Jomo Kenyatta (56) na Abdul Sykes (26) Katika Mkutano wa Siri, Nairobi 1950

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,127
30,476
IKIWA HUJAPATAPO KUZIONA TARIFA ZA KIKACHERO ZA SPECIAL BRANCH 1950s
"Tanganyika Political Intelligence Summary, March 1952":

"...it is reported that the Secretary of the Association, Abdul Wahid Sykes has dispatched letters to all branches asking members for suggestions under the following heads for a memorandum to be prepared for the Royal Commission..."

...Abdul Wahid Kleist Sykes, Secretary of the African Association who, as reported in last month's summary (paragraph 20) was going on safari up country, visited Mwanza, where he met Paul Bomani, President of the Bukoba African Association, and accompanied him to Bukoba. Sykes then visited Kampala alone..."

Mwaka huu wa 1950 Abdul Sykes akiwa Secretary wa TAA na mjumbe wa TAA Political Subcommittee, Abdul alikuwa na umri wa miaka 26.

Kijana mdogo sana.
Jomo Kenyatta alikuwa na miaka 56.

Jomo Kenyatta kazaliwa mwaka wa 1894 sawasawa na umri wa Kleist Sykes baba yake Abdul ambae alikuwa kafariki mwaka wa 1949.

Utaweza vipi kuandika historia ya TANU na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika ukaacha historia kama hii na wala usiwataje wahusika wa harakati hizi?

Kisha anatokea mtu anasema kuwa chama cha TAA kilikuwa chama cha starehe.

Ningeweza kueleza mengi katika uandishi wa historia ulifanywa na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini tutosheke na haya.

Kila nipitapo mitaa ya Maktaba nakutana na kumbukumbu hizi.

Hizi ni taarifa kutoka Rhodes House Library, Oxford kutoka majalada ya kikachero ya Waingereza baada ya miaka 50 yanawekwa wazi kwa mtafiti yeyote kuyasoma na kufanya nakala akipenda.

Historia hii alinihadithia Mzee Ahmed Rashaad Ali tumekaa nyumbani kwake Ali Hassan Mwinyi Road tunazungumza.

Ahmed Rashaad Ali ni huyo kuliwa kwa Jomo Kenyatta.

Mzee Rashaad aliniomba nisimtaje jina katika kitabu cha rafiki yake Abdul Sykes nilichokuwa natafiti.

Wakati huo nilikuwa sijapata nyaraka hii ya Special Branch.

Siku nilipoletewa nyaraka hii nilinyanyua mikono juu kumshukuru Allah kwa kuthibitisha kile ambacho Mzee Rashad alinieleza.

Wakati huu Mzee Rashad alikuwa tayari keshafariki.

Huko tulikotoka miaka hiyo watu walikuwa wakihofu kueleza historia ya kweli ya TANU.

Hakika tumetoka mbali na leo ukweli umedhihiri.

1715783034052.png

1715783093772.png

1715783127491.png
 
Mzee Said unaweza kutusaidia kutujibia haya maswali machache muhimu ili kujenga au kukuza msingi wa hoja yako hapa.

1. Ni akina nani ndio waliohusika kuhakikisha historia ya TANU katika kudai uhuru inapotoshwa? Tutajie ili tuwajue.

2. Nini lengo la historia ya TANU katika kudai uhuru kupotoshwa?

3. Kwanini hadi sasa (zaidi ya miaka 60) tangu kupatikana uhuru, bado historia ya TANU imebakia ile ile?

4. Ni historia ipi katika harakati za kudai uhuru ambayo haukupotoshwa?

5. Kwa sasa ni nani wanufaika na nani waathirika wa upotoshwaji wa historia ya TANU katika kudai uhuru?
 
Huwa natafakari mchonga alitokaje vijijini huko Butiama kwa wachunga ng'ombe na wakulima akaja kuwazidi akili hawa watoto wa mjini na akawazidi vyeo, madaraka na ushawishi?

Watoto wa Dar hadi leo hawana hamu na yule mzanaki, dah yule mzee alitia fora.

Sisi watoto wa mjini tutabaki kulalama tu hadi kesho. Kuna kosa la kiufundi lilifanyika.

Kwa huo uwezo tu naona kiaina mchonga apewe maua yake, yule mzee sijui alisomea ujasusi? Noma sana.
 
Mzee Said unaweza kutusaidia kutujibia haya maswali machache muhimu ili kujenga au kukuza msingi wa hoja yako hapa...
Zanzibar,

Majibu ya maswali yako yote utayapata katika kitabu cha Abdul Sykes.

Pia unaweza kuingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Fanya name search kuna makala zaidi ya 10,000.
 
IKIWA HUJAPATAPO KUZIONA TARIFA ZA KIKACHERO ZA SPECIAL BRANCH 1950s
"Tanganyika Political Intelligence Summary, March 1952":
Kisha anatokea mtu anasema kuwa chama cha TAA kilikuwa chama cha starehe.

Ningeweza kueleza mengi katika uandishi wa historia ulifanywa na Chuo Cha CCM Kivukoni lakini tutosheke na haya.
Kwa hiyo taarifa za taasisi ya wakoloni ya SPECIAL BRANCH unaziamini kuliko zile za Chuo cha Kivukoni?
 
Huwa natafakari mchonga alitokaje vijijini huko Butiama kwa wachunga ng'ombe na wakulima akaja kuwazidi akili hawa watoto wa mjini na akawazidi vyeo, madaraka na ushawishi?...
Mkuu kwani Magufuli (msukuma wa kuunga unga wa huko Chato) aliwazidi vipi ujanja magwiji wote wa mjini ndani ya CCM na nje ya CCM na kuwa rais wa Tanzania?

Ama yule mama yetu wa Kizanzibar akawa Rais wa Tanzania?
 
Zanzibar,
Majibu ya maswali yako yote utayapata katika kitabu cha Abdul Sykes.
Pia unaweza kuingia: mohamedsaidsalum.blogspot.com.

Fanya name search kuna makala zaidi ya 10,000.
Mimi ni mvivu wa kusoma vitu vingi, hivyo honesty ninaweza nisifanikiwe sana kuperuzi huko.

Upande wa pili, wasomaji wengi wa JF pia ni watu wenye tabia kama hizo.

Kwa kuwa mada umeileta hapa JF, kama hutojali, unaweza ukatupa majibu rahisi (muhtasari) ya hayo maswalo na kuweka hizo rejea ili tutakaovutiwa zaidi tukazipitie huko kwa kina.
 
Huwa natafakari mchonga alitokaje vijijini huko Butiama kwa wachunga ng'ombe na wakulima akaja kuwazidi akili hawa watoto wa mjini na akawazidi vyeo, madaraka na ushawishi?
Others...
Haya si ya kufanyia kejeli.

Baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes historia ya uhuru wa Tanganyika ikawa imebadilika.

Ikaonekama ni lazima historia ya Mwalimu sasa iandikwe na akaombwa idhini ya kufanya hivyo kwa kuelezwa kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimebadili hata historia yake.

Mimi ni mmoja wa waliohojiwa kuhusu historia ya Mwalimu.

Angalia hapo chini kitabu cha Mwalimu Nyerere kipo pamoja na kitabu cha Abdul Sykes.

Vile vile walimu wakisomesha Historia ya Uhuru wa Tanganyika baadhi huwaambia wanafunzi wao wafungue Dictionary of African Biography (DAB) 2011 wamsome Dr. Kwegyr Aggrey kisha wamsome katika kamusi hilo hilo Kleist Sykes.

Hivi ndivyo sasa historia ya uhuru wa Tanganyika inavyosomeshwa katika vyuo vingi.

Haya si mambo ya kejeli.
Hii ni historia ya Tanzania inayostahili kuheshimwa.

1715786152250.jpeg

1715786202396.png
 
Mkuu kwani Magufuli (msukuma wa kuunga unga wa huko Chato) aliwazidi vipi ujanja magwiji wote wa mjini ndani ya CCM na nje ya CCM na kuwa rais wa Tanzania?

Ama yule mama yetu wa Kizanzibar akawa Rais wa Tanzania?
JPM si alitoka kwenye ubunge, kaingia uwaziri utendaji wake ukaonekana.

Huyu rais wa sasa si inajulikana ni kwa mujibu wa katiba.

Nyerere ilikuaje ametoka Butiama na bukta kuchunga ng'ombe na kulima aje kuwazidi visiki wa mjini wenye mji wao? Ni swali najiuliza tu, kwa sababu hadi leo wajukuu na watoto wa wazee wale wa mjini hawaachi kulalama nao wanashangaa ilikuaje mzanaki yule akawazidi akili wazee wao?

Kwa upande mmoja mchonga aliwazidi akili wale wazee, akageuza mchezo mzima juu chini na chini juu, kimekua kilio kuanzia wazee hadi wajukuu.
 
Mimi ni mvivu wa kusoma vitu vingi, hivyo honesty ninaweza nisifanikiwe sana kuperuzi huko.
Upande wa pili, wasomaji wengi wa JF pia ni watu wenye tabia kama hizo.
Kwa kuwa mada umeileta hapa JF, kama hutojali, unaweza ukatupa majibu rahisi (muhtasari) ya hayo maswalo na kuweka hizo rejea ili tutakaovutiwa zaidi tukazipitie huko kwa kina.
Zanzibar,
Ukiwa wewe ni mvivu sina la kufanya.
 
Others...
Haya si ya kufanyia kejeli.

Baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes historia ya uhuru wa Tanganyika ikawa imebadilika.

Ikaonekama ni lazima historia ya Mwalimu sasa iandikwe na akaombwa idhini ya kufanya hivyo kwa kuelezwa kuwa kitabu cha Abdul Sykes kimebadili hata historia yake.

Mimi ni mmoja wa waliohojiwa kuhusu historia ya Mwalimu.

Angalia hapo chini kitabu cha Mwalimu Nyerere kipo pamoja na kitabu cha Abdul Sykes.

Vile vile walimu wakisomesha Historia ya Uhuru wa Tanganyika baadhi huwaambia wanafunzi wao wafungue Dictionary of African Biography (DAB) 2011 wamsome Dr. Kwegyr Aggrey kisha wamsome katika kamusi hilo hilo Kleist Sykes.

Hivi ndivyo sasa historia ya uhuru wa Tanganyika inavyosomeshwa katika vyuo vingi.

Haya si mambo ya kejeli.
Hii ni historia ya Tanzania inayostahili kuheshimwa.

View attachment 2990891
View attachment 2990892
Mzee nilikua sina nia ya kufanya kejeli bali udadisi na kufahamu.

Nashukuru pia kwa vyanzo ulivyopendekeza ambavyo vinaweza kuwa na majibu ninayojiuliza.
 
Nakuona mdini
Vichekesho,
Mimi nakuona huna uwezo wala ujasiri kwa kukubali ukweli.

Wataalamu wa African History: John Iliffe, Jonathon Glassman na James Brennan wao baada ya kusoma kitabu wakafanya review zao na zikachapwa katika Cambridge Journal of African History.

Jonathon Glassman akanialika chuoni kwake Northwestern University, Evanston, Chicago nikazungumze.

Naamini unajua uzito wa jambo hili.

1715788129103.jpeg
 
Hakuna kitu kinamuuma mleta mada kama kusikia Nyerere akiitwa Baba wa Taifa na sio watu wake anaowafahamu. Pole sana mzee. Nyerere alikua mjanja sana ila akatudumbukiza kwenye muungano wa mchongo
Numbisa,
NIngeandika kitabu changu kwa nia ya kumdogosha Mwalimu Nyerere kitabu kingekufa na sidhani kama ningeweza kupata mchapaji wa maana na vilevile kuweza kupata mialiko kutoka kwa wasomi wa historia ya Afrika.

Halikadhalika kitabu kisingependwa kwa kufikia kuchapwa sasa mara nne na tunakwenda toleo la tano.

Mimi napongezwa kote hakuna anaenihurumia.
Hivi sasa nishapokea nishani tano kwa kazi hii.

Mimi nakupa pole wewe.

1715788465020.jpeg

Mzee Said unaweza kutusaidia kutujibia haya maswali machache muhimu ili kujenga au kukuza msingi wa hoja yako hapa.

1. Ni akina nani ndio waliohusika kuhakikisha historia ya TANU katika kudai uhuru inapotoshwa? Tutajie ili tuwaju...
Akikujibu najamba kwa sauti makusudi kabisa mbele ya watoto wangu halafu nacheka wasikie
 
Hakuna kitu kinamuuma mleta mada kama kusikia Nyerere akiitwa Baba wa Taifa na sio watu wake anaowafahamu. Pole sana mzee. Nyerere alikua mjanja sana ila akatudumbukiza kwenye muungano wa mchongo
Nyerere ni ICON wa Taifa hili na itabaki hivyo vizazi vyote mpaka atakapoondoka huyu Mdini Mohamed Said

Yaani umfananishe Nyerere Mwalimu Msomi na Wacheza bao waliokuwa wanatawadha na kukaa vibarazani? THUBUTUUU 🤣🤣🤣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom