Baada ya kukosa saini ya Jonas Mkude, Yanga wapiga hodi Azam FC

isackkallindi

Member
Jan 10, 2014
24
45
BAADA YA KUKOSA SAINI YA JONAS MKUDE, YANGA WAPIGA HODI AZAM FC
.............
Na isack kalindi
DAR ES SAALM: YANGA baada ya kumkosa Jonas Mkude wa Simba aliyeamua kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo, imehamisha macho yake kwa kiungoHimid M ao wa Azam FC huku ikiwa tayari kumpa Sh milioni 60 alizotaka ili asaini mkataba.

Kiongozi mmoja wa Yanga ambaye hakutaka jina lake litajwe, alisema mwanzoni walikuwa wakisuasua kuhusiana na kumsajili Himid kutokana na kuwa na uhakika wa kusajili Mkude ambaye alikuwa akishawishwa vilivyo na Ibrahimu Ajibu, lakini dili lake limebuma.

“Hatuna kingine cha kufanya isipokuwa kilichobakia ni kumsajili Mao na aliomba tumpatie Sh milioni 60 na mshahara wa Sh 3,000,000.

“Kwa hiyo inatubidi tufanye hivyo kwani awali tulikuwa tunamvizia Mkude ambaye alikuwa anataka milioni 50 lakini Simba wametuzidi ujanja, hivyo ni lazima Mao tumsajili sasa,” kilisema chanzo hicho cha habari na kuongeza:

“Mpaka kufikia sasa, kila kitu kipo tayari na tunachosubiri ni yeye kuja tu kusaini, kwa hiyo muda wowote mambo yanaweza kuwa safi.”

Endapo Yanga itafanikiwa kumsajili Himid itakuwa imepata kiungo mkabaji sahihi kwani kwa muda mrefu ilikuwa ikisumbuliwa na hilo, tangu alipoondoka Frank Domayo........
....... ************* *
OKWI,,, ATAJA KIASI ANACHO ITAJI ILI ASAINI SIMBA.....
..........
na isack kalindi
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi, amewataka viongozi wa Simba kama wanahitaji saini yake, waweke milioni 110 mezani ili aweze kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa ligi kuu.

Simba imekuwa katika mazungumzo ya muda mrefu na Mganda huyo kwa ajili ya kumrejesha kwa mara nyingine kufuatia awali kuitumikia klabu hiyo kwa mafanikio makubwa.

Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe, alitua Uganda kwa shughuli zake binafsi lakini akatumia fursa hiyo kuweka mambo sawa juu ya Okwi ili asaini mkataba.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka ndani ya uongozi wa Simba, Okwi ameomba apatiwe kiasi cha shilingi milioni 110 ili aweze kuanguka wino.

“Mwenyekiti wa kamati ya usajili Hans Poppe alikuwa Uganda kuzungumza na Okwi ambapo moja ya vitu alivyovihitaji mchezaji huyo ni kuona anapatiwa dau la milioni 110 ili aweze kusaini mkataba mpya ikiwa ni pamoja na nyumba ya kuishi.

“Viongozi wanaendelea kufanya tathmini na mazungumzo yanaendelea, iwapo tutafikia makubaliano, ataingia mkataba,” alisema bosi huyo.

Alipoulizwa juu ya hilo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Said Tully, alisema: “Nawaomba wanachama na mashabiki wa Simba wawe na subira. Kwa sasa hakuna chochote kinachoendelea juu ya Okwi. Kama kuna taarifa itatolewa, lakini sasa watu wawe na subira.”
*****************
NI vigumu kuamini kwamba kweli wazo la Cristiano Ronaldo ‘CR7’ kuondoka Real Madrid majira haya ya joto linaweza kutokea.

Baada ya taarifa hizo kuripotiwa katikati ya wiki, inadaiwa nyota huyo amewaambia wachezaji wenzake wa Ureno kwamba huo ndio msimamo wake na hakuna nafasi ya kubadili uamuzi huo tena.

Ronaldo amefikia uamuzi huo baada ya kukerwa na tuhuma za udanganyifu wa ukwepaji kodi Hispania kiasi cha Euro milioni 14.7.

Hivyo, wakati CR7 kukiwa na uwezekano wa kuondoka, klabu inayopewa nafasi kubwa kuunasa mtambo huo wa mabao ni Manchester United. Mbali ya yote, Ronaldo bado ni shujaa Old Trafford. Ronaldo mara zote amekuwa muwazi kuhusu kuipenda klabu yake hiyo ya zamani.

Huku Sir Alex Ferguson, Jorge Mendes [wakala wake] na kocha Jose Mourinho wote wakiwa na nguvu, hiyo inamaanisha kuna watu wa kutosha kumuunganisha na kurejea Old Trafford… kama watahitaji kufanya hivyo.

Hivyo, kurudi kwa Ronaldo United kwa ujumla kunaonekaje? Hapa kuna mawazo machache kuhusu kitakachotokea mapema mara baada ya kutua:

1. Bifu za Ronaldo, Mourinho
Kutakuwa na habari nyingi kuhusu bifu za Ronaldo-Mourinho wakati wakiwa Real Madrid.

Nyota hao wawili wa Ureno, tunaweza kusema kulikuwa na uhusiano wa kutatanisha wakati Mourinho akiinoa miamba hiyo ya Santiago Bernabeu, na katika matukio tufauti walikuwa wakitibuana, hizo ni habari zitakazokuwa zikikumbushiwa mara kwa mara.

2. Fergie atahusishwa haraka

Kocha Fergie mara moja atahusishwa katika mahusiano ya karibu na timu.

Hiyo ni kwa sababu ya asili ya uhusiano wa Ronaldo na Mourinho - na sehemu nyingine itakuwa ni kutokana na yeye kuchoshwa na kustafu kwake- na Ronaldo kurudi Old Trafford kutamfanya Sir Alex kufanya zaidi ya anavyoonekana tu amekaa jukwaani akitabasamu na kupeana mikono na watu maarufu [VIPs].

Sababu ni kwamba Fergie ni mtu pekee ambaye Ronaldo bado anamuita 'bosi'.

3. Wapinzani wakuu watahoji umri
Mashabiki wa Liverpool, Chelsea, Arsenal, Man City wote haraka wataanza kumshusha Ronaldo kutokana na kigezo cha umri.

"Ndiyo, sawa, hivyo United sasa imepata mmoja wa wachezaji wakubwa kwa kumrejesha kikosini. Na kweli amefunga zaidi ya mabao 40 kwa kila msimu.

"Lakini ana miaka 32, hana ubora kama aliokuwa nao hapo awali. Na ndiyo, hiyo inamaana bado ni bora kwa zaidi ya asilimia 99 ya wanasoka katika Premier League… lakini United bado inalipa fedha kubwa.

4. Ibrahimovic atasahaulika mepema
Ni wazi kazi nzuri ya Zlatan Ibrahimovic aliyoifanya Man United itasahaulika mapema.

Mabao aliyofunga Msweden huyo yatasahaulika mara moja na mashabiki wa Man United kutokana na kutua kwa mtambo huo wa mabao kutoka Real Madrid.

5. Griezmann hatatajwa tena
Jina la nyota wa Atletico Madrid, 'Antoine Griezmann' pia litatupiliwa mbali katika historia ya Man United na itabaki "Griezmann' ni nani?"

6. Mtukufu wa jezi namba 7
Jezi namba saba Man United itarejeshwa kwa ajili ya utukufu wake halali.

Ikumbukwe jezi namba saba United imevaliwa na mastaa kama George Best, Denis Law, Bryan Robson, Eric Cantona na David Beckham, kwa siku za hivi karibuni imekuwa kama pango kutokana na kumkosa mchezaji anayeitendea haki.

Baada ya Michael Owen, Angel Di Maria na Memphis Depay ambao wote walipewa na kuondoka, kurudi kwa Ronaldo kutamfanya kuonekana mmiliki bora wa jezi namba saba Man United tangu alipoondoka.

7. Rooney anaweza kubaki
Wayne Rooney na Ronaldo walikuwa 'mapacha' bora wakati wakicheza pamoja United, hivyo nyota huyo wa kimataifa wa England anaweza kufikiri kucheza pembeni kwa mshindi huyo wa kubobea wa Ballon d'Or kunaweza kumrejesha tena kwenye mafanikio.

8. Messi atachekelea kimya kimya
Lionel Messi atachekelea kimyakimya mwenyewe.

"Ukweli Ronaldo atafunga mabao machache kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na United - na hatayakaribia aliyofunga akiwa na Real Madrid. Na unajua hilo litakuwa na maana gani…

"Ukinara wa ufungaji utakuwa wangu! "Kila kitu changu!"

9. Mashabiki City watautaka usajili wa Messi
"Sasa tazama hapa, Pep. Tunajua ulikuwa unatusumbua tu hapo kabla kutokana na kuhusishwa na Messi. Lakini unajua kijana huyu unaweza kumpata katika masikio yake.

"Fanya hilo litokee… na haraka."

10. Mashabiki wa Arsenal watakasirika
"Kwa nini isiwe sisi kumsajili Ronaldo?", kwa nini hatumsajili staa yeyote?". "Arsene Wenger sajili staa
 
May 26, 2017
40
95
Hv hao viongozi wetu wa hzi clabu wamelogwa na nani? Inakuaje mchezaji anaomba dau la usajili kubwa zen unampatia mkataba wa miaka miwili?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom