John Mnyika awe mwenyekiti CHADEMA...

John Mnyika awe mwenyekiti CHADEMA...

Mnyika anafaa lakini sio kwa hali ya sasa. Uongozi uliopo ni mzuri sana wala usiguswa. Sisi tuendelee kuwapa ushirikiano mpaka tuuone ukombozi. Watu wengine bana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! wanawaza madarakatu. Hi kamba tuikazie hapo hapo mpaka tupate katiba mpya.
 
Ukifuatilia matatizo meengi ya nchi hii
utakuta tatizo la 'age gap' kati ya viongozi wanaotawala na wananchi..

zaidi ya nusu ya watanzania ni 'below 30 years old...inasemekana almost 60
au 75 percent ya watanzania umri ni below 35
na ukichukua below 40 unaweza kukuta ni almost 65-80 percent....
mwenye accurate data
tafadhali aweke hapa.......

sasa basi mimi kwa maoni yangu naona viongozi kama Zitto,Mnyika,January,Kafulila na wengineo vijana
angalau wana 'advantage' ya kuwa connected na masula hasa ambayo viongozi
kama Kikwete na wazee wenzake wengi hawaelewi kabisa...
kuna a 'A BIG DISCONNECTION' kati ya wananchi na wazee kwa hakika...

Mimi ningependa Zitto awe mwenyekiti CHADEMA....lakini
ameshaanza kuwa 'na wapinzani wengi' ndani ya CHADEMA itakuwa ngumu kwake kupata
Uenyekiti au 'legitimacy' inayohitajika pengine kwa sasa....

sasa nilipomuangalia John Mnyika jinsi alivyoendesha kampeni ya ubungo
bila 'kumjeruhi' Julius Mtatiro na jinsi 'anavyo perfom bungeni now'
pamoja na kutomkubali huko nyuma,ameni convince now kuwa 'he is a better leader'
kulinganisha na wengine ndani ya CHADEMA....

1.Sifa ya kwanza ni 'uniter'..ataweza kuunganisha CHADEMA na vyama vingine.


2.Sifa ya pili anapenda 'dialogue' kuliko 'maandamo'....


3.Sifa ya tatu ambayo mimi naona ni muhimu mno now ni age...
ata 'connect' na wananchi ambao wengi ni vijana
yuko engaging na watu....

4.hana 'political garbage' ya aina yeyote for now...haitaji kulipa fadhila kwa yeyote
yuko free kufanya maamuzi kwa jinsi anavyoona,ana uwezo wa kuwa 'ndependent'
kimawazo...

na sifa zingine nyingi kumlinganisha na wengine......

now its time,tukisubiri 'azeeke' atakuwa 'corrupt' na mazoea na culture za siasa za makundi

Chadema wafanye kama DEMOCRATS walivyofanya kwa OBAMA....

mimi nafikiri its time Mnyika awe Mwenyekiti,CHADEMA itawasaidia
1.hoja ya uchagga na ukaskazini
2.hoja ya chama cha familia...

na hoja zingine...nyiingi....Urais anaweza kugombea SLAA au yeyote but Mnyika awe Mwenyekiti....

Naunga mkono hoja 100%. Mbowe na silaa wawe background characters.
 
Hey! guys, you can't convince me to prove dat mbowe has proved failure in his leadership and dis iz coz av the below reasons

1. The political system av Tz neccesitates the environment to set for demonstrations,strikes and even violence especially to antagonistic part like CHADEMA coz no altenative to set peace among political parties since a ruling part(CCM) seems to dominate everything in a concern ov Tz politics

2.Bob Makani a preriorly chairman av CHADEMA proved failure to set equality among parties kwa kutumia hiyo busara unayosema Mnyika is behaved too. sasa leo huyo Mnyika atafanya nini ktk mfumo dharimu wa siasa wa kina Jaji Lewis Makame,Werema na kina Tendwa?

3. Mnyika unaemsema leo ni zao la Chadema chini ya Mbowe. unachotaka kufanya wewe hapa ni kutaka Mzee.Yusuph Makamba kuanzia leo aanze kumpa shikamoo January(mtoto wake) maana ktk karne hii mtoto ameonekana kuwa na busara ya siasa zaidi ya Baba yake Mlopokaji.

Zamu ya Mnyika ipo tuu! ila Zitto aende tuu huko kwenye Magamba, maana ni mna'...
 
naunga mkono hoja na umelezea Vzuri sana Mnyika ni mbunge ambaye anajua kupangilia hoja na huwa hakurupuki na wala si mlopokaji sio siri ni Mmoja kati ya wabunge wachache ninao waheshmu. But suala la akizeeka atakuwa corrupt hilo siwez kukukatilia wala kukuunga mkono kwasababu siasa ya 3rd World countries sio siri haielewek ndugu yangu.

