Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 734
Willy Gamba alikuwa kachero wa ukweli hasa kwenye vitabu vya Kikosi cha Kisasi na Njama
Ulikuwa unavutiwa zaidi na yupi kati ya wakali hao?
JORAM KIANGO yupo juu, hasa kitabu chake cha DIMBWI LA DAMU na SAUTI TOKA KUZIMU
Tumerudi toka kuzimu au sauti toka kuzimu ?
Ulikuwa unavutiwa zaidi na yupi kati ya wakali hao?
Joram Kiango malaika wa Shetani..lakini wote kwa ujumla Riwaya zao zilikuwa nzuri sana .
Hivi mbona sasa hazipatikani?anayejua zunzuzwa waoi tafadhari tuwasiliane
Zawadi ya ushindi mtunzi alikuwa nani nimesahau?
Jamani hii thread imenikumbusha mbali sana,nilisoma karibia vya waandishi wote lakini vya Willy Gamba ni funga kazi!!niliwahi pata uvumi kuwa alipigwa stop kuandika vitabu vya namna ile kwani vinaweza kufundisha watu technique za kijasusi na hata ujambazi,don't know kama ni kweli!:confused2:Yaani umenikumbusha mbali sana! Hiyo miaka ya mwanzoni mwa 80, nikiwa sekondari, alikuwa hatumwi mtoto sokoni!!! Mwalimu anaandika notisi ubaoni, mimi ninamsoma Willy Gamba kwenye Kikosi cha Kisasi, Njama,nk, nimekiweka chini ya benchi! Msisimko wa ajabu kama unaangalia sinema vile!
All in all,Ben Mtobwa alikuwa juu zaidi ya Musiba,kuna kile kitabu chake cha "pesa zako zinanuka",kinaelezea jinsi gani mafisadi wanavyoweza kubadilisha moyo wa kijana mpya kwenye ajira mpaka akafanya wanayotaka wao,"zawadi ya ushindi",ambacho kinatumika mpaka mashuleni,Dar es salaam usiku,nyuma ya pazia,tutarudi na roho zetu,mtambo wa mauti,malaika wa shetani,roho ya poka,(rip)ben
sio sauti toka kuzimu ni salamu toka kuzimu.ebana hata mie nampa saluti joram kiyango.JORAM KIANGO yupo juu, hasa kitabu chake cha DIMBWI LA DAMU na SAUTI TOKA KUZIMU
<br />Hakuna sehemu naweza pata softcopy jamani?