Joseph Mbilinyi (SUGU) MB afanya kweli Mbeya Mjini

Joseph Mbilinyi (SUGU) MB afanya kweli Mbeya Mjini

Ingependeza kama watu wazima na akili zetu tukabishana bila kugombana na kwa kujenga hoja, aina ya ushabiki wa siasa za namna hii na usio na upeo wa maendeleo unatufanya kama watanzania tuwe tulivyo hadi leo na hakuna anaejali na hii ni hatari sana kwa sisi kama wazazi wa watoto wetu kwa dhamana adhimu tuliopewa na jinsi tunavyolichukulia kimzaha suala la na mustakbali wa taifa letu na vizazi vijavyo!


Nimeona nianze kama nilivyo anza hapo juu ili kuonyesha msimamo wangu binafsi na bila kuegemea upande wowote. Nikiwa mtu ambaye naifahamu mbeya kwa kiasi cha mwenyeji yeyote ningependa nichangie mjadala huu kama ifuatavyo:
1. Barabara zinazojengwa sasa hivi mbeya hazina uhusiano wowote na ama uwepo au kutowepo kwa sugu kama mbunge. Kinachoendelea katika mengi ya majiji yetu mengi ni msaada/mkopo wa kuboresha hali ya majiji katika baadhi ya majiji katika nchi za afrika, kwa wanaopenda ukweli wanaweza wakaangalia vibao vya kazi husika vinaonyesha pesa zimetoka wapi na mkandarasi ni nani, mshauri wa mradi ni nani na msimamizi ni nani (mara zote msimazi huwa ni halmashauri ya jiji)

Utaona kwamba hii haihusiani na siasa za ndani bali siasa za kimataifa ambazo zilisharatibiwa zamani na kwamba imetokea tu kwamba utekelezaji wake unafanyika wakati huu.

2.Kwa wenye maslahi na mradi huu, badala ya kufanya siasa za majukwaani na upambe tunatakiwa kuwa makini na yafuatayo: a). kwa maoni yangu mimi viwango vya barabara husika mpaka hatua zilizo fikia haziridhishi hivyo wasimamizi wana kazi ya ziada ya kufanya hapa vinginevyo tutatumia barabara hizi kwa kipindi kifupi sana halafu tutarudi kwenye hali tuliokuwa nayo.
b). Hali ya mtiririko wa asili wa maji (drainage system) ya mbeya imeathirika vibaya na ujenzi holela, hii inapelekea sehemu kubwa ya hizo barabara kuwa na tatizo la wapi maji ya mvua yaende. CICO (kampuni ya ujenzi) imejenga vikutanisha barabara na mifereji (culvert) tatizo bado linakuwa kwamba maji yaende wapi? Mfano mahsusi wa hili ni eneo la mafiat airport ambako maji yakishafika kwenye culvert yanakosa uelekeo.

Hivyo badala ya kuchapa politic kwenye screen za komputa tuangalie mambo ya msingi kwani barabara ningi kama sio zote za Arusha hazikuwepo miaka miwili iliyopita nilipotembelea huko mara ya mwisho lakini kwa sasa Arusha barabara zake za mjini nikichukulia makao mapya kama mfano zimejengwa vizuri na zina viwango vizuri naamini suala ni usimamizi na si vinginevyo kwani mafungu ni hayo hayo kwanini viwango vitofautiane?

TAFAKARI CHUKUA HATUA.

Nakubaliana nawe, hii miradi ilibuniwa katika kipindi cha mwaka 2004/05 na utekelezaji wake ulikuwa uanze 2010 kwa Mbeya lakini mienzi ya kuanza kwa Mbeya haikuwa muafaka ilikuwa kipindi cha mvua ndipo imeanza mwaka jana. Sugu hana mchango wowote kwenye hiyo miradi na wala sio ya kisiasa, ilibuniwa na wakurugenzi na timu zao za wataalamu na ipo kwenye majiji na manispaa kadhaa hapa nchini.

Ufanisi unaonekana hivi sasa katika Jiji la Mbeya umetokana na Mkurugenzi aliyepo, ana misimamo na hayumbishwi na wanasiasa, amedhibiti wizi wa fedha za jiji kiasi cha kundiwa mikakati ya kumg'oa. Msimamo wa RC Kandoro na PM ndio kikwazo cha mikakati ya Meya wa jiji hilo na wafuasi wake wakiwemo wakuu wa idara waliotesha mizizi yao hapo, mikakati yenye lengo la kumg'oa.

Hizo barabara kwa kiwango kikubwa zimefanikishwa na misimamo ya Mkurugenzi huyo baada ya kuwawekea ngumu Meya na timu yake waliokuwa wakilazimisha 10pc.

Mkurugenzi habagui chama, husikiliza kila mtu na kutokana na uwezo wa kujenga hoja wa madiwani wa CDM mara nyngi amekubaliana na mawazo/hoja zao, but sio Sugu.

Kuna watu hapa wanalazimisha kumnyanyua Sugu, hapana kama ni utendaji basi ni madiwani wa chadema Mbeya, hawa wameonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa tofauti na Mbunge, na mchango wao kwenye Baraza la Madiwani tunauona na unakubalika na viongozi wengi hapa mkoani.

Msaidieni Sugu kwa kumweleza ukweli badala ya kumpatia sifa asizostahili.

Kuhusu ubora, wengine sio wataalamu, bali tunaangali tu kwa macho, kwa ile ya Airport iliyokamilika naiona iko katika kiwango kizuri, ila suala la mifereji ni lamsingi sana kwa Mbeya, ni kweli maji hayana kwa kwenda kwani mifereji ya tangu mkoloni na ile ya miaka ya 70 iliyotengezwa kuelekeza maji kwenye mito imeziba yote.
 
Mkuu naona umebugia chimpumu unabwabwaja Kama kichaa
Nitakuwa napoteza muda nisipokuonea huruma! kwani naamini kwa haki ya mungu sio tatizo lako ila upeo ulionao, pole sana na mungu akubariki na akuongezee upeo ili angalau uweze kuwa na upeo wa kawaida tunaojivunia wenzio.
 
jking katika vipofu na matahira na vihiyo nawe pia unaongoza . Mtu mwenye akili timamu na si mjinga mjinga kama mkwawa na wewe hii haiwezi kua hoja ya kujidai. Ni wazi unajua hamna anachofanya sugu zaidi ya kurukaruka tu. Plz kwa heshima ya wanambeya hoja zisizo na mashiko kumsifu mpuuzi wenu sugu mkome. Hizi ndo siasa mtelezo sasa
Great thinkers wa mwaka 2013 mood itabidi itabidi aandae jopo kwa ajili ya kuchuja aina ya pumba zinazochangiwa humu. We badala ya kwenda madarasa ya jioni ukajiongezee ufahamu na maarifa ya maisha unashinda jf wakati sio dozi yako, unapoteza muda wako muhimu kwa ushabiki usiokusaidia chochote.
 
Mmm !!!! Mbeya yataka moyo usanii mwanzo mwisho !! mbaya zaid mpaka kwa watu wasomi tunaowategemea siasa imewachakachua kiasi kwamba wanacheza ngoma kama vipofu!!! ukifika mahali unabeza kazi na juhudi za wazi zilizofanywa na hata kufikia kuzichakachua kuwa ni kazi za sugu tumekwisha kwani "FELIX MWAKYEMBE NI MWALIMU WANGU" Namkubali sana ila kwa hii article ni shaka kwani anafahamu vizuri miradi hii??? na ni baadhi ya miradi ikiwepo ya hostel za jiji, soko (mwanjelwa) office ya jiji, na shule mbalimbali za kata zipatazo 28 na dispensary, zimetokana na watu kuandika paper zao na kushawishi kwa kwenda mbele kupata fedha hizo ili miradi iende, Mh wangu Sugu kwa mbeya anatakiwa kutuliza kichwa ili aweze kuja na legacy ya kwake badala ya kumdanganya kwa kazi za wenzake aonekane anaperform, kiufupi labda mwakyembe angeniambia kuzagaa kwa wamachinga na uchafu kukithiri ni juhudi za viongozi wa awamu hii ningeweza kukubaliana naye.


Mkuu Mbugi,

Sidhani kama umemtendea haki mwandishi wa makala hii, unayedai ni mwalimu wako. Nilivyomuelewa, yeye katujuza jambo la maendeleo linaloendelea hapo Mbeya, na sijasoma popote pale alipohusisha mradi huo na Sugu, kazi hiyo kaifanya mleta huu uzi.
 
Nakubaliana nawe, hii miradi ilibuniwa katika kipindi cha mwaka 2004/05 na utekelezaji wake ulikuwa uanze 2010 kwa Mbeya lakini mienzi ya kuanza kwa Mbeya haikuwa muafaka ilikuwa kipindi cha mvua ndipo imeanza mwaka jana. Sugu hana mchango wowote kwenye hiyo miradi na wala sio ya kisiasa, ilibuniwa na wakurugenzi na timu zao za wataalamu na ipo kwenye majiji na manispaa kadhaa hapa nchini.

Ufanisi unaonekana hivi sasa katika Jiji la Mbeya umetokana na Mkurugenzi aliyepo, ana misimamo na hayumbishwi na wanasiasa, amedhibiti wizi wa fedha za jiji kiasi cha kundiwa mikakati ya kumg'oa. Msimamo wa RC Kandoro na PM ndio kikwazo cha mikakati ya Meya wa jiji hilo na wafuasi wake wakiwemo wakuu wa idara waliotesha mizizi yao hapo, mikakati yenye lengo la kumg'oa.

Hizo barabara kwa kiwango kikubwa zimefanikishwa na misimamo ya Mkurugenzi huyo baada ya kuwawekea ngumu Meya na timu yake waliokuwa wakilazimisha 10pc.

Mkurugenzi habagui chama, husikiliza kila mtu na kutokana na uwezo wa kujenga hoja wa madiwani wa CDM mara nyngi amekubaliana na mawazo/hoja zao, but sio Sugu.

Kuna watu hapa wanalazimisha kumnyanyua Sugu, hapana kama ni utendaji basi ni madiwani wa chadema Mbeya, hawa wameonyesha ukomavu mkubwa wa kisiasa tofauti na Mbunge, na mchango wao kwenye Baraza la Madiwani tunauona na unakubalika na viongozi wengi hapa mkoani.

Msaidieni Sugu kwa kumweleza ukweli badala ya kumpatia sifa asizostahili.

Kuhusu ubora, wengine sio wataalamu, bali tunaangali tu kwa macho, kwa ile ya Airport iliyokamilika naiona iko katika kiwango kizuri, ila suala la mifereji ni lamsingi sana kwa Mbeya, ni kweli maji hayana kwa kwenda kwani mifereji ya tangu mkoloni na ile ya miaka ya 70 iliyotengezwa kuelekeza maji kwenye mito imeziba yote.
Mkuu heshima kwako, napenda kujadili mambo kwa utambuzi na uthibitisho. Kwa jinsi ulivyosema katika post yako.
Umeongea vyema kuhusu kwamba wengine sio wataalam, hiyo ni sahihi ila naamini hata katika hicho kiwango chako cha kutumia macho unaweza kugundua baadhi ya makosa ya wazi mwanzo wa barabara mpya ilipoungana na ile inayotoka Mafiat ni dhahiri kwamba hata kwa macho unaweza kugundua nilichosema.
Labda tu endapo watasema kwamba kutakuwa na layer nyingine ya lami vinginevyo tumeliwa!
 
wewe unajua sifa zinazoufanya mji kuwa jiji......nilichotolea maoni ni ulinganishi wako wa kutaka Mbeya iwe kama Moshi au Tanga......sijasema kusiwepo na mipango miji,la hasha.....nilichotaka kusema ni kwa nini mbeya iko hivyo.....hatuwezi kulazimisha dar wajenge juu kama Mwanza wakati hakuna vilima.
 
Naogopa kutukana siku ya leo, kwani ukianza na tusi utamaliza kwa matusi acha tu nikuache ila nikueleweshe.
Mimi nimekaa mza miaka zaidi ya 18 na mbeya naijua kama kiganja changu! Haya kama hapo si mbeya, mwanza ni sehemu gani? Hapo ni mbeya kwenye round about ya kwenda Hospital ya mkoa na ile ya kuelekea ofisi za jiji (Halmashauri) na barabara nyingine ndiyo hiyo unayoingilia kama unatokea Mafiati au CRDB.
Kamongo we.

Mkuu, hata mimi nilikua nashangaa, Mwanza ya wapi hii, imebidi nirudi tena kwenye hiyo picha ambayo watu wanaifananisha na Mwanza, ni kweli hiyo Keep left ukiitazama kwa haraka unaweza sema ni ya Mwanza, kwa wenyeji wa Mwanza, hapo kwenye hiyo Keep Left kuna Samaki aina ya Sato anatoa maji, hapa haonekani, watu wengine bana kwa ubishi! Watu wakubali tu kwamba huyo wanaemwita muhuni ndio kasimamia mipango ambayo iliwekwa tokea enzi na enzi na ikashindikana kwa wengine, lakini yeye nadani ya miaka 2 kitu kimeeleweka, wakimwita Mwanamuziki ni muhuni, basi hata rais Kikwete anapoendaga kwenye misiba hua anahudhuria misiba ya wahuni!
 
Tuache unafiki na ukada kama kuna mabadiliko yaliyotokea ni jambo la Kumpongeza SUGU na pia kama kama kuna Changamoto pia hatuna budi kumweleza azifanyie kazi. Maendeleo ya Tanzania yataletwa na Watanzania wote sio wabunge peke yao. Tuwe na kitu kitu ambacho kinaitwa utaifa kwanza kwa Sababu Sugu ndo mbunge kwa sasa tumpe support ya kutosha katika kuzipunguza hizo changamoto. Kamam kuchangia Bungeni kachangia vya kutosha ila serikali ndo haitmizi matakwa ya Bunge. Kwa stile hii hata akiwa Prof hawezi kuleta maendeleo peke yake bila jamii nzima kubadilika na kuweka utaifa kwanza
 
labda alichofanya nikujenga nyumba yake kule isesye na kuhama nyumba ya kupanga.... Hongera kwa hilo mzee! barabara ziko kwenye miradi ya WB kitambo tu......!
 
mwanza hakuna keep left moja kama ulivyokariri nitakuletea picha baadaye
 
Nitakuwa napoteza muda nisipokuonea huruma! kwani naamini kwa haki ya mungu sio tatizo lako ila upeo ulionao, pole sana na mungu akubariki na akuongezee upeo ili angalau uweze kuwa na upeo wa kawaida tunaojivunia wenzio.
Ni kweli kabisa mkuu sina upeo Kama viongozi wako wa ccm kwi! Kwi! Kwi! Kwi! Teh! Teh!
 
Kitu anachoweza kufanya msanii wenu ni kupiga miluzi tu, katurudisha nyuma maendeleo Mbeya mjini miaka mitano mizima!
Mtoa posti hapo kama huelewi kuwa hilo la machinga ni tatizo kubwa basi inaelekea umetoka kijijini jana, una uzoefu tu wa kuuza mazao kando kando ya barabara.
Sasa mnakuja mitandaoni kumtetea wakati muda umesha kwisha, 2015 Sugu kwishney!



[FONT=Arial, Tahoma, Helvetica, FreeSans, sans-serif][/FONT][h=3]Umoja wa wazee wastaafu wamtembelea Mbunge...[/h]

..Mbunge wa Mbeya-Mjini akiongea na M/kiti na Katibu wa Umoja wa Wazee Wastaafu wa Mbeya, walipomtembelea nyumbani kwake ...Umoja huu wa wazee wastaafu unatarajia kufanya mkutano wao mkuu wa kwanza jmosi hii mjini Mbeya...


 
Nakubaliana kwa asilimia mia moja na observeration hii ya huyu mkuu.

Sugu hana lolote wala chochote, uwezo wake wa kufikiri hauna tofauti na wamachinga wa ple Mwanjelwa.

Maendeleo sio populist cult, tunataka mikakati ya klifanya jiji la Mbeya kuwa jiji la kisasa. A siyo uwezo wa mtu kurap na kuuza mitumba barabarani.

Majiji ya watu makini kama Arusha na Mwanza yamebadilika na sisi tunayaona katika mika 10 iliyopita.

Ukiweka mbunge au muwakilishi aliye na upeo wa kufikiri sawa sawa n mtu anayeuza ndizi, viazi, mitumba barabarani tusitegemee makubwa kwa maana ya maendeleo.


Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ ameonesha falsafa ya kuongoza kwa vitendo baada ya kutoa msaada utakaowezesha kujengwa kwa daraja kwenye Kata ya Itende.
sugu%20daraja.jpg


Wananchi wa Itende, walimlilia Sugu kuwa daraja hilo limekuwa kikwazo kwa maendeleo yao, pia linahatarisha maisha ya watu ambao huvuka kila siku.
Daraja hilo, limewekwa miti juu, hivyo kuhatarisha maisha ya watu wanaopita, wakilitumia daraja hilo kama njia yao kuu.
Sugu, aliwatembelea wananchi wa Itende na kutoa fedha taslimu ambazo zitawezesha kujengwa kwa daraja hilo kwa kiwango cha zege.
Hata hivyo, vyanzo vya habari hii havijaweka wazi kiasi ambacho Sugu alikitoa kufanikisha ujenzi huo, isipokuwa vilieleza: “Mheshimiwa Sugu ametoa fedha zote zitakazofanikisha ujenzi wa daraja hilo.”
Baada ya kutoa msaada huo, Sugu aliwataka wananchi wa Itende kushirikiana naye katika kuleta maendeleo Mbeya Mjini.
 
Mwaka 2015 wananchi wa Mbeya Mjini hawatarudi kosa kumpa kura mpiga porojo-SUGU

[h=1]MBUNGE WA MBEYA MJINI JOSEPH MBILINYI (SUGU) AANZA ZIARA YA KUZUNGUKA JIMBONI MWAKE[/h]


Wananchi wa kata wa Ituha wakimsikiliza kwa makini mbunge wao Joseph Mbilinyi (Sugu). Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi akielezea shughuli za utekelezaji ahadi zilizofanyika mpaka kufikia kipindi hiki. Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (katikati), Katibu wa CHADEMA wilaya Criss Mwamasiku (kushoto) na Kamanda Kwame Elly Anangisye (nyuma) wakisikiliza kero na maoni ya wananchi wa kata ya Ituha. Wananchi wa Kata ya Ituha wakimsikiliza Mbunge wao Joseph Mbilinyi (Sugu) katika ziara yake ya kutembelea kata za Mbeya Mjini.

 
Mbunge wa Mbeya mjini amehakikisha na kuonyesha kwa vitendo jinsi maendeleo yanavyotakiwa kusimamiwa na wabunge. Kwa kipindi kifupi alichokaa bungeni Mbeya mjini inawaka waka lami, na miundombinu mingi inatengemaa.

Hongera sana Mbunge nakutakia mwaka 2013 wenye mafanikio makubwa. Wapige bakora kwa vitendo.


Jiji la Mbeya sasa barabara za lami kila kona
Felix Mwakyembe

Mbeya
Toleo la 274
26 Dec 2012


274_mbeya.jpg



  • Wananchi wafarijika, waendelea kuimwagia sifa Serikali ya JK


NDOTO ya wakazi wa Jiji la Mbeya kuona mabadiliko na maboresho muhimu katika sekta ya miundombinu, hatimaye imetimia baada ya kukamilika kwa moja ya barabara zinazoendelea kujengwa hivi sasa jijini humo.
Barabara hiyo muhimu iliyokamilika hivi karibuni, ni ile ya Airport- Samora, inayohudumia wakazi wa eneo la Iyela, au Airport, kama linavyofahamika kwa walio wengi, ambayo imekamilika kwa kiwango cha lami.

Hata hivyo, pamoja na barabara hiyo kukamilika na hivyo kurahisisha mawasiliano ya usafiri baina ya maeneo hayo, hofu iliyowajaa wananchi hao ni juu ya ajali. “Na sisi sasa tumekuwa watu baada ya kuletewa barabara ya lami. Kwa kweli ni kama ninaota vile, itasaidia kusafirisha mazao yetu kutoka mashambani. Sisi ndio tunalisha jiji la Mbeya kwa mboga mboga mboga na matunda,” anasema mkazi wa Swaya baada ya barabara hiyo kuwekwa tabaka la lami Jumamosi ya wiki iliyopita.
Kijiji cha Swaya kipo nje kidogo ya jiji la Mbeya, na ni maarufu kwa kilimo cha mboga mboga, soko lao kuu likiwa katikati ya jiji, na hivyo kwa wananchi wa eneo hilo kwao umuhimu wake ni usafirishaji wa mazao yao kwa urahisi na haraka zaidi.

Mbali ya usafirishaji wa mazao ya chakula kutoka kijiji cha Swaya, kukamilika kwa barabara hiyo ni faraja kubwa kwa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari Samora ambao walikuwa wanalazimika kutembea kwa miguu kwa takriban kilometa mbili kwa siku kutokana na kukosekana kwa usafiri kati ya kituo cha Mafiat na shuleni hapo ambako barabara hiyo mpya inaishia.
Barabara hiyo ya kilometa 1.24, inayojulikana kwa jina la Airport- Samora road, ni sehemu ya barabara zenye urefu wa kilometa 28 zilizomo katika mpango wa ujenzi wa barabara za jiji hilo kwa kiwango cha lami ulioanza Novemba mwaka jana na unatarajiwa kukamilika Juni mwakani.
Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Techniplan SpA- Itali, M. Haq, anasema ameridhika na kiwango cha ubora wa kazi kilichoonyeshwa na kampuni inayojenga barabara hiyo ya CICO China.

Anasema kiwango cha ubora na ufanisi wa kazi walichokionyesha mafundi katika ujenzi wa barabara hiyo kinampa matumaini ya kazi kukamilika kwa wakati uliopangwa na kwa ubora waliokubaliana kwenye mkataba.
Mtazamo wa mtaalamu huyo unafanana na wa wananchi wa jiji la Mbeya ambao walieleza wazi kuridhika kwao na ubora wa barabara hiyo kwa kuiangalia tu, huku baadhi ya wahandisi kutoka miji mbalimbali iliyomo kwenye mradi huo nchini, wakibainisha kuwa kiwango hicho kinathibitisha udhibiti katika zabuni kwa baadhi ya wahusika kujiwekea kamisheni maarufu kama ‘ten percent.’
“Hapa hakuna ‘ten percent,’ ndiyo maana hata Rais wa kampuni amekuja, tena na mke wake, ukijumlisha ‘ten percent’ wanazodaiwa makandarasi, si chini ya asilimia 40 ya malipo yote ya kazi, ndiyo maana hulazimika kuchakachua," anasema Mhandisi mmoja kutoka moja ya majiji ya hapa nchini.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Elimu), Jumanne Sagini, Halmashauri za Majiji yote nchini, Halmashauri za Manispaa saba na Mamlaka ya Makao Makuu Dodoma (CDA), zinanufaika na mpango wa uboreshaji wa miji nchini unaotekelezwa kwa fedha kutoka Benki Kuu ya Dunia (WB).

Kwa mujibu wa Sagini, mpango huo unaogharimu zaidi ya Sh bilioni 200, unahusu ujenzi wa miundombinu ya barabara, masoko, madampo, vituo vya mabasi, mifereji na uboreshaji mazingira. Anasema pamoja na mambo mengine, kwamba utekelezaji wa miradi hiyo inatofautiana kutegemeana na mahitaji ya kila jiji na manispaa.

Barabara hizo ni faraja kubwa kwa wakazi wa Jiji la Mbeya na mkoa huo kwa ujumla, ambapo sasa wanafunga mwaka huu wa 2012 wakiwa na miradi mikubwa mitatu ya kujivunia, kwa maana ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Soko la Mwanjelwa na barabara za lami zinazoendelea kujengwa ndani ya jiji.

Kukamilika kwa barabara hiyo ya Airport-Samora, kunafufua matumaini ya wakazi wa jiji hilo ambao awali walikata tamaa, kiasi kwamba haikuwa ajabu kuwakuta kwenye vijiwe wakihoji uhalali wa mji wao kupewa hadhi ya jiji, sababu kuu ikiwa ni kutoona mambo yakienda vema kama walivyotarajia, na hasa pale walipolinganisha na miaka ya kabla ya kupandishwa hadhi. Ni kwa msingi, baadhi ya wananchi hao katika vijiwe vyao, hawakosi kuimwagia sifa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kwa kazi nzuri za maendeleo inazozitekeleza katika mkoa wa Mbeya, na hasa uboreshaji wa miundombinu ya barabara za jiji hilo.
Uwanja wa Ndege Songwe pamoja na Soko la Mwanjelwa, vinatarajiwa kuzinduliwa wakati wowote kuanzia sasa, wakati ujenzi wa barabara za lami jijini humo utakuwa ukiendelea lakini baadhi yake zitakuwa zimekamilika tayari kufikia Juni mwakani, zikiwa na urefu wa kilometa 28.

Tangu Desemba 13 mwaka huu, Uwanja wa Ndege wa Songwe ulianza kutumika, na kwa mujibu wa Meneja wa Uwanja huo, Valentino Kadeha, kinachosubiriwa ni uzinduzi rasmi tu unaotarajiwa kufanywa na Rais Kikwete.
Hata hivyo, ujenzi ni jambo moja tu katika kuimarisha miundombinu ya barabara jijini humu, la msingi ni utunzaji wake, jambo ambalo kwa uzoefu ni tatizo kubwa sana, si kwa Jiji la Mbeya pekee bali kwa taifa zima.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Juma Iddi, maandalizi yamefanyika kuhusu matunzo ya barabara hizo, ikiwamo kukutana na viongozi wa kata na mitaa na kuwaeleza wajibu wao katika kusimamia matunzo ya barabara hizo, ikiwamo utupaji taka ovyo, ambapo jiji litahakikisha takataka hazikai kwenye ‘maguba’ yaliyoko kwenye barabara, na kwamba hata wananchi nao wameelimishwa tayari.

“Wananchi lazima wafahamu kwamba fedha hizi (zinazotumika kuboresha miundombinu ya jiji la Mbeya) ni mkopo kutoka Benki ya Dunia, kwa hiyo tutakuja kuzilipa,” anasema Iddi.
Katika hili la kutunza miundombinu ya huduma za jamii, Kaimu Katibu Mkuu, Sagini, anazichagiza mamlaka za serikali za mitaa nchini kusimamia sheria ndogo ndogo zilizopo kuhusu usafi wa mazingira ili kulinda barabara nchini ambazo anasema huigharimu nchi fedha nyingi.

Pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara, mpango huo wa uboreshaji Jiji la Mbeya (face lifting) unahusu pia ujezi wa kituo kikuu cha magari ya abiria na mizigo eneo la Nane Nane, taa za barabarani na shimo la takataka (land fill).
Barabara zinazojengwa kwa fedha kutoka Benki ya Dunia zimegawanywa katika awamu mbili. Awamu ya kwanza itahusu kilometa 13.2 kwa barabara inayoanzia Sae kupitia kituo cha umeme cha TANESCO hadi Chuo Kikuu cha Theofilo Kisanji (TEKU) pamoja na barabara ya Airport kupitia Jacaranda hadi kituo cha mafuta cha Bhanji, eneo la Forest.
Barabara nyingine kwenye awamu hiyo ni ile ya Kamishina Road ambayo inanzia kwenye Mnara wa Uhuru kuelekea Weru Garden hadi Uzunguni, barabara ya Block T inayoanzia Kabwe kuelekea Kanisa la KKKT Luanda hadi SIDO na kituo cha mafuta cha Oil Com Soweto, na ile ya kuanzia Sea (TANESCO) hadi Zahanati ya Ituha.

Ujenzi wa barabara hizo utahusu pia mifereji ya maji na madaraja madogo aina ya makarafati, ununuzi wa magari mawili kwa ajili ya usimamizi wa barabara, mtambo mmoja wa kushindilia na mwingine wa kuchota mchanga na mawe unaofahamika zaidi kama kijiko.
Awamu ya pili ya mpango huo itakuwa na kilometa 14.6 na itahusu barabara ya pili eneo la Sokomatola pamoja na kituo chake cha mabasi, barabara inayoanzia CCM Ilomba kuelekea VETA hadi Machinjioni, kabla ya kukutana na ile itokayo Ilemi na kuelekea hadi Makasini eneo la Uyole na barabara ya Hospitali ya Mkoa inayoanzia Ndiyo Mini Super Market.

Nyingine katika awamu hiyo ya pili ni pamoja na ile inayoanzia Forest Mpya ambayo itaungana na ile ya Airport hadi Sae, barabara ya Igawilo inayoanzia barabara kuu ya Mbeya- Tukuyu kuelekea Kituo cha Afya Igawilo hadi Shule ya Sekondari Igawilo.
Ni katika awamu hiyo ya pili, ambapo kitajengwa Kituo Kikuu cha Magari ya Abiria na Mizigo katika eneo la Nane Nane, shimo la taka kwa maana ya dampo litachimbwa, ununuzi wa mizani ya kupimia uzito kwenye shimo la taka, magari matatu ya taka (side loaders), magari manne ya kuzolea taka (skip master), makontena 109 ya kubebea taka (skip bucket) magari matatu madogo na vikusanya taka 200.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, katika fungu la awamu ya pili watapiga pia picha za makazi ya jiji (satellite image) ambayo itasaidia kuboresha mfumo wa ukusanyaji wa kodi ya majengo, na zaidi yatatolewa mafunzo kwa watendaji kuhusu ukusanyaji wa mapato, na kuweka mfumo wa kompyuta wa uendeshaji kazi za halmashauri ya Jiji hilo.
Katika mpango huo kabambe wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara, Jiji la Mbeya halitegemei fedha hizo pekee kutoka Benki ya Dunia, bali litajenga kilometa nane kwa kiwango cha lami likitumia fedha kutoka vyanzo vyake vya mapato.
Barabara hizo ni pamoja na ile ya Kambarage inayoanzia Hospitali ya K’s hadi Hospitali ya Wazazi ya Meta na kituo kidogo cha mabasi cha Meta, barabara ya Maktaba ya Mkoa, barabara zote zinazozunguka City Park, barabara za Sokomatola zikiwamo ya TANU, barabara ya tatu na nne, wageni street na Nonde street, maegesho ya magari mkabala na Hoteli ya Sombrero na eneo ilipokuwa City Pub na vituo vidogo vya mabasi vinane.
Kwa kutumia fedha zake, jiji la Mbeya litajenga kilometa kumi za barabara kwa kiwango cha changarawe ambazo hapo mwakani zitawekwa lami, ambapo zitakuwa ndio mwanzo wa mpango wake endelevu wa kujenga kilometa kumi za barabara kwa kiwango cha lami kila mwaka.

Miongoni mwa kero za muda mrefu katika Jiji la Mbeya, ni pamoja na kukosekana kwa taa za barabarani ambapo pamoja na kelele za muda mrefu za wananchi ziliwekwa kwenye barabara moja tu itokayo Mafiat kuingia katikati ya jiji. Hata hivyo, kero hiyo itabakia kuwa historia, kwa kuwa tayari mradi wa uwekaji taa kwenye barabara kuu ya Tanzania- Zambia umekamilika na taa kuwashwa.


- Saafi sana My Man Sugu, I am down sana great Leader, SALUTE!!

LE MUTUZ
 
Hivi mbunge gani anajenga jimbo lake kwa fedha za kutoka mfukoni mwake? Fedha zote za maendeleo ni ama kutoka kwenye kodi zetu, mikopo au miradi inayofadhiliwa na wageni au wafadhili. Kazi ya Mbunge ni kuhakikisha anasimamia keki yake ipasavyo.

Ndio maana miradi ya jimbo ikiwa tayari imepangiwa fedha halafu haijatizwa ni kazi ya Mbunge kuibana serikali au taasisi yeyote inayoleta masihara. Sugu anaibana serikali kuhakikisha miradi iliyoainishwa kwenye jimbo lake inatekelezwa la sivyo hapakaliki.

Sio miujiza kwamba ni majimbo tu ya wapinzani ndio hizo fedha sijui za world bank, Hazina, mgawo wa taifa ndio zinafika fedha hizo zinakwenda kila kona ya jimbo ya nchi yetu kwa miradi mbalimbali ila wajanja wanaiweka mifukoni ndio maana kuna kina mzee vijisenti. Msisahau umeme wa Richmond ndio unaonunua nyumba za ibada na kuwapeleka watu Monduli kula New year na kwa fedha zao wenyewe huku wakimtukuza mtu.

Tumeshuhudia fedha nyingi za miradi zikipotea na hao mnaoita wafadhili na wb wakilia. Sugu lazima apewe sifa kwani kaonyesha uwezo wa kutetea miradi ya wana-Mbeya kama ni swala sijui la Mpesya ainisheni ni nini alikifanya zaidi ya kuwa vuvuzela.

Angalieni Ubungo fedha ya kusambaza maji imetolewa na tender iko tayari ila inambidi Mnyika apige sana kelele la sivyo maji yanatokea tumbuni kwa Rtz1 au ikulu kwa Salva.

Mbunge anakabidhiwa Jimbo kama lilivyo tunaanza kumhesabia siku ya kwanza akiingia madarakani kila kinachotokea kwenye jimbo lake. Lazima awajibike kwa mambo kutokutendeka na asifiwe na apewa hongera yakitokea. Ndio maana tumezoe kusikia kiongozi atafanya nini ndani ya siku mia. Lazima ujue ni nini kipo mbele yako.

Sugu ameonyesha anaweza mara mia na zaidi. Hongera sana kamanda, wafitini mtaisoma namba ila wana Mbeya wamekubali na tunasema moto chini mpaka mpaka mbeya iwe Dubai. Wakati mnalalamika sisi tunawaletea wananchi maendeleo.

Waambieni wabunge wengine nao wahakikishe ni kiasi gani wametengewa au msaada upo, tunahitaji maendeleo leo. Deni la taifa linalokuwa lazima tujue misaada inakwenda wapi.
 
Sugu ana msimamia nani sasa Tanroads au Makandarasi wanaojenga barabara! Hongera CCM kwa kujenga barabara Jijini Mbeya
 
Mkuu, hata mimi nilikua nashangaa, Mwanza ya wapi hii, imebidi nirudi tena kwenye hiyo picha ambayo watu wanaifananisha na Mwanza, ni kweli hiyo Keep left ukiitazama kwa haraka unaweza sema ni ya Mwanza, kwa wenyeji wa Mwanza, hapo kwenye hiyo Keep Left kuna Samaki aina ya Sato anatoa maji, hapa haonekani, watu wengine bana kwa ubishi! Watu wakubali tu kwamba huyo wanaemwita muhuni ndio kasimamia mipango ambayo iliwekwa tokea enzi na enzi na ikashindikana kwa wengine, lakini yeye nadani ya miaka 2 kitu kimeeleweka, wakimwita Mwanamuziki ni muhuni, basi hata rais Kikwete anapoendaga kwenye misiba hua anahudhuria misiba ya wahuni!


angalia picha hizi za mwanza, keepleft hii ni tofauti na ile unayoisema yenye samaki, hii ilikuwa na sanamu ya baba wa taifa wakaitoa kwa sababu watu wengi walilalamika haifanani naye

mza1.png mza2.png mza3.png
 
Back
Top Bottom