Jokate katika ngoma ya wapiga zumari

Jokate katika ngoma ya wapiga zumari

Jokajeusi

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2018
Posts
6,332
Reaction score
10,913
JOKATE KATIKA NGOMA YA WAPIGA ZUMARI

Na, Robert Heriel.
Uzuri wake usiomithilika ndio kinga yake dhidi ya maadui na wazandiki wasiompenda na kumtakia mema. Mapozi yake ya kilimbwende yalivunja mioyo ya karibu kila mwanaume aliyekamilika. Wanaume kama si wote waomba dua kwa dini zao wampate yeye.

Mapozi yake yaliacha wazi midomo ya vijana chakaramu wakibaki kutoa udenda kwa tamaa za ngono. Si kwamba alikuwa malaika hasha! ila uzuri wake wengi waliufananisha na viumbe waishio mbali na sayari yetu ya dunia.

Pengine ningesahau jambo moja muhimu, nalo ni domo lake la manjonjo ambalo mara kwa mara lilikuwa alitulii kwani aliliweka kila mkao kuvuta wanaume wenye kupenda vitu vyenye kung'aa. Juu ya domo lake kulikuwa na kitufe cheusi kama battani ya kuwashia luninga bora za kisasa.

Kitufe hiki wengi walikiita kidoti ndipo hapo sasa mlimbwende huyu akapata ubini wake. Yaani JOKATE KIDOTI.
Hiki alikitumia kama fani katika kazi yake ya mitindo. Alihakikisha kila akibinjua binjua uso wake basi sharti Kidoti chake kiwe dhahiri. Looh! mambo si ndio hayo.

Ungependa kujua habari ya rangi yake na uso wake aliopenda kuutunisha kupitia mashavu yake malaini mithili ya nyama ya ini. Rangi yake ilimeremeta kama bilauri imulikwayo na miale ya mwanga. Rangi ya kiafrika yenye umvuto wa kimataifa.
Umbo lake sitaki kulielezea usije toa udenda hapa. itoshe kusema ni moja wa mabinti ambao wanamvuto wa kipekee sana.

Silaumu kwa mwanaume yeyote kupambana na hali yake katika harakati za kumpata huyu bibie. Kila mtu atumie mpini wake ila yule mwenye makali sharti aibuke mshindi katika kuwania tuzo hii bora.

Jokate yupo katika ngoma ya wapiga zumari. Wengi wameshangazwa na yeye kupewa moja ya nafasi nyeti katika serikali. Pengine hata mimi Taikon wa Fasihi ningemchagua ilo analolijua ni Maulana.

Jokate kama walivyo vijana na mabint wengi anazo haki za msingi kupewa nafasi mbalimbali za uongozi na taaluma kulingana na sifa zake. Sina wasiwasi na Elimu yake na uwezo wake wa kufikiri. Licha ya kwamba na uzuri umeingia mnadani lakini pasi na elimu basi nafasi hiyo huenda angeisikia kunako mitandao.

Kitu pekee ninachokiona cha msingi ambacho mabinti wadogo wanapaswa wajifunze ni kuwa wawe na maadili mema ili wasipate changamoto katika nafasi za dhahabu kama hii aliyoipata dada yetu Jokate.

Tabia ya Jokate aliyokuwa nayo ya kutupia picha tata zenye kuonyesha sehemu kubwa ya mwili wake ndizo zimegeuka wimbo kwa wapiga zumari. Bila shaka hii pia kwa sasa imekuwa changamoto kwake kila akizitazama picha zake zenye utamu ambazo hata watoto wake atakao wazaa wataziona.
Wito wangu kwa kina dada waache tabia hii kwani madhara yake ni makubwa sana si tuu katika fursa bali kwa maadili ya watoto wao baadae.

Mwisho nimalizie kwa kusema, Hongera Mhe. JOKATE MWEGELO AKA Jokate Kidoti Kwa kupata nafasi hiyo. Bila shaka utafuta mapungufu yako ya nyuma ili kuleta uaminifu kwa safari yako ya mbeleni kisiasa.


TAIKON WA FASIHI
jookate.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Mwalimu Nyerere Alisema
Huyu Jamaa Ameiweka Serikali Yangu Mifukoni Ana Mifuko Mipana Kiasi Gani
Wenye Akili Tukajua Anatoa Rushwa
Nikamweka Ndani Nikatiwa Misukosuko
Mwalimu Mwachie
Nikasema Mshenzi Sana Huyu Simwachii
 
Dunia hii kuna wenzetu wameishi/wanaishi maisha perfect sana. Sisi ambao tumepitia bangi,pombe na vurugu nyingine inabidi tusipate fursa yeyote vinginevyo TUTAPATA TABU SANA
Ukibadilika na maisha yenyewe yanabadilika
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Mwalimu Nyerere Alisema
Huyu Jamaa Ameiweka Serikali Yangu Mifukoni Ana Mifuko Mipana Kiasi Gani
Wenye Akili Tukajua Anatoa Rushwa
Nikamweka Ndani Nikatiwa Misukosuko
Mwalimu Mwachie
Nikasema Mshenzi Sana Huyu Simwachii
safi sana hii
 
Mungu Ni Mwema Wakati Wote
Mwalimu Nyerere Alisema
Huyu Jamaa Ameiweka Serikali Yangu Mifukoni Ana Mifuko Mipana Kiasi Gani
Wenye Akili Tukajua Anatoa Rushwa
Nikamweka Ndani Nikatiwa Misukosuko
Mwalimu Mwachie
Nikasema Mshenzi Sana Huyu Simwachii

hahahaa! unasemaje sasa?
 
Acha umbea wewe. Sasa unarudia rudia picha ili iweje. Mbona rais wa Croatia aliwahi kujiachia zaidi ya hapo na hukusema kitu?
We ndezi nini sasa tamaduni za ulaya ndio unataka kuzileta hapa?ni siku hizi tu ndio mmeamua kunajisi hizinyadhifa za U RC DC!!miaka ya nyuma huwezi kuta wahuni tu wanapewa nyadhifa kama hizi ila kwa kuwa siku hizi hakuna vetting ni kuteua tu ili uwakomeshe wengine ndio haya yanayotokea!!jokate ndio anaenda kuwa mwenyekiti wa ulinzi na usalama wa wilaya?kweli
 
Hakuna mtu duniania anaye penda unafiki kama sisi wa Tz.

Kuupinga Ukweli makusudi na kuamini uongo na kuusambaza .
Alaaniwe aliye tuloga ,siyo kwa ulozi huo .
 
Back
Top Bottom