John Mnyika: Sera ya Majimbo ya CHADEMA siri ya Maendeleo

John Mnyika: Sera ya Majimbo ya CHADEMA siri ya Maendeleo

Dats why nikasema utafte/u download hayo maandiko usome bro hata local government reform program unasema ni ya zamani? Civil services reform program,legal sector reform program and local gvnt reform program ni vitu current sana na ndo baadhi zimetoka kufanyiwa evaluation last year tu kaka.
Ok nitatafuta hayo mapendekezo, hila usichanganye sana mkubwa local government pia ni political system ambayo aim ni decentralizing power into local politics (and there is nothing new there). Huo ni mfumo ambao hupo kwenye both in unitary and federal government.

Hiyo ni ripoti tu ya mapendekezo ya local government itakavyokuwa au inatakiwa kuwa ndani ya Tanzania and how best to reach people, lakini the 'politics of local governance' huo si mfumo geni duniani,labda hatukuelewana.

Usiku Mwema.
 
Kiujumla ninavyoelewa mfumo wa majimbo upo hivi; Gavana ndiyo kiongozi wa jimbo ,anachaguliwa na wananchi wa jimbo lake. |Kisha wanakuwepo masenator wa kila sehemu kama wabunge. Ila sasa hakuna tena bunge kubwa la Jamhuri kwa sababu magavana wanawakilisha majimbo kwenye bunge la jamhuri. Kama majimbo ni 10,basi wawakilishi ni 10. Ila majimboni mwao wanakuwa na sanate ambayo ndiyo inapitisha bajeti na kutunga sheria. Serikali kuu inasimamia mambo ya nchi zaidi,ikiwa ni ulinzi(jeshi,police /or immigration),fedha,mambo ya nje tu
 
Ndugu Ritz usingeishia kukerwa na mchango wa Mnyika.Ingependeza sana kama ungetoa maoni yako juu ya maeneo unayopingana naye.Kwa maneno mengine ulitarajiwa upambanishe hoja ukionyesha kwa nini hoja zako,kama unazo, zikubaliwe na zake,alizotoa tayari, zitupiliwe mbali.
Pasipo kufanya hivyo ,mchango wako unabaki kama ''argumentum de hominem''.


......

Ritz is completely empty headed, ni mdini tu, I hardly see him in need of JF Vs.
 
Tunaomba takwimu za mapato yanayotokana na almasi (kwa awamu zote nne za utawala wa tanzania) na namna ambavyo tanzania (kama nchi) imefaidika na almasi za mwadui.

......
Na;
Tanzanite Gold Udongo unaosafirishwa NK
.
 
mawazo ya watu wengine nyie, hivi kwani watu wakitaka ulaji mpaka waitete CCM au watu wakikosoa CDM wanamaslahi na CCM katika hili jukwaa.

Mimi namjua mtu wala hakanyagi hapa JF na wala anashida ya kutokea kwenye ma-blog, lakini sasa anaoneshwa namna ya kubadili mboga tena kwa kutafutwa ni yeye tu kuamua. Mjomba kuna njia nyingi za kudandia band-wagon kama watu wana agenda hizo. CCM Afrika inawanachama luluki hadi JK akujue leo, we uoni jamaa wa diaspora wakitokea tu na raisi wanakutana nae, umewahi jiuliza kuna wanachama wanagapi ndani ya Tanzania wamekutana na JK au kukaribishwa mlo.

Isitoshe viongozi wakuu wakija kukutana nao kwa walio ulaya wa sio big deal, si unaona Mnyika kesha sema anakuja drinks bure kwa mtu mwenye tamaa za siasa hapo ndio pa kujitambulisha.

Acha ushamba wewe, waliokaa kisiasa ni wanasiasa na ambao wanakwambia hawapo kisiasa jua ni commentators tu (kwani tabu kuchukua form ya CDM au CCM kama kweli mtu ana nia, halafu umesoma hule ujumbe wa Ikulu wa kutaka diaspora wachangie taifa kwa mawazo, hata kwa kazi za mikataba kama bado hawataki kurudi) watu wanandoto za kuingia sehemu ambazo siasa za bongo hazilipi kabisa wewe unafikiria kujikomba-komba tu. Akili ya mtu mpuuzi bwana.

I guess uliandika hii thread ukiwa kwenye msongo wa mawazo kama siyo ya kufungwa basi life limebana!:nono:
 
Uzuri ni kwamba CHADEMA wamejipambanua bila kificho kuwa ni wapenda mabadiliko na wasioridhishwa na hali halisi ya maisha ya watanzania. Kwa watanzania wengi hiki ni kigezo tosha kwenye kampeni za uchaguzi wa 2015 kwa sababu wapiga kura wengi hawako tayari kuendelea kuukumbatia umaskini uliokidhiri miongoni mwa familia zao,
 
huko ni sawa na kumwambia mwanafunzi ni bora achukue nyenzo kuliko kufeli. Life doenst work like that unachotakiwa kumshauri ni kupigana na masomo hili afaulu.

Vilevile binadamu wana namna zao kuishi katika jamii zao, kwa maana hiyo sera ya majimbo might bring anarchism in the future if those who are selling the idea, miss even a single joint of our social structure (that is Tz's and not anywhere else, these things are determined by to society to society and people living in different societies do differ). Na kwa hali ya sasa, sera ya majimbo bado sana kwetu.


......

Unaweza kuniambia nini maana ya sera ya madaraka mikoani? anarchy kwa sasa hujaiona bado hapa nchini au bado iko kwenye projection?

Uamuzi gani unaweza kuwa makini wa watu wengi au wachache? nani rahisi kununuliwa watu wawili au watano?
 
Ni bora vyama vya siasa vikajikita zaidi katika matatizo yanayowahusu wananchi na kujenga mikakati isiyowagawa kitaifa.

Kiukweli leo hii ukimuuliza mtanzania kuhusu hii sera ya majimbo hakuna jibu la maana atakalokupatia kwa maana ya faida na hasara zake.

Wanasiasa ni bora wakatulizana kwanza katika hili,hakika ni wazo zuri ila kwa sasa sidhani kama lina nafasi labda 2025-2030.

Nimesema haya kwa sababu kuu nne'
1.Bado hatujawa na wanasiasa wakomavu na wenye kufanya wanayoamini ni kweli kwa manufaa ya taifa na kama wapo basi ni kwa maslai yao binafsi na wale waliowatuma kuyafanikisha.

2.Elimu ya uraia bado ni tatizo kwa suala kubwa la kiutawala kama hilo,ukizingatia kuwa utawala unazumgumziwa unaweza kupitiliza na kuwafanya watu wajitawale kikanda,kikabila na kidini na hivyo kupelekea taifa kukatwax2 vipandex2.(KUIFANYA CENTRE G'MENT KUKOSA NGUVU/MAMLAKA).

3.Umaskini bado ni tatizo kubwa kwa baadhi ya kanda/majimbo yaliyo mengi na hii itasababisha ubaguzi kwa watanzania na kuwapelekea kuwa wakimbizi wa ajira kwa majimbo mengine.Hii inaweza kusababisha wizi mkubwa kwa watu wa ukanda fulani ili waendelee kuuimalisha ukanda wao.

4.Ardhi yaweza kutumika vibaya na bila mpangilio wa utanzania na hivyo kupelekea ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kwa baadhi ya majimbo/kanda/ ambazo hazina ardhi.

Kiukweli ni wazo zuri sana,ila linahitaji pesa nyingi na utashi wa kisiasa hili kuzifinyanga vizuri kanda hizo kwa mtizamo wa Utaifa.

Democrasia siku zote ni kuwagawa na kuwatawala watu iwe kwa kutaka kwao au kwa lazima ya wenye nguvu ya pesa.

Uhuru na Umoja wetu ndio silaha iliyo bora zaidi ya kupambana na adui zetu,ebu tuitumie silaha hii hakika tutafika salama huko tunakokwenda.Ni bora kabisa kwa sasa vyama pinzani vikajiweka tayari kuwa HURU na kuunda UMOJA wenye nguvu ambao unaweza kutoka na wazo kama hili kwa pamoja lenye nguvu ya UMOJA,ebu jivueni mavazi yenu na kuvaa mavazi mapya yenye sura ya Kweli ya UMOJA wa Mtanzania ili 2015 wananchi wasipate mashaka juu yenu.
 
Unaweza kuniambia nini maana ya sera ya madaraka mikoani?
Swali kidogo lina utata, but one thing for certain it does not fall under federalism kama tunazungumzia muundo wa Tanzania. Hata kwenye federalism and unitary states kuna regional politics, so your question ought to be precise.
​
anarchy kwa sasa hujaiona bado hapa nchini au bado iko kwenye projection?
People power must be initiated by ppl themselves vinginevyo unaweza sema ni uchochezi wa wachache kinachoendelea sasa. The only movement that was tried and initiated by ppl themselves ni kama vile waman'gati kutaka kuchukua ardhi kinguvu, wameru kuchoma shamba la mwekezaji wakidai ni mali yao, au wamasai kuandamana mpaka ikulu.

Those were genuine people movements aroused by their own concerns for what they saw as the government trying take what is rightful theirs. Mengine ni demagogues fueled troubles (na matatizo haya yanaweza kuwa makubwa under federalism)
uamuzi gani unaweza kuwa makini wa watu wengi au wachache?
it depends on the numbers your talking about, nevertheless ancient Athenians democracy is no longer practicable in today's societies kwa hiyo kusemaa federalism itatatua hilo si kweli.
nani rahisi kununuliwa watu wawili au watano?
inategemea watu gani unanunua, bei ya Lowassa peke yake ni sawa na akina Le Mutuz mia labda (joke).
 
Hatujui hapa alichodandia nini, zaidi ya maelezo yenye akili ya mfumo wa kumkomboa mtanzania mnyonge wa Tanzania anayeendelea kunyonywa kutokea maelekezo ya magogoni. Amejibu tuhuma ya yule babu aliyetoka porini akawa mtu aliyoitoa pale kwenye TV ya CCM=TBC. BRAVO JJ MNYIKA, ENDELEA KUTOA MAELEZO YENYE SHULE KWA VILAZA.
John Mnyika siku hizi amekuwa mtu wa kudandia matukio tu. Juzi alidandia maandamo ya Mtwara, mara tena akadandia katiba hataki rais aingilie bahati nzuri Warioba akamfahamisha. Leo tena kaja na sera za majimbo.
 
Hili analosema mnyika ni kweli, kwa wale wanaoijuwa tanga ya miaka ya nyuma ya 85, ni ilikuwa ya neema kubwa ya viwanda, lakini leo viwanda karibu vyote vimeamishiwa Dar es salaam, chini ya utawala wa majimbo isingelikaa itokee hiyo ambayo imeuwa tanga kiuchumi by 98%
 
John Mnyika siku hizi amekuwa mtu wa kudandia matukio tu. Juzi alidandia maandamo ya Mtwara, mara tena akadandia katiba hataki rais aingilie bahati nzuri Warioba akamfahamisha. Leo tena kaja na sera za majimbo.

Acha porojo chambua hoja, tupe mapungufu au ubora unaouona kuhusu anachosema Mnyika
 
kuonesha kuwa sera ya majimbo ya Chadema yaweza kuwa mkombozi wa mtanzania katika nyanja mbali mbali, ivi karibuni baada ya matokeo mabovu ya mtihani wa kidato cha nne, Mkuu wa mkoa wa Mbeya pamoja na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mbeya wamepitisha maamuzi ya kimkoa kwamba wanafunzi wote wanaoandikishwa darasa la kwanza watajifunza K 3 yaan kusoma, kuhesabu na kuandika kwa mda wa miezi 3 hadi 6 na hatoruhusiwa kuendelea na masomo ya darasa la kwanza hadi atakapojua hizo K 3, pia wameazimia kwamba mara baada ya watoto kuhitimu darasa la saba watajifunza koz ya kiingereza kwa miezi 3(ocober - december) bila kujali atafaulu au la.

Hayo n maamuzi ya mkoa bila kujali wizala imepanga nn. sasa kama leo mkoa unapanga kujikomboa kielimu je haitakuwa zaidi kijimbo na katika nyanja nyingine pia ikiwemo uchumi?
 
kaka mnyika ulikua unafanya mazoez ya kuandika kuhusu majimbo au ndo ushaandika ivo?
 
Wadau naomba Chadema idadavue hii sera ya majimbo vizuri ili watanzania waweze kuifahamu vizuri. nimemskia mwanachama mmoja wa ccm anaipitisha jamii sana kuhusu sera hii nzuri ambayo inatumiwa na nchi nyingi zenye maendeleo kama Kenya, Ghana, USA Na kwingineko
 
Wadau naomba Chadema idadavue hii sera ya majimbo vizuri ili watanzania waweze kuifahamu vizuri. nimemskia mwanachama mmoja wa ccm anaipitisha jamii sana kuhusu sera hii nzuri ambayo inatumiwa na nchi nyingi zenye maendeleo kama Kenya, Ghana, USA Na kwingineko

Hizo nchi zote ulizotaja zina ubaguzi wa hali ya juu wa rangi na ukabila.Majimbo yao yamegawanywa kwa misingi ya kikabila na ubafuzi wa rangi.Nchi nyingine zenye mfumo huo wa majimbo ni zile zenye ubaguzi wa kikabila kama Afrika ya kusini na Nigeria ambako majimbo yamegawanywa kikabila na rangi.

