John Shibuda atangaza rasmi kuachana na CHADEMA

John Shibuda atangaza rasmi kuachana na CHADEMA

Status
Not open for further replies.
Tunamtaka arudishe kadi yetu na si kupiga kelele kwenye magazeti ya kufungia vitumbua,yeye kama mwamba ajiunge na chama kingine na kurudisha kadi ya cdm na wasaliti wote wangefanya hivyo wangeonekana angalau wanajisimamia

kadi yenu haina thamani siku hizi mkuu hata akirudisha
 
Mbaya zaidi hata CCM wenyewe hawamtaki huyu bwana. maana wana jua hana busara na hana namna zy kufunga domo lake au kujua nini cha kuongea...huyu ni muimba mashairi ndiyo jambno la maan anaweza kufanya
 
Ukiona wanaume wana kutenga kwenye maamuzi jua wameisha tambua hufai, juilize kwanini wengine washirikishwe... basi kama una hekima unaweza kujirekebisha, lakini si kukaa na kulaumu upppuzi, shibuda kuondoka ndani ya chadema ni sherehe kubwa sana...tatizo la CDM wamekuwa wakiwafuga dizaini hizi za majanga kwa muda mpaka wanaota mizizi...Shibuda aende tu kuwa ndani ya chama ni matizo...

hii ndo inaitwa Sizitaki Mbichi Hizi
 
Tunamtaka arudishe kadi yetu na si kupiga kelele kwenye magazeti ya kufungia vitumbua,yeye kama mwamba ajiunge na chama kingine na kurudisha kadi ya cdm na wasaliti wote wangefanya hivyo wangeonekana angalau wanajisimamia

Kumbe walimfata wap wenyewe kumuomba?? By the way kwa Maneno aliyosema haina haja ya kurudisha kadi mfukuzeni Muone Moto wake
 
Ukiwa mnafiki ujanani basi ukiwa mzee utakuwa mwanga! Ndivyo alivyo Shibuda kwa sasa! anakula matunda ya 'ujanani'
 
Hii ni nzuri kwa afya ya chama,ni DARWINISM: natural selection/survival of the fittest.
 
Mbunge wa Maswa Magharibi (Chadema), John Shibuda amesema katika suala la Katiba Mpya hawezi kuitwa ‘kubwa jinga’ na hataweza kuunga mkono hoja za Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wa kutaka muundo wa serikali tatu.

Akizungumza na wazee wa mji mdogo wa Malampaka mjini hapa, Shibuda alisema haelewi maana ya neno Ukawa kama mnyama ama la, bali hatokuwa ‘kubwa jinga’ kwani hoja za serikali tatu hazina mashiko kwake.

“Nafahamu wajibu wangu kama mbunge, nitasimamia maslahi bungeni na kuunga mkono serikali mbili na kamwe si tatu zinazopigiwa kelele na Ukawa,” alisema Shibuda.

Alisema anarejea bungeni kuungana na wajumbe wa bunge hilo la katiba kuhakikisha anasaidia kuwapo kwa serikali mbili ambazo alidai zitasaidia hatma ya Zanzibar na kudumu kwa Muuganno wa Bara na Visiwani.

Alisema chanzo cha kuwapo kwa Ukawa ni kwa CCM kutokuwa wa wazi na wakweli kwa viongozi na wabunge wake hali ambayo imesababisha kuwepo kwa Ukawa inayong’ang’ania kuwepo kwa serikali tatu.

Shibuda alisema haungi mkono kuwapo kwa serikali tatu kwa kile alichodai kutowatendea haki Wazanzibar na ni bora kukawa na serikali moja kuliko tatu.

Katika kuhakikisha hilo, mbunge huyo ambaye ametangaza kujiondoa Chadema, alisema hatawatendea haki Wazanzibar iwapo atawaunga mkono Ukawa.

“Siyo kubwa jinga miye, siwezi kukubali kuwaumiza wazanzibar hao ambao ni ndugu zetu, kuna wanyamwezi, waha na wasukuma huko visiwani kabla na baada ya biashara ya utumwa,” alisema.

Shibuda alisema faida kubwa ya Ukawa ni mambo ya Zanzibar na siyo maslahi ya Watanzania ambao alisema kwa historia wanatoka Bara kabla ya biashara ya utumwa.

Akizungumzia misimamo yake baada ya kurejea katika bunge maalum la katiba, Shibuda alisema anapeleka nguvu mpya kwa wajumbe wa wanaotetea haki za wafugaji na wakulima ndani ya bunge hilo.





CHANZO: NIPASHE
 
Shibuda ni kubwa jinga na ni kubwa la majinga nchini na dunia nzima hata machizi wanamjua.
 
Kumbe hata mwenyewe ameshajijua kwamba mambo anayofanya yanafanywa na Kubwajinga tu!
 
Mtu yeyote anayepigia chapuo serikali 2 haitakii mema tanganyika wala zanzibar. Shibuda ni maccm yaleyale kwa koti la upinzani!
 
Kubwajinga anachekesha sana, siku zote alikuwa wapi asiende kukinga kilo 3
 
Shibuda ni tahira fulani ndo maana alishirikiana na akina policcm kubambikizia akina kamanda kileo kuwambambikizia kesi za ugaidi ni mnonko
 
Sms yake imewapata vizur mmebaki kutoa mapovu na matusi. Mnataka serikali 3 ili mpate vya mteremko pasipo kuangalia maslahi mapana ya taifa...

Kwa taarifa yenu tukitoka serikali 2 tunaelekea 1, sisi tunasonga kwa kwenda mbele badala ya kurudi nyuma kwenye 3 kama mnavyotaka nyie.

Hatujadili katiba ya kugawana vyeo ile ya watu 17,0000/=, bali tunajadili katiba ya watu 45,000,000/=.
 
Sms yake imewapata vizur
mmebaki kutoa mapovu na matusi. Mnataka serikali 3 ili mpate vya
mteremko pasipo kuangalia maslahi mapana ya taifa...

Kwa taarifa yenu tukitoka serikali 2 tunaelekea 1, sisi tunasonga kwa
kwenda mbele badala ya kurudi nyuma kwenye 3 kama mnavyotaka nyie.

Hatujadili katiba ya kugawana vyeo ile ya watu 17,0000/=, bali
tunajadili katiba ya watu 45,000,000/=.

Hahaaaa unakata ile ya 17,000 halafu unakubari ya watu 600 kweli na wewe kubwa jinga
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom