Joseph Msukuma ni nani?

Joseph Msukuma ni nani?

Jamaa mtafutaji wala si utani. Mara kwanza kuonana naye nilidhani kijana mdogo. hapana ni umbo tu ila jamaa in 50+years. I personally asked him how come wewe mdogo tu badala ya kuwa mernyekiti WA UVCCM na sio CCM ndio akanijibu hadi umri wake. Simfahamu sana kiundani but nauhakika most of Mali zake ni za kupigana mwenyewe. maana ana miradi mingi ya biashara.
 
Jamaa mtafutaji wala si utani. Mara kwanza kuonana naye nilidhani kijana mdogo. hapana ni umbo tu ila jamaa in 50+years. I personally asked him how come wewe mdogo tu badala ya kuwa mernyekiti WA UVCCM na sio CCM ndio akanijibu hadi umri wake. Simfahamu sana kiundani but nauhakika most of Mali zake ni za kupigana mwenyewe. maana ana miradi mingi ya biashara.

Ni mjanja mjanja tu wa ccm , we unafikiri lowassa akishinda urais atalipa kodi kupitia hizo biashara zake?? Subutu yako.
 
Hivi helkopta kama hiyo sh ngapi?

inategemea unatafuta ya aina gani. mojawapo hii hapa chini inauzwa $134,900.

image.jpg
 
Best kichefuchefu kwani una mimba tayari? Usipate kichefuchefu bana. Mara ya kwanza kumuona huyo msukuma nilichoka......... V8 yake kwenye plate namba imeandikwa msukuma

Best ulichoka? Usichoke bhana, kwani una mimba??
 
  • Thanks
Reactions: ram
Kwa mara ya kwanza nilimuona Bwn. Msukuma akiwa kwenye kipindi cha siasa Star TV, akatambulishwa kama Mwenyekiti wa CCM Geita.

Sikumtilia maanani sana kwa kuwa alijaa majigambo kuliko hoja, tofauti na makamanda wa SAUT ambao walijenga hoja nzito. Alionekana bwana mdogo tu hivi!

Ghafla nikasikia Mh. Mwigulu anakata mawimbi na "Chopa la Msukuma". Na leo pale kwenye Safari isiyo na Matumaini kafanya taiz kutua na Chopa.

Sasa wanaomjua vizuri watupe details, huyu ni nani hasa, katoa wapi mapesa haya yote, halafu kama vile kwa umri mdogo!!

ni kweli msukuma ni kijana mdogo sana, tena kama ana elimu kubwa ni cha nne lkn mie najua ni la saba. kuna kipindi walikuwa wanamsema ni mpwa wa magufuri naagufuri ufisadi wake anawekeza kwake.

alikuwa anamiliki mabasi jijini Mwanza lkn siku hizi hayaonekani ni kama alifilisika au alibadili biashara lkn kwa sasa ni diwani ktk kata moja huko geita
 
ana kampuni ya mabasi classic sana yanaitwa king musukuma
 
msukuma ni janga la geita,upinzani watasumbua sana kama huyu mtu atabaki na nafasi hii kwa muda mrefu

Mkuu wapinzani watasumbua? Hivi wanaotaka kupata uongozi kutoka upinzani wanasumbua? Unataka kutuambia ccm ndio ina haki ya kutawa nchi kihalali?haki hiyo wameipata wapi? Naamini wapinzani hawasumbui bali ni haki yao kama hiyo ccm.
 
Huyu Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita anayeitwa Joseph Kasheku ‘Msukuma'alitumia helikopta kwenda kwenye mkutano wa Edward Lowassa ambao aliubatiza jina la Mwanzo wa Safari ya Matumani.

Kama hiyo haitoshi, alifanya juhudi zote kuhakikisha anatua kati kati ya kiwanja kuonyesha ulimwengu uwepo wake pamoja na uwezekano wa kuhatarisha maisha ya wananchi.

Huyu Mwenyekiti wa Mkoa wa Geita hakuishia hapo, alizunguka mikoani na Edward Lowassa kusaka wadhamini na kilele chake kilifikia pale alipojitokeza mbele ya vyombo vya habari wakati Lowassa anarudisha fomu na kudai CCM haina uwezo wa kuzuia mafuriko ya Lowassa na kufanya hivyo ni kujidanganya. Kwa lugha nyingine, alitaka CCM imteue Lowassa hata bila kufuata vigezo 13 iliyojiwekea na kutokufanya hivyo ni CCM kukumbwa na mafuriko ya Lowassa.

Kuonyesha kama alichokuwa anakisema kiligubikwa na ujinga au upumbavu, Kamati Kuu ilimkata Lowassa. Haikuishia hapo, bali Mkutano Mkuu ulimteua mwanachama ambaye siyo kwamba anatoka katika mkoa wake bali pia ni ndugu yake.

Na kama hiyo haikuishia hapo, Magufuli alienda kukaa kwenye kiti ambacho ni jirani na kiti cha huyu Joseph Kasheku kabla matokeo hayajatangazwa.

Magufuli alichokuwa anakifanya kwa Joseph Msukuma ni psychological taunting and torture.

Picha zinasema mengi yaliyokuwa yanapishana ndani ya ubongo wa Joseph Kasheku 'Msukuma'.

Kuna msemo wa kiswahili unaosema usibebe mayai yote kwenye kapu moja, hii ikimaanisha uchukue tahadhari maana ukipata ajali, mayai yote yatapasuka!

Mayai yote ya Joseph Kasheku ‘Msukuma' yamepasuka!

DSC_0573.jpg

John Magufuri akiwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Geita anayeitwa Joseph Kasheku ‘Msukuma' ndani ya ukumbi wa Mkutano Mkuu wa CCM.
DSC_0582.jpg

Wafanyakazi wa Usalama wa Taifa wakimzunguka Magufuli kabla ya kutangazwa kuwa mshindi wa kura za kugombea Urais.

MMGL0345.jpg

Picha inayoonyesha baadhi ya wenyeviti wa CCM wa mikoa mbali mbali walioambatana na Lowassa kwenda Makao Makuu ya CCM-Dodoma kurudisha fomu zake za ugombea Urais wa Tanzania. Mwenyekiti Joseph Kasheku 'Msukuma' (Geita) Mwenyekiti Bwarafia Silima (Unguja) Mwenyekiti Jesca Msambatavangu (Iringa) Mwenyekiti Madabida Madabida (Dar es Salaam), Mwenyekiti Hamisi Mgeja (Shinyanga), Mwenyekiti Msindai (Singida), Mwenyekiti Odo (Ruvuma), Mwenyekiti Sinani (Mtwara), Mwenyekiti Sanya (Mara), Mwenyekiti Mlao (Pwani), Mwenyekiti Kabouru (Kigoma) na Wenyeviti 3 (Pemba na Unguja).
 
Kingunge alikuwa mjamaa Enzi Za Nyerere, Enzi Za Kikwete Kawa fisadi, mtu unabadilika kutokana na mazingira na kucheza na fursa na yeye Sasa hivi atabadilika atamuunga mkono magufuli, kama alivyobadilika Sofia simba.
 
Back
Top Bottom