John Mnyika: Sera ya Majimbo ya CHADEMA siri ya Maendeleo

John Mnyika: Sera ya Majimbo ya CHADEMA siri ya Maendeleo

Mkuu tuambie Ni nchi ngapi za Afrika (iwe na isiyokuwa ya Majimbo) iliyotulia? Ili hoja yako iwe na Mashiko

Ama kweli kuna watu mna akili za punguani; mimi mpaka nikasema nilichosema ujue nafahamu sera ya majimbo hazina mshiko Afrika zaidi ya kusababisha migongano ya kijamii; sasa wewe unayedai Tanzania tufuate mfumo ambao hata hatuelewi ndio fanya utafiti wako uje na majibu ya kutuonyesha Tanzania tutanufaika vipi na sera ya majimbo; kama huelewi ama hujui rudi tena jamvini tukueleze; huyo Mnyika ni mtupu hana anachojua nenda kamuulize uone kama atakupa majibu.

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Mkuu chama,
Hao wakongwe uliowataja ni watu makini sana lakini bahati mbaya wamekimbizwa...siku hizi wanatoa michango yao kule Great Thinkers.

Mkuu Ritz
Wakongwe wangu Mkandara na Nguruvi3 wao wanaimba vanga makamanda wa Chadema wanapiga tokomile ni kujichanganya kutupu jamvi wamelikimbia!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Hebu anzisheni thread yenu muitane au pigianeni simu huwezi kujitegemea bila kuita chama ?

Mkuu Precise pangolin
Kikosi cha chama na Ritz kimekuwa tishio kwako; unao makamanda wengi tu humu jamvini suka kikosi sisi tupo tayari kukabiliana na makamanda wako tena nakuruhusu tengeneza cha watu 100

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Last edited by a moderator:
Biznocrats,

..hebu tueleze ni mikoa gani ilikuwa inainyonya mikoa ya kusini.

..mikoa ya kusini ilikuwa na zao la korosho ambalo lilikufa kutokana na utekelezaji mbaya wa zoezi la vijiji vya ujamaa.

..sasa baada ya korosho kufa ni kitu gani ambacho unaweza kusema kilikuwa kinatoka kusini na kwenda kuendeleza maeneo mengine ya Tanzania??

Kwanza kabisa ningependa kusema kwamba hoja ya msingi hapa ni je tunahitaji majimbo au hapana. Nimejenga hoja hizo zote ili kuonyesha kwamba utawala wa majimbo si sahihi kwetu kwa sasa. Sasa ukitaka kujibu hoja yangu kiuhalisia lazima uanze kwa kuelezea unakubaliana na mtazamo huo wa CHAUMMA au la. Baada ya hapo unaweza kuweka hoja yako kama hii kwamba ndio inayokufanya kwa nini uamini utawala wa majimbo unafaa. Kwa hiyo rudi kwanza kwenye mada yangu ya msingi uichambue kitija kama nilivyoeleza. Huu usanii wa kuruka hoja ya msingi na kuamua kushambulia matawi ya hoja kama ninavyoona wana JF wengi wanavyofanya hauwezi kuwaacha wafuatiliaji mada wawe focused kwenye issue ya msingi iliyokuwa posted.
 
Kama sera za kikoloni mmeshindwa kuzitumia kuiletea nchi maendeleo,ni wakati muafaka wa kutumia sera mbadala za majimbo nazo zitatutoa hapa tulipo na kutupa maendeleo mbadala.Mabadiliko katika nchi yetu kwa sasa ni lazima ili tuondokane na umaskini wa kulazimishiwa na kikundi kidogo cha watu wachache.

Nipe mfano wa nchi 3 Afrika zilizofanikiwa kwa sera ya Majimbo inaonekana hao walimu wenu wametamka neno sera ya majimbo bila kutoa ufafanuzi

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Nipe mfano wa nchi 3 Afrika zilizofanikiwa kwa sera ya Majimbo inaonekana hao walimu wenu wametamka neno sera ya majimbo bila kutoa ufafanuzi

Chama
Gongo la mboto DSM

Hawezi kujibu hilo.
 
Biznocrats,

..hebu tueleze ni mikoa gani ilikuwa inainyonya mikoa ya kusini.

..mikoa ya kusini ilikuwa na zao la korosho ambalo lilikufa kutokana na utekelezaji mbaya wa zoezi la vijiji vya ujamaa.

..sasa baada ya korosho kufa ni kitu gani ambacho unaweza kusema kilikuwa kinatoka kusini na kwenda kuendeleza maeneo mengine ya Tanzania??

