John, stuka au utaachwa solemba pale Ubungo mataa!

John, stuka au utaachwa solemba pale Ubungo mataa!

Don't underrate John. He told the king that he, the king has been living with hypocrites under one roof but he, John won't tolerate them. Let us wait for a big surprise. It is better to bring down a rotten system and build it afresh than living in it. John you are now the boss so don't listen to them. Good leaders take risks and learn by mistakes. Bomoa ujenge upya maana hapa tulipofika hamna jinsi.

A Good leader?

Leader vs Manager!

There are people with leadership traits, others do not have.
 
Hamjajua hesabu za Pombe ziko zipi,unadhani hajui?anajua sana ila anawalia taiming,Mwanasheria mkuu kurudishwa pale sio ishu ila ishu ni pale akilikologa Magufuli atamtimulia mbali na hapo ndipo fagia fagia ya mabaki mengine ya Mtalii wa anga yatakapoanza.
 
Uzuri wa john huwa anajielewa mwenyewe. aliwahi kuzenguana na mrisho na peter waka retain barua zake za kujiuzuru. wanaweza waka mremote ila siku watakayo kosea botton au betri kuisha ndo mwisho wa sinema john is unpredictable lets wait time will tell

Mkuu umesema sawa lkn kumbuka huku hakuna kukosea, ni kufanya maagizo, hata ukiwa mnyama amelala akiamka atataka kuiina njua, na elewa kwamb hiz ni deal na ulaji
 
John bado mgeni trust me siku akishajua jiko liko wp sebule ipo upande upi na majirani zake ni nani!? Nyumba itakuwa yake
 
Tatizo mnadhani John ni level yenu. Wekeni heshima wacheni ujinga. Nyie mlikuwa wapi kugombea uraisi kama mna Akili sana??
 
Mara hii tu umesahau kwamba ccm kuwa ktk madaraka kipindi hiki wanachukulia km ni golden chance ya wao kurekebisha makosa yao na hivyo kuendelea kuaminiwa, na hio si kazi ya magufuli peke yake, ni kaz ya cabinet nzima ya ccm. Sasa mnaposema kuwa eti atendeshwa kwa remote mmetafakari hayo? Km kushauriwa mambo ya msingi napo nikushikiwa remote bas tuite huo ni msamiati mpya!

Hata hivyo km ccm imejisahau kias hicho na haikuridhika kuona magari ya kuzuia ghasia iliyoyaagiza hayakufanya kazi bas ijaribu kufanya kile kinachosemwa kuhujumiana na kumtenga raisi, ingawa naamini raisi Magufuli si mtu wa kujaribu kumhujumu na kumtenga, atajua tu! Kumbuka John si typical CCM, ila kwake CCM ni daraja tu kuelekea kufanya siasa za kikemia, kwenye kemia hakuna probability wala mizengwe, atakachokifanya hapo itakuwa ndo kutimia kwa ile kauli ya mwalimu kuwa 'upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm'
CCM ina kila wajibu kuhakikisha kuinampa kila aina ya ushirikiano John ili heshima ya chama irudi mahala pake wala si swala la John tu.

John hana cha kupoteza wakicheza anakabidhi nchi kwa UKAWA hata kabla ya kumaliza muhula wake.
Hapo ndipo utakapoelewa maana ya Pombe.

Mnavyotoa maoni nikm vile hamna ibada nyie watu, maana it's too soon kumjudge rais,
Naona baadhi mmekazana kumwombea mabaya, mnafanya kukata mti mlioukalia,

Kwa mawazo mepesi kabisa mtu yupo hapa anaandika porojo zake halaf naye anaona ameshusha nondo na hivyo anatamani rais apitie haka kauzi atoke na mawazo ya kufanyia kazi (lkn lengo lake ni kumchanganya akili rais), hiki ni kichekesho!

Ndg naona umechukizwa sana na watu wanaomwambia ukweli Magufuli....Najua kuna watu wanamuamini sana sababu alivyokuwa anaongoza Wizara sio wewe peke yako hata Mchungaji wangu ana mawazo km yako anatamani Rais aigeuke CCM kwanza napenda kusema jambo 1 kwako na kwa wt wanaomuamini Magufuli ukweli nikwamba alipokuwa kwenye Wizara alijatahidi sana lkn tambueni ile ni Wizara tofauti na uRAIS wenye maslah na watawala uRAIS ni taasisi inayohusisha mambo mengi Nakumbuka CCM nidubwashika kubwa ambalo linaweza kufanya chochote na watu wakashangilia kwahiyo Magufuli ni Rais kupitia ccm na atabaki kuwa mwana CCM ataweza kumwaga povu huku mtaani akiingia kwenye vikao vyao anatulizwa ndg yangu CCM niile ile hata OBAMA aje kugombea kwenye hicho chama hakuna jipya litatokea JPM angekuwa mgombea binafsi lands lkn kuipitia CCM poleni mnaotarajia mapya
 
A Good leader?

