Johnson Mbwambo amesema kweli! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Johnson Mbwambo amesema kweli!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kashaija, May 25, 2009.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Katika gazeti la Raia Mwema toleo la Mei 13 - Mei 19, 2009, Mwandishi Johnson Mbwambo aliandika Makala yenye kichwa cha habari "Ya Profesa Watson na Urais wa kina Zuma".

  Katika makala yake hii nilifurahishwa na mifano yake miwili aliyoitoa na ambayo inaonyesha wazi si tu jinsi viongozi wetu walivyo na akili finyu, bali pia wenzetu wenye akili timamu wanavyotushangaa. Nanukuu mifano hiyo hapa chini.

  ".........Nilitoa mifano kadhaa ukiwemo wa waziri wetu mmoja aliyekatiwa tiketi ya ndege ya daraja la kwanza wakati akienda Ulaya kutembeza bakuli la ombaomba kwa wafadhili , na kwamba katika ndege hiyo hiyo alipakia balozi wa nchi hiyo inayokwenda kuombwa misaada hiyo; lakini yeye akiwa daraja la tatu.

  Nilitoa mfano mwingine wa Mzungu mmoja aliyetoa pesa zake Tsh. milioni 5 kwa ajili ya kujenga kisima cha maji katika kijiji kimoja nchini. Nilisema kwamba wakati wa uzinduzi wa kisima hicho, Mzungu alikwenda katika kijiji hicho kwa gari la kawaida kabisa Suzuki, lakini Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya husika yeye alikwenda kwenye sherehe hizo kwa gari la kifahari la Serikali aina ya Landcruiser VX! Nilisema kwamba Tsh. milioni 120 zilizotumika kununua gari lile zingeweza kujenga visima 24 kwa vijiji 24 vya Wilaya hiyo"! Mwisho wa kunukuu.

  Jamani tutapata wapi viongozi wa kweli, ambao wana akili timamu, wasiopenda makuu? Au tuwarejeshe wazungu watutawale?

  Naomba kuwakilisha.
   
  Last edited: May 25, 2009
 2. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kama mzee Mwambo alimaanisha hayo aliyoyasema basi angetaja huyo waziri aliyepanda first class kwenda kuomba misaada wakati balozi wa nchi fadhili kapanda coach kwenye ndege hiyo hiyo. Na angetaja huyo waziri aliyekuja na shangingi kwenye project ya kujenga visima.

  Anaogopa nini, si ataje? Au kama anaogopa kuwa sued basi hana hakika na anachokisema, ni kama mdaku tu.
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,524
  Trophy Points: 280
  Mbwambo ni Great Mind, hana haja ya ya kutaja majina.
   
 4. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #4
  May 25, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Watu wengine bana..mnakuwa critical hata sehemu ambazo hazifai...sasa wewe interest yako ni kujua jina la waziri au kuangalia relevance ya huo mfano alioutoa bwana Mbwambo? Kama ungekuwa unaishi kwenye vijiji vyetu wala usingeuliza hilo swali lako na kufanya hilo hitimisho..maana alichokisema muungwana Mbwambo ndo tunakishuhudia kila kona ya nchi yetu.

  I always say Africa inarudishwa nyuma na wasomi...wana-focus kwenye nitty gritties..procedures badala ya substance... badala ya kuangalia the bigger picture. Leo mtu kaiba lakini tunaambiwa hakuna ushahidi kisheria. Sometimes nadhani waafrika tuliiga sheria ambazo haziendani na mzingira yake..we just copied everything from the west bila kuangalia kama zinatufaa au hazitufai. Wengi tunaenda shule lakini hatuelemiki kuyaelewa mazingira yetu. Its sad but true. uelewa na elimu ya wasomi wetu vinaacha maswali mengi kuliko majibu.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Dilunga,
  I know for a fact that US government officials travel economy on official duties. Kwa hiyo sishangai kama balozi wa Marekani Tanzania amesafiri economy wakati Waziri mkuu anayeelekea Marekani amesafiri first class.
   
 6. N

  Nsololi JF-Expert Member

  #6
  May 25, 2009
  Joined: Mar 8, 2007
  Messages: 290
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Dilunga check hoja iliyopo mbele yako badala ya ku-critisize. Kashija kaleta hoja kama ilivyowasilishwa na bwana Mbwambo full stop. Huna hoja kaa pembeni wenye hoja wachangie.

  Back to the point:

  Hayo ndiyo matatizo ya viongozi wetu waliopo madarakani na waliostaafu. Ni wachache kama akina marehemu Kambarage waliojali zaidi wananchi kuliko ukuu wao.
   
 7. J

  JokaKuu Platinum Member

  #7
  May 25, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,983
  Trophy Points: 280
  ..tunaingia gharama kubwa zaidi kutokana na posho za ziara za nje.

