John Shibuda atangaza rasmi kuachana na CHADEMA

John Shibuda atangaza rasmi kuachana na CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Aibu kubwa kwake, anajua kuwa yeye ni msaliti. Namshauri ajiunge kwenye chama cha sisiem b (Act) Hakika chama kitabaki na wazalendo safi.
 
Hamna adhabu kali kama kupuuzwa. Shibuda alijifanya mjanja akapuuzwa.
 
NCHI HII!! BASI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA agombee urais maana kila mtu tuhuma but for this comment no research take it easy
 
NCHI HII!! BASI MBUNGE WA JIMBO LA BUNDA agombee urais maana kila mtu tuhuma but for this comment no research take it easy

huyo nae ana tuhuma za kunyofoa meno,kucha na jicho la watu tutanyofolewa sana macho huyu jamaa akiupata ukikwete..
 
Teh teh, kwa nini asirudishe kadi ya chadema sasa? Kwa shibuda ni mzigo kwa upande wa upinzani.
 
Tulikwisha sema humu jf kuwa chama ni wanachama. Tabia ya fukuza fukuza haitakisaidia CHADEMA itakiangamiza. Tukaendelea kuwasihi viongozi wa CHADEMA kuwa hakuna hata mmoja kati yao aliye msafi mthili ya theruji, wote wamepungukiwa na utukufu. Tusikilizane, tuvumiliane, tuonyane tusameheane kwa upendo kama wamoja. Tukiwa wamoja adui yetu CCM atatuogopa. Kwa bahati mbaya mwenye akili hujifunza kwa kosa la wengine, mjinga hujfunza kwa kosa lake mwenyewe, lakini mpunbavu hanalo la kujifunza hata yakimkuta.
Sijui viongozi wa chadema watakuwa wapo kundi lipi. Ikiwa kila mtu ataitwa msaliti halahala wasije wakabaki Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Mnadhimu na Msemaji wa chama. Hapo sasa hawa ndiyo watakuwa wasaliti wakubwa wa CHADEMA kwa kukisambalatsha.

Mbona ndugu yangu unapindisha mada? sasa Shibuda huyu kafukuzwa na nani kama sio matendo yake yanamsuta mwenyewe? - Amekuwa akipuuzwa muda wote, alileta za kuleta hapo nyuma kashfa nyingi kwa viongozi wa CDM alifikiiri hao viongozi hayawaumi leo yeye anamlalamikia TL ambaye anafata tu sheria ktk yale mabaya anayofanya.

Shibuda huna ubavu wa kumtishia nyau TL!
 
Itakuwa vizuri CDM ikajiandaa kutafuta mbadala wa Shibuda, na itakuwa vizuri zaidi wakishinda hico kiti alichokuwa anakalia shibuda, kinyume na hapo itamaanisha kuwa CDM wamepoteza katika malumbano yao na Shibuda.kwani ubunge wa Shibuda kwa ticket ya CDM uliongeza idadi wka CDM,sasa ni kiti kimoja ambacho kitapunguza idadi hiyo,Kiongozi mzuri anatakiwa aweke mkakati kuanzia sasa kuhakikisha kiti hicho kinabaki CDM.
Kinyume na hapo zitakuwa porojo. viongozi wa CDM itabidi waepuke porojo hizo come 2015.
 
Ongera CDM huyu shibuda alikuwa anachafua chama,watu wanazungumzia madini yeye anazungumzia pamba kwenye bajeti za madini ili kupoteza mwelekeo wa makamanda wanaomaanisha.
VIVA shibudddda kwa kurudi nyumbani nadhani umejifunza kitu kwamba si kila mahali unaweza kufanya usanii ukafanikiwa.Nadhani umekimbia kuwa mbunge wa mahakama mtarajiwa
 
Michadema mnaimbishwa nyimbo za usaliti, huku chama kinaendelea kujifia
 
Ndugu yangu wa Mjengoni mtu kukutukana sio lazima akuambie kitu fulani chake. Matendo yanaonyesha zaidi maneno. Kazi kubwa ya viongozi wa chama cha ksiasa ni pamoja na kujenga mshikamano wa wanachama ndani ya chama na pia kuwavutia walioko nje ya chama, wangie. Ni wajibu wa viongozi kuweka mazingira mazuri kwa wanachama wake ili wasione haja ya kwenda chama kingine. Hata kama wakikosea, na ni lazima watakosea kwa sababu ni binadamu, waonywe kwa lugha ya staha. Lugha ya kashifa na vitisho haileti mshikamano kwa wanachama. Maridhiano ndani ya chama sio kiashiria cha unyonge kwa viongozi. Katika siasa idadi kubwa ya watu wanaokikubali chama ndiyo mtaji kuliko hata hoja zenye nguvu.
CCM wapo pale kama kunguru anaye subiri panzi waanze kupigana ili yeye aanze kuwadonoa mmoja mmoja. Mnapogombana CHADEMA, CCM wanashangilia. CHADEMA kikipasuka kinaingozea nguvu CCM. Viongozi wenye busara walipaswa wayajue haya mapema. Kwao CCM ni shangwe mwanachama mmoja akikiasi chama chenu au hata akifukuzwa. CHADEMA kikipoteza mbunge mmoja kinapoteza pia wanachama waliompigia mbunge husika pamoja na ruzuku inayotokana na mbunge huyo. Hii ni hasara kwa chama. Asiye liona hili ni kipofu ingawa ana macho. Ni heri kipofu anaweza akapapasa au akanusa kuliko kiongozi wa namna hii. Ukihesabu wanachama wa CHADEMA walioondoka kwa kuondolewa au kujiondoa wenyewe kuanzia mwezi Machi 2014 ni wengi. Mpaka kufikia uchaguzi kuna hatari kubakia wachache zaidi, Lazima tubuni mbinu mbadala ya kuwafanya wanachama wabakie ndani ya chama (retain) . Hakuna jamii ambayo inakosa wasaliti hata ndani ya CCM wapo. Katika harakati zote za ukombozi wasaliti walikuwepo, lakini walishughulikiwa kwa busara sio kwa papara
Mbona ndugu yangu unapindisha mada? sasa Shibuda huyu kafukuzwa na nani kama sio matendo yake yanamsuta mwenyewe? - Amekuwa akipuuzwa muda wote, alileta za kuleta hapo nyuma kashfa nyingi kwa viongozi wa CDM alifikiiri hao viongozi hayawaumi leo yeye anamlalamikia TL ambaye anafata tu sheria ktk yale mabaya anayofanya.

Shibuda huna ubavu wa kumtishia nyau TL!
 
Shibuda quitting CHADEMA is more than a blessing. Shibuda is a great misfit to any reliable political party. He must be considering going to ACT - where all traitors have prepared their graveyard.
 
Itakuwa vizuri CDM ikajiandaa kutafuta mbadala wa Shibuda, na itakuwa vizuri zaidi wakishinda hico kiti alichokuwa anakalia shibuda, kinyume na hapo itamaanisha kuwa CDM wamepoteza katika malumbano yao na Shibuda.kwani ubunge wa Shibuda kwa ticket ya CDM uliongeza idadi wka CDM,sasa ni kiti kimoja ambacho kitapunguza idadi hiyo,Kiongozi mzuri anatakiwa aweke mkakati kuanzia sasa kuhakikisha kiti hicho kinabaki CDM.
Kinyume na hapo zitakuwa porojo. viongozi wa CDM itabidi waepuke porojo hizo come 2015.

Bwana Kimweri umetoa funzo muhimu sana kwa Chadema kuwa lengo liwe kukichukua tena kiti kinachoachwa na Shibuda. Ahueni ya kuachana nae tu haitakisaidia chama kama hawatafanya maandalizi kuanzia sasa kwa kumuandaa mtu sahihi, anaekubalika jimboni na mwenye uwezo wa kupambana na Shibuda kwenye majukwaa. Kinyume na hivyo ni kuwa chama kitakuwa kimepoteza jimbo na kupungukiwa na idadi ya wabunge. Uchaguzi ujao hautakuwa lelemama unahitaji maandalizi mapema haswa kwa vyama vya upinzani.Kwangu ningeshauri ukawa uimarishwe na waingie uchaguzi mkuu wakiwa wamoja na endapo isipopatikana katiba mpya waachane na suala la kugombea uraisi ila wajikite kujiongezea idadi ya wabunge.
 
Najaribu kuukadiria uwezo wa kufikiri wa huyu jamaa, watu anaoongea nao, hali ya siasa ilivyo, uwezo wa kushawishi ili aaminiwe na wenye upeo mkubwa, nakosa kumpa jina linalomfaa!!! Kwa ujumla heri kijana mwerevu kuliko mzee mjinga :angry:.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom