Joseph Msukuma ni nani?

Joseph Msukuma ni nani?

nikijaribu kufikiria katika mazingira yalivyokuwa wengine wengi walikuwa wanafuata mikumbo na hofu ya baadae tu.

kama akiwasiliana na wewe na kukutaka umuunge mkono na ukakataa itakuwaje akishinda? na hapa inategemea - je ni mtu wa kuja kulipiza kisasi au akishinda hatokuwa na muda huo. hii ni muhimu kuzingatia.

kuna wagombea wengine akikutafuta ukakataa wala hatakuwa na muda wa kukulipizia akishinda. kwa wengine inawezekana inakuwa tofauti

wengi wetu pia katika maisha ya kawaida tuna mapungufu ya hapa na pale na kwa namna moja au ingine tumewahi pata fadhila hii au ile toka kwa huyu au yule. sasa mtu anaweza kukufuata akitaka nae umsaidie katika jambo lake ....

watu wanaochapa kazi, wanaojiamini na wasio na matatizo ya ovyoovyo ndio watu wa kuwategemea na kuwaamini - maana wao wanapofanya kitu huwa hawaendeshwi au kupelekeshwa ovyo kama gari bovu
 
Kingunge alikuwa mjamaa Enzi Za Nyerere, Enzi Za Kikwete Kawa fisadi, mtu unabadilika kutokana na mazingira na kucheza na fursa na yeye Sasa hivi atabadilika atamuunga mkono magufuli, kama alivyobadilika Sofia simba.

Kingunge alikuwa fisadi tu toka enzi za Mwalimu ndo maana Mwalimu hakuwa akimpenda hata kidogo.
 
Hata wewe mahaba yako na CCM yatakutokea puani Ukawa itapotia timu
Mkuu,
Unafahamu maana ya neno mahaba?

Mimi mwenyewe ninaamini hunifahamu kama nisivyokufahamu wewe!

Una maana gani unaposema ''ukawa itapotia timu''.

Nisaidie kunielimisha zaidi kwa sababu nimeshindwa hata kujenga hoja mbadala ya angalizo lako!
 
Nimezungumza na mkazi mmoja wa Kata ya Nzera Wilayani Geita Bwana JOhn Peter Bashite anasema, "Magufuri ni Msukuma wa Chato ambako alizaliwa ila ana ndugu zake kijiji kimoja cha mwaramba kata ya Nkome wikayani geita,'pia hapa Nzera ana ndugu zake akiwemo mh.Msukuma diwani wa kata ya Nzera wilayani Geita ambaye ni Mdogo wake na Mama yake Magufuli..yaani mjomba mtu!pia hata wao walishangazwa kwa mh.Magufuli kuteuliwa na chama chake kupeperusha bendera ya ccm kuwania uraisi maana wengi hawakutarajia.Msukuma kiasili ni msukuma mwenye asili ya Kisesa na huko Chato wazazi walihamia kutafuta maisha...mzee mmoja alisema,"unajua huku geita wasukuma tulihamia kwa wingi kutoka Magu na maeneo mengine tukisaka malisho ya mifugo na kilimo...hivyo tukayapenda maeneo haya na kuyafanya makazi..hivyo tunashukuru sana ndugu yetu huyu amekuja kutukomboa kwani mifugo wetu wamenyanyasika sana...Hapo ndipo nikaamini kumbe huyu jamaa ni msukuma?Maana ya jina Magufuli maana yake makufuli katika wingi.....ni majina ya wasukuma waliitana kipindi cha ngoma na mavuno.kilala kheri mh.magufuri mtu wa watu.
.
 
We huwajui hawa jamaa. Ulisikia alichokisema? kwanza kwa taarifa yako, Magufuri na Msukuma ni mtu na mpwa wake. Alikuwa kambi ya Lowassa kwa kuwa alikuwa wazi, Magufuri hakuwa wazi. lkn ni ndg kabisa
Mkuu,
Hoja siyo suala la Magufuli kuwa muwazi au la, suala ni kwa Msukuma kutumia mtaji wote kucheza kamari ya kisiasa!
 
