Sishabikii machinga kuwa barabarani lakini nahoji kwa nini barabara kubwa kama ile imepita katikati ya mji mkubwa kama Mbeya!? Kwanini isinge kwepeshwa kama kuanzia Uyole mpaka Mbalizi hivi!! Hata kama machnga wasingekuwepo hapo Mwanjelwa baada ya miaka 5 kutoka sasa bado kutakuwa na foleni kwa sababu hapo ni center ya Mbeya. Barabara kama Mandela pale Dsm bado inafoleni ya kutupa hata baada ya kuipanua kwa sababu ya hizo transit vehicles, maeneo kama Tazara, Buguruni, njia ya panda ya Tabata, Tabata relini na Ubungo.
Alafu mbunge hafanyi hizo kazi pekee yake na pia sio anatoa pesa mfukoni mwake na hayo ndio matatizo yetu tunafikiri mbunge kazi ya kufanya hizo kazi au kuzilipia kwa pesa yake, badili mtazamo wako msaidie mbunge wako (SUGU) hata kama itikadi yako ni tofauti na ya kwake, kwa sababu usipofanya hivo subiri miaka 5 ya bila maendeleo
Asante kwa mchango mzuri
Zuberi Jr .
Tupo amoja katika kuliona tatizo la barabara ya Uyole mpaka Mwanjelwa.
Simlaumu Sugu kwa kulisababisha bali kwa kutokuwa chachu ya utatuzi wa tatizo hilo.
Tatizo kubwa la barabara hii ni mapungufu makubwa katika Master Plan ya jiji la Mbeya. Hiyo barabara haipo tena katika viwango vya highway bali sasa ni street-barabara ya mitaa.
Wakati barabara hiyo inajengwa hapakuwepo juhudi zozote kupanua au kujenga barabara za sambamba ili kuchukua traffic ya jiji la Mbeya.
Na vile vile hapakuwepo juhudi zilizokwenda shule kukidhi miundo mbinu mbadala kwa ajili ya shughuli za wananchi kama soko au viwanja vya michezo- hasa sehemu walipo watu wengi.
Na ndio tuaona sasa kila mwenye biashara anakimbilia Mwanjelwa, kuanzia mchoma mahindi, mchonga grilli hadi hoteli ya kisasa.
Picha inayojitokeza ni atotally unplanned settlement.
Sina uhakika kama ZuberiJr unajua kwamba zamani barabara kuu ilikuwa inapitia Mafiati,Lupa Way hadi Meta.
Tutaendelea kuhamisha barabara mpaka wapi badala ya kuwa ma mipangilio mizuri ya miundombinu.
Ndio maana kizazi hiki tunahitaji watu wa kusaidia kutatua matatizo sio nyimbo zisizoisha.
Utatuzi wa matatizo ya Mbeya mjini, pamoja na la machinga si kuwashabikia bali kutengeneza au kuboresha Masterplan ya jiji ili liondokane na sura ya "kijiji kikubwa".