Suala la msingi hapa ni kwamba CHAUMMA imejenga hoja dhidi ya utawala wa majimbo na imezitumia hoj a zote hizo including hiyo uliyoiraise hapa kama sababu kwa nini utawala wa majimbo hautufai kwa sasa. Kama hukubaliani
na hoja yangu, basi anza kwanza kwa kuikataa halafu kama unaona hiyo sababu moja uliyotoa inatosha then nitakujibu kwanza hiyo hoja yako halafu nitaelezea kwa nini bado naamini kwenye hoja yangu ya msingi.

Suala la kuacha mada muhimu bila kujibiwa na kukimbilia kwenye matawi ambayo unadhani ni rahisi kuyajibu halisaidii JF kwani linawatoa audience kwenye mada ya msingi na kuwapoteza kwenye conclusion ambayo ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu. Naelewa kwamba huu ni utambaduni wa members wengi wa JF lakini hauna tija kwa hoja zitakazosaidia wafuatiliaji wa JF kufanya maamuzi ya msingi kwa mustakabali wa nchi yetu.
 
Sera za majimbo ni ubaguzi wa rasilimali ni hatari sana.

Hivi wewe ni Mzalendo kweli? Unataka Watanzania waachiwe mashimo kama kule mererani, Geita, Kahama na nyamongo bila ya kufaidika na rasilimali zao? Sehemu zote zenye madini serikali wametenga kama eneo la hifadhi; mswahili akionekana anachimba madini hayo anakula shaba au kifungo kwa kisingizio cha kuharibu mazingira...Tembelea Geita ujionee mwenyewe sera zenu za kikuwadi.

ILA cha kustaajabisha Mzungu Mgeni huwa wanaruhusiwa kuchimba madini hadi kwenye hifadhi za Taifa (Uranium) kwa kisingizio cha MUWEKEZAJI na mikataba inakuwa SIRI...

Sera ya Majimbo ni muhimu sana kwa manufaa ya Watanzania wasasa na vizazi vijavyo...hivi ninyi makuwadi hamuoni haya? Aliwahi kuja CEO wa Barrick Geita nusura azirai kwa kushangaa umasikini uliokithiri, matarajio yake ilikuwa kuona CITY OF GOLD, High rising towers, lots of business activities zinazojumuisha watu wa mataifa ....

CCM ni JANGA KWA WATANZANIA....
 
Hii makala wala usingeileta huku, imekaa kishabiki na imepindisha ukweli. Tatizo la pipeline hiyo ni mazingira wala siyo kutofaidika kiuchumi. Ni environmental degradation ndiyo iliyofanya watu wapinge ... na wengi wao wala hawakai maeneo ambayo pipeline hiyo ingepita.

Nashukuru mkuu Kobelo kwa masahihisho.
Hata baada ya kuweka uharibifu wa mazingira kuwa sababu ya mradi husika kupata ukinzani,mantiki ya hoja ya M.M.Mwanakijiji inabaki palepale:wananchi wa maeneo husika walipinga mradi kwa kuwa hawakushirikishwa na watawala katika hatua za awali za mradi na pia watawala kushindwa kutambua na kuheshimu hisia na matakwa yao baada ya kuonyesha ukinzani baada ya mradi kuanza kutekelezwa.
Mfano hapo juu unatudokeza suala muhimu kuhusu Sera ya Majimbo:ushirikishwaji na ushiriki wa local community katika kuamua mustakabali wa maisha yao.
Ni wazi,kuwa ,moja ya matokeo chanya ya sera ya majimbo ni kuimarisha na kukuza utamaduni wa kidemokrasia ambao msingi wake mkuu ni ushiriki wa wananachi katika michakato mbalimbali ya maendeleo.
 
Mkuu MIZAMBWA....Tukiachilia mbali itikadi zetu......suala la gesi ya Mtwara linahitaji takwimu nyingi za kitaalam (kiteknologia) ili liweze kujadilika hapa....umekiri mwenyewe kwamba kule kusini hawana viwanda....na hata majiko ya gesi pia hawana.

Sijui kama umelinganisha gharama za ujenzi wa miundo mbinu ya kusafirisha gesi kutoka mtwara kwenda Dar...kusafirisha umeme kutoka mtwara hadi dar...na gharama za kusafisha umeme kutoka dar kwenda mtwara.

Kwa ujuzi mdogo nilionao kusafirisha umeme Dsm~Mtwara na Mtwara~Dsm gharama zinatofautiana........

Hivyo ukiangalia kwa undani hii hoja ya gesi si jambo la kisiasa...ni jambo linalohitaji utaalamu wa kujua ni ipi njia rahisi tunayoweza kuitumia gesi hii kwa gharama ndogo.

Ni sawa na ndugu zetu wa Kyela wakiamua kuuza wali badala ya mpunga...tutahitaji magari yenye majokofu ili tuweze kufikisha wali Arusha.......

Hapo kwenye hizo blue. Ndio maana ni wakati sasa wa kuanzisha viwanda na kuendeleza eneo hilo. Kwa mfano kama hiyo gesi ingeteneza umeme huko huko kusini then ingekuwa rahisi zaidi kuoperate viwanda zaidi, which means hata wazo la kuboresha bandari za kusini lingepata kipaumbele sababu ya mahitaji ya kusafirisha bidhaa zitokanazo na hivyo viwanda na faida nyingi zitakazofuatia kutokana na increased economic activities kwenye eneo hilo. Otherwise una suggest mikoa ya kusini ibaki bila viwanda forever. (Circle of poverty by your argument)!!!!!.

Hapo kwenye red. Labda nikupe angalizo kidogo. Umeme hausafirishwi kwa malori, ndege, treni kama bidhaa nyingine kama mahindi, ngano e.t.c. Umeme husambazwa kwa kutumia Grid (Mfuma wa nyaya zipitishazo umeme). Gridi ya umeme ya taifa haianzii dar, tayari ipo kwenye mikoa ambayo ki-jiografia(na ki-ufundi zaidi) iko karibu na kusini zaidi ya dar, hivyo inahitajika kuisogeza(kuiunganisha kwa maeneo ambayo bado hawajafikiwa) na gridi ya taifa then umeme unafika sehemu zote za nchi ambazo gridi ya taifa imefika(au ambazo gridi hiyo itafika) na sio Dar pekee(umeme hauzalishwi kwa ajili ya Dar pekee).

Umeme unatakiwa uingizwe kwenye gridi ya taifa. Utaleta manufaa kwa mikoa yote inayotumia(na itakayo ingizwa kwenye) gridi ya umeme ya taifa kwa gharama nafuu zaidi. Hivyo kusema(kulinganisha) suala la kufikisha umeme Dar(ambako kunahitaji marekebisho ya grid ya umeme ya taifa tu na kutaongeza maeneo yatakayofikiwa katika nchi) na kulinganisha na kusafirisha gas ni very misleading, kwa kweli kwa argument kama hizi ni dhahiri suala ambalo ni la kitaalam kabisa limegeuzwa kuwa la kisiasa zaidi.
 
Biznocrats
1. Kwanza tunatakiwa kujua kiini cha tatizo hapa nchini. Tatizo letu kuu ni umasikini. Umasikini chanzo chake ni ujinga. Tanzania ni taifa la wajinga wengi kutokana na mfumo mbovu wa elimu tuliojiwekea tangu tupate uhuru hadi leo hii.
2. Mikakati ya maana ya maendeleo nchini mwetu haiwezi kufanikiwa kama itapangwa kwenye ngazi ya jimbo hasa kwa nchi masikini kama ya kwetu. Kwa mfano unapotaka kuwa na mipango mizuri ya viwanda, inabidi serikali kuu iangalie kiwanda gani kianzishwe eneo gani ili kuwe na synergy itakayowezesha kiwanda hicho kuwa na ufanisi wa kutosha ili kiweze kushindana kwenye soko la dunia na sio kila jimbo lije na kiwanda chake cha aina hiyohiyo bila kuangalia synergy ya kuwa na kiwanda hicho mahala husika.

3. Hakuna uhakika wowote kwamba kuweka utawala kwenye ngazi ya jimbo kutapunguza ufisadi. Hii inaweza kuwa chanzo cha kuongeza ufisadi zaidi kwa kuongeza wigo wa viongozi mafisadi wenye mamlaka katika majimbo yao na kuiacha nchi katika ngazi ya majimbo na kwa ujumla wake katika hali mbaya zaidi kuliko hii tuliyonayo leo!!

4. Kuna maeneo ambayo yalitengwa kimaendeleo tangu tupate uhuru mpaka sasa hivi. Haya ndo yale yanayojulikana kama maeneo ya pembezoni. Mfano hapa ni suala la Mtwara na Lindi. Juu ya kuchangia kwa kiwango kikubwa kupitia zao la Korosho, bado hakukuwa na mipango makusudi ya kuiendeleza mikoa hii ili iweze kuzalisha zaidi.

5. Mgawanyo wa ziada utakaoenda serikali kuu kwa ajili ya kugawanywa kwenye majimbo mengine bado nao una uwezekano wa kuwa na utata uleule tulionao sasa kama viongozi wa juu wataamua kugawa kutokana na maslahi yao badala ya nchi nzima.
Ndugu Bizkratz, wa CHAMA CHA UMMA,ningependa kujibu hoja zako kama ifuatavyo.

Hoja yako ya 1.Msingi wa Sera ya Majimbo ni kukuza na kuimarisha misingi na utamaduni wa kidemokrasia katika ngazi ya Serikali za Mitaa.Ukuzaji huo wa misingi na utamaduni wa kidemokrasia aghalabu huenda sambamba na dhana ya Ushiriki na Ushirikishwaji jamii katika kuamua masuala yanayogusa maisha yao.Katika kutekeleza dhana hii,wananchi,si tu hupata uwezo wa kushiriki na kushirikishwa katika kufanya maamuzi bali pia nao huwa sehemu muhimu ya upangaji,utekelezaji,usimamizi,ufuatiliaji na hata tathmini ya shughuli mbalimbali za maendeleo.Kwa mfano,katika nadharia ya Usimamizi na Utawala Bora wa Rasilimali za Umma,wananchi huwa na uwezo wa kushiriki katika kupima thamani ya pesa katika Miradi na shughuli mbalimbali kupitia mfumo uitwao ''Public Expenditure Trucking Syestem'' (PEST).Kwa hakika,hii ni nyenzo muhimu katika kusimika,kuimarisha na kuendeleza misingi na tunu za uwajibikaji,uadilfu,ufanisi na utawala bora na demokrasia kwa ujumla wake.Ikiwa dhana ya PEST itatumiwa bila ubabaisghaji ,watawala waliopewa dhamana za uongozi wanalazimika kuwajibika kwa wananchi wa mahali miradi inapotekelezwa.Ikiwa kutakuwa na miondombinu imara ya ya aina hii na mingine kadiri itakavyobuniwa na kukawa na uwajibikaji na utawala dhabiti,sioni uwezekano wa wananchi kuendelea kuwa maskini.

Hoja yako ya 2.Ikiwa utungaji wa sera,programu,miradi,mikakati na shughuli utafanywa na wananchi wa maeneo husika ni wazi kuwa wananchi watajenga hisia za umiliki na hivyo kutoa hakikisho la uendelevu wa mradi husika na hatimaye kuweza kufikia malengo ama matokeo tarajiwa.Kwa sasa,watawala wetu,bila hofu yoyote,wanaweza kukaa ''Ubungo Plaza'' ,Dar Es Salaam,kwa minajili ya kupanga na kuamua masuala yanayowahusu wananchi wa Wilaya ya Nanamyere,Mtwara,pasipo ufahamu na uelewa wa kina wa mazingira na mahitaji halisi ya wakazi wake.Hoja hapa ni, kuwa, wananchi, kupitia Sera ya Majimbo,wanapata na uwezo ,nguvu na uhalali wa kupanga na kuamua vipaumbele vyao kadiri ya mazingira na mahitaji ya maeneo yao.Tutambue wazi kuwa moja ya sababu ya kutokutekelezeka kwa Miradi mingi katika meneo mengi hapa nchini ni kutoshirikisha wananchi wanaolengwa na miradi husika.

Hoja yako ya 4 na 5 juu ya ambayo kimsingi inahusu ''uwezekano wa matumzi mabaya ya madaraka'' inakosa ushawishi wa kimantiki na kiakili.Ukweli ulio wazi ni kuwa,Bara la Afrika kwa ujumla na Tanzania kwa pekee, haihitaji watu waadilifu na mahiri ilikuweza kupiga hatua.Tatizo la msingi la nchi za bara la Afrika ni ukosefu na uhaba wa Taasisi na Mifumo imara na inayotabirika ambayo ingeweza kudhibiti mienendo ,silka ,hulka na tabia za watawala wetu .Kwa sababu hii,tatizo la ufisadi haliwezi kumalizwa kwa kutafuta na kuweka watu waadilifu,na weledi na mahiri katika nafasi na ngazi mbalimbali za uongozi na utawala kwa kuzingatia ukweli kuwa watu waadilfu na mahiri hawadumu milele, na ukweli kuwa wanadamu habadilika kutokana na wakati na mzingira isipokuwa Taasisi na Mifumo,aghalabu,huweza kubaki kwa muda mrefu.Kupata watu waadilifu yaweza kuwa ni mbinu muhimu lakini si endelevu.Ni hatua ya muda mfupi tu.Kuweza kutatua tatizo hili,kwa uhakika na kiuendelevu, ni sharti ,basi,kusimika na kuimarisha miundombinu ya kitaasisi,kisera na kisheria ili hatimaye idhibiti matendo,maamuzi,silka na mienendo ya watumishi na watawala na hivyo kuondoa uwezekano wa matumizi mabaya ya nafasi na mamlaka zao kwa kujineemesha kibinafsi.Kwa kuwapa wanachi umiliki wa hatma yao,ni dhahiri,kuwa,watawala watajenga utamaduni wa uwajibika na ufanisi ambao ni msingi muhimu katika kuleta maendeleo.Ili kuweza kutekeleza adhama hii,Sera ya Majimbo,kama moja ya mihimili na mguzo ya Mfumo Mpya wa Utawala, kadiri ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya CHADEMA,inakusudia kuhakikisha,kuwa,watawala wa maeneo husika watapata nafasi za uongozi kwa kupigiwa kura na wananchi wa maeneo husika tofauti na sasa ambapo watawala wanateuliwa kutoka Dae Es Salaam na kwenda kutawala wananchi.Na wananchi wa maeneo husika hawana uwezo wa kitaasisi na kisheria kuwawajibisha ama kuwakataa kwa namna yoyote ile kwa kuwa watawala hao hawalazimiki kuwajibika kwao,isipokuwa kwa mamlaka yao ya uteuzi.

