Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Wakili Stadi, Mtoto wa Rais na mjukuu wa mpigania Uhuru anayewania kurithi kiti cha Tundu Lissu kwenye nafasi ya Urais wa Tanganyika Law Society.
Kama alivyo mtangulizi wake (Lissu), Fatma ni Mwanasheria anayeumizwa na uvunjifu wa katiba, uonevu na ukandamizaji wa haki za kiraia, hivyo daima amekuwa mstari wa mbele kutetea haki hizo Mahakamani na kusema kweli yeye ndiye Wakili kinara Mwanamke kwenye harakati za usawa wa kisheria; hivyo basi ni haki kusema Fatma ni kielelezo cha uwezo wa wanawake!
Ni mama ambaye akina baba wote tunapaswa kujivunia kwa kuzingatia ujasiri wake uliojaa tumaini.
Mitihani mingi iliyomtokea Fatma imewahi pia mtokea Mwanamke mwingine wa ki-Islam na binti wa kiongozi wa zamani (Kama alivyo Fatma) Benazir Buttho:
-Wote wawili, Baba zao wamekuwa viongozi wa juu kabisa katika nchi huru.
-Baba yake Benazir kama ilivyo kwa Babu yake Fatma aliuwawa kwa sababu za kisiasa.
-Wote wawili, ofisi zao zimewahi kulipuliwa na bomu.
-Wote wawili ni wapigania haki za raia kupitia majukwaa tofauti.
Na kwa mtiririko huo, kwakuwa Benazir amekuwa Waziri Mkuu nchini Pakistan, Fatma atakuwa Rais wa TLS, na pengine Rais wa nafasi nyingine kubwa zaidi inshā'allāh.
Kwa historia yake (lakini si kwa makuzi yake) Fatma angeweza jiungab na waminya haki na demokrasia, angekaa kimya na kufaidika na namna mambo yalivyo. Jina la Babu yake linaimbwa kwenye nyimbo za Taifa, sura ya Babu yake ipo kama picha kwenye vipande vya pesa halali za Tanzania; Hata hivyo hivi vyote havitoshi kumfanya Fatma kukaa kimya na kuridhika, anataka kuona Mahakama zinaheshimiwa, Sheria zinafuatwa, Katiba inalindwa na haki za raia hazitoweshwi na viongozi wasiojua miiko ya kisheria ya ukubwa wa mamlaka zao.
Mbadilishano wa madaraka kutoka Tundu Lissu kwenda Fatma Karume ndio zawadi kubwa ambayo wajumbe wa TLS wanaweza kujipa wenyewe na wananchi (wateja wao) wakafaidika nayo na kuifurahia.
Mimi namchagua Fatma.
John Mallya, Esquire
Wakili.