Jokate Mwegelo: Wanawake ifike mwisho kuwapigia kura wanaume

Mr Nyau

JF-Expert Member
Oct 18, 2018
1,128
2,337
2024_42_07_09_42_030.jpg

"Tutakwenda kuhakikisha tunaongeza ushiriki wa Wanawake kwenye hizi chaguzi kwa Wanawake wenyewe kugombea. Ufike mwisho wakati wa Wanawake kuwa ndugu watazamaji na wasindikizaji na ifike mwisho Wanawake kuwa ni sehemu ya kuwapigia kura Wanaume wakati ninyi mna uwezo wa kugombea".

Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu- Umoja wa Wanawake Tanzania, CCM (UWT)
 
View attachment 2927475
"Tutakwenda kuhakikisha tunaongeza ushiriki wa Wanawake kwenye hizi chaguzi kwa Wanawake wenyewe kugombea. Ufike mwisho wakati wa Wanawake kuwa ndugu watazamaji na wasindikizaji na ifike mwisho Wanawake kuwa ni sehemu ya kuwapigia kura Wanaume wakati ninyi mna uwezo wa kugombea". Jokate Mwegelo Katibu mkuu UWT

UWT = Umoja wa Wanawake Tanzania
CCM
Nitahama hii nchi ya vidole juu
 
Huwa kuna mambo mtu anaweza kufikiri ni marahisi kuyaongelea kumbe kiuhalisia ni magumu na yanahitaji busara ya hali ya juu

Hata hivyo sifa ya kuwa mwanamke au mwanamme SIO KIGEZO CHA KUWA KIONGOZI; tunahitaji Viongozi wenye sifa ya kuwa viongozi na sio jinsia....
 
Yeye yule aliemtia mimba akafanikiwa kumzalisha sio kwamba alimpigia kura akamkabidhi sifuri zero yake aweke kitu ndani au anataka kusemaje amepata mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu? Alafu kabla ya kuropoka jichuje kwanza sio unaropoka tu vingine utaropoka kumbe unapotoka
 
View attachment 2927475
"Tutakwenda kuhakikisha tunaongeza ushiriki wa Wanawake kwenye hizi chaguzi kwa Wanawake wenyewe kugombea. Ufike mwisho wakati wa Wanawake kuwa ndugu watazamaji na wasindikizaji na ifike mwisho Wanawake kuwa ni sehemu ya kuwapigia kura Wanaume wakati ninyi mna uwezo wa kugombea".

Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu- Umoja wa Wanawake Tanzania, CCM (UWT)
Sasa itakuaje Kwa Kassimu Majaliwa?
 
"Katika kuekekea mwaka wa uchaguzi kuanzia mwaka huu 2024 katika uchaguzi wa serikali za Mitaa na Vijiji, UWT tutahakikisha tunahamasisha Wanawake wanajitokeza kwa wingi kugombea na kushika nafasi za Uongozi kuanzia Vitongoji, Vijiji na Mitaa."

"Lazima tukaongeze idadi ya Viongozi wanawake kwenye mitaa na vijiji, UWT tukiongozwa na Rais wa kwanza Mwanamke Dkt. Samia Suluhu Hassan , tutahakikisha ushiriki wa wanawake kwenye chaguzi hususani kugombea utaongezeka, ufike mwisho wanawake kuwa ndugu watazamaji na wasindikizaji na sio kuwapigia tu kura wanaume na katika hili kielelezo na kinara wetu ni Rais Dkt. Samia na ndio chachu ya mafanikio kwa wanawake."

"Chini ya Mwenyekiti wetu Mama Mary Chatanda (MCC) tutahakikisha mwanamke akigombea atapitishwa na Chama na tutampambania ashinde, UWT inasema mwanamke usijione mnyingo na usijione upo peke yako, Jeshi la Mama Samia UWT litakushika mkono kila hatua."

"RAIS Samia ni msikivu, mvumilivu na anapenda kuona akina mama wanapata fursa na hatutakiwi kukatishana tamaa lazima tuungane na kutiana moyo."

"Viongozi wengi wanapokuwa wanawake matokeo huonekana na takwimu zinaonesha akina mama ni viongozi bora."

Ndugu. Jokate Mwegelo
Katibu Mkuu wa UWT - Taifa

📍Lumumba - DSM
🗓️ 7 Machi, 2024

IMG-20240307-WA1366.jpg
 
Back
Top Bottom