Kila mwanadamu ni rational na temptations za ku win in life zinamkuta kila mmoja hasa pale future inapokuwa uncertain. Tatizo kubwa la wanasiasa na hata viongozi wa zuri Tanzania ni swala la life after office risk ya kuamua kwa maslahi ya wengi ni kubwa zaidi kwani hao wengi ambao tunawapigania hawaelewi thamani ya kile wanapiganiwa wapatiwe na mara nyingi huweza kukugeuka wakati wowote ile burden ikawa born na familia yako.

Kwasababu ya hili ndiyo maana wengine wetu tunapigania kwa nguvu zetu zote katiba itakayo punguza risk ya individuals kuwa spoted nakuwa victimised badala yake kuleta collective responsibility ambapo kila mmoja anapata nafasi ya kusimamia anachokiamini bila kuwa victimised.

Hili lakatiba wengi wa elite hawalioni kwa sababu ya hiyo hiyo uncertainty ambayo inasababisha averse character inayoambatana na high level of risk katika kuamua jambo. Ukiwa na maskini wengi ambao hawawezi kusimama bila mtu fulani kuwapendelea mara zote hawako tayari kupoteza hicho kidogo wanachopata mpaka ifike mahali ambapo hata ukiangamia hunachakupoteza ndiyo huyo mtu anaweza akachukua risk so far mwendo wa elites wengi ni kuwa hawakosi chakula lakini pia hawajitoshelezi wako tu kwenye survival level (just enough). Viongozi wakawa wajanja kama wakoloni wakatengeneza devide and rule strategy ambapo chief executives wote wana more than enough ili waweze kuwadhibiti wenzao kwenye serikali na pia ruzuku kwenye vyma vya siasa ku serve the same interests. Chakujiuliza ni kuwa kwa faida ama hasara ya nani? Ndipo hapo uzalendo wa seniors unapohitajika kuondoa hizi connstraints ili kila moja awe better off.
 
Nakumbuka maneno ya mwalimu wangu aliniambia ukiona mtu uliokuwa mnajadaliana nae anaanza kutoka matusi hovyo...

Ujue umembwaga kwa hoja..

Sasa mambo ya masaburi yametoka wapi tena mkuu?

Au ndio matunda ya makuzi yako kutoka kwa wazazi wako!
Acha unafiki,namna ya kudeal na nyie inajulikana.

Mtu usiejibu hoja ujibiwe vipi?
 
Zitto mwanachadema damu.mnao msumbua mnalenu jambo.
Kafanya baya gani ndani ya chadema?

Ni kweli Zitto alikuwa kijana mzuri, alitushawishi wengi kwa hoja na misimamo yake bungeni tulimshabikia na kumpenda sana pale mwanzoni. Lakini kuna kipindi alitunyongonyeza kabisa na tukapoteza imani kwake ambayo kuirudisha itamcost sana.

He is controversial. alisupport kununua mitambo ya kampuni ilizotutapeli ya JK, Rostam na EL (aka Richmond-Dowans) na baaadaye alipoona wabongo wamemshtukia ndio akarudi kwenye ukweli na kushauri itaifishwe.
Ameanyisha mitandao ndani ya CDM, kama JK alivyoanzisha mitandao inayoitafuna CCM hadi leo, hivyo ataleta mgawanyiko ndani ya CDM.
Ana mawasiliano controversial na vigogo wa CCM, mafisadi kama RA na usalama wa taifa. Refer MWANAHALISI, madai ambayo hadi leo Yitto ameshindwa kuyatolea maelezo zenye mashiko, zaidi ya kuattach personalitz ya kubenea na kuwa hajasoma badala ya kujibu hoja zinazopinga evidence zilizochapwa na MWANAHALISI.
Anatumia gazeti la MWANANCHI kumkampenia n a wakati mwingine kufanya kampeni Chafu, mara kalishwa sumu amelazwa, na sasa hata akiumwa mafua anatolewa front page kuwin cheap popularity..

Mnyika ni tofauti sana, hajawahi kuwa controvesial kwa lolote, ni makini sana na halewi sifa, kuna email moja chafu ya Zitto aliinasa. sikumbuki kama Zitto aliwahi kikana au kuitolea maelezo.
 
Mnyika anafaa kwa Ukatibu mkuu, yupo kiutendaji zaidi.
 
haswaaaa ulipokuja wewe ndipo nilipo pataka
mimi nimemfananisha na wengine CHADEMA nimemuona yeye zaidi
tazama
1Zitto -yuko 'tarnished' na makundi ya CHADEMA
2.Mbowe- the same,background yake 'haiko convincing,hana kipya..
3. Slaa- yuko tarnished kwa waislam,na skendo ya ndoa yake..
4.Lissu- yuko so 'mwanaharakati' kuliko kuwa mwanasiasa...ana ugomvi na CUF na NCCR tayari
hawezi ku UNITE
5..Mdee- hayuko on her own ki chama,anaeegemea kundi..fulani

umeonaaa??????

