Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Magufuli


Baada ya kusoma mwanzo wa habari hii nimekuwa na mswali mengi kuliko majibu hapa chini nitajaribu kuyapitia tena……..

Habari zilizopatikana ndani ya wakala wa Majengo ya Serikali (TBA), zimethibitishia Rai wiki hii kwamba Magufuli alihakikisha anashiriki kama Mwenyekiti katika zoezi zima la kuuza nyumba, ambalo kimsingi lilistahili kusimamiwa na Mtendaji Mkuu wa TBA.


Kwa nini mtendaji mkuu wa TBA hakulishughulikia – Je mwandishi alimuhoji kuhusu suala hilo, kama ndivyo kwa nini asiandikwe jina lake na maelezo yake?


Kwa mujibu wa vyanzo kadhaa vya habari ndani ya TBA, Magufuli alifanya kila aina ya ‘fujo' katika zoezi la kuuza nyumba hizo, wakati mwingine akibatilisha maamuzi yaliyofanywa na Kamati ya TBA ya kuuza nyumba hizo, akiwapangia watu nyumba kwa utashi wake na wakati mwingine akiwakemea wale wote waliomshauri kinyume na matakwa.

Alifanya fujo zipi kwa mfano? Kama alivyosema hapo juu yeye alikuwa mwenyekiti je uamuzi ulitolewa na nani tena wakati yeye ni mwenyekiti -… alikuwa wapi?



Ni chini ya utaratibu huo, habari zinaeleza kwamba Magufuli, aliyabeba yeye mwenyewe mafaili ya ndugu zake; Musa Magufuli ambaye ni mdogo wake, na Sundi Malomo ambaye ni mzazi mwenzake na kuwalazimisha watendaji wa TBA wafuate matakwa yake katika kuwapatia nyumba ndugu zake hao.



nafikiri huu ni uongo, kama wewe unataka kumpa nyumba ndugu huna sababu ya kubeba mafaili – kama kuna ushahidi utolewe kwa wazi wazi.



Habari hizo zinaeleza kwamba awali Mtendaji Mkuu wa TBA alimshauri Magufuli kwamba suala la mauzo ya nyumba kwa ndugu zake ni kinyume cha utaratibu. Hata hivyo, imeelezwa kwamba Magufuli alilazimisha huku akisema mdogo wake hana tatizo kwa sababu alikuwa tayari mfanyakazi wa Serikali.


Mtendaji mkuu, yeye hakuwa mwenyekiti sasa ubishi huu ulitokea wapi? Kwenye kikao au katika misingi ipi?


Musa aliajiriwa kwa mkataba wa miezi mitatu, baada ya mwezi mmoja akauziwa nyumba na baada ya miezi miwili akaacha kazi.

"Kwa upande wa Sundi, kwanza ilikuwa Sundi auziwe nyumba moja kwa moja. Lakini Magufuli alipoonywa akashtuka na kusema suala hilo aachiwe yeye mwenyewe. Na ndipo akaibuka na jina la Stanley Manongi kwamba ndiye mnunuzi halisi na baba yake Sundi," vinasema vyanzo hivyo vya habari, vingine ambavyo vilishiriki moja kwa moja katika mchakato wa uuzaji nyumba hizo.


Tarehe za kuajiriwa na watu waliomuajiri na siku alipoacha kazi, hearsay without substancial evidence.


Habari hizo zinaendelea kueleza kwamba baadaye, Sundi alishtuka akitilia shaka uaminifu wa Manongi, kwamba angeweza kumdhulumu nyumba hiyo.

"Ndipo Magufuli aliibuka na mpango wa Sundi kuwa mtoto wa Manongi na mrithi wake na kisha kwa kuhakikisha kwamba hakuna dhuluma yoyote, mtoto wa Sundi naye akarithishwa na kama mrithi wa pili," chanzo hicho cha habari kinaeleza.


Kwa hiyo anataka kutueleza kwamba yeye Magufuli kuuza nyumba mbili tu kwa hawa ndugu zake kumechukua muda wote huu wakati yeye ni mwenyekiti? Unbelievable. Kwa sababu bongo pale ukitaka kufanya mambo yako huna sababu ya kufanya hivi tunavyoambiwa.


Chini ya sheria ya Executive Agency Act No. 30 ya mwaka 1997, TBA ilipewa madaraka yote ya kuuza nyumba za Serikali, kujenga nyumba mpya, kuzikarabati zilizopo pamoja na kugawa nyumba za madaraja A, B na C kwa wafanyakazi wa Serikali.

Sheria hiyo inaipa mamlaka ya kipekee ya kufanya shughuli zote bila kuingiliwa na chombo chochote.


Chini ya sheria hiyo, Waziri anaruhusiwa kuteua wajumbe wa bodi ya ushauri watakaomshauri Katibu Mkuu wa Wizara juu ya namna nzuri ya TBA kusimamia mamlaka yake.

Hadi Machi mwaka huu, wajumbe hao walikuwa ni J. Kijazi, E. Lipambila, E. Lugwisha, Msangi, E. Mwakalinga, D. Kisasi, P. Ncheye, F. Werema na A. Bukuku.

Hata hivyo, sheria haitoi nafasi yoyote kwa Waziri kusimamia shughuli za uuzwaji au upangaji wa nyumba za serikali.

Mtendaji Mkuu wa TBA Togolayi Makumba Kimweri, alipoulizwa kupitia kwa Katibu Muhtasi wake, alimwambia mwandishi wa Rai aandike maswali kisha asubiri kuruhusiwa kuingia ndani ya ofisi.


Sio kweli kwamba mtendaji mkuu wa TBA alimkimbia mwandishi wa Rai – Tupe jina la mwandishi huyo na siku na tarehe ili kuthibitisha kashfa hii pamoja na maswali yaliyoandaliwa (kwa kweli hii habari haina credibility)



Pamoja na maoni ya wanabodi hapo juu wote, (heshima kwenu) issue ambazo zimewekwa ni sawa kabisa kuhoji. Mimi kwa mawazo yangu binafsi naona ndio maana hata Magufuli mwenyewe haoni sababu ya kuzijibu kwa sababu ikitazama allegations zilizotolewa in content hazina credibility at all.

Sina sababu ya kumtetea Magufuli wala sisemi hana walakini au haandamwi ni mtu anayeishi bongo hivyo anahitaji kuishi kama wengine.

Without going into details kwa kukisia nyumba ambazo ameziuza kwa ndugu kama ni kweli (two of them) lets put the value at USA $0.2 million sio sawa na IPTL, Richmond and the like.

I think we better move on unless more evidence emerges on this or if there is any credible evidence.



Wacha
 
wizara ya katiba na ile ya nje ndio sehemu ya kuwaweka bench watu,mnakumbuka pia aliyekuwa kamishna wa operesheni na mafunzo LAURIAN TIBASANA bado yupo corridor pale wizara ya katiba,sijui ana kazi gani mwenzie adadi kashapewa ulaji
 
Madiwani wataka Magufuli ajiuzulu

2007-02-17 11:03:18
Na Frank Mbunda


Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wamemtaka Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, kujiuzulu kutokana na kile walichodai aliingilia mamlaka ya manispaa hiyo kutoa hati kwa mmiliki wa mgahawa wa Rose Garden.

Wakizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika jana chini ya Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Salum Londa, madiwani hao walisema hatua ya Waziri Magufuli ni sawa na upuuzwaji wa mamlaka nyingine za serikali.

Madiwani waliotoa hoja ya kumtaka Waziri Magufuli aachie ngazi ni Diwani wa Kata ya Kimara, Bw Mohammed Mringo, Diwani wa Kata Kibamba, Bw Ignas Mwitula, Diwani wa Kata ya Makuburi, Bw Busee Gigabase na Diwani wa Kata ya Mabibo, Bw Kassim Lema.

Aidha, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Bw Londa pia aliwaunga mkono Madiwani hao.

Diwani wa Kata ya Kimara, Mringo alisema hatua ya Waziri huyo kuruhusu kutolewa hati ya umiliki wa eneo hilo, ni sawa na kuwapuuza madiwani waliozuia eneo hilo la barabara kutumiwa kama makazi na biashara.

?Mheshimiwa Meya na Mwenyekiti, hapa inaonekana kuna aina fulani ya matusi, sisi ni madiwani katika mamlaka halali kwa mujibu wa sheria, lakini hapa tumedhalilishwa na Waziri wa Ardhi, alisema Bw. Mringo.

