John Kaduma!

John Kaduma!

Namkumbuka George Mwakingili. Kama sijakosea alikuwa akimtumia mpelelezi aliyeitwa Jim Mtemvu ilikuwa ni kama Joram Kiango alivyotumiwa na Ben R. Mtobwa au Willy Gamba wa Elvis Musiba.

Gazeti la Motomoto pia nalikumbuka. Jina "Motomoto" lilikuwa na maandishi mekundu kama lilivyokuwa gazeti la Shaba.
Sawa sawa kabisa na ndani yake ilipatikana makala ya stanslaus katabalo ikihusu loliondo.akiita loliondo-gate.wapo wengi tu kuna emmanuely kibiki yo man.
 
Sawa sawa kabisa na ndani yake ilipatikana makala ya stanslaus katabalo ikihusu loliondo.akiita loliondo-gate.wapo wengi tu kuna emmanuely kibiki yo man.

Stan Katabalo namfananisha na Saed Kubenea. Naona aligombana na "wakubwa." Emmanuel Kibiki nilikuwa naona stori zake katika Jarida la Tabasamu pamoja na Bakari Masasi (Ras).
 
hivi hadithi ya panga la shaba alichora nani? marco tibasima wapi b.mkora, mmenikumbusha mbali sana

Panga la Shaba alichora John M. Kaduma. Bado naitafuta stori hiyo...

Marco Tibasima yupo... anapatikana hapa. Bi Mkora nina muda sijaiona... alikuwa anachora Robert Mwampembwa.
 
Mtuhumiwa kwangu mimi ni riwaya ya pili kwa ukali kutoka kwa Tuwa ikitanguliwa na Mkimbizi.
Nilicheki na Tuwa na kumueleza juu ya kuiweka Mtuhumiwa katika kitabu,kipindi hicho ndio alikua anaandaa riwaya yake ya UTATA lakini aliahidi ataifanyia kazi ishu.
Msachi tu kwenye facebook,chapa Husein Tuwa na mambo yataenda...you know wha i'm sayin'!!!?
Mkuu asante kwa taarifa!
 
Umenikumbusha anga za wenyewe mkuu, hiyo nadhani alikuwa anachora fortunatus ndila.
Niliwahi kusikia ndila alifungwa kipindi fulani baada ya kushirikiana na mtoto wa kigogo flani wakamuibia huyo kigogo pesa ili waende marekani lakini baada ya kufanikiwa kuiba hiyo ela ndila akaamua baki hapa hapa tz, mwenzake akaondoka. Sijadhibitisha lakini nilisikia hiyo kitu.

Nadhani huyu ndo mchoraji wa ile hadithi ya "anga za wenyewe", mtanisaidia mnaokumbuka vizuri.
 
Mkuu elmagnifico hiyo skendo ya Ndilla sikuwahi kuipata, ngoja waje wadau wenye taarifa kamili watatusaidia.
 
Last edited by a moderator:
Kazi nyingine ninazozikumbuka za huyu gwiji john m kaduma ni ile ya MZUNGU WA UNGA (pablo zungu) ilikuwa inazungumzia masuala ya madawa ya kulevya katika jarida la KIU,
hata hivyo jarida hilo lilifutwa muda mfupi kwa sababu zisizojulikana.
Majarida mengine yaliyotamba enzi hizo ni pamoja na AMBHA na KINGO (james gayo wa kenya).
 
Tuwa ndiye alinifanya niache kusoma hadithi za shigongo... Hussein Tuwa ni mkali, ila pia riwaya za msiba na willy gamba zilikuwa zinasisimua kweli.
Hivi ni nani aliyeandika riwaya ya azina iliyo laaniwa?
 
Hakuna kama John Kaduma. Hata waliomtangulia akina Philip Ndunguru (Mchoraji wa mwanzo kabisa wa Sani) hawakuwa na uwezo kama wake. Never. Akina madenge wa siku hizi wabaaaaya.

BTW, nafanyia kazi namna ya kurudisha nguvu za akina madenge, lodilofa etc kwa kizazi cha sasa na cha miaka ya 80 kwa njia inayosisimua zaidi. Likely kuanzia mwaka 2016 naweza kuwa katika hatua muafaka. "Niko kambini najifua." Tuombe uzima.

Mkuu fanya hima tupate vitu vya ukweli tulivyovimiss miaka kadhaa iliyopita,
nasubiria kwa hamu sana mkuu.
 
Namkumbuka sana huyu jamaa kaniburudisha sana nikiwa primary kipindi icho tukawa tunacopy michoro yake R.i.p kaduma
 
Kazi nyingine ninazozikumbuka za huyu gwiji john m kaduma ni ile ya MZUNGU WA UNGA (pablo zungu) ilikuwa inazungumzia masuala ya madawa ya kulevya katika jarida la KIU,
hata hivyo jarida hilo lilifutwa muda mfupi kwa sababu zisizojulikana.
Majarida mengine yaliyotamba enzi hizo ni pamoja na AMBHA na KINGO (james gayo wa kenya).

daah kaka ume nikumbusha hii kitu pablo zungu aisee!! ilikua kwenye jarida la Tabasamu toleo la kwanza na hadithi ikaanza!
r.i.p john kaduma he inspired me to be a good artist especially kwenye uchoraji maskini kipaji changu hakija nifikisha popote mfumo wa elimu ya bongo shida sana inaua vipaji sana,shuleni wame nitumia sana kuchora vitu mbali mbali.
 
Enzi ZA TABASAMU, BONGO Daah siku zinaenda kasi sana asee
 
Kwenye jarida la ambha kulikua na love story Tanganyika na unguja sio mchezo zama zinaenda
 
Aisee niko serious sana. Kila siku, namaanisha kila siku, nawaza ama kufanya kitu fulani juu ya hili. Inawezekana ndani ya wiki moja na nusu ijayo nikawa na mazungumzo na wakubwa wa Sani. Implementation yake huenda ikachukua muda kidogo ila ningependa iwe nzuri kwa kadri ya uwezo wangu wote. Nachokusudia kufanya ni animation (3D). Kila siku ni lazima niwashe kompyuta yangu... kila siku. Asilimia 60 ya nayofanya katika kompyuta yanahusiana na haya. Hata hivyo animation nzuri ni extremely challenging ila nimeweka nguvu kubwa kwelikweli, amini hivyo. Najizuia nisiseme mengi.

Sina contacts za Tuwa ila naweza kufuatilia na nikizipata ntakucheki. Tuombeane uzima.

Mkuu vipi upon?
 
Namkumbuka George Mwakingili. Kama sijakosea alikuwa akimtumia mpelelezi aliyeitwa Jim Mtemvu ilikuwa ni kama Joram Kiango alivyotumiwa na Ben R. Mtobwa au Willy Gamba wa Elvis Musiba.

Gazeti la Motomoto pia nalikumbuka. Jina "Motomoto" lilikuwa na maandishi mekundu kama lilivyokuwa gazeti la Shaba.

Mkuu umenikumbusha mbali sana kwa kweli. Mpaka machozi. Hivi pia gazeti LA Watu lilikuwaje? Michapo nakumbuka lilifungiwa na Dr. William Shija kipindi hicho akiwa Waziri wa Habari na Utangazaji nadhani kwenye 1991-92 hivi
 
Back
Top Bottom