Mwisho kabisa,Chama Cha Umma,kinakosa sifa ya kuwa mtetezi wa maslahi ya ''Umma'' kwa kutoona umuhimu wa kuwapa wananchi uwezo na nguvu ya kuamua hatma yao na badala yake kurundika nguvu na uwezo huo kwa Serikali Kuu.Chama cha Umma lazima, sasa ,kibadili mwelekeo na mapendekezo yake juu ya Mfumo wa Utawala kwa kukuza na kuimarisha tunu na utamaduni wa kidemokrasia kwa kupeleka madaraka kwa wananchi.Bila kufanya hivyo,ni vema,Ndugu Bizkratz na wenzako mfikirie kukipa jina jingine na muachane na jina hilo.Jina linaloweza kukifaa Chama Cha Umma(,CHAUMMA)kulingana na hoja zako hapo juu ni Chama cha Watawala,(CHAWA).

Nashukuru mkuu Kobelo kwa masahihisho.
Hata baada ya kuweka uharibifu wa mazingira kuwa sababu ya mradi husika kupata ukinzani,mantiki ya hoja ya M.M.Mwanakijiji inabaki palepale:wananchi wa maeneo husika walipinga mradi kwa kuwa hawakushirikishwa na watawala katika hatua za awali za mradi na pia watawala kushindwa kutambua na kuheshimu hisia na matakwa yao baada ya kuonyesha ukinzani baada ya mradi kuanza kutekelezwa.
Mfano hapo juu unatudokeza suala muhimu kuhusu Sera ya Majimbo:ushirikishwaji na ushiriki wa local community katika kuamua mustakabali wa maisha yao.
Ni wazi,kuwa ,moja ya matokeo chanya ya sera ya majimbo ni kuimarisha na kukuza utamaduni wa kidemokrasia ambao msingi wake mkuu ni ushiriki wa wananachi katika michakato mbalimbali ya maendeleo.
Kama tatizo ni kutoshirikishwa, wakazi wa NY,DC na CA wanahusika vipi na mazingira ya pipeline hiyo?

hapo majimbo yanahusika vipi?
 
Kwanza kabisa ningependa kusema kwamba hoja ya msingi hapa ni je tunahitaji majimbo au hapana. Nimejenga hoja hizo zote ili kuonyesha kwamba utawala wa majimbo si sahihi kwetu kwa sasa. Sasa ukitaka kujibu hoja yangu kiuhalisia lazima uanze kwa kuelezea unakubaliana na mtazamo huo wa CHAUMMA au la. Baada ya hapo unaweza kuweka hoja yako kama hii kwamba ndio inayokufanya kwa nini uamini utawala wa majimbo unafaa. Kwa hiyo rudi kwanza kwenye mada yangu ya msingi uichambue kitija kama nilivyoeleza. Huu usanii wa kuruka hoja ya msingi na kuamua kushambulia matawi ya hoja kama ninavyoona wana JF wengi wanavyofanya hauwezi kuwaacha wafuatiliaji mada wawe focused kwenye issue ya msingi iliyokuwa posted.
mkuu wangu CHAUMMA ndo kitu gani hicho?
 
..hata mimi sikubaliani na mapendekezo ya kuanzisha utawala wa majimbo Tanzania.

..lakini pia napingana na hoja yako kwamba rasilimali za mikoa ya kusini zilikuwa zikiibiwa na kwenda kunufaisha mikoa mingine.

