Joseph Kusaga asema tuache malumbano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Joseph Kusaga asema tuache malumbano

Discussion in 'Celebrities Forum' started by figganigga, Nov 30, 2011.

 1. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,624
  Trophy Points: 280
  Mkurugenzi mtendaji wa Clouds Media bwana Joseph Kusaga kasema yeye ndo kawezesha vijana wengi wawe hapo walipo, so kashauli tuache malumbano tuchape kazi. amesema hayo katika pongezi za miaka 50 ya uhuru.

  MY TAKE:
  Yeye kwa mawazo yake anaona vijana wana hali nzuri ya maisha hasa wasanii. Kweli aliye shiba hamuoni mwenye njaa. Je anastahili kupongezwa?.
  Mia
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh anaongea ki neutral neutral
   
 3. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,811
  Likes Received: 36,886
  Trophy Points: 280
  mwambie kusaga asome hii hotuba hasa kwenye red:
  [​IMG]

  [h=3]HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI MHE. JOSEPH MBILINYI, (MB) WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO, KUHUSU MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2011/2012
  [/h]
  SEKTA YA SANAA
  Mheshimiwa Spika, nianze na sekta ya Sanaa. Na hapa natangaza maslahi, kuwa mimi ni msanii wa muziki wa kizazi kipya (Bongofleva) na nimekuwa kwenye fani hii kwa muda mrefu sasa. Kwa uzoefu wangu na kwa niaba ya Kambi rasmi ya Upinzani, nachukua fursa hii kuieleza serikali kwamba; "Sanaa si mapambo au burudani tu kama ilivyozoeleka, bali Sanaa ni ajira inayoweza kubadilisha maisha ya Mtanzania yeyote anayejihusisha nayo na inaweza kabisa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya mapato ya Bajeti ya Serikali, ikiwa Serikali yenyewe, itadhamiria kwa dhati kufanya mapinduzi makubwa katika tasnia hii".
  Mheshimiwa Spika, Ripoti moja nchini Marekani ya mwaka 2007 ilisema, nanukuu; "Makampuni yanayotengeneza na kuuza kazi za hatimiliki yataendelea kuwa moja ya nguvu kubwa za uchumi wa Marekani, kwani mapato yatokanayo na filamu, muziki, michezo ya video, na mifumo ya kompyuta yanachangia zaidi ya asilimia kubwa ya Pato la Taifa na kuajiri takribani watu milioni 5.4…" mwisho wa kunukuu.
  Mheshimiwa Spika, ni dhahiri kuwa sekta ya Sanaa ikifanyiwa mapinduzi makubwa inaweza kabisa kuwa moja ya vyanzo vikubwa vya bajeti ya Serikali yetu na kuchangia maendeleo ya taifa hili. Ikiwa Sanaa inachangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa kubwa kama Marekani; Je, Tanzania tuna maendeleo gani ya kujivunia hata tupuuze Sanaa? Bado hatujaipa sekta hii umuhimu wake unaostahili;
  Matokeo yake Mheshimiwa Spika, Wasanii pamoja na Serikali bila kujua, wamekuwa wakinyonywa kimapato na Wadhamini, Wazalishaji, na Wasambazaji wa kazi za Sanaa, hususan kwenye biashara ya kuuza muziki na filamu. Kwa mujibu wa utafiti wa Dkt. Jehovaness Aikaeli ambaye ni mchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema sekta ya muziki pekee ikifanyiwa maboresho, inaweza kuiingizia Serikali mapato ya kodi ya wastani wa shilingi bilioni 50 kwa mwaka.
  Mheshimiwa Spika, tafiti chache zilizowahi kufanyika, ukiwemo utafiti wa Taasisi ya RULU/BEST – AC, wa mwaka 2007/08, zimeonyesha kuwa Wasanii na Serikali kwa pamoja, wamekuwa wakipoteza mapato mengi yatokanayo na biashara ya kazi za sanaa, hususan muziki na filamu kama ifuatavyo;
  · Maharamia wameendelea kurudufisha santuri na kanda za muziki, filamu na kazi nyingine za sanaa, na kujipatia mapato haramu kwa jasho la Wasanii, lakini hakuna hatua kali zinazochukuliwa kukomesha hali hii.
  · Wasanii wengi wamekuwa wakiingia mikataba isiyo na manufaa kwao baina yao na Wadhamini, Wazalishaji, Wasambazaji wa kazi za Sanaa na hivyo kunyonywa kimapato, kwa sababu tu ya kukosa uelewa mzuri wa masuala ya mikataba na kutokuwepo udhibiti wa kutosha wa Serikali.
  · Serikali kwa mwaka 2007 pekee, ilipoteza mapato ya muziki, ya jumla ya shilingi bilioni 71 sawa na asilimia 0.5 ya Pato la Taifa.
  · Kodi inayokusanywa na Serikali katika Sekta ya Muziki, inapatikana katika asilimia 12 tu ya kiwango cha mapato kinachotakiwa kulipiwa kodi kwenye sekta hiyo.
  · Hasara inayotokana na ulipaji mdogo wa kodi kwa taifa kwenye sekta ya muziki pekee, inakadiriwa kuwa sawa na asilimia 0.1 ya Pato la Taifa na hasara hiyo ilitegemewa kuongezeka kwa kasi katika kipindi cha miaka mitatu kuanzia mwaka 2007.
  · Wakati wa utafiti iligundulika kuwa ni asilimia 12.5 tu ya Wafanyabiashara wa kazi za Sanaa, ndio waliokuwa wamelipa mirabaha, asilimia 87.5 hawakuwa wamelipa.
  Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na wizi na uharamia huu wa kazi za Sanaa na kuokoa mapato ya Wasanii na ya Serikali, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza yafuatayo;
  COSOTA iwe Mamlaka
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na.7 ya mwaka 1999 ifanyiwe marekebisho kwa lengo la kuipa meno zaidi ya kulinda haki na kuhakikisha Wasanii wananufaika na kazi zao. Jedwali zima lenye marekebisho yanayopendekezwa katika sheria hiyo, limo katika Kiambatanisho Na. 1 cha hotuba hii. Moja ya mapendekezo yaliyomo kwenye kiambatanisho hicho, yanalenga kuifanya COSOTA kuwa chombo chenye nguvu zaidi katika kulinda kazi za Wasanii kuliko ilivyo hivi sasa.
  Mheshimiwa Spika, kwa hiyo katika sehemu ya marekebisho tunayopendekeza, Kambi rasmi ya Upinzani tunataka Sura Na. 218 ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, ifanyiwe marekebisho ili kuunda Mamlaka ya Hakimiliki Tanzania (COPYRIGHT REGULATORY AUTHORITY OF TANZANIA (CORATA) badala ya kuiacha COSOTA kama ilivyo hivi sasa. Mamlaka haya yakishaundwa yatakuwa na nguvu zaidi ya kushughulikia mambo mbalimbali ya kazi za wasanii,yawe ndio msimamizi na mratibu wa masuala ya Hakimiliki kwa kushirikiana na vyama vya msingi vya wasanii vilivyopo chini ya BASATA,kama vile Chama Cha Muziki Wa Dansi Tanzania(CHAMUDATA) na kile cha wasanii wa muziki wa kizazi kipya yaani Tanzania Urban Music Association (T.U.M.A), tofauti na sasa ambapo COSOTA imebakiwa na kazi ya kusajili kazi za wasanii na kukosa nguvu ya kuzilinda.
