John Kaduma!

John Kaduma!

Na kwa katuni enzi hizo Sanifu ndio funga kazi. Walichora wataalam wa katuni wote unaowajua. Lilimilikiwa na wamiliki wa Majira, DarLeo na Business Times. Wanaitwa Business Times Ltd
 
Kitu bob mikwara, ndondi kati ya Mike Tyson dhidi ya Evander Holifid (sijui kama nimepatia majina), bob mazishi, zena na betina, profesa ndumilakuwili, dokta love pimbi, chepe, nk.
Hao ni miongoni mwa wahusika ndani ya Sani au Bongo.

Pamoja na J.M. Kaduma kuna mchoraji mwingine aliitwa Fortunatus Ndila sijui yuko wapi?

umemsahau lodilofa,bush stars & born town,mayuku,zuma,linda na obi ndani ya kisiwa cha kitintale kwa mzee ole.dah wengine mtaongezea wakuu.
 
Daaah!!! mmenikumbusha mbali sana khs WIMBI la KITINTALE! mambo ya Tajiri wakidosi MAYUKU kipindi hicho KJJN kupata hela ishu! waliokuwa wanaishi DAR wakija kjjn wanakuja na copy hata km imechanika mi nilikuwa naitunza mara nyingi nilikuwa napenda Stori ya OBY alivyokuwa mPambanaji dah kuna mambo mengi ya zamani yalikuwa matam sana acheni2! Kwa cc tunaoyatamani hata cjui tutayapata wapi! BIG UP kwaalieanzisha hii mada nimefurahi sn ndg yenu!
 
umemsahau lodilofa,bush stars & born town,mayuku,zuma,linda na obi ndani ya kisiwa cha kitintale kwa mzee ole.dah wengine mtaongezea wakuu.

Usimwache Mapung'o alipewa mke kwa sababu ya soka. Nilikuwa napenda shati lake linavopepea akichomoka na mpira
 
Wachoraji magwiji ambao sitawasahu ni hawa
1. Ndilla
2. Kaduma
3. Atakalo Soko
4. Prince Magic

Na story ambayo naikumbuka ya Ndila ni Anga za Wenyewe na story ya Aah mamdogo ya Prince Magic

Nadhani huyu ndo mchoraji wa ile hadithi ya "anga za wenyewe", mtanisaidia mnaokumbuka vizuri.
 
Kuna mtu mwingine wa riwaya akiitwa george mwakingili na hadithi ya kinywa cha mauti gazeti motomoto.
 
Hapana!!! usipotoshe mkuu, hiyo hadithi imechorwa na 4tunatus Ndilla.

Asante kwa kunikumbusha ila sijapotosha maana sikuandika kwa uhakika ndiyo maana nikatanguliza neno 'nadhani' kisha nikamalizia na ruhusa ya kukosolewa/kukumbushwa kwa atakaeweza. Yote kwa yote nasema asante kwa kuwekana sawa.
 
magembe R.Malima juhudi zako ni za kuungwa mkono!!
John Kaduma ni Gwiji wa kukumbukwa.
Masoud Kipanya najua upo humu jaribuni kuandaa siku japo mara moja kwa mwaka kuwakumbuka hawa magwiji ili na nyie mkumbukwe na vizazi vya mbele.

APEPE John Kaduma

Asante. Ni kweli kuwa Kaduma na wababe wenzake wanastahili kukumbukwa. Nitafanyia kazi ushauri wako juu ya kumbukumbu ya magwiji hawa.
 
Magembe nakumbuka michoro yako ile kipindi kile tuko kwa Mrisho, nadhani utakuwa unakamilisha mambo Fulani Fulani tu ili uanze ila kwa uwezo wa kuchora nakuaminia.

Baada ya kuanza kushika kompyuta naona nguvu za kuchora zikapungua, ila hata hivyo sijasahau sana... idea ya kuchora inanisaidia kutekeleza mambo kadhaa kwa urahisi katika 3D animation. Ngoja tuone mwisho wake.
 
Na kwa katuni enzi hizo Sanifu ndio funga kazi. Walichora wataalam wa katuni wote unaowajua. Lilimilikiwa na wamiliki wa Majira, DarLeo na Business Times. Wanaitwa Business Times Ltd

Ni kweli. Nakumbuka mwaka 1995 ndiyo mmoja wa Wahariri wa Business Times wakati huo, Sam Makilla ndipo alipoitisha mkutano wa wachoraji ili kuanzisha gazeti la "maroroso, mafinyufinyu.." Sanifu. Ukurasa wa kwanza wa toleo la kwanza la Sanifu ulikuwa na habari ya kioja cha ajuza wa miaka 80 kutaka kupima ukimwi... Lilikuwa gazeti balaa lile.. nasikia lilifungwa kwa sababu ya kuwa na kesi nyingi za kudaiwa kukashifu wanasiasa. Mengine yaliyofuatia kama Kasheshe na kisha Komesha hayakuwa na nguvu sana kama Sanifu.
 
Daaah!!! mmenikumbusha mbali sana khs WIMBI la KITINTALE! mambo ya Tajiri wakidosi MAYUKU kipindi hicho KJJN kupata hela ishu! waliokuwa wanaishi DAR wakija kjjn wanakuja na copy hata km imechanika mi nilikuwa naitunza mara nyingi nilikuwa napenda Stori ya OBY alivyokuwa mPambanaji dah kuna mambo mengi ya zamani yalikuwa matam sana acheni2! Kwa cc tunaoyatamani hata cjui tutayapata wapi! BIG UP kwaalieanzisha hii mada nimefurahi sn ndg yenu!

Wengi wetu tulikuwa tunalipata Sani likiwa limeshachanika lakini bado msisimko ulikuwa mkubwa. Hata kungfu za Ndumilakuwili za "Yan kibadachi yan shodan kataa..." nilizisoma katika jarida lililokuwa limechoka kabisa!!!
 
Usimwache Mapung'o alipewa mke kwa sababu ya soka. Nilikuwa napenda shati lake linavopepea akichomoka na mpira

Mapung'o alikuwa ni balaa katika soka... upepeaji wa shati lake ni kama ulivyokuwa wa Mzee Meko katika jarida la Sani... kuna vionjo fulani ambavyo John Kaduma alikuwa anavipenda ndiyo maana hata alipokuwa akihama jarida moja kwenda jingine ni lazima alivitumia tena.
 
Nadhani hadithi ilikua inaitwa Wimbi la Kitintale huenda ndani ya 'kisiwa cha kitintale' sikumbuki vizuri.

Iliitwa Wimbi la Kitintale na hadithi yake ilikuwa katika mazingira ya kisiwani. Ilichorwa na Chrissantus Katembo.
 
Kuna mtu mwingine wa riwaya akiitwa george mwakingili na hadithi ya kinywa cha mauti gazeti motomoto.

Namkumbuka George Mwakingili. Kama sijakosea alikuwa akimtumia mpelelezi aliyeitwa Jim Mtemvu ilikuwa ni kama Joram Kiango alivyotumiwa na Ben R. Mtobwa au Willy Gamba wa Elvis Musiba.

Gazeti la Motomoto pia nalikumbuka. Jina "Motomoto" lilikuwa na maandishi mekundu kama lilivyokuwa gazeti la Shaba.
 
Mkuu,

Hiyo project isiwe ndoto, manake nna hamu sana ya ku travel back in time and down memory lane! By the way, unaweza kuwa na contact details za Hussein Tuwa? Yule jamaa alinikosha sana na riwaya yake ya Mtuhumiwa. Natamani sana niipate
ili niisome tena.

Mtuhumiwa kwangu mimi ni riwaya ya pili kwa ukali kutoka kwa Tuwa ikitanguliwa na Mkimbizi.
Nilicheki na Tuwa na kumueleza juu ya kuiweka Mtuhumiwa katika kitabu,kipindi hicho ndio alikua anaandaa riwaya yake ya UTATA lakini aliahidi ataifanyia kazi ishu.
Msachi tu kwenye facebook,chapa Husein Tuwa na mambo yataenda...you know wha i'm sayin'!!!?
 
Back
Top Bottom