Kichaa cha ccm kimekupanda kweli. Naona mnaleta hoja za kukigawa chama na kujaribu kutuchagulia mtu soft. Mwk wetu ni kamanda mbowe na atakapostaafu TUNDU LISSU ndani, huyu anakwenda kumalizia kazi ya kamanda mbowe. Sijui mnyika, zitto nk, hao unawajua wewe. Cdm ni ya makamanda sio watu lelemama.
 
Chadema hawaitaji watu laini laini ni majembe tu,MBOWE Amekiweka chama mahali pazuri sana,ZITTO nae ni Jembe akiacha maringo ya kishamba.
 
Katika mazingira na historia ya kisiasa kwa hawa vijana wawili yani zitto na mnyika sio rahisi mmnyika awe mwenyekiti afu zitto apewe nafasi ya uongozi chini yake. Labda abaki mjumbe wa vikao tu vya cc na nec. Mana kwa vigezo vyote mnyika bado ni junior kwa zitto. Sijui ndani ya chama hali ikoje. Ingawa wakikubaliana wanaweza kuwa hivyo. Mnyika awe mwenyekiti na pengine zitto awe makamu.
 
Katika mazingira na historia ya kisiasa kwa hawa vijana wawili yani zitto na mnyika sio rahisi mmnyika awe mwenyekiti afu zitto apewe nafasi ya uongozi chini yake. Labda abaki mjumbe wa vikao tu vya cc na nec. Mana kwa vigezo vyote mnyika bado ni junior kwa zitto. Sijui ndani ya chama hali ikoje. Ingawa wakikubaliana wanaweza kuwa hivyo. Mnyika awe mwenyekiti na pengine zitto awe makamu.
CDM ni taasisi kubwa, hatuhitaji kufuata na kuiga kila kitu kutoka CCM. Democrasia ndani ya Chama itawale na ndiyo njia sahihi itakayotupa viongozi wazuri. Tatizo hapa watu wanatumia umaarufu wa mtu kumpa uongozi badala ya record za mtu kiuongozi, kimaadili, kiutendaji nk. Kwa hali ya kisiasa ilivyo saizi nchini, CDM wakicheza vibaya na moto wa nani awe mwenyekiti wa chama, basi watanzania tutaendelea kupigishwa kwata hadi kizazi kijacho. Hatutaweza kuwang'oa hawa magamba. Napendekeza njia mbali mbali ziandaliwe za kumpata mwenyekiti zikiwashirikisha wanachama wote kuanzia stage 1 hadi mwisho. Na baadae intelligency unit ya chama ifanye kazi yake.
 
Good analysis man..but ishu ni ukomavu wa siasa,siasa za bongo kwa hakika zinahitaji maamuzi magumu wakati mwingine nje ya majadiliano..uoga wangu ni kuwa Kaka Mnyika hataweza chukua maamuzi mengine magumu kama ya Kamanda Mbowe? Ambayo kimsingi hayakwepeki kwa siasa za sasa za bongo......
 
Mbona mnaanza mapema, mda ukifika mtafanya kampeni zenu, kwani uchaguzi unafanyika lini huko? waacheni kwanza CHADEMA watueleze namna ya kwenda na hili suala la mchakato wa mswada mnaanza siasa zenu humu wakati kuna jambo la mhimu mbele ya safari, kwasasa M/kiti ni Mbowe na binafsi namkubali hadi hapa alipokifikisha chama, kuendesha chama si lelema kama mnavyodhani, kwenye siasa si kama University unapokuwa Lecturer kuna mambo mengi tofauti na mnavyodhani. Mnyika ni mzuri na je ili akitumikie chama vema lazima awe M/kiti, basi mi napendekeza M/kiti awe Lema ni bonge la mpiganaji, kwani siasa za Tz kwa sasa zinahitaji watu wa kujitoa mhanga na Lema anaweza hiyo
 
Mnyika apewe kazi za Kiutendaji. Hata hivyo bado anahitaji kujifunza zaidi siasa za Kitanzania
 
Ni mawazo potofu sana kujadili haya Uenyekiti/ ukatibu na uTendaji wa mtu. Jambo la msingi ni "patriotism" aliyo nayo mtu ktk utedaji wa kazi aliyopewa kwa wakati huo ndivyo vyenye tija kwa wa-Tz. Wakati ukifika
 
Back
Top Bottom