John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Ni haki yake kutangaza nia mbona hata mimi nategemea kutangaza muda wowote? Tunayemjua ni Lowassa tuu. Hakuna wa kumkuta Lowassa kabisaaa.
 
Hapo ndio itakuwa kama enzi za kiongozi anayemaliza muda wake sasa kwani hata yeye mwenyewe hakuwa anakubalika kabisaa. Mtamwona lowassa atakavyopaa kama sunami.
 
Umeona mkuu Butola. Mm pia nina mtazamo chanya kuhusu huyu mheshimiwa.
 
CCM wanatafuta mtu mwenye unafuu,huyu ana unafuu ingawaje tukianza kuorodhesha shutuma zake hazitofautian na za wenzake,ingawaje yeye ni mzee wa kula na kupuliza staili ya panya.
 
Kwa kukusaidia tu, kama ulikua una suggest afanye research kujua performance ya magufuli au jinsi anavyokubalika, inaonyesha jinsi gani hauna hata rudimentary knowledge ya research. Yani unataka kupima performance ya a political leader like a minister sample yako unayo suggest ni wafanyakazi wa wizara na makandarasi? kama ndio ningekua supervisor hata kukusimamia ningekataa, ningekurudisha kwa coordinator ukapangiwe mtu wingine, from your sample tu naona jinsi uwezo wako ulivyo mdogo, a population specification error, that's your mistake! kama unataka kawaulize wananchi, the public, na sample yako iwe stratified random sampling hapo ndio utapata picha, wananchi wa mikoa yote ya tanzania wawe kwenye sample yako. uone kama uyo fisadi wako Lowassa anakubalika au anakubalika kwenye vyombo vya habari tu na wafanya research uchwara wasaka tonge. Wewe kama hamgobali ni vizuri ila kila pembe ya nchi hii jamaa anakubalika na wala hapiti makanisani n misikitina na bahasha.

Naona pia thinking yako ni rudimental na imetawalia na emotions kuliko hali halisi!
 
Thubutu! kama ccm wanataka kufa kabisa wampitishe mafunguo Hafai hafai hafai na nasisitiza tena kuwa huyo mafunguo hafai.

Kweli!!!
Upinzani hauwezi ku-endorse chagua la CCM ambalo litawaletea tabu kwenye kampeni.
Pamoja na yote wananchi wa kawaida wachache niliowasikia idadi kubwa wanamkubali Magufui.

Tusisahau wapig kura wengi hawasom mitandao wako mitaani na vijiweni ambako Magufuli anasemeka vizuri
 
Wewe ndo hujitambui kabisa. Magufuli hafai hata huo uwaziri. Ni msanii mzuri sana na ndio maana watu kama wewe mnamwona anafaa. Waulize wakandarasi anaofanya nao kazi. Waulize wafanyakazi wa wizara yake. HAFAI KABISA! Angalia track record yake, ni ubabe tu ndo anaujua!

kwenye nchi ya wakandarasi wababaishaji kama hawa na wafanyakazi wapiga dili kama hawa wa serikali uwaulize utendaji kazi wa mtu kama magufuli unategemea jibu gani, fikiri tena.
 
Naona pia thinking yako ni rudimental na imetawalia na emotions kuliko hali halisi!

Kuna emotion gani kwa kile nilichoandika? au cz unajua kuandika neno "emotion" basi unafikili linafaa kila sehemu, kaangalie lina maana gani kwanza ndio uje ulitumie
 
Magufuli ni jembe,CCM wakimteua huyu watapata kazi rahisi sana kwenye uchaguzi wa 2015..

Kwa uwezo wa utendaji kazi,hakuna mwanasiasa yeyote hapa nchini anayemzidi Magufuli kwenye hilo, akiteuliwa huyu kura yangu anayo...
Tatizo kubwa la Magufuli ni visasi, inda na papara. Hakuna atakayempa kura Wizara ya Ujenzi pengine Mfugale tu, mshikaji wake TANROADS. Vilevile itabidi CCM imsafishe sana kwa maamuzi ya papara ya meli ya samaki na nyumba za serikali.
 
SAM_2397.jpg

Magufuli: Nagombea urais Ezekiel KamwagaToleo la 393 18 Feb 2015 WAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli, amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Raia Mwema linafahamu. Gazeti hili limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kutoka ndani na nje ya nchi kwamba Mbunge huyo wa Chato tayari amewaambia rafiki zake wa karibu kuhusu hilo ingawa hataki suala hilo lisababishe "aache kuchapa kazi" ndani ya serikali na chama. Uthibitisho wa wazi kuhusu hatua hii ya Magufuli ulikuwa wakati wa msiba wa mtoto mkubwa wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Fidel, uliotokea Januari mwaka huu, ambapo waziri huyo anadaiwa kumuarifu kiongozi huyo wa chama cha Cord kuhusu suala hilo. Vyanzo vya Raia Mwema vimeeleza kwamba Raila na Magufuli ni marafiki wakubwa na ndiyo maana Mtanzania huyo aliamua kutumia nafasi hiyo kumueleza mwenzake yaliyo ya moyoni. "Utakumbuka alipofariki baba mzazi wa Magufuli, Raila alikuja msibani. Hawa ni marafiki wa muda mrefu. Sasa kule kwenye msiba mheshimiwa aliamua kumueleza mwenzake. Hili mimi nalifahamu,"

kilieleza chanzo hicho cha gazeti hili. Jina la Magufuli limekuwa likitajwatajwa kama miongoni mwa majina ya watu wanaofaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ingawa amekuwa hana spidi kwenye suala hilo kama walivyo baadhi ya wanasiasa wengine ndani ya CCM. Wiki mbili zilizopita, Raia Mwema lilibashiri kwamba Magufuli ni mmoja wa wanasiasa ambao wanaweza kupitishwa na CCM kumrithi Kikwete kutokana na sifa yake ya uadilifu na uchapakazi. Wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yaliyofanyika mjini Songea, Ruvuma, mwanzoni mwa mwezi huu, Kikwete alisema wapo viongozi wazuri ndani ya chama hicho wenye sifa lakini hawataki nafasi hiyo na wanatakiwa kushawishiwa. Kauli hiyo ilitafsiriwa na wengi kama kuwaandaa wana CCM na jina la mgombea ambaye hatajwitajwi kwa sasa; huku majina ya Augustino Ramadhani, Dk. Augustine Mahiga na Magufuli yakitajwa. Katika mazungumzo na mmoja wa wasaidizi wa Kikwete wiki mbili zilizopita, Raia Mwema liliambiwa kwamba kuna mambo makubwa matatu ambayo yamewafanya baadhi yao kudhani Kikwete alikuwa akimzungumzia Magufuli kwenye hotuba yake ya Songea. Mosi, ni ukweli kwamba katika ziara ambazo Kikwete amekuwa akifanya ndani ya nchi, Magufuli amekuwa akionekana kama waziri anayeonekana kuheshimiwa na Watanzania. "Mfano ambao Kikwete amewahi kuusema kwetu unahusu mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika Mwanza mwaka jana. Watu wa kule walikuwa wakizomea na kuonyesha alama za Chadema.

"Lakini alipopanda jukwaani Magufuli mkutano wote ulitulia. Mpaka Kikwete alipopanda jukwaani, mkutano ulikuwa umetulia. Nadhani Kikwete ameona kwamba labda huyu ndiye mwana CCM ambaye Watanzania wanamuamini," alisema. Wakati aliporejea kutoka kwenye matibabu nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana, Kikwete alitamka hadharani kwamba alitaka kutangaza mapema kuhusu ugonjwa wa kansa uliokuwa ukimsumbua, lakini ni Magufuli aliyemkataza kufanya hivyo wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri. Mwaka juzi, Magufuli pia aliwashangaza watu wakati alipopishana hadharani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu suala la magari ya mizigo kupita katika barabara yakiwa yamezidi mizigo. "Ile ilikuwa ni ishara kwamba Magufuli alikuwa akiamini nguvu iliyo juu ya Pinda. Katika hali ya kawaida, si rahisi kwa waziri wa kawaida kutofautiana na Waziri Mkuu hadharani," kilisema chanzo kingine cha gazeti hili. Msaidizi huyo wa Kikwete alilieleza pia Raia Mwema kwamba katika mojawapo ya misiba ya karibuni zaidi iliyoikumba familia ya Rais, Magufuli alikuwa waziri pekee ambaye alilala msibani kijijini Msata. "Kama walivyo wenzake, Magufuli anaonekana ni mchapa kazi na mtu ambaye hahusishwi na masuala ya ufisadi ingawa kuna wanaonong'ona kuhusu suala la uuzaji wa nyumba za serikali," Raia Mwema liliambiwa. Katika kuchagiza hilo, jarida la The Indian Ocean linalochapwa na taasisi inayoheshimika barani Afrika ya Africa Intelligence, katika toleo lake la Februari 13, 2014, limemtaja Magufuli kama kipenzi cha Kikwete na mtu ambaye anaweza kumuunga mkono. Jarida hilo ambalo hufanya uchambuzi wa masuala mbalimbali ya nchi zilizo katika mwambao wa bahari ya Hindi barani Afrika, limefanya uchambuzi kuhusu kinyang'anyiro cha kuwania urais kupitia CCM haswa baada ya kashfa ya akaunti ya Escrow. Tufuatilie

Huyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!

Unashangaza nazani wewe hauishi tanzania kama haumfahamu vizuri anatumia muda wake mwingi kuwatumikia watanzania sio kukaa kwenye mipasho kwenye media.
 
Tunasubili kama dira ya uchapa kazi,uadilifu na uongozi bora tanzania.
 
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang'anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos', muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong'ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

"Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri," alisema Dk. Magufuli.

"Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana," alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Chanzo: Nipashe

==============
UPDATE (1):

Tarehe 18, Feb 2015: Kwa mujibu wa magazeti ya leo; Magufuli katangaza nia kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano

Safi sana amefanya tumeona lakini ninawasiwasi na upofu wa ccm kutokumpitisha.
 
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Mimi in moja ya watu tunaokereketwa na kutaka kumsikia mh.Dkt magufuri akitangaza nia kwa kinywa chake mwenyewe kiukweli Dkt.mimi binafusi nakudimaya sana sio tu kwa utendaji wako uliotukuka Bali kwamamuzi magumu ulionayo ingawa wabaya wako kisiasa huwa wanapindisha na kuchafua.wewe in jembe ndani na nje CCM kiboko ya wapinzani MTU Wa watu Tanzania inakuhitaji nasubili utangaze nia Dkt.mimi na vijana wengine tunakuhitaji.
 
Makufuli rais wa Tanzania,Lowassa rais wa TanzaniTanzania,Makinda rais wa Tanzania,Kigwangwala rais wa Tanzania,Shein rais wa Tanzania,Migiro rais wa Tanzania,Makongoro rais wa Tanzania.Aliye iloga CCM Alisha kufa siyo bure.
Maguli ni jembe
 
Nitamchangia magufuli hela ya kuchukua form akitangaza kugombea Urais
 
Katika hali inayoonyesha kuwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, anautamani urais, amesema anaweza kutangaza nia hiyo kama atakidhi masharti yatakayowekwa kwenye Katiba mpya.

Alisema iwapo Katiba ijayo itakuja na sifa ambazo atakidhi vigezo kuna uwezekano mkubwa wa kuwania nafasi hiyo na kwamba iwapo atapungukiwa sifa zinazohitajika kwa mujibu wa Katiba hataingia kwenye kinyang’anyiro hicho.

Dk. Magufuli ambaye pia ni Mbunge wa Chato alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wazee wa wilaya hiyo kwenye ukumbi wa ‘Mshikamano Saccos’, muda mfupi baada ya mzee Paschal Nyambibo (87) kumsihi agombee nafasi hiyo mwaka 2015 kutokana na sifa zake za uchapakazi ndani ya serikali.

Nyambibo alisema kutokana na uwajibikaji mzuri aliouonyesha Dk. Magufuli tangu mwaka 2000 akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na katika wizara mbalimbali, Watanzania wamekuwa na imani kubwa na uwajibikaji wake na kwamba anastahili kupeperusha bendera ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ifikapo mwaka 2015.

Licha ya kauli hiyo kusababisha minong’ono mingi kwa wazee waliohudhuria kikao hicho, Dk. Magufuli alionekana kutuliza hali hiyo kwa kusema isubiriwe Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano iwapo itakuwa na masharti ambayo yatamfanya kujitathimini iwapo ana sifa za kugombea au vinginevyo.

Hata hivyo, Dk. Magufuli hakusita kuonyesha hisia zake za kukerwa na baadhi ya wananchi wanaobeza maendeleo aliyotekeleza katika jimbo lake tangu alipochaguliwa kuwa Mbunge.

Alimshutumu hadharani aliyekuwa Katibu wa CCM wilaya ya Chato kabla ya kuhamishiwa wilayani Mbogwe, Gervas Stephano, kuwa hana shukrani.

Dk. Magufuli alimwelezea katibu huyo kuwa hana fadhila kutokana na mambo mengi aliyomtendea tangu akiwa katibu wa ofisi yake ya jimbo ambapo alimsaidia kupanda ngazi na kuwa Katibu wa CCM wilaya Chato, Kwimba, Kasulu, Kilosa na kurejea tena Chato kabla ya kuhamishiwa wilaya ya Mbogwe mkoani Geita kuendelea na wadhifa huo.

“Tatizo lenu watu wa Chato hamna shukrani…mambo mengi nimefanya hapa Chato, lakini yote mnaona ziro…hata niliowasaidia kama Gervas naye sasa hivi ananiponda…lakini nawashukuru sana wazee wangu kwa kunikumbusha niliyoyafanya kwenye jimbo letu kupitia risala yenu nzuri,” alisema Dk. Magufuli.

“Kutokana na hali hiyo ninawazawadia Sh. 1,000,000 mfanye sherehe ya kujipongeza kwa kuwa natambua mmejitesa sana mpaka kufanikisha kikao hiki cha leo…na kwa kuwa hamna mradi wowote wa kuwaingizia kipato kama wazee, ninaahidi kuwapa Sh. 3,000,000 kutoka mfuko wa jimbo, ili muanzishe walau saccos ya kukopeshana,” alisema.

Baadhi ya viongozi na wananchi wamekuwa wakilitaja mara kwa mara jina la Waziri Magufuli miongoni mwa watu wanaodhaniwa kutaka kugombea nafasi ya urais wa Tanzania mwaka 2015, ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha uvumi huo.

Mbali na Dk. Magufuli, wengine ndani ya CCM wanaotajwa ni pamoja na aliyekuwa Waziri Mkuu ambaye pia ni Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa; Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ambaye anajiita mtaji wa urais; Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe; Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Ushirikiano wa Kimataifa –CCM, Dk. Asha-Rose Migiro na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano na Mambo ya Nje, Bernard Membe, ambaye alipata kusema anasubiri kuiteshwa na Mungu kuwania nafasi hiyo.
Chanzo: Nipashe

==============
UPDATE (1):

Tarehe 18, Feb 2015: Kwa mujibu wa magazeti ya leo; Magufuli katangaza nia kutaka kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano

Huyu anafaa kua rais 2015
 
Back
Top Bottom