John Mnyika: Sera ya Majimbo ya CHADEMA siri ya Maendeleo

Kwa akili yako ilivyo najua ipo siku utachapwa viboko ndo uelewe kuwa napato yatokanayo na madini hutumiwa na wachache na ndio maana ya kuibuka kwa jina la FISADI. Na kama hutochapwa viboko ukiwa hai, siku ukifa watoto au wajukuu zako watalichapa hata kaburi lako na kukulaani kwa jinsi ulivyotumia muda wako kuandaa mazingira mabaya kwa watoto zako kwa kushabikia ujinga na wizi wa jama zako wa CCM.

Badala ya kujenga hoja unaleta viroja.
 
M.M.Mwanakijiji
Wapo wengine walioandamana kupinga ujenzi wa barabara kwenye maeneo yao, wapo waliopinga kuchimbwa mafuta au madini, na wapo wengine ambao wamepinga ujengwaji wa bomba la mafuta!

Mojawapo ya mifano mikubwa ya upingaji huu ni ule unaoendeleaMarekani dhidi ya bomba la mafuta la TransCanada ambalo limekumbwa na upinzani mkubwa japo mafuta yake yanahitajika sana kwa uchumi wa Marekani. Wanaopinga bomba hili wamefanya kila aina ya upingaji ikiwemo kupinga nje ya Ikulu ya Marekani. Wamefanya hivi si kwa sababu wanaongozwa na vyama vya upinzani au hawajui manufaa ya kiuchumi.
Hili ni kweli hata Canada ambapo bomba la mafuta/gesi la Enbridge limejikuta kwenye upinzani mkubwa hasa kutoka kwa wakazi wa asili (first nations) wa maeneo ambayo bomba lilitakiwa kupita. Kwa karibu miaka kumi sasa bomba hilo limechelewesha kuanza kwa sababu wananchi wanaamini kuwa lina lengo la kunufaisha makampuni makubwa wala si watu wa maeneo bomba litakalopita. Viongozi wa Canada (kama wale wa Marekani) wamejaribu na wanaendelea kujaribu kuwashawishi wananchi na kusikiliza maoni yao na hata kubadilisha njia ya mabomba hayo na kuweka programu ambazo zitawanufaisha wananchi wa maeneo ya mabomba hayo.
Hivyo, wananchi wa Mtwara kama wa maeneo mengine nchini wana haki ya msingi kabisa na kwa hakika si usaliti kudai kuwa rasilimali zilizoko katika maeneo hayo ziwanufaishe. Hii ni haki ya msingi ya wananchi.

Chanzo.Tanzania Daima,Jumatano,9,1,2013
 
Mh FortJeasus
Mh M.M.Mwanakijiji
Heshima mbele
Mara nyingi tumekuwa tukijenga hoja huku tukitolea mifano sehemu mbalimbali duniani bila kujali mazingira yetu halisi...bila kulinganisha mahitaji yetu na yao....kiuchumi...kisiasa....kiteknologia...nk Kwa maoni yangu ni vema tukajenga hoja zinazolingana na hali halisi ya mazingira yetu. Ni kweli wao wanaweza kupinga kwa sababu zao.....labda nishati inasafirishwa nje ya nchi.au kwasababu ya uharibifu wa mazingira nk......Lakini hapa kwetu sababu si hizo...gesi inasafirishwa kwenda Dsm....sehemu ambayo zaidi ya robo tatu ya kodi inakusanywa hapo...inatumika kuwalipa madaktari...walimu...wabunge wa Mtwara....kujenga barabara za Mtwara..nk....Tujifunze kutoka kwao wazo kuu pekee....lakini ubunifu..uendeshaji na matumizi tuamue kulinganana hali halisi ya mazingira yetu ilivyo......
 
John Mnyika siku hizi amekuwa mtu wa kudandia matukio tu. Juzi alidandia maandamo ya Mtwara, mara tena akadandia katiba hataki rais aingilie bahati nzuri Warioba akamfahamisha. Leo tena kaja na sera za majimbo.
SERA YA MAJIMBO haikuanza leo wala jana,Mme ambiwa enzi zile mlitolea mf MTWARA/KUSINI Jimbo lisilo na lasili.Sasa nyie ndo mnagundua kuna mali (gesi)CDM hilo walilijua tangu enzi hizo.Sasa mnataka ije jirani na BAGAMOYO,huku si kuna BAHARI na VINYAGO vya Utalii gesi wa-achieni Machinga wafue umeme nanyi mtumie.
 
sasa mkuu wewe mbona ndio unaonekana punguani zaidi; si kila kitakachosemwa JF kitakufurahisha na si kila jambo lazima ulijibu Ritz ni mtu makini anayejibu hoja kwa bashasha na umakini wake jifunze kutokubaliana huo ndio uvumilivu wa kisiasa, naona kukosa uvumilivu ni kansa inayowakabili vijana wengi wa Chadema; tiba yake ni rahisi sana rudini kwenye chama chenye kufuata misingi ya demokrasia; mjifunze siasa baadaye mtokomee mnakotaka.

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz, Matola, Mohamedi Mtoi, Mwita Maranya

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums

Delusional!! you need a mental health counselling
 
Kuna sababu nyingi za kitaalam...si idadi ya nguzo pekee.....kuna kiasi cha nishati kitakachosafirishwa......upotevu wa njiani.....uharibikaji (realibity??)..nk....mahitaji ya umeme Dar ni makubwa sana kuliko Mtwara hivyo kama tungekuwa tunasafisha umeme kwa barabara ....basi tutahitaji barabara kubwa na imara kusafirisha umeme kutoka Mtwara kuja Dar kuliko kutoka Mtwara kuja Dar......vilevile kuwagawia umeme wanaishi njiani.....kitaalam ni rahisi zaidi kwa umeme unatoka dar kuliko utakao toka Mtwara........bado gharama za kutumia mabomba ni ndogo kulinganisha na minara ya umeme katika ujenzi na ukaravati......hazihitaji utaalam mkubwa sana ni kama vile kujua gharama ipi kubwa kati ya keki na mkate.....

Umbali kutoka DSM ahdi mtwara ni wastani waa km 560, na umbali kutoka Mtera hadi DSM ni wastani km400.

Pamoja na Umeme wa Kidatu, pia Umeme wa Mtera ndio unaotegemewa kwa jiji la DSM. hivyo kwa tofauti ya Km 160, tunawanyima haki ya kutumia umeme maeneo ya njiani kati ya DSM na Mtwara kwa kisingizio cha gharama.

Tunawanyima haki ya maendeleo watu wa Mtwara na Lindi kwa kigezo cha gharama

Ni pesa kiasi gani kimefichwa huko Uswisi??? na pesa kiasi gani kimetumika katika malipo ya mikataba ya IPTL, DOWANS na RICHMOND???

TAFAKARI........

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!!
 
Mh FortJeasus
Mh M.M.Mwanakijiji
Heshima mbele
......Lakini hapa kwetu sababu si hizo...gesi inasafirishwa kwenda Dsm....sehemu ambayo zaidi ya robo tatu ya kodi inakusanywa hapo...inatumika kuwalipa madaktari...walimu...wabunge wa Mtwara....kujenga barabara za Mtwara..nk....Tujifunze kutoka kwao wazo kuu pekee....lakini ubunifu..uendeshaji na matumizi tuamue kulinganana hali halisi ya mazingira yetu ilivyo......

Pia tuzingatie kuwa Mtwara ni moja ya mikoa ya Tanzania ambao wana haki ya kutafuna keki ya Taifa. KWa miaka mingi wamesahaulika nakuwa nyuma kimaendeleo na vijana wao kuishia kuhamia DSM. Kwa kuwa hawana hata elimu ya kutosha wanaishia kufanya kazi ya kuuza bidhaa mitaani (Wamachinga)

Sasa leo mkoa wao Mungu ameukumbuka kwa kuupatia neema ya Gesi na mafuta, sisi ambao miaka ya nyuma tuliwadhurumu Korosho tena tunakuja nasera mpya ya kuwadhurumu maendeleo yatokanayo na madini haya.

Tusiwe wabinafsi lazima tuwakumbuke nao kimaendeleo. Suala ya kukusanya Kodi DSM ni kwa sababu viwanda na ofisi nyingi zipo huko, lakini na Mtwara + Lindi kukiwa na Viwanda na maofisi kodi itakusanywa nyingi kuliko DSM.

TAFAKARI

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
John Mnyika siku hizi amekuwa mtu wa kudandia matukio tu. Juzi alidandia maandamo ya Mtwara, mara tena akadandia katiba hataki rais aingilie bahati nzuri Warioba akamfahamisha. Leo tena kaja na sera za majimbo.

"Machozi ya samaki hubebwa na maji" kwa maana hiyo hata akiwa na tatizo huwezi kujua kwa sababu hisia zake haziko wazi/hazikushawishi kumsaidia........RITZ Ungekuwa muungwana usingeongea hayo kuhusu mnyika.Hakuna kijana wa kitanzania anayefanya vema kwenye siasa za bongo kama mnyika,fanya utafiti....
Kutetea raia anaweza,
kujenga hoja zenye mashiko na kuzisimamia anaweza pia......
je!
Kuna lipi kwako usilolipinga au kulibeza na kulikosoa?

kwanini kila jambo lenye maslahi kwa raia wa nchi hii unakuwa mstari wa mbele kulibeza na kulikosoa?

kwa nini mara zote unakuwa juu ya mti kama kobe...unashindwa kushuka tukushushe?

Mnyika endeleza harakati zako tumeona,72.42% ya vijana wenye vichwa tzania tupo nyuma yako kaka mnyika tumekuelewa na tutazidi kukuunga mkono jimboni na nje ya jimbo lako,kuna mengi umetufungua macho.

Kila la kheri mnyika.
 
Mh FortJeasus
Mh M.M.Mwanakijiji
Heshima mbele
Mara nyingi tumekuwa tukijenga hoja huku tukitolea mifano sehemu mbalimbali duniani bila kujali mazingira yetu halisi...bila kulinganisha mahitaji yetu na yao....kiuchumi...kisiasa....kiteknologia...nk Kwa maoni yangu ni vema tukajenga hoja zinazolingana na hali halisi ya mazingira yetu. Ni kweli wao wanaweza kupinga kwa sababu zao.....labda nishati inasafirishwa nje ya nchi.au kwasababu ya uharibifu wa mazingira nk......Lakini hapa kwetu sababu si hizo...gesi inasafirishwa kwenda Dsm....sehemu ambayo zaidi ya robo tatu ya kodi inakusanywa hapo...inatumika kuwalipa madaktari...walimu...wabunge wa Mtwara....kujenga barabara za Mtwara..nk....Tujifunze kutoka kwao wazo kuu pekee....lakini ubunifu..uendeshaji na matumizi tuamue kulinganana hali halisi ya mazingira yetu ilivyo......

Mkuu Mtanzania1
Niliweka maoni ya Ndugu M.M.Mwaakijiji nikilenga kuonyesha kuwa upinzani dhidi ya miradi mbalimbali haujanzia na hautaishia Mtwara ama Lindi, isipokuwa umekuwa ukijitokeza hata katika nchi zinazopigiwa mfano katika maendeleo ya ujenzi wa demokrasia na uchumi sawia.
Ni dhahiri,kuwa,mradi husika hauwezi kutekelezwa bila kuhakikisha kunakuwepo makubalioano na maelewano kati ya na wananchi wa maeneo ambayo bomba linatarajiwakupita kwa upande mmoja na serikali kwa upande mwingine.Moja ya maelewano hayo ni kuweka bayana ni kwa jinsi gani wananchi watanufaika na mradi wa gesi.Hadi sasa,bado watawala hawajatafuta na kupata uungwaji mkono wa wananchi wa maeneo husika.
Kadiri ya makala ya Ndugu Mnyika hapo juu,jawabu la kudumu na la kuaminika juu ya usimamizi na utawala wa rasilimali asilia ni Sera ya Majimbo ikiwa moja ya component ya Mfumo Mpya wa Utawala.
 
Suala hili la majimbo ni suala ambalo naamini litaturudisha nyuma sana kimaendeleo kwa sababu zifuatazo:

1. Kwanza tunatakiwa kujua kiini cha tatizo hapa nchini. Tatizo letu kuu ni umasikini. Umasikini chanzo chake ni ujinga. Tanzania ni taifa la wajinga wengi kutokana na mfumo mbovu wa elimu tuliojiwekea tangu tupate uhuru hadi leo hii. Wajinga hawawezi kufanya shughuli zenye ufanisi katika maeneo yote ya uchumi - kilimo, viwanda, madini, utalii, n.k.
Hivyo adui yetu mkubwa kabisa ambaye anahitaji mikakati ya kitaifa ni mapambano dhidi ya ujinga. Hakuna serikali yeyote itakayokuja hapa Tanzania ikafanikiwa kama haitaelewa kwamba nchi yetu inatakiwa iwe vitani hasa kupambana na ujinga kwanza katika kila sehemu ya Tanzania. Sasa ukiacha hili suala lishughulikiwe kwenye ngazi ya jimbo kama maelezo ya sera hiyo ya majimbo inavyodai, basi tusahau taifa letu kutoka kwenye ufukara na kuwa taifa tajiri.

