John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Hatimaye: Magufuli uyooooo urais 2015 hana mpinzani. Kambi Lowasa mlie tuu imekula kwenu pamoja na kuanza kampeni chafu za kumchafua haitosaidia kitu.

My take: Watanzania tumuunge mkono Magufuli ni mzalendo na mchapa kazi si mfujaji wa fedha za umma na mwenye mtazamo wa mbali anayeweza kupambana na umaskini wa watanzania na kuwatatulia kero nyingi ikiwemo Elimu, Maji, Afya, Umeme, Ajira na kuongeza kipato kwa kila kaya.
 
Huyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!

Urais hausomewi .Uraisi ni kuuza na kutekeleza sera zako kwa wananchi.
 
Haaahaaaaa janabaaaaaaaa naongezea hapo ni nahisi hata akifa mzoga wake usiguseee nahisi haitakutoka mwaka mzima
 
Magufuli ni fisadi hafahi kuwa rais akiwa waziri wa nyumba na makazi wakati wa serikali ya awamu ya nne aliweza kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa leo hii tunaona viongozi wana yoangaika mpaka serikali inaingia gharama kuwapangishia nyumba aliuza nyumba zote zilizo kwenye maeneo ya Oysterbay,Masakia,Mikocheni,Upanga n.k sasa kama aliweza kufanya hivyo akiwa waziri tukimpa ursis si atauza kila kitu mpaka mbuga za wanyama mwisho wa siku tutakuwa watumwa ndani ya nchi yetu.Kingine huyu bwana Magufuli hana hekima wala busara hufanya maamuzi kwa kukurupuka na kuigharimu serikali kulipa fidia kwa waathirika mfano mara kwa mara tumeshuhudia akivunja majengo ya watu wakati wa utanuzi na ujenzi wa barabara bila kufuata sheria matokeo yake serikali huingia gharama kulipa fidia na mfano mwingine tumeona alivyokamata meli ya samaki bila kuwa makini leo tumeshindwa kesi na kuamliwa serikali iwalipe wamiliki wa meli sh.bilioni 2 .Kwa hali hiyo Magufuli hafahi kuwa raisi uraisi unahitaji maamuzi ya hekima na busara katika kuamua mambo lakini tukimpata kiongozi wa maamuzi ya kukurupuka kama Magufuli nchi inaweza ingia kwenye migogoro na wawekezaji na majirani zetu tukajikuta tunaingia kwenye vita na kurudi nyuma kimaendeleo.
Umesahau na kesi ya samaki wa ''magufuli'' sasa hivi serikali inatakiwa kulipa fidia mabilioni.
 
WAZIRI wa Ujenzi, John Magufuli, amejitosa katika kinyang'anyiro cha kuwania Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Raia Mwema linafahamu.

Gazeti hili limeambiwa na vyanzo vyake vya kuaminika kutoka ndani na nje ya nchi kwamba Mbunge huyo wa Chato tayari amewaambia rafiki zake wa karibu kuhusu hilo ingawa hataki suala hilo lisababishe "aache kuchapa kazi" ndani ya serikali na chama.


Uthibitisho wa wazi kuhusu hatua hii ya Magufuli ulikuwa wakati wa msiba wa mtoto mkubwa wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, Fidel, uliotokea Januari mwaka huu, ambapo waziri huyo anadaiwa kumuarifu kiongozi huyo wa chama cha Cord kuhusu suala hilo.


Vyanzo vya Raia Mwema vimeeleza kwamba Raila na Magufuli ni marafiki wakubwa na ndiyo maana Mtanzania huyo aliamua kutumia nafasi hiyo kumueleza mwenzake yaliyo ya moyoni.
"Utakumbuka alipofariki baba mzazi wa Magufuli, Raila alikuja msibani. Hawa ni marafiki wa muda mrefu. Sasa kule kwenye msiba mheshimiwa aliamua kumueleza mwenzake. Hili mimi nalifahamu," kilieleza chanzo hicho cha gazeti hili.


Jina la Magufuli limekuwa likitajwatajwa kama miongoni mwa majina ya watu wanaofaa kumrithi Rais Jakaya Kikwete baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ingawa amekuwa hana spidi kwenye suala hilo kama walivyo baadhi ya wanasiasa wengine ndani ya CCM.


Wiki mbili zilizopita, Raia Mwema lilibashiri kwamba Magufuli ni mmoja wa wanasiasa ambao wanaweza kupitishwa na CCM kumrithi Kikwete kutokana na sifa yake ya uadilifu na uchapakazi.

Wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 38 ya CCM yaliyofanyika mjini Songea, Ruvuma, mwanzoni mwa mwezi huu, Kikwete alisema wapo viongozi wazuri ndani ya chama hicho wenye sifa lakini hawataki nafasi hiyo na wanatakiwa kushawishiwa.


Kauli hiyo ilitafsiriwa na wengi kama kuwaandaa wana CCM na jina la mgombea ambaye hatajwitajwi kwa sasa; huku majina ya Augustino Ramadhani, Dk. Augustine Mahiga na Magufuli yakitajwa.

