Joseph Warioba na Salim A. Salim wazungumza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Warioba na Salim A. Salim wazungumza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Saint Ivuga, Nov 4, 2010.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,495
  Trophy Points: 280
  Joseph Warioba na Salim A. Salim wazungumza 04/11/2010  Mawaziri wakuu wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, pamoja na mwanadiplomasia wa Kimataifa, Dk. Salim Ahmed Salim, kwa nyakati tofauti wametoa maoni yao kuhusu nguvu ya vyama vya upinzani kutwaa majimbo mengi ya uchaguzi.
  [​IMG]
  Joseph Sinde Warioba​
  Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Utanganzaji Tanzania (TBC) jana Warioba, alisema CCM imepoteza majimbo si kutokana na upinzani, bali ni matatizo yaliyojitokeza ndani ya Chama chenyewe.

  “Nafiriki ndani ya CCM kura za maoni zilileta mgawanyiko.“

  Kwa mujibu wa Warioba, hivi sasa kuna mwamko pamoja na hamasa kwa wananchi ambao sehemu nyingine wamesikiliza sera za vyama hivyo na wamedhani wakiwapa ridhaa wanaweza kufanya mabadiliko.

  “Nadhani kuna mwamko… tulitokea katika historia ya chama kimoja na wananchi walielewa hicho chama, itikadi yake na sera zake na hasa vijijini walikuwa wamezoea hivyo,” alisema.

  Hata hivyo mwamko wao wa kule kupata fursa ya kusikiliza hizo sera za vyama vingine, umewachukua muda mrefu kuchukua uamuzi wa kufanya mabadiliko.

  “Ninaona vyama vya upinzani wanavyoongoza, kwa mfano Mwanza, mahali pazito pale, wanaingia vijana waliozalizwa miaka ya 1970 …na hata ukiona kwenye mikutano, vijana wameamka na hii ni dalili nzuri kwani vijana ndiyo nguvu ya Taifa,” alisema.

  [​IMG]
  Salim Ahmed Salim​
  Warioba alisema kuwa vijana ndiyo wanaoleta mabadiliko na kwamba ukikuta mahali mawazo ya vijana na wazee yanafanana, ujue hapo pamedumaa.

  “Lazima vijana wawe na mtazamo mpya tofauti na wazee, watachukua uzoefu wao na kuanzia hapo, lazima pawe na mabadiliko,” alisisitiza Warioba.

  Naye Dk. Salim, akitoa maoni yake kupitia TBC jana, alisema wakati umefika kwa CCM kujifanyia tathimini ya mambo mbalimbali.

  Alisema uchaguzi umekwenda vizuri, licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale ambapo hata wachunguzi wa kimataifa waliokuwepo nchini, wameridhika na ulivyofanyika kwa utulivu na amani.

  Pamoja na kuzungumzia mambo mbalimbali juu ya uchaguzi huo, Dk Salim ameshauri CCM sasa ifike mahali ijitathimini na akaongeza kuwa upinzani kushinda katika baadhi ya majimbo si jambo baya.

  “Tunazungumzia demokrasia, kuiimarisha demokrasia, hilo halina wasiwasi wowote …kuna mahali vijana wetu wanashinda na maeneo mengine, pengine ndugu zetu upinzani wanashinda,“ alisema Dk Salim.  from: Joseph Warioba na Salim A. Salim wazungumza -
   
 2. G

  GAMA LUGENDO Senior Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 131
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nawapongeza sana wazee wetu hawa, ndugu Salim Ahmed Salim na Joseph Sinde Warioba kwa uchambuzi wao ambao ni wa kina, objective, wa kiufasaha na mi binafsi nawapa pongezi kwa vile wanaonekana kujua na kuelewa vizuri si tu umuhimu wa demokrasia katika nchi, bali vile vile wanaonekana kutambua fika umuhimu wa mabadiliko hasa yale yanayosukumwa na watu wenyewe kwa ajili ya maendeleo na mustakabari wa taifa lao.Thanks and God grant them more wisdom and long life.
   
 3. J

  Jafar JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Nawaheshimu hawa wazee wangu wawili

  " ... wao wana pesa, sisi tuna Mungu .. " (Godbless Lema, MB)
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  na wamemchagua Bi Halima Mdee kuwawakilisha bungeni!!!!!
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Wazee hawa pamoja na UOZO ulioko CCM bado wamebaki humohumo. Hawana jipya. Waoga.
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,608
  Trophy Points: 280
  Wazee wetu kuweni wa kweli......CCM is a dying horse.....you do not flog a dead horse you just dig a grave and bury it..........................Ufisadi na wala siyo kura za maoni ndani ya CCM ndiyo chanzo cha wapigakura kukichukia..........mshahara wa dhuluma ni mauti yatokanayo na laana........
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Kama walivyompiga chini Kippi Warioba Kawe mpaka kinamama wakalia kwenye TV "Tunamtaka Kippi wetu"
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ni kweli mbona hawaweki wazi kwamba kuna wizi wa kura?
   
 9. Double X

  Double X Senior Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa ni wanafki tu,pamoja na kuvunda,kuoza na kunuka kote kwa CCM lakini bado wamo humo humo,hawana jipya.
   
 10. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hawa wazee ingekuwa hamu yao wangehama CCM tatizo wanaogopa hujuma za chama Tawala
   
 11. Bambo

  Bambo JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 237
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni analysis nzuri..nachukia sana ccm kuwakumbatia watu kama kinana ambao wanakurupuka na sababu za ****** eti alitoka na mavi kwa sababu alikosea hakuingia na maji!!!! hizi sabau za kusingizia kura za maoni ni mufilisi na kuacha ukweli kwamba utumishi wa ccm kwa maendeleo ya nchi yetu ni wa mashaka ili sasa kutoa mwanya wa kujirekebisha.Usalama wa Taifa wanatakiwa waongeze kasi ya kuelewa hilo ili waweze kuanza kuwatumikia watanzania wote badala ya kubaki kulinda maslahi ya matajiri wachache..uchaguzi huu umefungua ukurasa mpya wa kuelekea kwenye FAIR DISTRIBUTION of national resources hivyo hakuna wa kuendelea kuzuia hilo
   
 12. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #12
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Inamaana mkeo uliye nao kwenye ndoa ni lazima umuache na kumwoa mwingine ndio kutatua matatizo ya ndoa yako??? Tafakari kwa makini.

  CCM kwa sasa inahitaji kweli tathimini makini na angalifu sasa kwani wao kuwepo kwao ndani ya CCM ndio kusema waoga? Kama kweli wewe ni mfuatiliaje mzuri wa Siasa za TZ unawaelewa hawa wazee fika ni mangapi wameshauriwa CCM na wameyapuuzi wakiongozwa na JK na mpaka kufikia kutoa maneno ya kejeli oooh wakati wenu mlishindwa iweje sasa ati mwajua kutukosoa sisi, As a President hutakiwi kuji hivyo au kwani ungenyemaza na kuto ruhusu mipasho asinge pungukiwa na kitu is just a matter of working on issue mentioned period. Wajua yawezekana kabisa hata hao viongozi wa zamani walikuwa na mapungufu lakini usifananishe na yakwao waliyo yakosea unatakiwa uyatafutie ufumbuzi na unasonga mbele kwa Rais makini ndivyo anastahili kufanya hivyo na si kupuuzia tuuuu kwa kua ana IMMUNITY !!!

  Sasa kutokuwa makini kwa mambo ya kimsingi na Taifa lako na Chama chako ndiko kinaporomosha kwanza Chama chako ambacho ulitegemea kinge tawala miaka mingi na sasa tizama chafa mikononi kwao JK
   
 13. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #13
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Hazo ni Nyufa muhimu za kwanza kabisa zinazo kiua CCM

  Hawana Black and White ndani yao kuna majitu yakiambiwa ni mabishi, hawajui kujenga HOJA za kuwatoa matajiri ndani ya chama na wawe wanachama wa kawaida tuu ili kulinda uadilifu na uongozi bora.

  Kushindwa kurekebisha mapungufu machache yaliyomo kwenye Azimio la Arusha, ili kuleta usawa na haki kwa wananchi wote, viongozi kuwa wazalendo na kuijua miiko ya uongozi

   
 14. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #14
  Nov 4, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Hoja ya Warioba haina nguvu; hata kama ndani ya CCM kungekuwa shwari pigo lingekuwa pale pale - mimi si mwanachama wa chama chochote na nimepiga kura. Hoja ya msingi ni nusu karne bado watoto wanamaliza shule ya msingi wakiwa na uwezo wa kusoma na kuandika kama mwanafunzi wa darasa la tatu, mzazi gani atakubali? Bora hata hoja ya Dr. Salim.
   
 15. c

  chama JF-Expert Member

  #15
  Nov 4, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hawa wazee ni moja ya viongozi wachache ambao waliweka maslahi ya taifa mbele, utendaji wao kazi ulikuwa mzuri si lazima kila kiongozi ahame chama kama hakubaliani na chama chake, kwa nafasi zao walizoshika serikalini ni vigumu sana wao kuihama CCM lakini wameongea ukweli.
   
 16. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #16
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  NILIPATA NAFASI YA KUTEMBELEA SHANGHAI EXPO 2010 KATIKA PAVILION YA "AU" African Union Jina la Dr.salim Ahmed Salim ni maarufu sana , huyu mzee ametuletea heshima kubwa sana nchi yetu alipokuwa AU.. nilipowaambia natoka TZ i thought ningepewa strory za nyerere ! kwa mshangao walikuwa wakiongea na mimi kwa furaha na bashasha wakinipa sifa za huyu bwana! nikawa najiuliza hivi hawa watu hamjui nyerere ama.?
   
 17. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #17
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Sawa sawa hapo tupo pamoja sana kama nilivyosema mapema, naona hatuko mbali sana, CCM ijiangalie maana imepigana na kivuli chake kwenye huu uchaguzi.

  William.
   
 18. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #18
  Nov 4, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Hawa wazee kuna mambo mengi mazuri walifanya, lakini kitendo chao cha kukaa kimya na kutozungumzwa chochote juu ya uchakachuaji unaonendelea kinawavunjia heshima mbele ya wananchi. Ni lazima ifike sehemu watu wajifunze kuweka maslahi ya taifa mbele, CCM sio Tanzania!
   
 19. J

  JokaKuu Platinum Member

  #19
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,747
  Likes Received: 4,967
  Trophy Points: 280
  ..hawa ni wawili ni waoga wakubwa.

  ..wana mtandao wa CCM wamewachafua lakini wameendelea kung'ang'ania humohumo ndani ya CCM.

  ..kama walishindwa kujitetea wenyewe dhidi ya siasa za maji taka za wanamtandao usitegemee wakawatetea wananchi hata siku moja.
   
Loading...