Tunatakiwa kama taifa tuwe na mkakati mmoja nchi nzima na rasilimali nyingi kutoka maeneo mbali mbali ya nchi yetu zipewe kipaumbele kuwekezwa kwenye eneo hili la elimu. Hii ni vita kwani ikibidi itabidi tuibe technologia kutoka nchi nyingine zilizoendelea ili kuwawezesha watu wetu kupata elimu ya uhakika ya kuweza kutawala mazingira yetu na ya nchi zingine bila kutegemea mataifa mengine. Sasa hii sio kazi ya kuachiwa kwenye ngazi ya jimbo kama vile ambavyo huwezi kuacha vita na nchi nyingine kwenye ngazi ya jimbo.

2. Mikakati ya maana ya maendeleo nchini mwetu haiwezi kufanikiwa kama itapangwa kwenye ngazi ya jimbo hasa kwa nchi masikini kama ya kwetu. Kwa mfano unapotaka kuwa na mipango mizuri ya viwanda, inabidi serikali kuu iangalie kiwanda gani kianzishwe eneo gani ili kuwe na synergy itakayowezesha kiwanda hicho kuwa na ufanisi wa kutosha ili kiweze kushindana kwenye soko la dunia na sio kila jimbo lije na kiwanda chake cha aina hiyohiyo bila kuangalia synergy ya kuwa na kiwanda hicho mahala husika. Kwa mfano kiwanda cha kutengeneza mvinyo kinaweza kuwa bora zaidi kuwepo Dodoma kutokana na malighafi iliyokuwa nayo lakini ghala la kuhifadhia mvinyo huo ili uive na kuongeza thamani yake zaidi utategemea na soko la mvinyo huo uko wapi ili kupunguza gharama ya usafiri wa kusafirisha kiasi kidogo kidogo kutoka kwenye eneo la uzalishaji kupeleka kwenye eneo lenye soko. Vile vile malighafi zingine mfano chemicals kiwanda chake kinaweza kuleta tija zaidi kama kitajengwa kwenye jimbo jingine ampapo malighafi hiyo inapatikana. Hii mipango lazima iwe kwenye ngazi ya taifa kama tunataka kuwa na mipango yenye lengo la kuongeza tija kwa manufaa ya majimbo yenyewe na taifa kwa ujumla.

3. Hakuna uhakika wowote kwamba kuweka utawala kwenye ngazi ya jimbo kutapunguza ufisadi. Hii inaweza kuwa chanzo cha kuongeza ufisadi zaidi kwa kuongeza wigo wa viongozi mafisadi wenye mamlaka katika majimbo yao na kuiacha nchi katika ngazi ya majimbo na kwa ujumla wake katika hali mbaya zaidi kuliko hii tuliyonayo leo!! Ufisadi ni hulka iliyojengeka kwenye jamii yetu na haitafutika kwa kuanzisha majimbo bali inahitaji kupata viongozi wazuri ngazi ya taifa watakaokuwa committed kupambana na ufisadi nchini kote.

4. Kuna maeneo ambayo yalitengwa kimaendeleo tangu tupate uhuru mpaka sasa hivi. Haya ndo yale yanayojulikana kama maeneo ya pembezoni. Mfano hapa ni suala la Mtwara na Lindi. Juu ya kuchangia kwa kiwango kikubwa kupitia zao la Korosho, bado hakukuwa na mipango makusudi ya kuiendeleza mikoa hii ili iweze kuzalisha zaidi. Utajiri wa mikoa hii ukawa unahamishiwa kwenye maeneo mengine na kuiacha mikoa hii kubaki masikni na hivyo kuathiri sio tu mikoa hii bali taifa kwa ujumla kwani ufanisi wa uzalishaji ambao ungepatikana kwa kuiendeleza mikoa hii ungeongeza tija zaidi na kuinufaisha Tanizania nzima. Sasa haitakuwa sahihi kuanzisha sera ya majimbo na kuiweka mikoa hii kwenye kapu moja na mikoa ambayo ilikuwa inainyonya mikoa hii na kuhamishia utajiri kwao. Ni sawa na kumfunga mtoto mmoja mikono na kumwambia mwingine ampige ukijua kabisa kwamba kwa kumfunga mikono hatakuwa na uwezo wa kurudisha ngumi!!!

