Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,145
- 13,216
Mtangazaji Mashuhuri wa Kipindi cha Wanawake Live Bi Joyce Kiria leo 06/03/2012 ameweka bayana kiwango chake cha elimu na kusema kwamba licha ya kwamba ameishia darasa la saba tu lakini ni mwanamke anayeweza kujivunia kwa mafanikio aliyonayo hadi sasa kwa kuweza kumiliki kampuni mbili ikiwemo ya Local Media Entertainment.
Ameyazungumza hayo na kuishia kububujikwa machozi wakati wa maadhimisho ya kuelekea siku ya mwanamke duniani aliyoandaliwa na WiLDAF katika ukumbi wa Karimjee (mtoa makala alikua shuhuda) na kusema kwamba mfumo wa elimu uliopo sasa unamkwamisha kuendeleza kipaji chake.