  Mheshimiwa Spika, pamoja na kuwa mwenye Hakimiliki ana jukumu la kulinda haki zake kwa kwenda mahakamani pale anapoona haki yake imepokwa na mtu au kikundi chochote, bado ipo haja ya kuhakikisha kuwa Polisi wetu wa upelelezi wanahusika moja kwa moja katika kulinda haki za Wasanii.
  Mathalan, nchini Marekani hawana polisi wa kulinda hakimiliki moja kwa moja, lakini Shirika lao la Upelelezi (FBI), limekuwa likifanya uchunguzi wa mara kwa mara kuhusu hakimiliki za wasanii, kila kunaporipotiwa suala la wizi wa kazi za msanii, na limekuwa linahusika moja kwa moja katika kutoa ushahidi na kusaidia kupatikana kwa haki ya msanii husika.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza kuwa taasisi za Serikali: Polisi na Forodha washirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Hakimiliki na Hakishiriki tunayotaka ianzishwe (CORATA), kukomesha uharamia wa kazi za Sanaa. Jeshi la Polisi liunde kitengo cha kukabiliana na wasiotekeleza sheria ya hakimiliki. Forodha watengeneze utaratibu wa kutoza kodi kikamilifu kwenye kazi za muziki, filamu na Sanaa nyingine zote zinazouzwa nje ya nchi. Na mashirika ya uzalishaji wa kazi za muziki –waunde ushirikiano na taratibu zao za kukabiliana na uharamia wa kazi za sanaa kwa mapana yake.
  Mheshimiwa Spika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari mwaka huu, wakati akizindua kampeni ya kuzuia malaria ambayo iliwashirikisha baadhi ya wasanii, aliahidi kuundwa kikosi kazi (task force) kitakachowashirikisha COSOTA, Polisi, Tume ya ushindani, TRA, BRELA, Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na wasanii mbalimbali wanaojihusisha na sanaa ili kutafuta ufumbuzi dhidi ya uharamia na wizi wa kazi za Sanaa.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka wizara kuliarifu Bunge hili, je kikosi kazi hicho kiko wapi mpaka leo? Na kama kiliundwa, kiliundwa kwa taratibu zipi, na kwanini suala hilo haliko wazi?
  Mradi wa Stickers kwenye kazi za Sanaa
  Mheshimiwa Spika, mbali na marekebisho hayo ya kisheria na kimfumo tuliyopendekeza, Kambi rasmi ya Upinzani pia tunaitaka Serikali ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012, itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kuanzisha utaratibu rasmi wa kuwa na Stickers kwa ajili ya kazi zote za Sanaa, hususan kwenye kanda na Santuri za muziki, filamu, na kazi zote za Sanaa zinazoshikika na kuuzika. Hapa tunashauri kuwa mamlaka tunayotaka ianzishwe, yaani COPYRIGHT REGULATORY AUTHORITY OF TANZANIA) ishirikiane kwa karibu na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kuandaa utaratibu mzima wa kuwa na Stickers hizo na jinsi ya kuusimamia.Na sio kuwaachia tena watu binafsi kusimamia hili.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inaamini kuwa utaratibu rasmi wa kuwa na Stickers ukitumika sekta ya Biashara ya Kazi za Sanaa inaweza kupata mafanikio ya kuridhisha ndani ya muda mfupi. Mfano mzuri ni Sticker yenye nembo ya TRA inayowekwa kwenye bidhaa za Konyagi. Faida kubwa ambayo itapatikana kwa kuwa na Stickers za TRA kwenye kazi za Sanaa ni kuwa stickers hizi zitawezesha kubaini kazi halisi (Original) iliyofanywa na msanii mhusika dhidi ya kazi za bandia zilizorudufishwa au kughushiwa.