Tanzania imeiga mfumo wa Ulaya ambao haubagui mtu kwa kabila au rangi ambao mwasisi wake ni mbaguzi wa rangi mmarekani.
 
Hizo nchi zote ulizotaja zina ubaguzi wa hali ya juu wa rangi na ukabila.Majimbo yao yamegawanywa kwa misingi ya kikabila na ubafuzi wa rangi.Nchi nyingine zenye mfumo huo wa majimbo ni zile zenye ubaguzi wa kikabila kama Afrika ya kusini na Nigeria ambako majimbo yamegawanywa kikabila na rangi.

Tanzania imeiga mfumo wa Ulaya ambao haubagui mtu kwa kabila au rangi ambao mwasisi wake ni mbaguzi wa rangi mmarekani.
unaongea nini wewe,kwahyo nchi kama Marekani waligawa maeneo ya weusi na weupe au kabila flani likae jimbo hili na lingine likae jimbo lile!!!ukabila na ubaguzi sio kitu chakuzuka tu...huwa na mwanzo wake, Nchi kama Kenya hata wasingekuwa na mikoa au wilaya...bado ubaguzi ungekuwa pale pale tu...Tz ni tofauti na Kenya,nchi ambayo watu wanasoma pamoja,wanaoleana,wanafanya kazi pamoja na n.k ningumu kuzalisha ubaguzi...kama ni ishu ya ubaguzi hapa Tz itaanzia kwenye huu upuuzi wa shule za kata,mtu amezaliwa Matombo-Morogoro,anasoma msingi hapo hapo,secondary hapo hapo...hapati hata muda wakuishi na makabila mengine zaidi ya Waluguru wenzake tu.
 
Hizo nchi zote ulizotaja zina ubaguzi wa hali ya juu wa rangi na ukabila.Majimbo yao yamegawanywa kwa misingi ya kikabila na ubafuzi wa rangi.Nchi nyingine zenye mfumo huo wa majimbo ni zile zenye ubaguzi wa kikabila kama Afrika ya kusini na Nigeria ambako majimbo yamegawanywa kikabila na rangi.

Tanzania imeiga mfumo wa Ulaya ambao haubagui mtu kwa kabila au rangi ambao mwasisi wake ni mbaguzi wa rangi mmarekani.

Ndo mnavyowapotosha watanzania, si kweli hata kidogo, labda nianze kwa kukuuliza je mikoa haijawagawa watu kwa makabila, udini na rangi? mfano ukienda mikoa yote ya ukanda wa pwani utakuta makabila flani na dini flani na hata rangi flani, ukienda kusini mwa tanzania utawakuta kabila flani na dini flani na rangi flani sihitaji kukueleza zaidi hapo. unachotakiwa kufahamu ni kuwa, majimbo yana nia yakusaidia wananchi wa eneo husika kuweza kusimamia raslimali zao nakuzitumia kwa ufanisi kwa maendeleo ya sehemu husika, pia inaongeza uzalendo katika utumzaji na udhamini katika raslimali hizo. lakini poa majimbo yatacut off automatically matumizi mabaya ya kodi za wavujajasho hasa by central givernment sioni harufu ya ubaguzi kwny majimbo ni propaganda feki za wasio weza kufikiri kwa undani
 
Wadau naomba Chadema idadavue hii sera ya majimbo vizuri ili watanzania waweze kuifahamu vizuri. nimemskia mwanachama mmoja wa ccm anaipitisha jamii sana kuhusu sera hii nzuri ambayo inatumiwa na nchi nyingi zenye maendeleo kama Kenya, Ghana, USA Na kwingineko


Chadema hawana cha kukufafanulia hapo wao ni wasaka tonge na ukawa itakufa kabla ya july niamini. Chadema na cuf pamoja na nccr watashindwa kuelewana katika mambo haya
- kugawana majimbo
-kusimamisha mgombea mmoja wa uraisi


Na wakati ukawa wanajadiliana kuhusu ili swala CCM itawabiga bao la kisigino.
 
Back
Top Bottom