John Mnyika, kuulalia mkeka uliochanika kunahitaji akili nyingi sana na sio nguvu

Mtondoli

Member
Nov 9, 2021
70
174
Comred Mnyika mdogo wangu na Katibu Mkuu wa chama kikuu Cha upinzani CHADEMA tunataka tuuone utashi na hekima na busara zako katika kipindi hiki kigumu, chama chako kina Kariba kubwa ya vijana ambao bado wana mihemko.

Mkeka uliolalia umechanika Sana, usitumie nguvu kubwa utauchana zaidi. Maneno yako yawe na busara ya kiuongozi tunachotaka Mbowe aachiwe hayo mengine tunayoyasikia kwa vijana wenu mtayafanya akiishaachiwa.

Isingekuwa maneno yenu ambayo nasema yametokana na mihemko ya vijana wenu huenda krismass hii Mbowe tungekuwa nae.

Ukiwa na njaa usichague mkono utakaokulisha kula ili ushibe mengine yatafuata. Kumshambulia Zitto na Rais Samia kumerudisha nyuma mchakato wa kumtoa Mbowe hata mamlaka zinaweza kuhisi mna kiburi.

Mjumbe hauawi.
 
Mnyika ni mwanasiasa wa hovyo sana ambaye jimbo limemshinda kitambo

USSR
 
Ndugu mjumbe unaongea ulichokuwa na uhakika nacho au unabahatisha .
 
Unaongea wakati umebana pua kisa buku 7?
 
Jifunze kwanza kuandika wewe sukuma gang.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…