Joseph Mbilinyi (SUGU) MB afanya kweli Mbeya Mjini

Joseph Mbilinyi (SUGU) MB afanya kweli Mbeya Mjini

Hivi mbunge gani anajenga jimbo lake kwa fedha za kutoka mfukoni mwake? Fedha zote za maendeleo ni ama kutoka kwenye kodi zetu, mikopo au miradi inayofadhiliwa na wageni au wafadhili. Kazi ya Mbunge ni kuhakikisha anasimamia keki yake ipasavyo.

Ndio maana miradi ya jimbo ikiwa tayari imepangiwa fedha halafu haijatizwa ni kazi ya Mbunge kuibana serikali au taasisi yeyote inayoleta masihara. Sugu anaibana serikali kuhakikisha miradi iliyoainishwa kwenye jimbo lake inatekelezwa la sivyo hapakaliki.

Sio miujiza kwamba ni majimbo tu ya wapinzani ndio hizo fedha sijui za world bank, Hazina, mgawo wa taifa ndio zinafika fedha hizo zinakwenda kila kona ya jimbo ya nchi yetu kwa miradi mbalimbali ila wajanja wanaiweka mifukoni ndio maana kuna kina mzee vijisenti. Msisahau umeme wa Richmond ndio unaonunua nyumba za ibada na kuwapeleka watu Monduli kula New year na kwa fedha zao wenyewe huku wakimtukuza mtu.

Tumeshuhudia fedha nyingi za miradi zikipotea na hao mnaoita wafadhili na wb wakilia. Sugu lazima apewe sifa kwani kaonyesha uwezo wa kutetea miradi ya wana-Mbeya kama ni swala sijui la Mpesya ainisheni ni nini alikifanya zaidi ya kuwa vuvuzela.

Angalieni Ubungo fedha ya kusambaza maji imetolewa na tender iko tayari ila inambidi Mnyika apige sana kelele la sivyo maji yanatokea tumbuni kwa Rtz1 au ikulu kwa Salva.

Mbunge anakabidhiwa Jimbo kama lilivyo tunaanza kumhesabia siku ya kwanza akiingia madarakani kila kinachotokea kwenye jimbo lake. Lazima awajibike kwa mambo kutokutendeka na asifiwe na apewa hongera yakitokea. Ndio maana tumezoe kusikia kiongozi atafanya nini ndani ya siku mia. Lazima ujue ni nini kipo mbele yako.

Sugu ameonyesha anaweza mara mia na zaidi. Hongera sana kamanda, wafitini mtaisoma namba ila wana Mbeya wamekubali na tunasema moto chini mpaka mpaka mbeya iwe Dubai. Wakati mnalalamika sisi tunawaletea wananchi maendeleo.

Waambieni wabunge wengine nao wahakikishe ni kiasi gani wametengewa au msaada upo, tunahitaji maendeleo leo. Deni la taifa linalokuwa lazima tujue misaada inakwenda wapi.

Mkuu dont oversimplify mambo , na hakuna kiongozi wa kisiasa duniani aliyejenga miundombinu toka mfukoni kwake.

Hivyo nakushauri umjenge tu kama unavodhamiria nd Sugu na mimi si mmoja wa kumtaka alete mshahara wake kujenga miundo mbinu, thats too shallow.

Ninachomlaumu Sugu na viongozi wenzake Mbeya ni lack of vision of the future city.
Matatizo tunayoyaona leo ni lack of planning hiyo hiyo na ndio maana kuna viongozi, tena wakubwa tu wanadiriki kuita jiji la Mbeya kijiji kikubwa.

Hivi tuahitaji wafadhili kutengeza Master Plan?
Tunahitaji mfadhili kutuambia nyumba za TOPE doesent comprise to make a city?
Tunahitaji mfadhili kututolea kutuondolea machinga barabarani?
Tunahitaji mfadhili kutengeneza traffic control na separation kwa local na international traffic?

Na hapo ndio nasema kama haya hayawezi kutatuliwa uwakilishi wa kishkaji kama wa Sugu na viongozi wengine jijini Mbeya ni wa ubabaishaji.

Inabidi tujiulize kama Mwanza, Moshi,Arusha wameweza kwa kutumia utaalam uliopo nchini, Mbeya wanashindwa nini?

Kama mkazi na mwenyeji wa Mbeya nitaendelea kulaumu miango na ushabiki usio na tija ili ingalau Mbeya ibadilike.
 
''unajuwa watu wengi hawajajua
huwezi kuzuia mvua
sugu ni kama mvua,
nikitaka kunyesha, nanyesha''

lyrics zake tu ni inatosha kusema amefanya kweli, anafanya kweli na atafanya kweli

  • moto chini
  • mikononi mwa polisi
  • miaka chini ya 18
  • sugu
  • anti virus ......

unaleta nukuu za bangi?????? bangi ni bangi tuuu nandio maana anaungwa mkono na wavuta bangi wenzake
 
Naogopa kutukana siku ya leo, kwani ukianza na tusi utamaliza kwa matusi acha tu nikuache ila nikueleweshe.
Mimi nimekaa mza miaka zaidi ya 18 na mbeya naijua kama kiganja changu! Haya kama hapo si mbeya, mwanza ni sehemu gani? Hapo ni mbeya kwenye round about ya kwenda Hospital ya mkoa na ile ya kuelekea ofisi za jiji (Halmashauri) na barabara nyingine ndiyo hiyo unayoingilia kama unatokea Mafiati au CRDB.
Kamongo we.
wakati mwingine usibishane na washamba maana bora kukosa elimu kuliko ushamba.
 
Mkuu dont oversimplify mambo , na hakuna kiongozi wa kisiasa duniani aliyejenga miundombinu toka mfukoni kwake.

Hivyo nakushauri umjenge tu kama unavodhamiria nd Sugu na mimi si mmoja wa kumtaka alete mshahara wake kujenga miundo mbinu, thats too shallow.

Ninachomlaumu Sugu na viongozi wenzake Mbeya ni lack of vision of the future city.
Matatizo tunayoyaona leo ni lack of planning hiyo hiyo na ndio maana kuna viongozi, tena wakubwa tu wanadiriki kuita jiji la Mbeya kijiji kikubwa.

Hivi tuahitaji wafadhili kutengeza Master Plan?
Tunahitaji mfadhili kutuambia nyumba za TOPE doesent comprise to make a city?
Tunahitaji mfadhili kututolea kutuondolea machinga barabarani?
Tunahitaji mfadhili kutengeneza traffic control na separation kwa local na international traffic?

Na hapo ndio nasema kama haya hayawezi kutatuliwa uwakilishi wa kishkaji kama wa Sugu na viongozi wengine jijini Mbeya ni wa ubabaishaji.

Inabidi tujiulize kama Mwanza, Moshi,Arusha wameweza kwa kutumia utaalam uliopo nchini, Mbeya wanashindwa nini?

Kama mkazi na mwenyeji wa Mbeya nitaendelea kulaumu miango na ushabiki usio na tija ili ingalau Mbeya ibadilike.

Mbona Karoleni pana nyumba za tope za kutosha mkuu.
 
Back
Top Bottom