kumekuwepo na chapisho ambalo linasambazwa kwenye mitandao ya kijamii likimunukuu John mnyika kutoa kauli inayosema kuwa tusipo muangukia mbowe wanachadema hatutoboi
Baada ya kufanya ufuatiliaji wa kina kwa kutumia njia ya utafutaji wa maneno tumebaini kuwa taarifa hiyo nipotoshi na ina nia ya kupotosha umma
ufuatiliaji unabaibnisha kuwa kauli hiyo haijatolewa na john mnyika kwani kwa siku za hivi karibuni hajazungumza na vyombo vya habari
kando na hilo ukurasa rasmi wa chnazo tv siku ya tarehe 20 haujachapisha habari hiyo sehemuyoyote ikiwa ni facebook , instagram na x zamani twiiter
sambamba na hilo ufuatiliaji umeonesha kuwa kupitia mitandao ya kijamii wa john mnyika haujachapisha maudhui yanayomuhusu aliyekuwa mwenyekiti wa chadema taifa freeman mbowe

- Tunachokijua
- John Mnyika ni katibu mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Tanzania (CHADEMA), Aliyeteuliwa kuendelea kutumikia nafasi hiyo mara baada ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho January, 2025 ambapo Tundu Lissu aliibuka kidedea akimshinda aliyekuwa mshindani wake Freeman Mbowe.
Madai
Kumekuwapo na Taarifa inayosambazwa mtandaoni kwa kutumia grafiki zenye utambulisho wa The Chanzo kuwa John Mnyika amesema "Tusipomuangukia Mbowe wanachadema hatutoboi"
Je, ni kweli kauli hiyo imetolewa na John Mnyika?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa inayomnukuu Mnyika kuhusu kauli hiyo.
Aidha, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa CHADEMA, Brenda Rupia akizungumza Uhalisia wa taarifa hiyo amesema Si ya Kweli, huku Mnyika akibainisha kuwa ni ya kutengenezwa kwani hajatoa kauli hiyo.
Sanjari na hilo Februari 20, 2026 kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya The Chanzo haijachapisha taarifa hiyo bali wapotoshaji wametumia utambulisho huo kusambaza taarifa isiyo ya kweli.
Kadhalika fonti iliyotumika katika grafiki hiyo inatofautiana na ile inayotumiwa na The Chanzo jambo linaloashiria kuwa ni taarifa ya Kughushi.