  Sambamba na hilo ni kwamba mapato ya Wanamuziki, Watunzi wa filamu na washirika wao pamoja na Serikali yataongezeka na hivyo mchango halisi ya sekta hii kwenye uchumi wa nchi utakuwa wazi.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani inatambua kuwa baadhi ya makampuni ya usambazaji na utangazaji wa kazi za Sanaa, yamekuwa yakijiwekea yenyewe Stickers kwenye kazi zao za Sanaa, lakini bado Stickers hizo hazijaweza kuwasaidia vya kutosha katika kulinda kazi hizo, kwani bado umma hauna taarifa za kutosha, na mbaya zaidi Stickers zenyewe zimekuwa zikighushiwa hivyo kutotoa msaada unaotakiwa.
  Kwa kutilia maanan hilo, Kambi rasmi ya Upinzani inasisitiza kuwa ni muhimu sana utaratibu wa kuwa na Stickers rasmi za kiserikali kwa kazi zote za Sanaa, ukaanzishwa mara moja ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012, ili kuokoa mapato ya Wasanii na mapato ya kodi ya Serikali yanayopotea kwenye sekta hii ya sanaa.
  Mheshimiwa Spika, pia tuna taarifa kuwa Wasanii wengi kutoka nje ya nchi wanaofanya maonyesho mbalimbali hapa nchini wamekuwa hawatozwi kodi licha ya kulipwa fedha nyingi. Kwa hiyo, tunaitaka Serikali kuanzia mwaka wa fedha wa 2011/2012, ihakikishe kuwa Wasanii hao wa nje ya nchi ambao wamekuwa wakilipwa dola laki 1hadi dola laki 4 kwa onyesho moja hapa nchini, wawe wanatozwa kodi ya kutosha, ili fedha hizo ziongezee bajeti kuu ya Serikali na kuwasaidia Watanzania wengi maskini.
  Mheshimiwa Spika, tunaitaka Serikali kwa kushirikiana na vyombo husika, iweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa pale Msanii wa ndani anapofanya onyesho au kazi ya pamoja na Msanii kutoka nje, basi kuwe na mgawanyo mzuri na wa haki wa mapato kati ya Msanii huyo wa Nje na Msanii Mzawa. Pendekezo hili linazingatia ukweli kuwa kwenye maonyesho ya muziki yanayofanywa kwa kuwashirikisha kwa pamoja Wasanii wa Nje na wale wa Ndani, wa Nje wamekuwa wakilipwa fedha nyingi sana kuliko wale wa ndani, licha ya kuwa kazi iliyofanywa ni moja na wote wameingiza mapato.
  Mheshimiwa Spika, ili kuboresha Sekta nzima ya Sanaa nchini, na kuhakikisha inaongeza ajira zenye tija, na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji uchumi, Kambi rasmi ya Upinzani inapendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe;
  · Serikali ndani ya mwaka wa fedha wa 2011/2012,pamoja na kufanyia kazi tafiti zilizokwishafanywa na wadau mbalimbali wa sanaa, ifanye utafiti mahsusi na wa kina kuhusu Sekta nzima ya Sanaa (Feasibility Study), ili kubaini fursa na vikwazo vyote vilivyopo, na kuainisha njia na mikakati kabambe ya kuboresha na kuisimamia sekta husika, kwa manufaa ya Wasanii na uchumi wa nchi.
  · Kupitia matokeo ya utafiti huo, Wizara ndani ya mwaka wa fedha 2011/2012, iandae Mpango mahsusi wa Maboresho ya Sekta ya Sanaa, ambao pamoja na mambo mengine, ulenge kuziba mianya yote ya upotevu wa mapato ya Sanaa na kuchochea ajira nyingi na zenye tija kwa vijana.
  · Chuo Kikuu cha Sanaa cha Bagamoyo kipandishwe hadhi na kuwa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Kawawa cha Bagamoyo (Kawawa Memorial University – Bagamoyo). Lengo liwe ni kuhakikisha kuwa chuo hiki kinatoa mafunzo yote ya hali ya juu ya mambo ya sanaa, michezo na utamaduni kwa vijana wa Kitanzania na wale wanaotoka ng'ambo, huku tukimuenzi Hayati Mzee Rashid Mfaume Kawawa, kwa mchango wake mkubwa katika taifa hili alioutoa kwenye uongozi na Sanaa.
  · Serikali ihakikishe kuwa asilimia 90 ya bajeti zote za Wizara, Idara, Taasisi na Wakala wa Serikali zinazotengwa kwa ajili ya kunaksisha ofisi, iwe inatumia kazi za sanaa na samani zinazopatikana hapa Tanzania au zinazotokana na ubunifu wa Watanzania. Hii itachochea ajira katika kazi za Sanaa na kuweka ushindani wa kibiashara ambao utainua ubora wa kazi hizo.
  · Masomo ya Sanaa yarudishwe katika ngazi zote za elimu katika shule za binafsi na serikali, ili kuchochea ubunifu na umahiri wa vijana katika kazi za sanaa na kuinua vipaji vyao mbalimbali.
  · Serikali ihakikishe mafunzo ya Sanaa yanatolewa kwa vyuo vya elimu ili kuweza kupata walimu wa kutosha wa sekta hii.
  · Mashindano ya ubunifu wa kazi za Sanaa yaanzishwe yakiwa ni sehemu ya mashindano ya michezo ya UMISHUMTA na UMISETA.
  Kashfa ya Nyumba ya Sanaa
  Mheshimiwa Spika, Nyumba ya Sanaa ilianzishwa mnamo 1972 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya Sanaa kwa vijana, wanawake na wasiojiweza pamoja na kutafuta masoko ya Sanaa na kazi za mikono. Hata hivyo, kuanzia mwaka 1995 kumekuwepo hali ya kutoelewana baina ya wajumbe wa Bodi ya wadhamini baada ya kutiliana shaka wenyewe kwa wenyewe, pia kati ya Bodi ya Wadhamini na Wanachama waanzilishi wa Nyumba ya Sanaa.
  Mheshimiwa Spika, matokeo ya hali hiyo ni kufunguliwa kwa kesi mahakamani. Katika kesi hiyo, iliyotolewa hukumu tarehe 24 Februari, 2005, Msajili aliamua kufuta rasmi usajili wa Bodi ya Wadhamini ya Nyumba ya Sanaa akiwataka wakabidhi mali na shughuli za NYUMBA kwa asasi mbadala. Uchunguzi uliofanywa na Kambi rasmi ya Upinzani umebaini kuwa tangu kutolewa kwa hukumu hiyo, Bodi haijawahi kukasimisha amali na majukumu ya Nyumba ya Sanaa kwa asasi mbadala, na badala yake imeendelea kuwepo na kupelekea Nyumba hiyo kuendeshwa kama kampuni binafsi kwa faida ya wajumbe wachache wa Bodi.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani ina taarifa kuwa Mwenyekiti wa Bodi hiyo iliyofutwa na baadhi ya wajumbe wake wameleta mwekezaji ambaye wameshaingia naye ubia kimkataba, kwa ajili ya kujenga jengo la ghorofa katika eneo lenye jengo la sasa. Izingatiwe hapa kuwa mwekezaji atapaswa kulivunja au kubadilisha mfumo wa jengo la sasa la Nyumba ya Sanaa, ndipo aweze kujengwa la ghorofa.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani, inaitaka serikali na Bunge lako tukufu lizingatie yafuatayo;
  · Tujue kuwa Nyumba ya Sanaa hivi sasa inawanufaisha wachache ambao si walengwa waliokusudiwa. Tufahamu kwamba wanufaika hawa hawana rekodi ya uwekezaji katika Nyumba ya Sanaa, hivyo wanavuna matunda yaliyopandwa na wengine hasa kupitia ushirikiano mwema baina ya serikali ya Tanzania (kupitia Ikulu), Norway (kupitia shirika la NORAD) na Uholanzi (kupitia shirika la NOVIB).
  · Tutambue kuwa Nyumba ya Sanaa ilikuwa ni mlango wa masoko ya Sanaa na kazi za mikono, hivyo kutokuwepo kwake kunakwamisha juhudi za wazalishaji kazi za sanaa wa Tanzania kuweza kushiriki vyema masoko na hasa soko la pamoja la Afrika Mashariki.
  Mheshimiwa Spika, kwa kuyazingatia yote hayo na kwa manufaa ya wadau wote wa Sanaa na taifa zima kwa ujumla, Kambi rasmi ya Upinzani inaitaka serikali ichukue hatua zifuatazo kuhusiana na Nyumba ya Sanaa:-
  Mheshimiwa Spika, kwanza tunataka Nyumba ya Sanaa irudishwe Serikalini kwa Mdhamini Mkuu wa Serikali ili mchakato wa uanzishwaji wa Bodi huru ya kusimamia malengo yake anuai ufanyike. Uhuishaji wa Nyumba ya Sanaa utachangia sana kuongeza ajira na pato la taifa, hivyo kupunguza tatizo la uzururaji na kilio cha masoko ya kazi za sanaa.
  Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tangu kufutwa kwake mnamo mwaka 2005, Nyumba ya Sanaa imeendelea kufanya biashara pamoja na kuingia mikataba ya biashara mpaka sasa, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka serikali ifanye tathmini na ilipwe kodi kutokana na faida ya biashara zilizoendeshwa mara baada ya kusitishwa uendeshaji wake.
  Mheshimiwa Spika, Kambi rasmi ya Upinzani tunaitaka Serikali isitishe mara moja uvunjwaji wa jengo lililopo sasa, kwani ni utalii na ni alama ya taifa inayoonyesha jinsi serikali za Norway na Tanzania zilivyothamini juhudi za wasanii na wazalishaji kujikwamua kiuchumi na kuchangia pato la Taifa.
  Tunataka Nyumba ya Sanaa ifufuliwe upya bila kubadili malengo yaliyopelekea kujengwa kwake, na badala yake kila kitu kiboreshwe kwa kuheshimu malengo yale yale. Tunaamini Serikali hii inayojiita Serikali sikivu, itaheshimu matakwa ya Watanzania hususan Wasanii ambao pasipo shaka yoyote ile wanataka Nyumba yao irudi kwenye mikono salama kama tulivyopendekeza.
  Ahadi ya Studio ya Wasanii
  Mheshimiwa Spika, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, kupitia Bunge Tukufu la Jamhuri ya Muungano alitangaza kuwa amewapa Wasanii Studio ya kufanyia kazi zao. Hata hivyo, baadaye wananchi na wadau wengi wa sanaa, nikiwemo mimi binafsi, tulishangaa kusikia Studio hiyo wamepewa NGO binafsi ya Tanzania House of Talent (THT)! Pia Rais aliahidi na kutoa nyumba ya Serikali kwa Wasanii ambayo ingetumika kuendeshea Studio husika, lakini nyumba hiyo ya Serikali iliyotolewa na Rais sasa iko chini ya THT na ndio makao ya THT!
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Joseph mtu peace sana ili kuna watu wanamzunguka na kumchafulia Radio wakiwemo rafikize wa karibu.
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,120
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  wanakuita sugu, sugu, sugu, sugu.
   
 7. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
 8. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  he is waving the white flag now!kasurrender huyo...
  what's beef?beef is when you can't sleep at night
  wake up with no appetite so you can't eat....that's beef
   
 9. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  mfa maji haachi kutapatapa.
   
 10. L

  LIALIA Member

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He ( kusaga) initially thought it was going to be a simple game fighting Sugu, Anakuja mwanamuziki wa america anapewa dola laki moja shoo ya lisaa na kabla ya hiyo shoo yake madogo ( wasanii wanaopiganiwa haki zao na sugu ila-waliobado usingizini) wanalipwa shilingi laki moja na wanaperform masaa nane, kudadadeki. Go sugu go, they will soon give up, you the harmer to smash them
   
 11. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naona Ruge sasa kaamua kumpa kazi hando,muda mwingi anatumia kumtukana sugu,nakama wao wanaona hiyo ndio solution waendelee kutukana mwanzo mwisho,vinega nao wataendelea kupambana hadi kieleweke.
   
 12. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama kasaidia vijana wengi kufika hapo walipo mbona karibia 90% ya wasanii ni masikini na wengi wao washatoa vibao vingi na vikatamba? Au anaongelea maendeleo gani? Maana na wengine wanakimbilia kuigiza sasa
   
 13. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,381
  Likes Received: 22,251
  Trophy Points: 280
  anti virus imesha anza ku erase viruses
   
 14. Rural Swagga

  Rural Swagga JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,400
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  hehehe WAFU fm,,,Nimetokea kuichukia sana hii Radio:smash:
   
 15. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuna jamaa yangu yupo Arusha alikuwa anaoa miezi kama miwili hivi iliyopita,huyu jamaa anafahamiana sana na Barnaba wa THT,akampigia simu akamwambia aende akapafomu yeye pamoja na Linah, siku ya harusi yake.Jamaa akawaambia ntawalipia tiketi ya ndege kwenda na kurudi wote wawili,na sehemu ya kufikia gharama zote zitakuwa juu yangu(bwana harusi).

  Barnaba akahoji kuhusu malipo,jamaa akamwambia ntawalipa laki nne(400,000) kila mtu(linah+barnaba)=800,000
  Mje ijumaa jioni mtafanya show jumamosi siku ya harusi jumapili mtaondoka,wakasema aina shida hiyo imekaa fresh.


  Ruge akanasa habari,sijui kutoka wapi,ikabidi ampigie jamaaa wa Arusha(bwana harusi)na kuanza kumuhoji vipi mbona unawachukua vijana wangu bila kunitaarifu maswali mengi,sijui umeelewana nao shilingi ngapi?mara hivi mara vile,Mshikaji ikabidi amwambie ruge kuwa huyo barnaba ni kama family friend kwa hiyo mimi nimemuomba tu aje kwenye harusi yangu na sio kama ntamlipa wala nini,Ruge akazidi kukomaa na mshikaji,mbona nasikia kuna pesa mmeelewana kama laki nne kwa kila mmoja,jamaa akamwambia ndio,Ruge kusikia hivyo akasema sasa sikia utawapa laki mbili mbili tu laki nne zangu,alafu awana aja ya kupanda ndege watakuja kwa basi ijumaa asubuhi.


  Mshikaji akaona ujinga pesa yakwangu alafu unipangie akaamua kuachana nao.

  Huyu ndio ruge banaaa.

  SWAHILI ORIGINAL WORLDWIDE
   
 16. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wafu fm wanatapatapa sana sasa hivi wanatumia muda mwingi sana kuponda show ya vinega iliyofanyika ustawi,badala ya kuendelea na vipindi vyao vya kishoga kama kawaida.


  Leo kundi zima la vinega litakuwa Channel 5 kwenye planet bongo saa 3.30 usiku usikose.
   
 17. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,624
  Trophy Points: 280
  mkuu naomba ufafanuzi.planet bongo itaanza saa tatu kamili au saa tatu na nusu? samahani kwa kukusumbua. mia
   
 18. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,624
  Trophy Points: 280
  hivi si gerard hando kashafukuzwa kwa kashifa ya kumchukua demu wa ruge au ulikuwa uzushi? lakini rughe inabidi awaonee huruma wasanii wetu. aache kuwanyonya. ni hayo tu. mia
   
 19. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Kusaga mmetoka mbali sana,jasho lenu litapotea kwa namna ya kuwashangaza! Acheni siasa,kuweni upande wa wananchi,someni alama ya nyakati.
   
 20. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,676
  Trophy Points: 280
  Kusaga mmetoka mbali sana,jasho lenu litapotea kwa namna ya kuwashangaza! Acheni siasa,kuweni upande wa wananchi,someni alama za nyakati.
   
Loading...