  ..safari zingekuwa chache na zenye tija, nisinge-mind sana hata kama wakuu wa msafara wakisafiri 1st class.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  May 25, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Mbwambo hana shuruti ya kumtaja huyo waziri aliyepanda first class wakati balozi wa nchi fadhili alikuwa coach kwasabababu mawaziri wetu ndio kawaida yao wote!! sasa atawataja wangapi? We Dilunga nadhani huijui nchi hii; si mawaziri tu bali hata wakurugenzi karibuni wate wa halmashauri zetu wanatumia mashangingi sembuse mawaziri, wanapokwenda kutembelea miradi wengi huenda na mashangingi yao!! Kwa taarifa yako Dilunga, Johnson Mbwambo is one of the few remainimg talented and analytical journalists in the country and his pieces are a delight to read ; he cannot write UDAKU nonsense!!
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  May 25, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,769
  Likes Received: 4,983
  Trophy Points: 280
  ..kisa cha waziri wa Tanzania kusafiri 1st class wakati mabalozi wa nchi wafadhili wanasafiri economy nilikisoma kwa mara ya kwanza 1995 kwenye Rai, na ilikuwa makala ya Jenerali Ulimwengu.

  ..baada ya makala ya Jenerali Ulimwengu, Prof.Lipumba akaahidi kwamba tukimchagua kuwa Raisi atasafiri economy badala ya 1st class.

  ..huyo Mbwambo angetuletea habari mpya. we need more investigative articles kuhusu matumizi mabaya ya serikali kuliko hizo makala zao wanazoandika.

  ..sasa serikali ikija na jibu kwamba ticket zote za 1st class wanazipata at a discounted price ya economy class tutasema nini?
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  May 26, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mwenye low mind ndio hawezi kutaja! maana ni mwoga na hajiamini. Unataka kusema Dr Slaa ni low minded?
   
 11. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #11
  May 26, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Bulesi, kama wewe unaijua hii nchi, taja mmoja basi. Unasema Mwambo atataja wangapi, ataje huyo aliyemwona. Si wako wengi? Taja mmoja!

  Jasusi, swala hapa sio ku "know for a fact" kwamba hivi vitu si vya "kushangaza." Si kwamba nasema hayo hayafanyiki au hayawezekani. Ila nasema, kama Mwambo ameshuhudia hayo, na awataje. Kigumu nini?

  Kama anasita kutaja inaweza kuwa ni 1) habari ni kweli lakini anaogopa kushitakiwa, 2) katunga. Kama ni kweli, na anaogopa kushitakiwa, basi aache kuandika makala za kudokeza dokeza watu tu, hana ujasiri na uzalendo kuonyesha vidhibiti. Hatuwezi kujirekebisha kama tunakosoana kwa kuoneana aibu. Hakuna kiongozi atakae ogopa kufanya jambo la aibu iwapo anatunziwa identity yake kwa uaminifu humo magazetini.

  Waziri aliyeenda kuomba msaada na 1st class na balozi wa nchi fadhili yuko coach ndege hiyo hiyo, nani huyo?

  Na kiongozi aliyekwenda kwenye mradi wa visima na shangingi la milioni 120 halafu akazodolewa na mzungu alietoa msaada wa visima kwamba gari hilo lingejenga visiwa 24 kwenye vijiji 24, nina hakika Mzee Mwambo alikuwepo na ukamwona huyu mtu. Basi taja ni nani huyo kiongozi aliyeumbuliwa na mzungu hadharani?

  Naamini Mzee Mwambo hakutunga hizi hadithi. Basi na awataje.
   
 12. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #12
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naona kuna ki-split kinatokea hapa between the radical views of mkuu Dilunga na wakuu wengine kiasi cha kutufanya tupoteze focus kwenye original article ya Mbwambo na ku turn on each other to an extent.

  Kama mara nyingi napata parallels katika historia ili kuweza kuangalia mambo vizuri.Katika mwamko wa historia ya mapinduzi ya Urusi, wakati warusi walipotaka kumpindua Tsar Nicholas Romanov the second, kulitokea mgawanyiko mkubwa sana kati ya Mensheviks (wafuasi wa Julius Martov) na Bolsheviks (Wafuasi wa Vladimir Illyich Lenin) tofauti zilikuwa nyingi lakini moja kubwa ilikuwa kwamba Bolsheviks walitaka mapinduzi ya ghafla na yaliyo radical wakati Mensheviks walitaka mapinduzi yaliyo na kiasi na yatakayochukua muda. Eventually Bolsheviks wakashinda na yaliyofuatia ni mapinduzi na chama cha kikomunisti cha Russia.

  Sasa basi, tuelewe kwamba sisi sote tunapigana na ufisadi (Tsar Nicholas Romanov the Second) na whether tunataka atoke haraka kwa radical means pamoja na kutaja majina (Bolsheviks like Dilunga) au tunataka kutumia ustaarabu (Mensheviks / kutotaja majina) tusikubali kugombana wenyewe kwa wenyewe kuliko tunavyogombana na ufisadi, ama sivyo tutakuwa tunapigana katika vita vya panzi (Bolsheviks and Mensheviks) ambayo itakuwa furaha ya wapinzani wetu kunguru (Tsar Nicholas Romanov/ mafisadi)

  There is room for diplomatic dialogue, even one carrying radical view, without splitting us asunder.I would like to think the enlightened minds at JF can agree to disagree on some issues without losing sight of the big picture concerning the predicament of our homeland.
   
  Last edited: May 26, 2009
 13. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #13
  May 26, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unajua sana world history. Umewahi kusikia maneno kama haya, yalikuwa popularized na nani? Naomba jina tu.

  Ukiona watu wanakubaliana kubaliana ovyo ovyo kila kitu ujue kuna matatizo hapo.
   
 14. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #14
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyo Mzee General George S. Patton, mbona nimetoka kumquote kule kwenye thread ya kumuua Mwanakijiji kitambo kifupi tu?

  Huyu general ilikuwa ndiye apewe command ya Allied Forces huko Ulaya katika WW2 sema yeye alikuwa msela sana na hakuwa na diplomasia na wakaona anawawakia warusi ambao walikuwa allies, akaenda kupewa the lesser soldier Dwight "Ike" Eisenhower, ambaye ingawa alikuwa a lesser soldier alikuwa a better diplomat. The lesson here being sometimes diplomacy pays. However, some uncompromising radicals would deem such spoils as adulterated with the compromise of some basic principles (In the end Patton was proved right in that the Russians/ Soviets were untrustworthy and were only united with western Europe and America to get rid of Hitler) .

  Baada ya hapo Ike akaja kuwa bonge la war hero akaingia White House kirahisi, wakati Patton akabaki kuwa a much decorated General.
   
 15. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #15
  May 26, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Aksante. Ungeishia hapo, ndilo lilikuwa swali. Sikuomba dissertation kuhusu uongozi wa jenerali Patton.

  Sasa, ukiona watu wanakubaliana kubaliana tu kwa vile wote wanajifanya kupigana na ufisadi, ujue kuna tatizo.

  Mwambo ataje Waziri aliyeenda kuomba msaada na 1st class huku balozi mfadhili yuko coach ndege hiyo hiyo.
   
 16. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #16
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Nyamaza wewe huwezi kusema natakiwa kusema nini na nini sitakiwi kusema, kutoa dissertation ndiyo middle name yangu, sema kingine.

  Kuna vijana wanaenda shule humu wana appreciate kama wewe hutaki acha kusoma.

  Wee jamaa mnoko huheshimu hata freedom of speech!
   
 17. Masanja

  Masanja JF-Expert Member

  #17
  May 26, 2009
  Joined: Aug 1, 2007
  Messages: 3,595
  Likes Received: 3,762
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo ndo unapoteleza kidogo.

  Jenerali alikupa mfano huo mwaka 1995. LAKINI leo ni mwaka 2009 na tatizo ni hilo hilo..kwa hiyo unataka mfano upoteze relevance wakati bado tatizo lipo? Sana sana tungejiuliza..ni kipi kimefanyika kuli-address hili tatizo? Kwa mantiki hii..ni sawa na kusema..hili tuliache tumeshalizungumzia sana..hawa jamaa hawasikii..tuachane nao..ingawa kodi zetu zinazidi kuyoyoma. I dont think this is what you imply mkuu.
   
 18. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #18
  May 26, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Unatoa shule sio? Unajua hata Dr. Shayo ni Chancellor wa MICHUZI online university, na provost wakeMashaka.

  Sasa kama wewe ndio Dr. Shayo wetu hapa Jamii Forums online university kumbuka maneno ya yule mwanasayansi wa Kijerumani aliyesema, atakae jifanya anajua kitu fulani ujue hajui. Kitu gani kile tena alisema?
   
 19. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #19
  May 26, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako una mawazo mgando kwamba kuna "mtoa shule" na mwingine "mpewa shule" wakati the essence ya JF ni kuelimishana na kubadilishana mawazo, katika vijana hao hao ninaoona nawatolea shule na wao wanaweza kunipa their take ikawa shule kwangu, ndiyo point nzima ya JF.

  Sasa wewe unataka kuleta ukiritimba na umangimeza kuwa tukitaka kutoa anecdotes lazima tujaze form zenye kopi nne nne kupeleka ofisi ya Vogon Mkuu Dilunga ili zipitiwe halafu aamue kama atatupa nafasi tuandike ama la, unaishi katika ulimwengu wa kufikirika.People can't even do genuine moderation, it's like trying to herd cats in here, halafu leo unataka kutuletea Draconian standards zako huko?
   
 20. H

  Hondo Member

  #20
  May 26, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi naona kwamba anayetaka jina la mawaziri watajwe naomba atuletee Garama ya RAIS JK anayotumia na rafiki zake wanaompeleka safari kila kukicha. halafu atuambie matumizi yake pia na mapato yake huko anakopeleka bakuli na atuambie akikinga bakuli lake analeta kiasi gani ?.Huyo BWAMBO ameweza kufikisha ujumbe huo kwa wakati unaofaa kabisa kwani viongozi hawafikirii kwanini wamepewa dhamana ya uongozi .
   
Loading...