..unapopinga jambo fulani ufanye hivyo kwa hoja za kweli na siyo kuleta mambo ya kutunga tu.
 
- Sasa Mnyika hivi amemaliza hoja ya Baraza la Taifa la Vijana? Hii ya majimbo inazungumizka ila Mnyika haelewi inazungumzikaje, so anahitaji darasa zaidi kwamba bila Federal Government iliyo strong, huwezi kuwa States strong, sasa angekazania kuwa na Strong Instituions za Serikali kwanza ndio arukie majimbo!! le mutuz
Du!!! We ndugu!!! Ufinyu wako wa mang'amuzi hata haufanani na vazi ulilovaa!!!!
 
Kama tatizo ni kutoshirikishwa, wakazi wa NY,DC na CA wanahusika vipi na mazingira ya pipeline hiyo?

hapo majimbo yanahusika vipi?......

Ukweli kuwa Marekani inatumiaUtawala wa Majimbo haumaanishi kuwa masuala yote ya kiutawala na kimenejimenti yatakuwa perfect.

Hakuna mfumo usio na mapungufu.Lakini tunapaswa kuwa na mifumo inayopunguza mapungufu.Hatuwezi kudai kuwa kwa kuwa Marekani,pamoja na Mfumo wao wa Kiutawala wa Majimbo wanakutana na matatizo kadha wa kadha ,basi nasi tutakutana na matatizo ya aina hiyo hiyo.La hasha!

Sera ya Majimbo inatilia maanani upekee wa kimazingira unaoamua vipaumbele vya mahali na kutafuta majawabu kulingana na tofauti hizo.

Ni wazi sasa ,wakazi wa maeneo ambayo hiyo pipeline inapitishwa wanachukulia utunzaji na uhifadhi wa rasilamali za kimazingira kama moja ya vipaumbele vyao.

Hoja hapa ni kuwa kwa kuwa na Utawala wa Majimbo magnitute na pace ya wananachi kudai,kwa mfano,utawala bora katika rasilimali itaongezeka.

The problem no one is answering the important question here unawafanyaje wananchi wasupport mwekezaji whether ni katika madini au viwanda or agriculture if they cannot see anything which is direct related to these investment.

hii ndio jambo linalotokea Mtwara, wamecontribute through cashew-nuts but there is nothing to show for it, na serikali ya DSM haina jibu wala ya Mtwara haina majibu pia.

Kila mtu analeta siasa (with abstract notions) no tangible solutions) if the proposed structure of states doesn't work after 50 years of indipendence which way will you go? CCM government solution has been to divide the geographical areas increase number of wabunge. have they got feedback that there is development if the thinking is still the same the source of income is still the same and people are still frustrated with the pace of development?

The problem with Tanzania we love Inertia thinking (afraid of changes) this happens if we are afreaid of losing our positions in power

Ritz & co Let answer this question. How do you ensure that the Mwadui feels and know that their diamond is what has made them poor to this day? (that is what you call development while the feel its poverty)

kujibu hoja yako hapo juu ni kuwa Mwadui na Mtwara wanashindwa kuwatofautisha CCM na wakoloni because they havent seenj any change wakati dar-es-salaam ikiendelea hali in bandari na ikulu wao wanzidi kuwa maskini na wanaamua kuja DSM

Lets all love TZ

Mkuu chama.

Kwa muda mrefu tangu ukoloni almasi za Mwadui zimechimbwa na kuuzwa nje ya nchi, mapato yatokanayo yameingia kwenye mfuko wa nchi na kutumika kwa manufaa ya wananchi wote.
 
Biznocrats

Ndugu Bizkratz, wa CHAMA CHA UMMA,ningependa kujibu hoja zako kama ifuatavyo.

Hoja yako ya 1.Msingi wa Sera ya Majimbo ni kukuza na kuimarisha misingi na utamaduni wa kidemokrasia katika ngazi ya Serikali za Mitaa.Ukuzaji huo wa misingi na utamaduni wa kidemokrasia aghalabu huenda sambamba na dhana ya Ushiriki na Ushirikishwaji jamii katika kuamua masuala yanayogusa maisha yao.Katika kutekeleza dhana hii,wananchi,si tu hupata uwezo wa kushiriki na kushirikishwa katika kufanya maamuzi bali pia nao huwa sehemu muhimu ya upangaji,utekelezaji,usimamizi,ufuatiliaji na hata tathmini ya shughuli mbalimbali za maendeleo.Kwa mfano,katika nadharia ya Usimamizi na Utawala Bora wa Rasilimali za Umma,wananchi huwa na uwezo wa kushiriki katika kupima thamani ya pesa katika Miradi na shughuli mbalimbali kupitia mfumo uitwao ''Public Expenditure Trucking Syestem'' (PEST).Kwa hakika,hii ni nyenzo muhimu katika kusimika,kuimarisha na kuendeleza misingi na tunu za uwajibikaji,uadilfu,ufanisi na utawala bora na demokrasia kwa ujumla wake.Ikiwa dhana ya PEST itatumiwa bila ubabaisghaji ,watawala waliopewa dhamana za uongozi wanalazimika kuwajibika kwa wananchi wa mahali miradi inapotekelezwa.Ikiwa kutakuwa na miondombinu imara ya ya aina hii na mingine kadiri itakavyobuniwa na kukawa na uwajibikaji na utawala dhabiti,sioni uwezekano wa wananchi kuendelea kuwa maskini.

