Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 54,363
- 58,386
Joseph Warioba na Salim A. Salim wazungumza 04/11/2010
Nafiriki ndani ya CCM kura za maoni zilileta mgawanyiko.
Kwa mujibu wa Warioba, hivi sasa kuna mwamko pamoja na hamasa kwa wananchi ambao sehemu nyingine wamesikiliza sera za vyama hivyo na wamedhani wakiwapa ridhaa wanaweza kufanya mabadiliko.
Nadhani kuna mwamko tulitokea katika historia ya chama kimoja na wananchi walielewa hicho chama, itikadi yake na sera zake na hasa vijijini walikuwa wamezoea hivyo, alisema.
Hata hivyo mwamko wao wa kule kupata fursa ya kusikiliza hizo sera za vyama vingine, umewachukua muda mrefu kuchukua uamuzi wa kufanya mabadiliko.
Ninaona vyama vya upinzani wanavyoongoza, kwa mfano Mwanza, mahali pazito pale, wanaingia vijana waliozalizwa miaka ya 1970 na hata ukiona kwenye mikutano, vijana wameamka na hii ni dalili nzuri kwani vijana ndiyo nguvu ya Taifa, alisema.
Lazima vijana wawe na mtazamo mpya tofauti na wazee, watachukua uzoefu wao na kuanzia hapo, lazima pawe na mabadiliko, alisisitiza Warioba.
Naye Dk. Salim, akitoa maoni yake kupitia TBC jana, alisema wakati umefika kwa CCM kujifanyia tathimini ya mambo mbalimbali.
Alisema uchaguzi umekwenda vizuri, licha ya kuwepo kwa dosari za hapa na pale ambapo hata wachunguzi wa kimataifa waliokuwepo nchini, wameridhika na ulivyofanyika kwa utulivu na amani.
Pamoja na kuzungumzia mambo mbalimbali juu ya uchaguzi huo, Dk Salim ameshauri CCM sasa ifike mahali ijitathimini na akaongeza kuwa upinzani kushinda katika baadhi ya majimbo si jambo baya.
Tunazungumzia demokrasia, kuiimarisha demokrasia, hilo halina wasiwasi wowote kuna mahali vijana wetu wanashinda na maeneo mengine, pengine ndugu zetu upinzani wanashinda, alisema Dk Salim.
from: Joseph Warioba na Salim A. Salim wazungumza -
Mawaziri wakuu wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jaji mstaafu, Joseph Sinde Warioba, pamoja na mwanadiplomasia wa Kimataifa, Dk. Salim Ahmed Salim, kwa nyakati tofauti wametoa maoni yao kuhusu nguvu ya vyama vya upinzani kutwaa majimbo mengi ya uchaguzi.
Joseph Sinde Warioba
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wakati wa mahojiano maalumu na Shirika la Utanganzaji Tanzania (TBC) jana Warioba, alisema CCM imepoteza majimbo si kutokana na upinzani, bali ni matatizo yaliyojitokeza ndani ya Chama chenyewe. Nafiriki ndani ya CCM kura za maoni zilileta mgawanyiko.
Kwa mujibu wa Warioba, hivi sasa kuna mwamko pamoja na hamasa kwa wananchi ambao sehemu nyingine wamesikiliza sera za vyama hivyo na wamedhani wakiwapa ridhaa wanaweza kufanya mabadiliko.
Nadhani kuna mwamko tulitokea katika historia ya chama kimoja na wananchi walielewa hicho chama, itikadi yake na sera zake na hasa vijijini walikuwa wamezoea hivyo, alisema.
Hata hivyo mwamko wao wa kule kupata fursa ya kusikiliza hizo sera za vyama vingine, umewachukua muda mrefu kuchukua uamuzi wa kufanya mabadiliko.
Ninaona vyama vya upinzani wanavyoongoza, kwa mfano Mwanza, mahali pazito pale, wanaingia vijana waliozalizwa miaka ya 1970 na hata ukiona kwenye mikutano, vijana wameamka na hii ni dalili nzuri kwani vijana ndiyo nguvu ya Taifa, alisema.
Salim Ahmed Salim
Warioba alisema kuwa vijana ndiyo wanaoleta mabadiliko na kwamba ukikuta mahali mawazo ya vijana na wazee yanafanana, ujue hapo pamedumaa. Lazima vijana wawe na mtazamo mpya tofauti na wazee, watachukua uzoefu wao na kuanzia hapo, lazima pawe na mabadiliko, alisisitiza Warioba.