Katika mazungumzo na mmoja wa wasaidizi wa Kikwete wiki mbili zilizopita, Raia Mwema liliambiwa kwamba kuna mambo makubwa matatu ambayo yamewafanya baadhi yao kudhani Kikwete alikuwa akimzungumzia Magufuli kwenye hotuba yake ya Songea.


Mosi, ni ukweli kwamba katika ziara ambazo Kikwete amekuwa akifanya ndani ya nchi, Magufuli amekuwa akionekana kama waziri anayeonekana kuheshimiwa na Watanzania.

"Mfano ambao Kikwete amewahi kuusema kwetu unahusu mkutano mmoja wa hadhara uliofanyika Mwanza
mwaka jana. Watu wa kule walikuwa wakizomea na kuonyesha alama za Chadema.

"Lakini alipopanda jukwaani Magufuli mkutano wote ulitulia. Mpaka Kikwete alipopanda jukwaani, mkutano ulikuwa umetulia. Nadhani Kikwete ameona kwamba labda huyu ndiye mwana CCM ambaye Watanzania wanamuamini," alisema.

Wakati aliporejea kutoka kwenye matibabu nchini Marekani mwishoni mwa mwaka jana, Kikwete alitamka hadharani kwamba alitaka kutangaza mapema kuhusu ugonjwa wa kansa uliokuwa ukimsumbua, lakini ni Magufuli aliyemkataza kufanya hivyo wakati wa kikao cha Baraza la Mawaziri.


Mwaka juzi, Magufuli pia aliwashangaza watu wakati alipopishana hadharani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuhusu suala la magari ya mizigo kupita katika barabara yakiwa yamezidi mizigo.

"Ile ilikuwa ni ishara kwamba Magufuli alikuwa akiamini nguvu iliyo juu ya Pinda. Katika hali ya kawaida, si rahisi kwa waziri wa kawaida kutofautiana na Waziri Mkuu hadharani," kilisema chanzo kingine cha gazeti hili.

Msaidizi huyo wa Kikwete alilieleza pia Raia Mwema kwamba katika mojawapo ya misiba ya karibuni zaidi
iliyoikumba familia ya Rais, Magufuli alikuwa waziri pekee ambaye alilala msibani kijijini Msata.

"Kama walivyo wenzake, Magufuli anaonekana ni mchapa kazi na mtu ambaye hahusishwi na masuala ya ufisadi ingawa kuna wanaonong'ona kuhusu suala la uuzaji wa nyumba za serikali," Raia Mwema liliambiwa.
Katika kuchagiza hilo, jarida la The Indian Ocean linalochapwa na taasisi inayoheshimika barani Afrika ya Africa Intelligence, katika toleo lake la Februari 13, 2014, limemtaja Magufuli kama kipenzi cha Kikwete na mtu ambaye anaweza kumuunga mkono.


Jarida hilo ambalo hufanya uchambuzi wa masuala mbalimbali ya nchi zilizo katika mwambao wa bahari ya Hindi barani Afrika, limefanya uchambuzi kuhusu kinyang'anyiro cha kuwania urais kupitia CCM haswa baada ya kashfa ya akaunti ya Escrow.

Wiki ijayo, tutachapa ripoti kamili ya jarida hilo kwenye gazeti hili

Chanzo:
Raia Mwema
 
Mbona unaleta habari za mwaka 47 hii habari tushaisoma sana hapa jukwaani.
 
Msindikizaji tu. Enzi zake zimeshapita kitambo. Hajitambui mtu huyu.
 
mgawa nyumba za serikali.. mkuza deni la taifa kwa miradi ya barabara zilizo chini ya kiwango...mnajua hasara aliyoisababishia serikali so far?

Msindikizaji tu. Enzi zake zimeshapita kitambo. Hajitambui mtu huyu.

Mbona unaleta habari za mwaka 47 hii habari tushaisoma sana hapa jukwaani.

Team Lowassa hiyo....naona "kiwewe" kimewaingia... Muelezeni boss wenu awaongezee dau maana ni ngumu sana kuchomoa hiko kisiki cha mpingo!!
 
Hatuwezi kuweka rais mgonjwa tena..tumechoka ..magufuli aende akawe rais wa mkewe lakini sio kwa watanzania
 
Magufuli ni kabila lipi na lina siha katika uongozi ?
Na kama anatoka moja ya kabila kubwa nchini,ni hatari kwa taifa !
 
Naomba,timu ya Magufuli mniondolee hofu kwamba hawezi kuwa kiongozi mkuu bali mwongozwaji kwa kipawa chake katika kaya !
 
Ni kijana mchapakazi. Hodari.ana msimamo. Ana maamuzi.anachukia rushwa na ufisadi. Magufuli kwa tanzania yenye neema.
 
Duh, ila mnahangaika wakina ifweero. Mwisho mtasema twende Vuai. Mimi nadhani wewe ndio uende nae.
 
Mimi Nitakwenda na Chadema, sitaki kuidanganya nafsi yangu hata kidogo,
 
Back
Top Bottom