Hoja yako ya 2.Ikiwa utungaji wa sera,programu,miradi,mikakati na shughuli utafanywa na wananchi wa maeneo husika ni wazi kuwa wananchi watajenga hisia za umiliki na hivyo kutoa hakikisho la uendelevu wa mradi husika na hatimaye kuweza kufikia malengo ama matokeo tarajiwa.Kwa sasa,watawala wetu,bila hofu yoyote,wanaweza kukaa ''Ubungo Plaza'' ,Dar Es Salaam,kwa minajili ya kupanga na kuamua masuala yanayowahusu wananchi wa Wilaya ya Nanamyere,Mtwara,pasipo ufahamu na uelewa wa kina wa mazingira na mahitaji halisi ya wakazi wake.Hoja hapa ni, kuwa, wananchi, kupitia Sera ya Majimbo,wanapata na uwezo ,nguvu na uhalali wa kupanga na kuamua vipaumbele vyao kadiri ya mazingira na mahitaji ya maeneo yao.Tutambue wazi kuwa moja ya sababu ya kutokutekelezeka kwa Miradi mingi katika meneo mengi hapa nchini ni kutoshirikisha wananchi wanaolengwa na miradi husika.

Hoja yako ya 4 na 5 juu ya ambayo kimsingi inahusu ''uwezekano wa matumzi mabaya ya madaraka'' inakosa ushawishi wa kimantiki na kiakili.Ukweli ulio wazi ni kuwa,Bara la Afrika kwa ujumla na Tanzania kwa pekee, haihitaji watu waadilifu na mahiri ilikuweza kupiga hatua.Tatizo la msingi la nchi za bara la Afrika ni ukosefu na uhaba wa Taasisi na Mifumo imara na inayotabirika ambayo ingeweza kudhibiti mienendo ,silka ,hulka na tabia za watawala wetu .Kwa sababu hii,tatizo la ufisadi haliwezi kumalizwa kwa kutafuta na kuweka watu waadilifu,na weledi na mahiri katika nafasi na ngazi mbalimbali za uongozi na utawala kwa kuzingatia ukweli kuwa watu waadilfu na mahiri hawadumu milele, na ukweli kuwa wanadamu habadilika kutokana na wakati na mzingira isipokuwa Taasisi na Mifumo,aghalabu,huweza kubaki kwa muda mrefu.Kupata watu waadilifu yaweza kuwa ni mbinu muhimu lakini si endelevu.Ni hatua ya muda mfupi tu.Kuweza kutatua tatizo hili,kwa uhakika na kiuendelevu, ni sharti ,basi,kusimika na kuimarisha miundombinu ya kitaasisi,kisera na kisheria ili hatimaye idhibiti matendo,maamuzi,silka na mienendo ya watumishi na watawala na hivyo kuondoa uwezekano wa matumizi mabaya ya nafasi na mamlaka zao kwa kujineemesha kibinafsi.Kwa kuwapa wanachi umiliki wa hatma yao,ni dhahiri,kuwa,watawala watajenga utamaduni wa uwajibika na ufanisi ambao ni msingi muhimu katika kuleta maendeleo.Ili kuweza kutekeleza adhama hii,Sera ya Majimbo,kama moja ya mihimili na mguzo ya Mfumo Mpya wa Utawala, kadiri ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ya CHADEMA,inakusudia kuhakikisha,kuwa,watawala wa maeneo husika watapata nafasi za uongozi kwa kupigiwa kura na wananchi wa maeneo husika tofauti na sasa ambapo watawala wanateuliwa kutoka Dae Es Salaam na kwenda kutawala wananchi.Na wananchi wa maeneo husika hawana uwezo wa kitaasisi na kisheria kuwawajibisha ama kuwakataa kwa namna yoyote ile kwa kuwa watawala hao hawalazimiki kuwajibika kwao,isipokuwa kwa mamlaka yao ya uteuzi.

Mwisho kabisa,Chama Cha Umma,kinakosa sifa ya kuwa mtetezi wa maslahi ya ''Umma'' kwa kutoona umuhimu wa kuwapa wananchi uwezo na nguvu ya kuamua hatma yao na badala yake kurundika nguvu na uwezo huo kwa Serikali Kuu.Chama cha Umma lazima, sasa ,kibadili mwelekeo na mapendekezo yake juu ya Mfumo wa Utawala kwa kukuza na kuimarisha tunu na utamaduni wa kidemokrasia kwa kupeleka madaraka kwa wananchi.Bila kufanya hivyo,ni vema,Ndugu Bizkratz na wenzako mfikirie kukipa jina jingine na muachane na jina hilo.Jina linaloweza kukifaa Chama Cha Umma(,CHAUMMA)kulingana na hoja zako hapo juu ni Chama cha Watawala,(CHAWA).

Kwanza kabisa ningependa kukufahamisha kwamba umejibu hoja zangu kisanii. Kama ulikuwa unataka ku quote points zangu ili kujibu basi ulitakiwa u quote point nzima na si ku quote vipande vipande ili kuwapotosha watu maana ya points zangu.

Majibu yangu kwa hoja zako ni kama ifuatavyo:

Si lazima kuwa na majimbo ili kukuza ushirikishaji wa wananchi kwenye maamuzi. Mikoa inatosha kufanya kazi hiyo kama wakuu wa mikoa watachaguliwa na wananchi wa mikoa husika wakati wa uchaguzi mkuu. Tatizo tulilonalo sasa hivi ni kuongezeka kwa idadi ya mikoa kwa ajili ya malengo ya kisiasa. Katika kipindi cha TBC 1 mara baada ya kuzindua chama chetu, tulielezea umuhimu wa kushirikisha wananchi wote kwenye mikakati ya maendeleo kuanzia ngazi ya kata na tukaelezea kwamba wananchi lazima washirikishwe kwenye maamuzi yote nyeti kwa ajili ya mstakabali wa nchi yetu na lazima washirikishwe kwenye ufuatiliaji wa maamuzi tuliyokubaliana na sio kuwaachia viongozi peke yao kupanga sera kama ilivyo sasa hivi. Tulielezea kwamba kila shilingi iliyopangwa kwenye bajeti lazima wananchi wajue kama imetumika kwenye malengo tuliyoyapanga au vipi. Tulieleza kwamba Serikali ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) itahakikisha hilo kwa kuwataka mawaziri wa maeneo husika kutoa taarifa kwa umma utekelezaji wa bajeti kila baada ya miezi mitatu kwa wananchi. Tukaelezea kwamba kila mipango iliyokubalika na kuingia kwenye bajeti pamoja na hela zilizopitishwa kushughulikia mipango hiyo lazima itangazwe kuanzia ngazi ya kata kwa kutumia mtandao wa taifa wa mawasiliano tutakaouanzisha pamoja na kubandika ripoti kwenye ofisi za kata na zingine ili wananchi waweze kufuatilia utekelezaji wake. Tukaeleza kwamba ripoti za utekelezaji (variance analysis) za miradi mbali mbali ziwekwe kuanzia ngazi ya kata kwenye mtandao na vile vile kwenye ofisi za kata na maeneo mengine ngazi ya kata kila baada ya miezi mitatu ili wananchi waweze kufuatilia na kuona kama kweli miradi hiyo inatekelezwa kama ilivyoelezwa kwenye ripoti husika. Kwa mfano kama Wizara ya Ujenzi ina mpango ulioidhinishwa wa kujenga daraja mahali fulani, lazima wizara iutolee maelezo utekelezaji wake kwenye kata husika ili wananchi waweze kufuatilia kama kweli mradi huo unaendelea kama ulivyoripotiwa na wanachi kwa kutumia wawakilishi wao katika ngazi ya kata wataweza kutoa comment kwenye Mtandao wa Taifa kama maelezo yaliyotolewa na wizara kuhusu maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ni sahihi au la. Hivyo maelezo haya yanajibu maelezo yako uliyoyaweka wakati wa kujibu hoja yangu ya kwanza na ya pili.

Kuhusu kwamba hakuna haja ya kuwa na viongozi waadilifu huo si mtazamo sahihi kwa sababu huwezi kuwa na taasisi za ufuatiliaji makini kama viongozi si waadilifu. Tunayo TAKUKURU kwa mfano lakini haifanyi kazi yake kama inavyotakiwa kwa sababu viongozi sio waadilifu.
 
Back
Top Bottom