Leader vs Manager!

There are people with leadership traits, others do not have.

Our president as per constitution is both a leader and manager because he is an executive president. He can even have several ministries under him.
 
Kuna ukweli kwenye hii maada. Ile cheka ya mwenda zake alipokuwa akimkabidhi Mh. John kijiti inabeba maudhui flani hivi.
in communication skills we say words present 7% of the whole message, vocal 33% and body language 55% kwa tunaofahamu tuliona ujumbe wa mkwele.

Ila JPM nae aliupokea na alimjibu the same so kuna kazi sana kwenye hii transition period, it will take JPM not less than three years to form his own territorial.
 
Mara hii tu umesahau kwamba ccm kuwa ktk madaraka kipindi hiki wanachukulia km ni golden chance ya wao kurekebisha makosa yao na hivyo kuendelea kuaminiwa, na hio si kazi ya magufuli peke yake, ni kaz ya cabinet nzima ya ccm. Sasa mnaposema kuwa eti atendeshwa kwa remote mmetafakari hayo? Km kushauriwa mambo ya msingi napo nikushikiwa remote bas tuite huo ni msamiati mpya!

Hata hivyo km ccm imejisahau kias hicho na haikuridhika kuona magari ya kuzuia ghasia iliyoyaagiza hayakufanya kazi bas ijaribu kufanya kile kinachosemwa kuhujumiana na kumtenga raisi, ingawa naamini raisi Magufuli si mtu wa kujaribu kumhujumu na kumtenga, atajua tu! Kumbuka John si typical CCM, ila kwake CCM ni daraja tu kuelekea kufanya siasa za kikemia, kwenye kemia hakuna probability wala mizengwe, atakachokifanya hapo itakuwa ndo kutimia kwa ile kauli ya mwalimu kuwa 'upinzani wa kweli utatoka ndani ya ccm'
CCM ina kila wajibu kuhakikisha kuinampa kila aina ya ushirikiano John ili heshima ya chama irudi mahala pake wala si swala la John tu.

John hana cha kupoteza wakicheza anakabidhi nchi kwa UKAWA hata kabla ya kumaliza muhula wake.
Hapo ndipo utakapoelewa maana ya Pombe.

Mnavyotoa maoni nikm vile hamna ibada nyie watu, maana it's too soon kumjudge rais,
Naona baadhi mmekazana kumwombea mabaya, mnafanya kukata mti mlioukalia,

Kwa mawazo mepesi kabisa mtu yupo hapa anaandika porojo zake halaf naye anaona ameshusha nondo na hivyo anatamani rais apitie haka kauzi atoke na mawazo ya kufanyia kazi (lkn lengo lake ni kumchanganya akili rais), hiki ni kichekesho!
Mkuu naunga mkono hoja yako, nadhani tusiangalie kila jambo kwa jicho la nje tu na tukawa wasahaulifu wa haraka kudhani kwamba CCM imepita kilaini kwenye uchaguzi huu!

Kama kuna chaguzi zilizo watia kiwewe CCM ni huu uliopita, uliwavuruga kuliko matarajio yao kila kitu kiliwakalia hovyo na hata kusababisha uwe ni uchaguzi wenye gharama kubwa sana kwao.. nimesikia hazina ilikombwa, sishangai ilibidi iwe hivyo. Kwa hiyo huu ni uchaguzi ambao wameponea tundu la sindano tena niseme makosa ya wapinzani wao ndio yaliwasaidia... hasa la kujiaminisha ushindi kwa hisia bila kuweka mipango madhubuti pia kutokuwa na resorces za kutosha.

Kwa sasa CCM lazima iwe team moja kwa sababu madeni ya kuaminiwa yamepanda naweza kusema kwa asilimia 48 kitu ambacho ni kikubwa sana na matokeo yake ni kama comment tunazo ziona humu watu bado hajaanza kurudisha imani ndio kwanza wanaifanyia CCM tathimini upya.

Nacho weza kusema JPM ni unpredictable creature anajua anachokitaka na anakisimamia ni mtiifu ila si muungwana kwa atakae mkwamisha. Kipindi hiki lazima ashikwe mkono na chama ikiwa ni pamoja na mamlaka za Juu Ili kukinusuru chama.

After two to three years ataweza kukiongoza chama na nchi akiwa in charge mkuu. Tumpe muda awatambue maadui wa nje na Ndani katika kutimiza ahadi zake kwetu kwa sasa ni mapema mno.
 
Bilion 2 toka hazina kwenda Muhimbili halafu ndani ya wiki mashine inakufa? Hii kali.
Hizo Bilioni 3 zilikuwa ni kwa ajili ya kulipia madeni wanayodaiwa na hiyo kampuni ya Phillips . Wanadaiwa bilioni 7 kwa hiyo walikuwa wanapunguza tu deni ili waje kutengeneza baada ya Phillips kukataa kuitengeneza sababu ya hilo deni.
 
Uzuri wa john huwa anajielewa mwenyewe. aliwahi kuzenguana na mrisho na peter waka retain barua zake za kujiuzuru. wanaweza waka mremote ila siku watakayo kosea botton au betri kuisha ndo mwisho wa sinema john is unpredictable lets wait time will tell

hahahahahahaaaaaaaa nimekukubali mkuu "the undomitable guy" ila akizubaa wana kula kichwa it will be game over "anahitaji John macho ya bundi
 
umenarrate matukio, hakuna jipya uliloandika.

Ndugu ungeacha tu kuandika ukasoma waliyo andika wenzako au kama unaona unaumia na huu ukweli basi usingefungua kabisa hii thread kuliko kuandika ulichokiandika umejiaibisha.
 
Watoto wa mjini wanasema ukizubaa,utaingizwa kingi.

Napenda kukupa tahadhali ewe mkuu John, unatakiwa ushtuke mapema kwani mambo yanavyokwenda utalala doro!

Mkuu hujiulizi, inakuwaje watu wateuliwe kushika nyazifa kubwa siku tatu kabla ya kukabidhiwa rungu? Tena yule wa mwisho aliteuliwa kuwa katibu tawala pale Lindi siku moja tu kabla hujaapishwa, mwingine ukapewa umwapishe kuwa mshauri wako wa mikataba yote utakayoingia, ikiwa ni masaa 18 tu toka upewe rungu, duh! Kwani hujui kule Kusini kuna nini kinatakiwa?

Haya sasa, leo unatenguwa uteuzi halafu unafanya uteuzi kwa mtu huyo huyo kuwa mbunge, siku hiyo hiyo mtu huyo anajitoa kutaka cheo kile na siku hiyo hiyo anataka kingine hivi ni kweli haya maamuzi ya kiswahili umeyatoa wewe jembe letu John au umebambikiwa?

Haya juzi uneenda kuikagua ile mashine pale hosipitalini, ikatengenezwa, siku tatu tu imeharibika. Tena, imeharibika moyo wake. Kwa kukufafanulia tu ni kuwa, ile mashine imeharibika kifaa kiitwacho (Redio frequence amplifier) ambacho ndio moyo wake, bila hicho hakuna hiyo mashine!! Kwa mujibu wa mtandao wa hiyo kampuni iliyopewa zabuni ya ya ukarabati kifaa hicho kinauzwa usd 97,000! Mil. 200 za madafu, upo mkuu?

Ukienda lesi tena unapigwa kivingine hujashtuka tu?

Mkuu John ngoja nikuache, usiposhtuka sasa, solemba pale Ubungo mataa inakuhusu !

Nasikitika hata atakaoteua kuwa MAWAZIRI ni wale waliopita kwa RUSHWA tena safari hii wamezimwaga hasa.Na kwa uhakika watataka kurudisha pesa zao na kufanya RUSHWA na UFISADI kuwa chakula cha kila siku.

Kwenye hii ya CT SCAN na MRI ni bora angeomba ushauri wa kitaalamu wa kununua mpya kabisa kuliko kutengeneza.

Hapa ameingia kichwa kichwa na kutoka sidhani.Nilifikiri angeliacha BUNGE lifanye uchaguzi wa viongozi wao wenyewe bila kuingiza msukumo,kumbe nilisahau kwamba CCM ni ile ile na mambo ni yale yale,tutaisoma number,tutegemee watanzania wote bila kujali ITIKADI zetu tutaisoma number.

Na leo kosa lakwanza KATIBA imevunjwa maana bunge si la MUUNGANO bali la TANGANYIKA kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom