Jonas Mkude ameshakula zaidi ya Tsh mil 300 za Yanga mpaka sasa na amecheza mechi 3 tu msimu mzima

mdukuzi

JF-Expert Member
Jan 4, 2014
16,299
36,725
Wachezaji ni kama kausha damu tu, msimu mzima ucheze mechi tatu na uikamue klabu milioni 300 za mshahara, usajiri na bonus, wastani wa milioni 100 kwa kila mechi.

Je, huu ni uungwana?

Kwanini timu zisisajili wachezaji 24 kila mtu acheze kuliko kurundika watumishi hewa vilabuni
 
Jipange uwe mchezaji pia uvune hizo pesa
 
Katika hizo mechi 3 alizocheza ameingizia club Tsh ngapi? Tuanzie hapo kwanza kwenye mapato ili tujue kama club imepata hasara au faida.
 
Huwezi kupata jibu la moja kwa moja maana team ni collective efforts za watu zaidi ya 50 sio kama ngumi au riadha
 
Wachezaji ni kama kausha damu tu, msimu mzima ucheze mechi tatu na uikamue klabu milioni 300 za mshahara, usajiri na bonus, wastani wa milioni 100 kwa kila mechi.

Je, huu ni uungwana?

Kwanini timu zisisajili wachezaji 24 kila mtu acheze kuliko kurundika watumishi hewa vilabuni
Hivi unaijua 300milioni wewe au unaandika hapa JF?
Yaani mchezaji ambaye mkataba wake Simba ulikwisha, umri ukiwa umesogea, hayuko sokoni kugombaniwa na klabu yoyote kubwa, klabu inayomtaka inawezaje kupeleka dau kubwa ili kumchukua?

Mleta mada jiulize hili swali, Mkude kama asingechukuliwa na Yanga ilikuwa aende klabu gani nyingine?
 
Nadhani umesoma heading tu bila content,usajiloi milioni 60,mshahara milioni 10 kila mwezi,kwa miezi 12 inakuwa 120+60=180.
Bonus,Marupurupu NK inafika 300.
Kila mtu na bahati yake,Saido alitemwa Yanga Simba ameshawalia kama milioni 500 ila angalau yeye amechezapo na uzee ule ungejiuliza angeenda wapi maana pake Geita Gold alikuwa amejiegesha ni karibu na kwao,kutoka geita mpaka bujumnura ni masaa 6 tu kwa gari
 
Kwakuwa ni mtanzania mwenzetu acha tu ale angekuwa wa kuja kama Chama ningeumia sana
 
Na anachangia uchumi wa nchi pesa haitiki nje ya nchi maana nusu inarudi TBL kupitia pombe anazolewa,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom