John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Waziri wa Ujenzi mh. John Pombe Magufuli ametangaza kugombea uraisi 2015.

Chanzo; Gazeti la Uhuru.
Naona na Raia Mwema pia wameandika habari hiyo.
sasa kumekucha kwa hakika. Kuingia kwa Magufuli kutabadili kabisa muelekeo wa mbio hizo ndani ya CCM.
Bado naamini kwamba CCM wataamua kumsimamisha Magufuli ili awaokoe kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
 
Lowassa kwanza
 
huyo ndio JK alisema ataombwa kugombea?/
 
Magufuli siyo tu hana nguvu ndani ya Chama , bali pia Hana sifa za kuwa Rais. Rais lazima awe mtu mwenye uwezo aw kujenga Hoja , siyo wa kukariri kilometer au idadadi ya Samaritan haharini. Anatakiwa mtu mwenye uadilifu usiotiliwa shaka. Magufuli si madilifu, licha ya kupiga makelele, ni mpokeaji mkubwa we rushwa kutoka kwa makandarasi. Vile vitisho anayo toa kwa makandarasi ndiyo mbinu yake ya kujizolea milungula kutoka Kwao. Ni mtu asiyesikiliza ushauri wowote kutoka kwa watalaamu wake, kwa vile anadhani anajua kila kitu. Ndiyo maana Aliza nyumba zote za serikali mpaka za hospitali na Vito vya polisi na kuuza nyumba za serikali kwa hawala na nudge zake walikuwa watumishi aw serikali. Mbali na hayo wizard yake inashindwa kueleza ziliko shs 260 bn zilizotengwa kulipa madeni ya makandarasi ambayo haya kulipwa na fedha hazijulikani zilipo. Kama hayo yote anayafanya akiwa waziri je akiwa itakuwaje. Hafar Hafai Hafai.

Uaandika hypothetically..pole sana kwa kubeba hoja usizozijua. Unaandika pumba tu, hauna data zozote to substantiate your claims. izo stori za vijiweni usizilete humu.
 
By mavumbi Hana haiba, uwezo, msimamo, ujasiri, wala IQ ya kutosha

1. Haiba: Mvuto, bashasha
2. Uwezo: Uthabiti, Ufanisi
3. Ujasiri: Uthubutu, Bila woga
4. I.Q. : Uwezo wa kutambua / kuchambua mambo

Mifano Hai:

Samahani nitumie lugha yetu na ya kigeni:
1. Lacks fluency and application of proper speech iwe Swahili au Kiingereza (yawezekana ni suala la kabila)
2. Wizara anayoiongoza imejaa ufisadi na rushwa ya ajabu (uliza wanaoendesha magari makubwa wakifika vituo vya weigh-bridges)lakini anachofanya ni kukimbizana na miradi ya barabara .
3. Alitumwa na nanin kwenda Kenya kutoa salamu kwenye campaign ya Raila Odinga? Huyu ametuweka mahali pagumu sana na Wakenya ...Kama angekuwa jasiri angemwambia aliyemtuma kule kwamba hakikuwa kitendo muafaka. Haya ..yako wapi?
4. Ameuza nyumba za serikali halafu serikali hiyo hiyo inaingia gharama ya mamailioni ya shilingi kuwaweka watumishi waandamizi nkwenye mahoteli... tena ya kifahari? Hiyo sio questionable IQ?

SEMA... NIONGEZE NYINGINE?

Mkuu inaonekana una hofu sana na huyu jamaa. najua Lowassa anaewatuma hataki kumsikia huyu jamaa au hao CDM cz hamtapata kura, inawatia watu hofu kuu cz wanajua tsunami ya JP Magufuli, omba sana asipitishwe ila akipitishwa hata lowassa ahame na nusu ys wanachama atashinda tu.
 
Aliyebaki Ccm hajatangaza nia ni Asumpta sasa. Yaani viongozi wa Ccm wameashaona Urais mi sawa na kuwa mwenyekiti wa mtaa.
 
Nyumba zetu kwanza mengine baadaye. Kama uliuza nyumba ukiwa Waziri si utauza baadhi ya Mikoa ukiwa Rais.
Hatudanganyiki, hatukubali
 
kupokelema ostabey na mabango ndio kilichomsisimua? Mbona mwigulu alipokelewa na mabango. Lowasa kwanza magufuli baadae.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.Yule mwanasiasa mwandamizi ndani ya Ccm na serikali za awamu ya tatu na nne Mhandisi John Pombe Magufuli aichanganya kambi ya Lowassa akili baada ya kuamua kujitosa kugombea urais wa Tanzania 2015.Kabla ya kujitangaza alikuwa akitajwa kuwa atagombea ila jamii ilikuwa haina uhakika.Ni dhahiri sasa jamii imepata uhakika na kundi la Lowassa ambalo lilikuwa likijitapa kuwa litazigawa kura za kanda ya ziwa limekutwa na hali ya sintofahamu.

Ni vilio na simanzi katika viunga vya maeneo ya kujidai ya wanamtandao wa Lowassa kwasababu tangu awali katika watu waliokuwa wanawahofia ni pamoja na Magufuli.Mmoja wa vijana watiifu wa Lowassa alinukuliwa na chanzo kimoja cha habari kuwa hatua ya Magufuli kutangaza nia sasa hivi ni sawa na shambulio la kivita la kushtukiza.Alisema,"Sikia ndugu yangu hivi sasa mzee kachanganyikiwa,haamini kwasababu hakudhani kama Magufuli atagombea urais.Ni dhahiri sasa sherehe yetu ya kutangaza nia pale viwanja vya Sheikh Abeid imeingia doa".

Kutokana na hatua ya Magufuli kutangaza nia kumeamuliwa vikao vya dharura kuanza kufanyika maeneo ya Mbezi Beach,Regency Hotel,Sinza Madukani na Rose Garden.Wahusika wa vikao hivyo ni pamoja na Lawrence Masha,Daniel Nsanzugwako na mmoja wa wenyeviti wa Ccm kutoka mkoa wa Kanda ya Ziwa mwenye tabia ya kupenda kuvaa kofia aina ya kibalagashea.Hakika hii ni sudden attack.Tutajionea mengi sana.
 
Ni jambo la kushangaza sana kuona Magufuli anajinadi kugombea uraisi kwa kudai kuwa amejenga mtandao wa barabara nyingi hapa Tanzania.Nadiriki kusema wazi wazi kuwa barabara nyingi zinazojengwa nchini ziko chini ya kiwango cha kimataifa, mfano mzuri ni barabara mwenge-tegeta iliyofunguliwa karibuni,iko kwenye kiwango duni na baada ya mwaka mmoja tu kila anayeitumia barabara ile atakuwa shahidi.kuna barabara ya msata ambayo imejengwa hivi karibuni iko hoi.Nafikiri Magufuri angemaliza muda wake vizuri na kustaafu ili awaachie vijana wenye maono ya kimaendeleo kwa kasi wachukue nafasi.Tunahitaji kukimbia kwani tuko nyuma sana.
 
No Maghufuli katangaza kweli au zile zile za kumtangazia bila yeye kujua? Kama ni kweli mwambieni fisadi lowassa apumzike.
 
Ukweli ni mchungu ni kwamba kanda ya ziwa siku zote ndio uamua rais wa Tanzania anakuwa nani.
 
Lowassa anajisumbua sana, historia inaonesha hakuna mtu aliyetumia nguvu nyingi nchi hii kuusaka urais akaupata.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa.Yule mwanasiasa mwandamizi ndani ya Ccm na serikali za awamu ya tatu na nne Mhandisi John Pombe Magufuli aichanganya kambi ya Lowassa akili baada ya kuamua kujitosa kugombea urais wa Tanzania 2015.Kabla ya kujitangaza alikuwa akitajwa kuwa atagombea ila jamii ilikuwa haina uhakika.Ni dhahiri sasa jamii imepata uhakika na kundi la Lowassa ambalo lilikuwa likijitapa kuwa litazigawa kura za kanda ya ziwa limekutwa na hali ya sintofahamu.

Ni vilio na simanzi katika viunga vya maeneo ya kujidai ya wanamtandao wa Lowassa kwasababu tangu awali katika watu waliokuwa wanawahofia ni pamoja na Magufuli.Mmoja wa vijana watiifu wa Lowassa alinukuliwa na chanzo kimoja cha habari kuwa hatua ya Magufuli kutangaza nia sasa hivi ni sawa na shambulio la kivita la kushtukiza.Alisema,"Sikia ndugu yangu hivi sasa mzee kachanganyikiwa,haamini kwasababu hakudhani kama Magufuli atagombea urais.Ni dhahiri sasa sherehe yetu ya kutangaza nia pale viwanja vya Sheikh Abeid imeingia doa".

Kutokana na hatua ya Magufuli kutangaza nia kumeamuliwa vikao vya dharura kuanza kufanyika maeneo ya Mbezi Beach,Regency Hotel,Sinza Madukani na Rose Garden.Wahusika wa vikao hivyo ni pamoja na Lawrence Masha,Daniel Nsanzugwako na mmoja wa wenyeviti wa Ccm kutoka mkoa wa Kanda ya Ziwa mwenye tabia ya kupenda kuvaa kofia aina ya kibalagashea.Hakika hii ni sudden attack.Tutajionea mengi sana.

Hivi huu uzushi wenu unawasaidia nn ktk harakati zenu za kwenda ikulu?
 
Waziri wa ujenzi John Magufuli amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania urais kupitia chama cha mapinduzi
Kwa kwa mujibi wa marafiki wa magufuli wamesema tayari ameweka nia ya kugombea urais

Chanzo raia mwema
 
Back
Top Bottom