John kitime amvaa Mheshimiwa Sugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John kitime amvaa Mheshimiwa Sugu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by KIM KARDASH, Dec 28, 2011.

 1. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hebu pata vionjo vya MR2.....enzi hizoooooo
  Mwaka 1995, nikiwa najaribu kusambaza kazi za wanamuziki wa Tanzania kupitia kajimradi kadogo, mwanamuziki Innocent Nganyagwa alinijia na kunihadithia kuhusu mwanamuziki mpya wa Rap ambaye alikuwa tofauti na wasanii wenzie, kimawazo na hata jinsi ya sanaa yake ilivyo, na ndipo nikakutana na kusikia kazi ya MR2.

  Muziki wake ulinifurahisha kwa sababu mbili ya kwanza alikuwa akitumia Kiswahili kilichoeleweka tofauti na wasanii wengi wa Rap wa wakati huo ambao walighani Kiswahili utadhani wameshuka leo toka Marikani, pili alikuwa na ujumbe mzito, ambao hata leo miaka zaidi ya 15 toka ulipotolewa bado una maana kwa jamii ya Tanzania. Sishangai kuwa yeye sasa ni Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi.

  Lazima nijisifu kuwa sikukosea kuanza kusambaza kazi yake ya kwanza album ya NI MIMI. Angalia video hii kwa makini utakuta mengi aliyosema atatimiza alitimiza.


  http://www.youtube.com/watch?v=2X9MREzjT5s

   
 2. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Hayo ni maoni yake na ana haki ya kuona hivyo. lakini kuna wengi wanaoona kuwa Sugu hakustahili kuwa hapo alipo. Isipokuwa alitakiwa kuwa na mafanikio zaidi kwenye muziki. Huko kuna mfaa na yeye ni expert wa huko.
   
 3. Sr. Magdalena

  Sr. Magdalena JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 770
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 45
  The ROM, badilisha hiyo subject kaka, inashtua kidogo kumbe jamaa anampa shavu Norton - Anti Virus
   
 4. Nyamburi

  Nyamburi JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  sijakuelewa mkuu,wanaoona kua hukustaili kuwa hapo kivipi?
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Mkuuu mbona ajamvaa kama tittle inavyoonyesha? Mbona kampa shavu au ni hit stunt?
   
 6. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #6
  Dec 28, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  umenitisha kweli mkuu,nikaanza kuwaza kunani tena mzee wetu tunaemheshimu

  nadhani tungekuelewa tu hata pasipo kuweka kichwa cha habari kilicho tofauti na mada yako

  kiukweli Sugu tangu kitambo sana alikuwa ni mpigania haki hata ukisikiliza ile nyimbo yake(ana miaka chini ya 18) utaona jinsi alivyofikisha ujumbe kwa njia ya muziki na kupinga vitendo viovu wanavyofanyiwa wanawake wa umri ule

  Hongera SUGU
  mambo mengine ni mchakato wa maisha,ipo siku tu watakubari(wanachotaka wewe upate tabu raha kidogo maneno kibaoooo)
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  ndio zake:alien:
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Kichwa cha habari na habari yenye tofauti kabisa.
   
 9. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  yaani huyu lazima atakuwa ni mwandishi wa global publisher aisee..
   
 10. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani kuna kitu sijakielewa? hiyo headline na habari zenyewe mbona ni tofauti sana? au The Romantic ni mwandishi wa magazeti ya udaku?
   
 11. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  i did that purposely cuz subject niliyoiweka "inauza" si unajua humu chadema wengi ..ukiiweka hivyo ndio itapata wasomaji wengi maana wataingia kwa jazba kwa lengo la kuja kumdefend mtu wao sasa kabla ya kufanya hivyo itabidi wasome kwanza,it was just a strategy usijali mwisho wa siku ujumbe umefika!
   
 12. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mzee umekuja tena eeeh.....karibu sana
   
 13. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,087
  Likes Received: 6,554
  Trophy Points: 280
  kijana katoka mbali sana,
  toka enzi hizo mzee wake yuko hai (R.I.P)
  kabaki na familia, kahangaika na wadogo zake,
  kaendelea kumtunza mama yake,
  hata leo ni mheshimiwa,
  kweli maisha yataka uvumilivu wa hali ya juu sana.
   
 14. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 878
  Trophy Points: 280
  Habari nzuri amei-title kiudaku!!
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Kwani Hatman(brother ake)alikua alikua wapi..maana yeye sio first born wa mzee mbilinyi
   
 16. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #16
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Ukikata tamaa hapa duniani ujue ndo umekufa ukiwa hai. Sugu amepambana sana. Nadhani pacha wake ni Prof. Jay
  Hawa ni mabalozi wa kweli muziki wa kizazi kipya hapa TZ
   
 17. K

  Kolero JF-Expert Member

  #17
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2010
  Messages: 493
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ni mbinu ya kutufanya wengi tukimbilie kuisoma, asingefanya hivyo wengine wangepita tu!:poa
   
 18. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #18
  Dec 29, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kweli kiswahili kigumu!!!
   
 19. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kiswahili rahisi tu ni kama kioo ukicheka nacho kinacheka ukinuna hali kadhalika...
   
 20. M

  Madenge Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hartman ni brother wake kwa mama mwingine..jipatie kopi ya kitabu cha historia yake ya maisha.
   
Loading...