John Kaduma!

Mmenikumbusha na mwandishi wa hadithi Eddy Ganzel ((RIP)

Baada ya Kaduma kutoka Sani alikwenda Bongo ambapo nakumbuka hadithi ya maneno ilikuwa imetungwa na Eddie Ganzel, siikumbuki jina ila ilikuwa inahusu upelelezi juu ya kifo cha bosi mmoja aliyegongwa na gari. Dah!!
 
John Black!, huyu jamaa alikuw tishio ktk fani uchoraji wa katuni balaa!!! mpaka sasa bado sijaona wa kumlinganisha, ingaw wapo akina Katembo, Aloyce Jacob nk. Namkumbuka sana Madenge, Lodilofa nk
 
Huyu ndiye baba yake na Yohane Kaduma ? ambaye kwa sasa ni MD wa Commercial Bank of Africa?

Sina hakika na hilo ila nachojua John Kaduma alikuwa na mtoto mmoja binti aliyeitwa Jackqueline. Mojawapo ya a.k.a. za John Kaduma ilikuwa ni Baba Jack. Katika mojawapo ya hadithi alizochora (Nadhani ilikuwa ni Mzungu wa Unga) aliandika... "Hadithi hii ni tunu pekee kwa mwanangu mpendwa Jackqueline John Kaduma." Kwa mazingira hayo sidhani kama alikuwa na mtoto mwingine. Namkadiria Jack kuwa na umri kama miaka 20-24.
 
John Black!, huyu jamaa alikuw tishio ktk fani uchoraji wa katuni balaa!!! mpaka sasa bado sijaona wa kumlinganisha, ingaw wapo akina Katembo, Aloyce Jacob nk. Namkumbuka sana Madenge, Lodilofa nk

Hakuna kama John Kaduma. Hata waliomtangulia akina Philip Ndunguru (Mchoraji wa mwanzo kabisa wa Sani) hawakuwa na uwezo kama wake. Never. Akina madenge wa siku hizi wabaaaaya.

BTW, nafanyia kazi namna ya kurudisha nguvu za akina madenge, lodilofa etc kwa kizazi cha sasa na cha miaka ya 80 kwa njia inayosisimua zaidi. Likely kuanzia mwaka 2016 naweza kuwa katika hatua muafaka. "Niko kambini najifua." Tuombe uzima.
 
Mkuu,

Hiyo project isiwe ndoto, manake nna hamu sana ya ku travel back in time and down memory lane! By the way, unaweza kuwa na contact details za Hussein Tuwa? Yule jamaa alinikosha sana na riwaya yake ya Mtuhumiwa. Natamani sana niipate
ili niisome tena.
 
Nililipenda sana jarida la sani lakini siku hizi sijui limekuwaje mara wakabadili likawa gazeti ndipo likawa kero kabisa.

:focus: Pumzika kwa amani J.M. Kaduma
 
Aisee niko serious sana. Kila siku, namaanisha kila siku, nawaza ama kufanya kitu fulani juu ya hili. Inawezekana ndani ya wiki moja na nusu ijayo nikawa na mazungumzo na wakubwa wa Sani. Implementation yake huenda ikachukua muda kidogo ila ningependa iwe nzuri kwa kadri ya uwezo wangu wote. Nachokusudia kufanya ni animation (3D). Kila siku ni lazima niwashe kompyuta yangu... kila siku. Asilimia 60 ya nayofanya katika kompyuta yanahusiana na haya. Hata hivyo animation nzuri ni extremely challenging ila nimeweka nguvu kubwa kwelikweli, amini hivyo. Najizuia nisiseme mengi.

Sina contacts za Tuwa ila naweza kufuatilia na nikizipata ntakucheki. Tuombeane uzima.
 
Ni tatizo. Unakuta ukurasa wa mbele habari ni "Jimama lasasambua mtaani", sasa ukitaka kununua ili umsome Madenge watu wanadhani unataka kusoma habari ya "Jimama...."
 
Kitu bob mikwara, ndondi kati ya Mike Tyson dhidi ya Evander Holifid (sijui kama nimepatia majina), bob mazishi, zena na betina, profesa ndumilakuwili, dokta love pimbi, chepe, nk.
Hao ni miongoni mwa wahusika ndani ya Sani au Bongo.

Pamoja na J.M. Kaduma kuna mchoraji mwingine aliitwa Fortunatus Ndila sijui yuko wapi?
 
Yeah Ndilla alikuwa anachora Bongo sijui yuko wapi... unajua siku hizi majarida yamekosa nguvu.. mambo yamebadilika, nguvu iko katika kutazama (sinema). Kwa ujumla kizazi cha sasa kinaona shida sana kusoma.... inasikitisha kuona Dr Love pimbi hana nguvu tena... ndumilakuwili hajulikani tena...!!
 
Majarida yanakosa nguvu kutokana na kukosa wachoraji na watunzi mahili.
 
Namkumbuka j.kaduma bila kumsahau ibrah radi washokera,na marehem bawji hawa kweli walikuwa vichwa,old is gold
 
magembe R.Malima juhudi zako ni za kuungwa mkono!!
John Kaduma ni Gwiji wa kukumbukwa.
Masoud Kipanya najua upo humu jaribuni kuandaa siku japo mara moja kwa mwaka kuwakumbuka hawa magwiji ili na nyie mkumbukwe na vizazi vya mbele.

APEPE John Kaduma
 
Last edited by a moderator:
Aisee niko serious sana. Kila siku, namaanisha kila siku, nawaza ama kufanya kitu fulani juu ya hili. Inawezekana ndani ya wiki moja na nusu ijayo nikawa na mazungumzo na wakubwa wa Sani. Implementation yake huenda ikachukua muda kidogo ila ningependa iwe nzuri kwa kadri ya uwezo wangu wote. Nachokusudia kufanya ni animation (3D). Kila siku ni lazima niwashe kompyuta yangu... kila siku. Asilimia 60 ya nayofanya katika kompyuta yanahusiana na haya. Hata hivyo animation nzuri ni extremely challenging ila nimeweka nguvu kubwa kwelikweli, amini hivyo. Najizuia nisiseme mengi.

Sina contacts za Tuwa ila naweza kufuatilia na nikizipata ntakucheki. Tuombeane uzima.

Magembe nakumbuka michoro yako ile kipindi kile tuko kwa Mrisho, nadhani utakuwa unakamilisha mambo Fulani Fulani tu ili uanze ila kwa uwezo wa kuchora nakuaminia.
 
Back
Top Bottom