Mkuu Izzo ata mimi ili swala lilinitatiza kwelii!,nilijiuliza kwanini wanafanya hivyo wakati Mh.J.P.M bado ni mgombea tuu! kama wagombea wa vyama vingine...au sisi hatujui labda hao wanaomlinda mh. wameajiriwa na wanalipwa mishahara yao na chama tawala!..you never know!
mkuu mmoja namjua tena yupo kwenye security detail ya mr invisible
 
hv hawa jamaa wanaomlinda maguful ni usalama wa ccm au usalama wa taifa kama ni wataifa basi wapelekewe ulinzi na wagombea urais wengne dah ccm wanatumia nguvu kaz ya wote kwa matumiz yao ya chama wale wanalipwa ela ya kodi ya wananchi tena wengne c wanachama wa ccm au wanalipwa ela za ccm?

Ile dhana ya kufikiri ccm ikimsimamisha mgombea yeyote atashinda imepitwa na wakati uwt mbona naona mrembo Huyo na mijizee inaweza mititi kweli au wanategemea miguu ya kuku waliyoificha kiunoni?
 
Ninavyojua ni kuwa, Musukuma ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita & Magufuli anatokea mkoa wa Geita. Raisi Kikwete aliwaambia wagombea wakakae katika mikoa yao, na Magufuli alifanya hivyo. Musukuma ndiye kiongozi au boss wa Magufuli kichama kwa mkoa & he was the best option to seat next to. Wewe unaona kuna shida hapo? Mimi sidhani.
Mkuu,
Jaribu kusoma mtiririko wa hoja zangu ili uelewe msingi wa hoja yangu.

Msukuma hakukitendea haki kiti cha Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM kwa sababu Kanuni haziwaruhusu Wenyeviti kumdhamini mtia nia yoyote achilia mbali kusimama kwenye media na kutoa vitisho kwa Kikao cha juu kabisa cha chama.
 
sina uhusiano na ccm lakini kumtenga ndugu yako kwa sababu ya njaa haikubaliki .
 
Ng'wamapalala

Ng'wamapalala, nashukuru kwa habari yako nimekuwa nikipigia kelele umaarufu wa Lowassa wakati alikuwa na tuhuma mbalimbali huku akizungukwa na watu mbalimbali kumbe zote hizo ni kutafuta maslahi wala si kuwatetea watanzania mbali na kumuoa Msukuma kwenye mikutano ya Lowassa akimshabikia na kumpigia chagizo na sasa anaonekana pembeni ya Magufuli badala ya kuwa Masaki kwa mtu wake usishangae wiki ijayo akaanza kuporomosha matusi na kashifa dhidi ya Lowassa watanzania wengi hawana nia halisi ya kuleta mabadiriko ya kutetea wanyonge bali ni wasakatonge na madaraka hawana jipya. Msukuma ni mnafiki hana jipya msakatonge kama wengine wa kariba yake
 
Last edited by a moderator:
DSC_0582.jpg


Tuseme kweli hawa jamaa usalama wakiulizwa mbele ya dunia inakuwaje mgombea tayari anaanza kupewa such an attention na Dr.Slaa naye atapewa akishatangazwa tu? Why does a presidential candidate deserve such a public attention kuna uchaguzi kweli and why the F should the government spent so much money on BRV.

Ushamba wa mwafrika bwana these people can not disguise anything hivi marekani iwaachie ulinzi wa raisi wao kwa watu kama hawa kweli, no wonder mzungu nayeye keshajua ndio maana anasema its pretty much a one party state.
 
naona hii topic ya msukuma na magufuli watu mmeanza kuingiza ukabila, huu ni unafiki msukuma ana haki na kupenda popote sio kumlazimisha kumpenda magufuli kisa wote kanda ya ziwa, ingekuwa hivyo basi watu wangelaumiwa sana kwa kuoa au kuolewa na watu wasio wa kabila au mahali pamoja, hii ndio tz ambayo baba wa taifa alituachia jmn tuache mambo ya ukabila na undungunization
 
Mkuu,Jaribu kusoma mtiririko wa hoja zangu ili uelewe msingi wa hoja yangu.Msukuma hakukitendea haki kiti cha Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM kwa sababu Kanuni haziwaruhusu Wenyeviti kumdhamini mtia nia yoyote achilia mbali kusimama kwenye media na kutoa vitisho kwa Kikao cha juu kabisa cha chama.
Uko sahihi mkuu. Kwa upande huo Alifanya kosa!
 
Back
Top Bottom