5. Mgawanyo wa ziada utakaoenda serikali kuu kwa ajili ya kugawanywa kwenye majimbo mengine bado nao una uwezekano wa kuwa na utata uleule tulionao sasa kama viongozi wa juu wataamua kugawa kutokana na maslahi yao badala ya nchi nzima. Kuleta majimbo hakuondoi hali hii ya uwezekano wa wakuu wa nchi kuegemea kwao. Solution ni kuwapata viongozi makini wanaoona uchungu na kuona aibu kuwa kwenye taifa ambalo ni tajiri lakini watu wake ni masikini wa kutupwa.

Kwa hiyo badala ya kuwa na sera za majimbo ni bora tukaweka nguvu zetu kwenye kupata viongozi wenye uchungu wa kweli na nchi yetu na ambao wana vision ya kuelewa nini kinatakiwa kufanyika ili kuiokoa nchi yetu kwenye hali hii ya umasikini. Tukishawapata hao, basi nguvu ielekezwe kwenye kuendeleza maeneo ya elimu na kutoa kipaumbele kwa kuendeleza maeneo ya pembezoni kwani Tanzania haiwezi kuendelea kwa ujumla wake kama maeneo haya hayataendelezwa. Maendeleo ya maeneo haya ya pembezoni yataleta tija kwenye maeneo yao na hivyo kuongeza uzalishaji utakaofaidisha maeneo mengine. Yatawafanya watu wa pembezoni kuwa na uwezo wa kiuchumi na hivyo kuongeza wigo wa soko kwenye maeneo yenye neema. Kifupi yataongeza synergy kwa ajili ya kuharakisha maendeleo ya watanzania wote kwa haraka zaidi kuliko ilivyo hivi sasa.

Haya ndio mambo ambayo Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) ikipata madaraka itayashughulikia na tunaomba watanzania mtuunge mkono kwani tuna mtazamo sahihi zaidi wa nini kifanyike kwenye nchi yetu kuliko chama kingine chochote hapa Tanzania. Chama chetu ni chama ambacho kimedhamiria kuwa chama darasa sio tu kwa vyama vilivyopo Tanzania bali Africa yote kwani tunaona aibu sana kwa Tanzania in particular na Africa in general kuwa maeneo ya watu wanaodharauliwa kwa sababu ya umasikini wao, kwa sababu ya kuwa ombaomba wa kutupwa na kwa sababu ya kutojiamini kwa watu wao kunakotokana na viongozi matapeli wanaoweka mbele maslahi yao ya kisiasa na ndugu na jamaa zao kuliko maslahi ya taifa kutokana na ufinyu wa uwelewa wao kwa nini wako pale kama viongozi wa nchi.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRICA.
 
Umekuwa wakati muafaka wa kuongelea kuhusu kusini, hoja ni wananufaika vp na gesi, hata mahojiano ya Prof Muhongo kwenye dkk 45 hajajibu hii hoja.
Dar tuna maslahi nako sawa but wenzetu tutaendelea kuwaacha nyuma hadi lini mana kama rasilimali sasa wanayo
 
Kama sera za kikoloni mmeshindwa kuzitumia kuiletea nchi maendeleo,ni wakati muafaka wa kutumia sera mbadala za majimbo nazo zitatutoa hapa tulipo na kutupa maendeleo mbadala.Mabadiliko katika nchi yetu kwa sasa ni lazima ili tuondokane na umaskini wa kulazimishiwa na kikundi kidogo cha watu wachache.
Mkuu Mnyika kasikia Marekani kuna sera ya majimbo basi imemuingia akilini ila hajui wamarekani iliwachukua miaka mingapi kujenga sera ya majimbo; hivi sasa Chadema hata ile demokrasia ya uhuru wa kutoa mawazo hakuna angeanza kwa kujenga demokrasia ya kweli ndani ya chama chake; msingi mkuu wa sera ya majimbo ni demokrasia ya kweli kitu ambacho Chadema hakipo; angeanza na somo la demokrasia kabla ya kurukia majimbo!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Na hii itasaidia kuepukana na viongozi wasiofaa kwa jamii husika, wenye historia mbovu huko watokako wanaopewa kwa ushoga na urafiki na baadhi ya wakubwa. e.g. DC's na RC's kama yule jamaa wa GEITA rafiki wa wenye mgodi..
 
M.M.Mwanakijiji
Wapo wengine walioandamana kupinga ujenzi wa barabara kwenye maeneo yao, wapo waliopinga kuchimbwa mafuta au madini, na wapo wengine ambao wamepinga ujengwaji wa bomba la mafuta!

Mojawapo ya mifano mikubwa ya upingaji huu ni ule unaoendeleaMarekani dhidi ya bomba la mafuta la TransCanada ambalo limekumbwa na upinzani mkubwa japo mafuta yake yanahitajika sana kwa uchumi wa Marekani. Wanaopinga bomba hili wamefanya kila aina ya upingaji ikiwemo kupinga nje ya Ikulu ya Marekani. Wamefanya hivi si kwa sababu wanaongozwa na vyama vya upinzani au hawajui manufaa ya kiuchumi.
Hili ni kweli hata Canada ambapo bomba la mafuta/gesi la Enbridge limejikuta kwenye upinzani mkubwa hasa kutoka kwa wakazi wa asili (first nations) wa maeneo ambayo bomba lilitakiwa kupita. Kwa karibu miaka kumi sasa bomba hilo limechelewesha kuanza kwa sababu wananchi wanaamini kuwa lina lengo la kunufaisha makampuni makubwa wala si watu wa maeneo bomba litakalopita. Viongozi wa Canada (kama wale wa Marekani) wamejaribu na wanaendelea kujaribu kuwashawishi wananchi na kusikiliza maoni yao na hata kubadilisha njia ya mabomba hayo na kuweka programu ambazo zitawanufaisha wananchi wa maeneo ya mabomba hayo.
Hivyo, wananchi wa Mtwara kama wa maeneo mengine nchini wana haki ya msingi kabisa na kwa hakika si usaliti kudai kuwa rasilimali zilizoko katika maeneo hayo ziwanufaishe. Hii ni haki ya msingi ya wananchi.

Chanzo.Tanzania Daima,Jumatano,9,1,2013
Hii makala wala usingeileta huku, imekaa kishabiki na imepindisha ukweli. Tatizo la pipeline hiyo ni mazingira wala siyo kutofaidika kiuchumi. Ni environmental degradation ndiyo iliyofanya watu wapinge ... na wengi wao wala hawakai maeneo ambayo pipeline hiyo ingepita.
 
Mimi naliona Tatizo kubwa ni uelewa mpana wa maana na uendeshwaji wa serikali ya majimbo.watu wangesoma kwa undani na kuuulewa zaidi na kuchambua kipengele kimojakimoja kuonyesha mapungufu yake na faida zake , tupate conlussion nzuri yenye tija kwa taifa letu wote, badala ya kutumia muda mwingi kushabikia vyama kwa kujibizana.
 
Ni kweli watu wanatakiwa wasome kwa makini sera ya CHADEMA kuhusu Majimbo kabla ya kuchangia. Mimi hapo juu nimeweka post yangu ambayo inatoa mtizamo wa CHAUMMA nayo inabidi muiangalie kwa makini ili muone kama kweli sera ya majimbo itatusaidia au la kwa mazingira tuliyonayo sasa hivi.
 
majimbo ni sera za wanasiasa uchwara wasioijua historia ya Tanzania. Tunahoji upeo wao kitaaluma. Nani asiyejua kuwa utawala wa majimbo itakuwa ni kuigawa Tanzania?? Ushauri wa bure elimu za wabunge zithibitishwe TCU. Kuna vihiyo maarufu lakini watatu cost
 
Biznocrats,

..hebu tueleze ni mikoa gani ilikuwa inainyonya mikoa ya kusini.

..mikoa ya kusini ilikuwa na zao la korosho ambalo lilikufa kutokana na utekelezaji mbaya wa zoezi la vijiji vya ujamaa.

..sasa baada ya korosho kufa ni kitu gani ambacho unaweza kusema kilikuwa kinatoka kusini na kwenda kuendeleza maeneo mengine ya Tanzania??
 
Last edited by a moderator:
Napata wasiwasi na uelewa wa hawa wanaopinga umuhim wa sera ya majimbo kamba ambavyo john mnyika na cdm walivopendekeza mbele ya tume ya maoni ya katiba.
Ni ukweli ulio wazi kuwa utaratibu wa umeshindwa kuleta maendeleo ambayo kila mtanzania anahitaji hasa kwa kuzingatia uwingi wa rasilimali zilizopo kila kona ya nchi hii.
Hata kama si mwanachama wa cdm kwa hili la majimbo wanastahili pongez na uungwaji mkono.
 
Back
Top Bottom