Kinachotakiwa ni kwamba hizi Rasilimali ziwanufaishe wananchi wa eneo husika.
Wananchi wa Mtwara si kwamba hawatakia Gesi itumike sehemu zingine za nchi, na ikizingatiwa wenyewe hata majiko ya gesi hawana, viwanda hakuna. Lakini kinachotakiwa ni kwamba kwa nini kiwanda kama kilichopo Ubungo cha gesi kisijengwe Mtwara na Lindi??
mbona Umeme toka Kidatu hauletwi DSM kwa ajili ya kufua umeme bali kumekuwa na mitambo kule, ambayo inatoa ajira kwa wananchi wa eneo husika na pia wananchi wanaozunguka wanapata umeme, inaboresha eneo husika na kulifanya liwe na maendeleo.
mbona kwenye migodi ule mchanga hauletwi DSM badala yake kuna viwanda vya kusafishia kule migodini??? ambavyo vinatoa ajira, na maendeleo kwa eneo husika???
Haya ndiyo baadhi ya mambo wanayoyataka watu wa Mtwara na Lindi na kwao yafanyike ndio kunufaika na Gesi wanakohitaji.
Sidhani kama pale Ubungo kuna watu wanatoka Mtwara na Lindi kuja kufanya kazi kila siku pale Songas!!!!!!!
Tubadilike tusiwe kisiasa zaidi, itatugharimu.
MIZAMBWA
NABII MTARAJWA!!!