Joti na tangazo la Tigo "Mzee Mwalubadu"

Joti na tangazo la Tigo "Mzee Mwalubadu"

Huyu mzee mwalubadu...si alimtajaga nature kwenye mzee wa busara? Yule mzee mfupi anaeuza ngadu? Na yeye alipwe walau fidia

kweli mzee mwalubadu apewe chake sio kumuuzisha tu
 
Alafuu weeee dereeeeeeeee!!!!!!
 
lakini tuongee ukweli, huyu mzee mwalubadu anakaa wapi haswa?? Upanga au magomeni kagera? na huyu dere hajui alipotumwa?
 
huwa najiuliza kwanini hawa wasanii wetu wasiwe mamilionea kama kina Kelvin Hart,ukiangalia comment zote hapa jukwaani kwenye hii post kuna asilimia wameshawishika kujiunga na mtandao wa Tigo na wengine kubadiri mawazo ya kuuhama..roughly hata kama Joti angekuwa anapata 10% kwa kila tangazo linapo ruka hewani angekuwa mahali pazuri sana..ila sina uhakika wa term and condition za contract ya yeye na Tigo,mostly na mkubali AY kwenye issue kama hizi za kibiashara
 
Mimi hili tangazo nimelipenda sababu ya wanangu...niliwasikia wakiongea kwa pamoja "siyo ukerewe ni ubungo msele"

Nilicheka sana...hata hawajui kuwa alisema Ubungo Msewe...eti msele...
 
Tigo Kwa matangazo wako vizuri sana

Ndio wanaosema jisimatifonishe...ha ha ha...

Sababu wameajiri vijana zaidi...hawachukulia maisha serious kihiiiivyo....ku make profit hakuhitaji PhD ni u smart tu...
 
Hili tangazo nimelipenda. Haswa ile sehem lile box liliteleza bahati mbaya.. Daaaaa
 
Hivi tigo bado inatumiwa na watu wazima au bado ni ya wanfunzi?
 
Hivi tigo bado inatumiwa na watu wazima au bado ni ya wanfunzi?

Wale wanafunzi, wameshakuwa wafanyakazi sasa, wengine wana degree, wengine wana diploma, wengine wana certificate, wengine wana masters, wengine wana chukua PhD time hii, bila kuwasahau wale walioko kitaa Kama wewe.
Tigo wametoka mbali, na walianza na wanafunzi wa kipindi hichoooooo.........
 
Ila kuna kosa la muendelezo wa kisa yaani 'action continuity error' wakati wa kupeana boksi awali lilionekana Lipo mikononi mwa dereva hali bado mdada anamuongelesha hali akiwa ameshika boksi I.e wote wana boksi Mara ya pili akapewa tena hilo boksi.

Wenye taaluma zao wengine tunaangalia na kufurahi kumbe kuna makosa ya kiufundi, asante mkuu, credit kwako
 
wenzetu waliondelea wanaweza ila kwetu ka utaalam hako naona bado utujakawezea, kwenye tangazo la tigo ni watu wawili wameigiza sio joti peke yake ndo maana hakuna sehemu hata moja ukaona sura za wote wawili kwa pamoja

Mkuu acha kupotosha huu utaaram wa kuingiza sehemu moja watu wawili uko zaman saaana, fuatilia movie ya the LOST TWINS ya Steve kanumba utaona, kama ni suala la kuonekana wote sehemu moja kuna scene moja ya wazaz wa pacha (maskini/mlokole)mmoja wanapompeleka kwa pacha mwenzie (tajiri) wanaonekana wote sebuleni.
Angalia tangazo la joti (tigo) la facebook ya kiswahili joti mzee (mteja) ameonekana akiwa na joti kijana (customer care) alipokuwa anampa maelekezo.
Am out
 
Hivi tigo bado walikuwa hawajasambaa nchi nzima ndio saa hizi wanatangaza wakati wenzao matangazo ya kusambaa hayapo tena!
 
Back
Top Bottom