Diwani huyo alisema kwamba baraza hilo linapaswa kutoa tamko kali la kulaani uamuzi wa kupuuzwa kwa madaraka na mamlaka yake kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha Manispaa hiyo, hatua iliyochukuliwa na Waziri huyo.

``Hivi kwa nini sisi kama madiwani tunaweza kukaa katika vikao kama hivi humo ndani kwa dhamana kubwa kutoka kwa wananchi waliotuchagua, tukamua kwa mujibu wa sheria kuzuia jambo lakini baadaye tukapingwa na kudharauliwa kiasi hiki,`` alisema Bw. Mringo.

Diwani wa Kata ya Kibamba Bw. Ignas Mwitula, alilalamikia hatua hiyo na kuifafanisha na uchokozi kwa mamlaka halali na kutaka Waziri huyo aifute hati aliyoitoa au ajiuzulu wadhifa wake.

``Msimamo wetu sisi madiwani wa Manispaa ya Kinondoni ni kumtaka Waziri Magufuli kujiuzulu nafasi aliyonayo hivi sasa, au aifute hati aliyoitoa, kwani ni kinyume cha sheria na taratibu,``alisema Diwani Mwitula.

Madiwani wengine waliochangia suala hilo na kusisitiza kumtaka Waziri Magufuli kuitema nafasi hiyo ni Bw. Lema, wa Kata ya Mabibo na Bw. Busee Gigabase wa Kata ya Makuburi.

Madiwani hao kwa pamoja walisema kitendo cha wizara kutoa hati kwa mmiliki wa mgahawa huo ni sawa na kuingilia uhuru, kulinyima au kuliondolea haki baraza la madiwani kushughulikia masuala ya ndani.

``Sina hakika kama tunaweza kutembea kifua mbele kama Madiwani, kwani tayari tunapanga jambo hapa, Waziri na mamlaka nyingine zinaingilia jambo hilo na kusitisha kasi yetu,`` alisema Bw. Lema.

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bw. Hassan Kattanga, alisema ndani ya kikao hicho kuwa watendaji wake wanashindwa kutekeleza azma ya kuvunja mgahawa huo, kutokana na kinga iliyotolewa na Waziri.

``Tunashindwa kutekeleza yale yaliyofikiwa na baraza la madiwani, kwani inaonekana kuwa yupo pale kihalali, amepewa hati na wizara``, alisema Bw. Kattanga.

Hata hivyo, akionyesha kuunga mkono malalamiko ya madiwani wake Meya Londa, alisema suala hilo limewavuruga watendaji na madiwani wengi na kuanza kuwapotezea heshima.

``Wapo wanaodhani kwamba suala hili lilikuwa likifanywa na Manispaa kwa ajili ya kutisha ili kujipatia kitu kutoka kwa mmiliki huyu, lakini sio kweli, tulifikia uamuzi huo kulingana na taratibu zetu, ``alisema Bw. Londa.

Meya huyo alimuagiza mkurugenzi kuendelea na mkakati wa kuuvunja mgahawa huyo licha ya kuwapo kwa hati iliyotolewa na Waziri, akidai kitendo hicho kimefanywa bila kuishirikisha manispaa na mmiliki hakupewa ofa,`` alisema Bw. Londa.

``Lile sio eneo la biashara wala makazi, kwa hiyo sisi kama mamlaka kamili tutaendelea na utaratibu wetu, hatuwezi kuogopa kwani haya tunayafanya kwa mujibu wa kanuni, sheria na taratibu za uendeshaji wa halmashauri,`` alisema Bw. Londa.

SOURCE: Nipashe
 
Hawa kweli wanataka kumuua huyu Mh. KWANI AMERUDI TU KWA MATATIZO YA UGONJWA WA MOYO,TAYARI WANAGONGA MSUMARI KWENYE KIDONDA AU NDIYO BAADHI YAO WALIOVUMISHA AMEFARIKI NINI? Kiubinadaamu nafikiri wangempa muda hata kama ni mkosaji Halafu wamfahamishe kupitia Ofisi yake.
 
MADIWANI wa Manispaa ya Kinondoni, wamesema uamuzi wao wa kuibomoa baa maarufu ya Rose Garden iliyopo Mikocheni jijini Dar es Salaam uko pale pale.

Uamuzi huo ni sehemu ya maazimio ya kikao cha Baraza la Madiwani uliotangazwa jana, kueleza namna wanavyoshangazwa na hatua ya Waziri wa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli kutoa hati ya kiwanja kwa mmiliki wa baa hiyo maarufu, hali ikijulikana wazi kwamba, sehemu hiyo iko katika eneo la hifadhi ya barabara.

Madiwani hao walitoa msimamo huo jana kwenye Ukumbi wa Manispaa wakati wa uwasilishaji wa taarifa za utekelezaji wa kamati mbalimbali kwa kipindi cha miezi mitatu.

Kabla ya kuhitimisha kikao hicho, Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Hassan Katanga alisema waziri mwenye dhamana ya ardhi, alitoa hati ya umiliki wa eneo la Rose Garden wakati manispaa ilishatoa uamuzi wa kubomoa majengo katika eneo hilo.

“Hili eneo lina utata kisheria. Zilikuwa zimebaki siku tatu kabla ya kwenda kuvunja majengo yale… waziri akampa leseni yule bwana mwenye Rose Garden, na sasa anamiliki kihalali.

“Kama mnavyojua waheshimiwa madiwani, yule bwana alitufungulia kesi mahakamani, akilazimisha kupewa umiliki wa eneo la hifadhi ya barabara… baada ya kupata hati ya kumiliki eneo kutoka kwa waziri, akafuta kesi, hivyo mahakama ikatupa mamlaka ya kuvunja,” alisema Katanga.

Diwani wa Kata ya Makuburi, aliyejitambulisha kwa jina moja la Batenga, alisema: “Ni lazima mamlaka ya juu iheshimu uamuzi wa madiwani. Tunataka waziri aliyehusika na hili ajiuzulu ili kuondoa hizi ‘double allocation’ (ugawaji viwanja mara mbili).

“Huku ni kuingiliana kiutawala, kama anashindwa kuheshimu uamuzi wa madiwani, atuambie mipaka ya utendaji wetu. Kuendelea kutudharau sisi ni kuwapa kiburi wenye fedha.”

Naye, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa, alisema aliwahi kwenda kwa waziri anayehusika kuzungumzia suala hili, lakini hakuonyesha ushirikiano kwa kutoa majibu ya kukatisha tamaa na kuwafuta kazi baadhi ya watumishi wa chini, aliodai wanavujisha siri za wizara.

“Nakumbuka tuliwahi kwenda kwa waziri anayehusika katika kutafuta suluhu ya hili, nilikuwa na Mheshimiwa Charles Keenja, Janeth Kahama, na baadhi ya wabunge wengine.

“Majibu tuliyopata siku hiyo yanasikitisha, huwezi kuamini kama ni kiongozi mkubwa serikalini… tena baadhi ya wafanyakazi wa chini walifukuzwa kazi kwa madai kuwa walivujisha siri za waziri,” alisema Londa.

Septemba 23, mwaka jana, baraza hilo lilikaa kupinga uamuzi wa Waziri Magufuli kuingilia uhuru wa mahakama kwa kutoa kibali cha umiliki wa eneo la Rose Garden lililopo kwenye ramani namba E 3201220 ambalo ni hifadhi ya barabara.

Mgogoro wa eneo hilo ulianza mwaka 1995 na kushirikisha viongozi wa juu wa serikali bila kuwashirikisha manispaa.
 
hodi hodi,
alikuwa airport kumuaga muungwana hivyo hiyo ni dalili kwamba kapona na yuko fit kufanya kazi.
 
Well,
Ikiwa alikiuka sheria hapa sina la kutetea zaidi ya kumuomba afuate sheria.

Kibaya zaidi ni kwamba hawa wamemshikia bango hali hakuna plan wala fedha za ujenzi wa barabara hiyo. Wengi tumepoteza viwanja ktk mazingira kama haya kiasi kwamba barabara hazikujengwa na viwanja kugawiwa upya.
 
I dont understand this guy Kazi ndiyo -------.Can he quote any example where Magufli cancelled a BOMOA BOMOA order because the occupant was sick or aged , with nowhere to go. Dont worry my friend these are Gods chosen people.
 
hapa bwana madiwani wasitudanganye na umbeya wao,raha ya bongo bwana ni fitina juu ya fitina,huyo mringo kapata udiwani kwa fitina.
 
Hapa pana fuka moshi .Wacha tukae pembeni tuangalie. Je kuna umtandao haid chini ? Maana jamaa alikuwa analia namafiga matatu ndiyo haya sasa yanachomoa makucha ?
 
Hivi Tanzania kweli tumefika hapa? Hata mmiliki wa baa, tena baa iliyokwenye hifadhi ya barabara anaweza ku - influence maamuzi ya Waziri? Mungu tunusuru na hili janga na balaa.... HATA MUUZA KILEVI HAVUMI KUMBE NAYE YUMO?

Kwa mnaoijua Rose Garden jinsi ilivyoanza palikuwa na bustani ya mbegu za miti na maua... mwenye baa hiyo ndo alikoanzia.

TANROADS WANASEMAJE?
 
Kumbe ule ujumbe wa kifo cha Magufuli uliotanda Dar ulianzia huku? Hatari sana!
Mbona uongozi wa Kinondoni wana matatizo sana? Hivi lile ghorofa lililoamriwa kuvunjwa mwanzoni mwa mwaka jana lilishavunjwa?
Hawa madiwani ni njaa tu ndiyo inayowatuma.
 
Pamina na njaa lazima kuangalia kama kweli habari za kuhusika Magufuli ni za kweli ama ni njaa na uana mtanbdao ?
 
hapa bwana madiwani wasitudanganye na umbeya wao,raha ya bongo bwana ni fitina juu ya fitina,huyo mringo kapata udiwani kwa fitina.

Katibu Tarafa,

Umbea na uongo wa hawa madiwani wetu ni nini. TUNACHOJIULIZA HAPA INAKUWAJE WAZIRI MOGO ANABATILISHA AMRI ALIYOTOA WAZIRI MKUU WA KUBOMOA BUSINESS PREMISES ZOTE ZILIZOJENGWA NJE YA MAENEO YALIYOPIMWA. Sisi tunaoishi Dar na kuijua mno ndicho kinchotushangaza.
 
Wambwanda,
Kama kulikuwepo na bustani ya miti na maua, je wakati huo haikuwa kosa kuwepo hiyo bustani?
Rose Garden ni biashara kama ilivyokuwa hiyo ya maua! na sidhani kama tatizo la kiwanja hiki ni mfanya biashara gani inamiliki kiwanja.
 
sasa jamani nyie mnadhani magufuli atajibu nini ? mliokuwepo bongo naombeni mtugee info: kwani, huyumagufuli, na hao madiwani wote wapo kundi moja ndani ya ccm ? je viongozi wa ngazi za juu watasema lolote kuhusiana na hili ? tusubiri tuone !!
 
Kuna haja ya kutafuta undani kulikoni!!Magufuli kweli kumkatia mtu kipande cha barabara!!ILa nao hawa madiwani wanakuja juu baada ya kuingiliwa ulaji,watuambie na hizo beach ambazo sasa wazawa hawarusiwi kwenda kupata upepo na kupunguza mawazo ya maisha magumu nani ajiuzulu.

Wambandwa unashangaa nini ndugu yangu, tumeshapita hapo,ila mie naamini kuna mkono wa zaidi ya Magufuli.
 
I dont understand this guy Kazi ndiyo -------.Can he quote any example where Magufli cancelled a BOMOA BOMOA order because the occupant was sick or aged , with nowhere to go. Dont worry my friend these are Gods chosen people.

Sijasema kama amekosea asiadhibiwe lakini kilichonifanya niwe na wasiwasi na hawa madiwani ni kule kukurupuka kwao kwani hii rose garden ni ya leo?Toka hata magufuli hajawa waziri wa hiyo wizara Rose garden ilikuwepo ,Sasa ni nani alimpa huyo rose garden ajenge pale?Na huenda kama sikosei nihao watu wa HALMASHAURI,Kwa mnaoijua Rose Garden mtakubalina nami.Mimi sipo hapa kumfurahisha yeye au mkosaji yeyote, Lakini nikiliangalia hili swala ndiyo nachelea kusema isije ikawa ndiyo hao kwa tofauti zao walimzushia kifo.Kwa siasa za bongo ya leo inawezekana japo sina hakika ni katika kulitazama jambo hili kwa pande zote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom