakati ufaao, fikiri kidogo, ikiwa umeambiwa dhahiri kuwa watenda dhambi watahukumiwa adhabu ya kutupwa kwenye ziwa la moto milele hiyo haijakusaidia kuacha dhambi, unadhani hata ukijua siku ya mwisho kwa ugumu wa shingo ulionao unaweza kumlilia MUNGU kwa mapenzi yake akurehemu!!! Kumbuka si utakavyo wewe bali yeye!!.
 
Jamani, kama unataka kutabiri we tabiri mambo mengine, kutabiri mwisho wa dunia unajitafutia kuumbuka bure tu na watu wote kukushangaa.. Mi sijui kwanini watu hua wanajisumbua.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom