Mkude akaribia kutua Yanga

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,260
15,151
19:27LIGI KUU BARA
Shaffihdauda

Kudai haki yake ya msingi kumesababisha mchango wake ndani ya timu kutothaminika na kutishiwa kutemwa mwishoni mwa msimu huu
Klabu ya Simba ipo kwenye mpango wa kusajili mbadala wa nahodha wao Jonas Mkude, baada ya mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya huku akiutolea maneno ya hovyo viongozi wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal, wamechoshwa na maneno ya mchezaji huyo na sasa wanaona nivyema wakamtafuta mchezaji mwingine ambaye atamudu kwenye nafasi hiyo.

“Tumeanza mipango ya kutafuta mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Mkude, wa nafasi ya kiungo mkabaji kwasababu mchezaji huyo amekuwa na maneno mengi kuliko mchango wake kwenye timu,”amesema Hans Poppe.

Kiongozi huyo amesema mchezaji Mkude anataka kupewa dau kubwa kama ilivyo kwa wachezaji wa kimataifa, lakini kiwango chake ni chakawaida hivyo wanaona nivyema wafanye maamuzi mapema katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

Amesema hadi sasa hakuna mchezaji waliyemlenga lakini wamepanga kumtafuta mchezaji huyo kwenye mataifa ya nje kwakua wanataka mtu mwenye uwezo tofauti kwa ajili ya kuifikisha mbali timu yao hasa ukizingatia wanamatarajio ya kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa siku zijazo.

“Mkude ni mchezaji ambaye tumemkuza wenyewe na tumekabidhi majuku, lakini anajifanya amekuwa na wakati hata asipokuwepo kwenye timu hatupati madhara yoyote,”amesema Hans Poppe.

Yanga yamtema rasmi Mbuyu Twite

Katika siku za karibuni Mkude, aligoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simb, baada ya viongozi wa timu hiyo kumpa kiasi kidogo cha pesa na yeye kutaka kupewa dau la milioni 80 badala ya 50 wanazotaka wao.

Baada ya uongozi kugoma kutoa kiasi hicho cha pesa Mkude amesema ataondoka na kujiunga na mahasimu wao Yanga baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Mkude amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba, na amecheza mechi zote za mzunguko wa kwanza wa ligi ya Vodacom Tanzania na kuifaya timu hiyo kumaliza nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 35.





1480830561975.png
 
Endeleeni kuamini kuwa mtakuwa Mabingwa wa LigiKuu msimu huu ikiwa wachezaji wameshasoma alama za nyakati.....
 
Maneno ya Hans ni upuuzi,kusema mkude hana mchango mkubwa ni undezi sana. Singano aliondoka kwa upuuzi wa huyu huyu, kumlea na kumkuza mchezaji siyo justification ya kutompa dau zuri. Ina maana players wasihitaji maslahi mazuri kisa tu timu imewalea na kuwakuza!!! I bet round ya pili timu itapotea kwa upuuzi wa hawa akina Hansi & Co.

KADA
 
Sio mbaya akienda, yanga naona inakuwa simba B sasa kuanzia kwa Barthez, kessy, mkude na tambwe, hapo tayari idara zote covered. Kipa, beki, kiungo na straika.


Mkuu naomba tu nikusaidie.!

Simba SC ndio academy ya Yanga..! Kwa kuwa wachezaji wanatoka simba kwenda Yanga kuishi ndoto zao....za Mafanikio...

Umeona wapi Kikosi cha pili cha Barca kikawa kinashinda Ubingwa wakati kikosi cha kwanza hakijatwaa ubingwa kwa miaka 5?
 
Maneno ya Hans ni upuuzi.
Mkude ameshaona umri unaenda hivyo anastahili kushinda Mataji na kucheza soka la kimataifa.... Ili afanikishe hayo malengo inabidi acheze Yanga SC tu. Hakuna namna yeyote ilee....


Hiyo pesa anayotaka huko simba ni kisingizio tu cha kutaka kuondoka..... Ameona hamumchakachulii mkataba ili asepe akaamua atumie kisingizio hiki.


 
Mkubwa anadaiwa bilioni 13 au mali zinapigwa mnada wewe umekalia kushahadia ya wenzako. Tembeza bakuli kama enzi za Matunda. Wakati huu sio wa mchezo. OCH shauri yako.
 
Mkubwa anadaiwa bilioni 13 au mali zinapigwa mnada wewe umekalia kushahadia ya wenzako. Tembeza bakuli kama enzi za Matunda. Wakati huu sio wa mchezo. OCH shauri yako.
Umesoma mada lakini.....?

Au umetumia cha Arusha asubuhi badala ya Chai?...
 
Unajinyea unashangaa mtani wake kujamba. Nimeandika metaphor wewe kilaza kuelewa shida. Changisha dogo zama ngumu hizi. Hakuna utapeli na kutolipa kodi.
 
Mkodisho fc.. kila mchezaji mzuri wa Simba wanamtaka

Safari hii kwa mkude hamuwezi nyinyi Simba B
 
Na Kuna watu wanajua kuchungulia kandarasi za wachezaji!
 

Mkuu naomba tu nikusaidie.!

Simba SC ndio academy ya Yanga..! Kwa kuwa wachezaji wanatoka simba kwenda Yanga kuishi ndoto zao....za Mafanikio...

Umeona wapi Kikosi cha pili cha Barca kikawa kinashinda Ubingwa wakati kikosi cha kwanza hakijatwaa ubingwa kwa miaka 5?
Mpira wa Barcelona unaangaliaga chooni au?
 
Ans pope kakosea kuongea,ila mkude ndo anakosea zaidi,hakuna mchezaji Mkubwa zaidi ya timu,mkude simba kaikuya na ataiacha,ni bora angekuwa mpole adai haki yake kimya kimya
 
Duu kweli bongo tuna safari ndefu sana. Sijawahi kusoma au kusikia kiongozi wa timu zilizoendelea huko ulaya, Amerika na kwingineko kiongozi akitoa komenti kama hizo. Eti 'mchezaji mwenyewe hata asipokuwepo kwenye timu madhara hayaonekani' Sasa kwa nini bado wanamchezaji ambaye ni mzigo!? Mimi nashabikia Yanga lakini km ni kweli Hans amesema hivyo amenisikitisha. It's unprofessional!!
 
Back
Top Bottom